Kombani na Lissu Live on Star TV

Ukweli nimeukuta mjadala uko katikati kabisa,lakini huyu mama kombani hajui chochote.
Ameulizwa katika kikao chabunge kilichoukataa mswada mwezi wa nne,spika alisema
mswada sasa uko bungeni na haitakiwi kurudishwa tena serikalini kwa marekebisho
bali ufanyiwe marekebisho na kamati ya bunge ni kwanini wao waliupeleka serekalini?Kombani
akasema kuwa kamati ya bunge ilitoa ruhusa urudishwe serekelini lakini wakati huo Mh. Lisu
alikuwa Tarime.Sasa Lisu akamwambia aonyeshe maandishi yaliyoruhusu urudishwe serikalini
mama akabaki anacheka na kuona aibu.Kwa ujumla huyu mama ameonyesha wazi hakuwa
amejipanga na alifurahi sana muda kwisha manake alishachanganyikiwa kabisa.
 
mmmh huyu jamaa (LISSU), respect sana.. kila kitu alichokuwa anaongea WAZIRI WENU ANASEMA NIMEKUBALI duuu, jamani huyu jamaa mmoja tuu kawagalagaza CCM wote bungeni wamebaki kumponda tu

Kwani Ukijadili Hoja na Mtu asiyeweza Kujenga Hoja yeye Huishia Kukutukana na Kukuelezea Ulivyo Kimaumbile na Kusahau Kujadili Hoja kwa Hoja!! Poor Magamba Watanzania wa leo sio wale wa Jana Jadilini Hoja na sio Kuzomea!! Kuzomea ni dalili ya Ujinga!!!
 
Ukweli nimeukuta mjadala uko katikati kabisa,lakini huyu mama kombani hajui chochote.
Ameulizwa katika kikao chabunge kilichoukataa mswada mwezi wa nne,spika alisema
mswada sasa uko bungeni na haitakiwi kurudishwa tena serikalini kwa marekebisho
bali ufanyiwe marekebisho na kamati ya bunge ni kwanini wao waliupeleka serekalini?Kombani
akasema kuwa kamati ya bunge ilitoa ruhusa urudishwe serekelini lakini wakati huo Mh. Lisu
alikuwa Tarime.Sasa Lisu akamwambia aonyeshe maandishi yaliyoruhusu urudishwe serikalini
mama akabaki anacheka na kuona aibu.Kwa ujumla huyu mama ameonyesha wazi hakuwa
amejipanga na alifurahi sana muda kwisha manake alishachanganyikiwa kabisa.

Huyo Mama ndio Nahodha anayetegemewa Kutuvusha Kunako Mawimbi Yote Haya!! Iliyobaki Tusali na kukabidhi Maisha Yetu Kwa Muumba!!!
 
Kombani anasema serikali ilipewa ruhusa na kamati kufanya mabadiliko wakati yeye Tundu Lissu yupo Tarime kwa iyo atakua hana taarifa kama mjumbe wa kamati. Lissu anamwambie aonyeshe hansard iliyowapa ruhusa naona bibi Kombani ameishia kujichekesha tu

Huyu Celina Kombani ana wazimu? Ina maana siku zooote Lissu alikuwa Tarime? Na kama mtu yuko Tarime hawezi kupata taarifa? Tarime hakuna mawasiliano? Na hii kamati kila ikukutana huwa hawachukui minutes? Nilisema huko nyuma na sasa narudiai, Serikali ya ccm haina nia ya kuandika katiba mpya ndio maana wakamuweka huyu kilaza Celina Kombani maana haelewi kushoto wala kulia. Worse mwenyekiti na makamu wa kamati ya katiba na sheria wote ni wabunge novice - ccm viti maalum. Hawana uelewa wala uzoefu wa mambo ya katiba. Spika Makinda kwa sababu na yeuye alipachikwa hakuna umuhimu wa kuweka watu wenye uwezo wa kusimamia huu mchakato. Sasa wasubiri hukumu ya watanzania. Watatoa povu sana bungeni lakini huku kiama kiko huku uraini. Ni maandamano kwa kwenda mbele.
 
mama kombani hakutakiwa kuendelea na swala la katiba mara baada ya ile kauli yake ya kusema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya, sasa mtu ambaye ndiye aliyetoa kauli leo hii ndio anashugulikia swala la kupatikana kwa katiba mpya hii ni ajabu na kweli.
 
Komban aliwahi kusema kuwa wanaodai katiba mpya ni watu wa mtaani wasio na kili nzuri. Namkubali mzee Mkinga alipoomba wanachuo wampe haki yake siku moja akiwa kwenye mjadala wa katiba mpya hapo UDSM.

Pinda nae alisema haoni tatizo na katiba iliyopo kwa sasa.

Wasira naye akasema katiba iliypo iko sawa na hatuhitaji katiba mpya

Mwnasheria mkuu naye akarudi kama wasira

JE, kuna sababu ya kuendelea kumwangalia kombani Star tv!? Hakuna kiongozi wa CCM aliye tayari kuona katiba mpya kwakuwa nchi hii ni yao. Ni kama shamba au plot yao wanaolithishana. Ni jukumu letu kuwaondoa madarakani alafu wakajibu mabaya yote wanayoendelea kutufanyia hasa wanapojilinda na ufisadi wao.
 
Kama kila mtanzania atapata uhakika wa kupata chakula, maji, umeme, elimu na afya sina muda na katiba mpya hata raisi awe anasema aitwa muungu, sina time nae ili mradi basic rights are realized
 
Katiba ni mali ya wananchi wote siyo mali ya mtu wala chama. Hawa CCM wasitake kutuzubaisha zubaisha wakati tunazidi kuchelewa! We need changes, the changes that must begin with "katiba mpya".
 
Ameshasahau mkuu kama alitoa kauli hiyo.Lakini hata kama anakumbuka,anachofanya si kwa matakwa yake,anasukumwa na upepo wa nguvu ya umma.Nao upepo unavyovuma wanauona sema tu wapo sugu kinoma.Tukirudi nyuma au kogopa jeshi na polisi we will end up with same or more worse constitution.
mama kombani hakutakiwa kuendelea na swala la katiba mara baada ya ile kauli yake ya kusema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya, sasa mtu ambaye ndiye aliyetoa kauli leo hii ndio anashugulikia swala la kupatikana kwa katiba mpya hii ni ajabu na kweli.
 
Ukweli inatia hasira sana hata pale palipo na ukweli wao wanapindisha sheria kwa manufaa yao.
Manake muswada unasema wazi kuwa ripoti zote za mchakato mzima mpaka uundwaji wa katiba
yenyewe lazima ripoti zake zipitie kwa Raisi kwanza apitie ndipo ziende hatua inayofuata.Sasa
ukiangalia mswada wenyewe unasema wanasiasa hawataruhusiwa kuhusika kwenye uundwaji
wa katiba mpya.Je Raisi si mwanasiasa?Na je kama alichakachua kura atashindwa nini kwa katiba.
Kombani ameulizwa na Lisu kuwa tume ya uchaguzi ndiyo inayolalamikiwa na watanzania wote
lakini leo hii ndiyo itakayosimamia mchakato mzima je hawaoni kuwa haitakuwa fair kama
inavyofanya kwenye uchaguzi?Kombani akajibu tena huku anacheka eti tuwaamini hawataweza
kufanya hivyo.
 
I salute you all Thinkers. It is true I initiated the thread without bringing more updates only because immediately after the post I got another business that forced me off the TV and hence missing all what went on there after.
 
Back
Top Bottom