Kombani na Lissu Live on Star TV

Mh. Tundu Lissu anajaribu kutufafanulia ni kwanini CHADEMA kimekuwa na msimamo huu walionao dhidi ya Muswada wa Katiba Mpya.
Wabogojo, kwanza asante kutujulisha hili.
Pili, tunaomba utujulishe wanaongea nini, najua sio kila mtu ana uwezo wa kuripoti kila kinachoongelewa, ila unaweza kuweka kwenye point format mfano
  • Lissu amezungumzia .....
  • Kombani akazungumzia .....
  • na kuendelea, itatosha kutufanya tufuatilie mjadala unavyoendelea, maeneo mengi tangu jana usiku, Mhe. Ngeleja alitukumbuka, na mpaka sasa anaendeleo kutukumbuka!
 
mmmh huyu jamaa (LISSU), respect sana.. kila kitu alichokuwa anaongea WAZIRI WENU ANASEMA NIMEKUBALI duuu, jamani huyu jamaa mmoja tuu kawagalagaza CCM wote bungeni wamebaki kumponda tu
 
Mnakera watu humu mnaleta habari nusu nusu huku mkijua nusu ya dar no power bora msingeleta hii habar
 
kweli wapendwa ukiamua kutoa thread ambao inahusu mjadala kwenye tv jitahidi kutoa update maana sio wote wenye access ya tv wakati huo.. hizi habari nusunusu sio nzuri ..ingawa sinatupa awareness tu

Kweli mkuu, sasa hata maana kupata taarifa kupitia Jf hamna! Kuna mwingine naye kaanzisha kama huu uzi ila hamna kitu. Watu wanamuomba updates kapotea kabisa
 
Hebu tueleze kama Kombani alikuwa anatabasamu, kwa maana ninamfahamu hajui kutofautisha KUCHEKA na KUTABASAMU. hupenda kuonyesha mwanya alionao wakati hajuikuwa hilo ni pengo.
 
Studio na 3 Dodoma alikuwepo Lissu,Kombani na Mwanaharakati mmoja toka kituo cha sheria na haki za binaadam,Studio na.2 alikuwepo Paul Mabuga na Mwanaharakati mmoja.Kombani kimsingi kabisa anasema anakubaliana na mawazo ya akina Lissu,ila angependa akina Lissu wawepo Bungeni ili waujadili kwa pamoja.Lissu anasema kuwepo kwao Bungeni ni sawa na kuubariki,kuhalalisha mswada ambao kimsingi ni haramu kwa kuwa umekiuka kanuni za kudumu za bunge na haujafuata matakwa ya wananchi ambao kimsingi ndo wanaipa madaraka serikali.

Komboni anasema muswada ni halali kwani serikali iliagizwa na bunge kufanya marekebisho,alivyouliza aeleze ni hansadi ipi na ya tarehe ngapi ambayo imelekodi maagizo hayo akaishia kukenua kwa aibu.kuhusu wananchi kutoa maoni yao Kombani anasema ana file kubwa lenye maoni ya wananchi.alipoulizwa maoni hayo kama ni ya muswada uliosomwa bungeni mwezi wa nne au huu wa mwezi wa kumi na moja,hakutoa majibu.Kwa ujumla Kombani hakuongea lolote la maana zaidi ya kuinama na kucheka cheka nahisi ilikuwa aibu pamoja na maswali ya haja aliyoulizwa na watangazaji.

Mungu tusaidie watanzania,Kiukweli kwa Serikali hii,tusipoweka woga wetu kando,tutaangamia.

AMANI HAIJI ILA KWA NJIA YA UPANGA-----------KIjua ndicho hiki Usipouanika
 
Thanx so much mkuu!
 
Back
Top Bottom