Kisa cha Rais Ali Hassan Mwinyi kipigwa kibao akihutubia

Halafu huyo Mwinyi ni tapeli,yeye ndie anamuandaa mwanawe eti akatawale Zanzibar ,ni kibaka kwa sababu ni mmoja alieamua CCM ishinde kwa vyovyote na ndie mmoja alieweka mkakati wa kutumia nguvu za kijeshi kuisimika Usultani wa CCm Zanzibar ni mtu mmbaya sana ambae kuuwa kwake ni rahisi sana kwa tamaa ya madaraka,ila ukimsikiliza ana maneno mazuri lakini ni mnafiki wa kutupwa hana ukweli anaitumia dini kama kivuli cha kujificha au anaitumia kama ukuta mkubwa uliozunguuka wacheza ngoma,hivyo huwezi kuwaona wanaocheza kwa jinsi ukuta ulivyo mkubwa.Ndivyo mheshimiwa huyo alivyojivika dini. Na watu wamemsitukia ndio moja ya sababu ya kuzabwa kibao
mwiba kwa kuchemsha au bado mgando uanaendelea.tunaongelea kupigwa kibao hilo la kumuandaa mtoto wake linatokea wapi
 
Kuna uzembe mkubwa lazima tukubali. Watu hawafanyi kazi zao na wakati mwingine tunawalaumu viongozi kwa mambo ambayo hayawahusu.

Bush kurushiwa viatu ilikuwa tendo baya na mtu yeyote ambaye anajua jinsi ambavyo security installations inatakiwa zifanye kazi hawezi kutia shaka kuwa mtu aliyemrushia bush viatu, kimoja baada ya kingine, angeweza kuzuiwa baada ya kurusha kimoja. Hata hivyo alifanikiwa kurusha vyote viwili.

Mtu aliyempiga mwinyi, angeweza kumuua. Kwani mlangoni wakati watu wanaingia hakukuwa na ukaguzi!!! Kule kwa bush mlangoni watu walikaguliwa kwa hiyo lilikuwa ni tendo la embarassment tuuu.

Hapa diamond jubilee ilikuwa kama uwanjani tuu. Hivyo walioingia wangeweza kuwa na kitu chochote cha kudhuru. Hata kisu mzee Mwinyi kingemuua. Labda yule mtu ni miongoni mwa watu wa usalama. Au hapa watu wa usalama hawakuwepo kabisa. Au alikuwa mfanyakazi wa ukumbi wa diamond jubilee. au.........

Lakini raia tuu, unakuwa na wasiwasi. Raia huwa tunaamini kuwa wanapokuwepo viongozi basi si kila mtu anaweza kwenda karibu na viongozi. Watu wengine huwa wanasema, kazi zote hufanywa na usalama wa taifa. Sasa tumejua kuwa si kweli. Viongozi wako open tuuu na yale mamisafara tunayoyaona ni show-off tuuuuu kudanganya watu. Ukweli hata akitokea kichaaa mmoja (kama ilivyotokea kwa Changirai huko zim), aka-intercept msafara wa rais, au akaingia jukwaani aliko rais, anaweza kufanya hivyo bila shida yoyote.

Kujaribu kujastify failure yetu, tuna-quote similar failures kama za bush kupigwa viatu. Jambo moja ni kuwa security apparatus duniani kote zilijifunza nini bush kupigwa viatu?

sasa hivi siamini kabisa kuwa viongozi wanalindwa!!!!
 
Mkuu mimi nafikiri kwa maisha ya sasa sioni Kosa la Mzee Mwinyi na naamini kabisa kwamba you cant compete with nature na hili ndilo waumini wa madhehebu yote hawataki kulikubali. Issue ya ngono ni very complex hasa kwa sisi waafrika na wengineo sasa kama tutafumbia macho issue ya kondom nafikiri tutazidi kuangamia ingawa naelewa kusema kwamba watu wavae kondom kwenye dini ni kuchochea ngono ila nafikiri akili inakuwa kumkichwa kwa kila muhusika.

Kinachotakiwa watu wapige debe kuzuia ngono haramu (nje ya ndoa) na si kupigia debe kufanya ngono kwa kondom. Ni dini gani inayofundisha ngono kwa kondom? Nadhani dini zote zinafundisha watu wasifanye ngono haramu.
 
Wadau...Nimepata data muda si mrefu...
Inasikitisha ila habari ndiyo hiyo
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo jumanne pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam amelambwa kofi na Muumini kwa kile kinachoelezwa kama kutetea matumizi ya KONDOMU kwa waumini. Alikuwa akizungumza katika baraza la Maulid lililofanyika jioni hii.

Kwa wale waliohudhuria, basi watupe data zaidi...

...

Pole mzee wetu Alhaji A. H. Mwinyi
 
Asalamaleko,

Pole mzee ruksa! Udini na ungwini vinaimaliza Tanzania....

Ngono bila kondomu ni hatari kwa maisha yako! Kwanza uislamu haukatazi kondomu kihivyo, vilaza kama huyu bwana aliyemchapanga kelbu Mzee Mwinyi ndio wanaturudisha nyuma ktk mpambano dhidi ya gonjwa la ukimwi.....

Uislam hauruhusu kuvaa kondom na kufanya ngono haramu, circumstances za kuvaa kondom muIslam zimeelezwa vizuri tu hapo juu na Kiranga.
 
Sitaki kabisa kuwa drawn katika alichokuwa anakizungumzia Mwinyi!! Hata rais kuna mengi anayoyazungumzia ambayo si wote tunayakubali. Sasa ikiwa rais anazungumzia jambo nisilolikubali, nipande jukwaani nimzabe?? Au nimzuie kuzungumza kwa kuwa mimi sikubaliani na anachosema?

Vipi Kiongozi mwingine? inabidi ajue kuwa haya nitakayoongea inabidi woote waliopo wawe wanakubliana nayo, vinginevyo naweza pigwa?

Hii ni failure ya security installations. Ni failure kubwa. Watu wameshajua kuwa ulinzi huwa ni dhaifu.
 
aah so sad but kwa nini jamani huyu mzee ni wakupigwa kibao kweli ni aibu kubwa
au ndio kutafutafuta umaarufu kama yule jama aliyempiga rais bush kipindi kile mmh sijui
huko selo kapata kichapo cha aina gani naona hakisemeki
 
Hii inadhihirisha jinsi elimu yetu isivyotuandaa Watanzania. Watu wanashindwa kuvumilia maoni tofauti hadi kuchukua sheria mkononi. Hii ni aibu hata kwa baadhi ya wachangiaji hapa wanaoshabikia Mwinyi kupigwa eti kwa kukiuka misingi ya uislamu! Hata kama hukubaliani na matumizi ya kondomu ni wewe na wala si lazima kila mtu awe upande wako, hata kama ni muumini mwenzako! Kwani wewe ndio uliyepewa jukumu na Mwenyezi Mungu la kuilinda amri yake? Wacha watajibu wenyewe watakapofika mbele ya hukumu! Sio kazi yako wewe!
 
Jamani shida hapa ndipo inapoanzia. Kupigia propaganda matumizi ya kondomu kuzuia ukimwi kwa njia ya zinaa kwa kweli si dini zote zinakubaliana maana hakuna dini inakubali jambo hili.
Kondomu kutumika kwa mume na mke katika ndoa ni ruksa hata kwa waislamu au vipi?
Mimi siamini kama nikitumia kondomu na mke wangu nimetenda dhambi. Maana hii inasaidia sana family planning. Tena kondomu ilikuwepo miaka na miaka mingi iliyopita kusaidia family planning. Shida ni kwamba kwa miaka ya karibuni imetekwa na wazinzi na sasa inaonekana kama kitu haramu.
Mi nadhani wanasiasa hawana choice mbali na kuruhusu kondomu zitumike hata na wazinzi ili kufikia malengo yao ya kisiasa. Ndicho alikuwa anafanya Mwinyi. Lakini je ni sawa kumpiga kofi?
No si sawa. Hii ni sawa tu na alivyofanya Mnali. Na ni sawa na yule msukuma wa Mwanza alivyomfanyia Kikwete wakati wa kampeni.
 
Siyo ajabu kwa watu kufanya hivyo ni ukosefu wa elimu ndio tatizo wako wengi tu kama hawa wasio na heshma na kujua maadili na wanaofata maneno ya kuambiwa bila ya kuwa na upeo wowote wa kutenganua baina ya masuala ya dini na ya kijamii.

SAHIBA.
 
Wadau...Nimepata data muda si mrefu...
Inasikitisha ila habari ndiyo hiyo
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo jumanne pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam amelambwa kofi na Muumini kwa kile kinachoelezwa kama kutetea matumizi ya KONDOMU kwa waumini. Alikuwa akizungumza katika baraza la Maulid lililofanyika jioni hii.

Kwa wale waliohudhuria, basi watupe data zaidi...

...

Mzee mwinyi ni fasiki na ni mnafiki ipo siku hilo litadhihirika kwa wa TANZANIA wote ni muda tu aliopanga mpangaji haujawafika huyu yeye na mkewe ndio waliokuwa majenti wa kuingiza Beer za stelar hapa Tanzania sijuwi sasa kama wamesha acha au la siwezi wazulia kama wanaendelea halafu yeye hutowa aya katika quran imesema hivi na vile pia ni yeye alitowa amri ya kuliwa nguruwe dhahiri shahiri Mwalimu julias hakuwahi hata siku moja kufanya tendo kama hilo huyu mzee ipo siku atakuja sema MAHANISI wapewe nafasi katika jamii yetu kuongoza ikiwa makanisa au misikiti maneno yake mzee huyo ni sawa na Asali lakini Rohoni mwake ni shubiri
 
kwa kweli kitendo alichofanya huyo mpigaji sio cha kiungwana kwani yeye kama mwinyi kwanza alimwakilisha Rais, hivyo mpigaji alitakiwa amtafute rais ndo amchape.

halafu viongozi wa bakwata watakuwa wameona risala mapema na wameipitisha ndio walitakiwa kupigwa badala ya kumpiga mzee wa watu.
 
Nadhani kuna sababu mbili kwa nini kanaswa kibao, na zote hazitokani na yale aliyokuwa akihubiri wakati huo: 1. Kama mzee anayetumainiwa kuwa ni wa hekima alipaswa kuweka mguu ktk mgogoro wa Z'bar kwa namna ya kutafuta maelewano. Inavyosemekana badala yake alikuwa akilikoroga gogoro hilo na kuna habari kuwa yeye ndiyo alipenyeza hoja ya kuwepo kwa kura ya maoni kuhusu muafaka ambao tayari ulikuwa umekubaliwa na pande zote mbili.

2. kama mzee wa busara hatujamsikia hata siku moja akikemea kwa nguvu zake zote ufisadi. Kwa hivyo anaonekana hana maana kabisa kama mzee wa kuweza kukanya au kutoa ushauri kwa wenzake wanaoipeleka nchi pabaya.

Haya ni maoni yangu tu, lakini nalaani kitendo cha kupigwa. (ingawa nilisapoti kutupiwa kiatu Bush hasa kutokana na jinsi alivyosababisha vifo vya malaki ya watu wasiokuwa na hatia).
 
This is totally unacceptable,

Huyu mzee wetu jamani nadhani watu wataandamani kupinga kitendo hicho na I hope huyo jamaa atapelekwa keko asap

tungependa kusikia hao TISS wamefanywa nini kwa uzembe kama huu...!

Kupigwa kofi hadharani hata mtu wa kawaida ni udhalilishaji, sembuse mtu mkubwa na muhimu kwa nchi kama Rais mstaafu!

am i dreaming or what?
 
Hili ni jambo la aibu si kwa kiongozi mstaafu tu bali kwa taifa pia! Lazima watu tuheshimu mawazo ya watu wengine, sasa watu wengine kwa kukosa hoja, wanakimbilia kupigana!! SI SAWA. Kwenye swala la uzembe wa walinzi hata G.W.Bush alikoswakoswa na kiatu ingawa ulinzi wake uko tight,sa sembuse wabongo!!?
 
tungependa kusikia hao TISS wamefanywa nini kwa uzembe kama huu...!

Kupigwa kofi hadharani hata mtu wa kawaida ni udhalilishaji, sembuse mtu mkubwa na muhimu kwa nchi kama Rais mstaafu!

...kwa ujinga kama huu, ipo siku JK naye kwa anavyopenda kujichanganya, atakula kipondo!

i242_JKSimple.JPG


...Mjinga kama huyo anayejidai kutumia kivuli cha uislamu kuonyesha ujahili wake kiasi cha kumdhalilisha Mtu mzima kama huyo, achilia mbali urais Mstaafu, ni kitendo kinachofaa kulaaniwa kwa nguvu zote!
 

Attachments

  • 8D6U3421[1].JPG
    8D6U3421[1].JPG
    98.8 KB · Views: 93
Hujui kitu wewe na ni mgumu wa kuelewa....issue ni ngono haramu na sio uvaaji wa kondomu!! Unaweza kumdungua mke wako halal tena wa ndoa kwa kondomu.....tulia na acha kukurupuka!! Na zaidi ni kuwa kondomu zilikuwepo hata kabla ya ngoma haijaingia.......ukielewa hapa then utakuwa umeelewa tofauti ya binadamu na ng'ombe!!

Misimamo kama yako na huyu mpuuzi aliyemchapa kelbu Mwinyi ndio inafanya uislamu unaonekana ni dini ya kifedhuli. Again, kupigia debe kondomu sio sawa na kuhalalisha matendo ya ndoa nje ya ndoa.....kwanza ni waislamu wangapi ambao hawakuwahi/hawajawahi kufanya ngono kabla ya kuoa/kuolewa?? Wewe unavimada wangapi? Anza kuvaa kondomu, la sivyo utaiachi udhuni familia yako....

Acha unafiki.......

Wabongo tuache jazba, msije mkachafua hali ya hewa hapa. Cha msingi hapa ni kujua kuwa hatuna ulinzi kwa viongozi wetu. Kwa maana hiyo basi kunapokuwa na shughuli kama hii (kanisani ama msikitini) waandaaji wa shughuli lazima wawe makini na wajipange kuhakikisha kuwa wahusika tu ndio wanaotakiwa kuonekana kwenye meza kuu na sio nyang'au mwingine yeyote. Ndio maana huwa naona kwenye sherehe za baadhi ya makanisa ya wakatoliki hata wapiga picha huwa wanapewa vitamburisho na wale viongozi wanaotoa huduma wanavaa mikanda. kama huna kitamburisho unapigwa chini kutakiwi kufanya kitu kisichokuhusu. Inawezekana hilo halikuwa na mlengo wa kiusalama (sijui), lakini inabidi kuanzia sasa tujifunze hilo.
 
Kila kitu kinamahali pake, kuna choo sehemu ya kujisaidia na jiko sehemu ya kupikia. Kila dini inamisingi yake na mwelekeo wake sasa huwezi peleka siasa kwenye dini utaleta tabu. Wapo magei duniani na wanaamini kuwa gei ni haki yao. zipo dini kadhaa zinakataa huu uchafu sasa ukitaka kuanza hubiri mambo ambayo sio sehemu yake utaleta kasheshe.Waisilamu naamini wanapinga matumizi ya kondon kutokana na kuruani, sasa sijui mwinyi alikuwa anazungumza nini kuhusu hilo ila kama alisema ruksa kweli pale sio mahala pake angeweza sababisha makubwa zaidi ya kibao.

Pili ni vyema hawa viongozi wakanyukwa waelewe sio tu usalama wa taifa umekufa bali ulinzi wa rai haupo. Albino wanauwawa wezi kila kukicha wanaibia masikini wezi na mafisadi wanaiibia serikali usalama wa taifa wanakula rushwa wapo tu na mishahara ya kodi zetu wako bize na dili za kina Rostam na kuwapelekea habari nini kinaendelea na kuwalinda. Remember mafia time.

Watauwa mmoja baada ya mwingine ndipo uwajibikaji utakapokuja. Kikwete alipigwa mawe mbeya, mwinyi kazabwa kibao.
Ila tusisahau madhila wameyaanza wenyewe, mudhihir alimzaba asha baraka vibao ikaonekana sawa hakupelekwa hata kuhojiwa mpaka mkono wa kuzabia ulipotolewa.
 
...Kibaka tu huyu, kweli kijana kama huyu ambaye Mzee Mwinyi anaweza kumjukuu anadiriki kunyanyua mkono wake kumchapa kofi? ...*%$"+@:^%$**&&$$zake huyu!!!!

Kibaka_Mwinyi.JPG
...picha kwa hisani ya blogu ya drfaustine!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom