Kisa cha Rais Ali Hassan Mwinyi kipigwa kibao akihutubia

Invisible,

..ALHAJI kashambuliwa kwenye shughuli ya KIDINI.

..halafu wachangiaji wameshaanza kuleta hoja za KADHI,BAKWATA, etc etc.

..hata huyo aliyemshambulia inawezekana kabisa amefanya hivyo kwasababu za KIDINI.

..moderator fanya kazi yako. peleka hii kwenye ukumbi wa DINI-DINI.

Jokakuu, hii sio ishu ya kidini bana. Wewe unayesema ni ya kidini ndio unataka kuigeuza kuwa ya kidini.

Habari hapa ni raisi mstaafu kuzabwa kibao (kama ni kweli) mbele ya watu.
 
Halafu huyo Mwinyi ni tapeli,yeye ndie anamuandaa mwanawe eti akatawale Zanzibar ,ni kibaka kwa sababu ni mmoja alieamua CCM ishinde kwa vyovyote na ndie mmoja alieweka mkakati wa kutumia nguvu za kijeshi kuisimika Usultani wa CCm Zanzibar ni mtu mmbaya sana ambae kuuwa kwake ni rahisi sana kwa tamaa ya madaraka,ila ukimsikiliza ana maneno mazuri lakini ni mnafiki wa kutupwa hana ukweli anaitumia dini kama kivuli cha kujificha au anaitumia kama ukuta mkubwa uliozunguuka wacheza ngoma,hivyo huwezi kuwaona wanaocheza kwa jinsi ukuta ulivyo mkubwa.Ndivyo mheshimiwa huyo alivyojivika dini. Na watu wamemsitukia ndio moja ya sababu ya kuzabwa kibao

Acha kuchafua hewa bana..
 
L'afaanaaleki kufa hakuna breki.

Wameenda kumpiga kibao Mze Walii mwenyewe?? Ama wameitafsiri vibaya ile "ruksa" kuwa "hata kunipiga kibao ruksaaaa"?

OK, kupigana vibao ni barbaric, lakini kama ni lazima kumzaba kibao mtu kwa nini msimzabe fisadi Mkapa?

Nutheads wamezidi. Lakini kwangu mimi, badala ya kumvunjia heshima mzee Mwinyi, swala hili linamuongezea mvuto kwa kuonekana jasiri aliyeongea ukweli mchungu mbele ya mahafidhina wasiopenda kwenda na wakati.Sema Mzee Ruksa, brutal force will never conquer reason.

Naona huyu jamaa naye kaiandika katika blog yake hapo chini.

lukwangule entertainment: Mzee Mwinyi azabwa kibao
 
Kama kazabwa kibao kwenye sherehe ya kiIslam na yeye ni muIslam na kenda kuwaambia waIslam wenzake wavae kondom, wakati kama ni muIslam anatakiwa ajuwe kuwa uIslam hauruhusu kabisa ngono bila ndoa, iwe kwa kondom au bila kondom, basi hilo ni kosa, hata kama ni Rais hayuko juu ya uIslam, hawezi kuleta mafundisho mapya kwenye uIslam.

Kama ni kwa hayo niliyoyaeleza hapo juu, nampa pongezi huyo muIslam na kama si kwa hayo kuna data zingine zaidi ya hayo, basi ntaamuwa ntakapozipata.
 
Nyani Ngabu,

..Mzee Mwinyi hakushambuliwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa.

..tukio hilo limetokea ktk shughuli ya Baraza la MAULIDI.

Game Theory,

..Slaa akishambuliwa ktk shughuli ya Kanisa akiwa kama muumini basi hoja hiyo haitakuwa na nafasi hapa. nitapendekeza ihamishwe.

..wewe mwenyewe umeanza kushambulia BAKWATA, na SHEIKH MKUU. ukumbi huu siyo mahala pa mashambulizi kama hayo.
 
Naona kila mtu sasa asiyeridhika na mwenzake anachukuwa hatua mkononi juzi waziri mkuu alitoa maagizo wanaouwa maalbino washugulikiwe , mnali nae kachapa walimu sasa mwananchi kaamua kujaribu kwa kiongozi
 
Jamani huu ni utani mmeamu tutaniane au ndiyo kweli? nafikiri wamemuonea sasa kondom unaikataa msikitini mtaani inakubalika ya nini tuchapane? kila mtu ana haki ya kusema.

Anyway kama kofi limeshampata basi tena hatuna jinsi but its not fair.
 
Nyani Ngabu,

..Mzee Mwinyi hakushambuliwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa.

..tukio hilo limetokea ktk shughuli ya Baraza la MAULIDI.

Haijalishi Mwinyi kazabwa wapi kibao! Yeye ni mwanasiasa mkongwe Tanzania. Siasa ni sehemu ya nyanja zote za maisha. Siasa imo kwenye kila kitu. Hata hii forum ina siasa zake pia.

Hii habari hapa ni mahala pake.
 
Inaonyeshwa kwenye TV sasa Tanzania....got sms kutoka kwenye vyanzo vyangu!
 
kama kazabwa kibao kwenye sherehe ya kiislam na yeye ni muislam na kenda kuwaambia waislam wenzake wavae kondom, wakati kama ni muislam anatakiwa ajuwe kuwa uislam hauruhusu kabisa ngono bila ndoa, iwe kwa kondom au bila kondom, basi hilo ni kosa, hata kama ni rais hayuko juu ya uislam, hawezi kuleta mafundisho mapya kwenye uislam.

Kama ni kwa hayo niliyoyaeleza hapo juu, nampa pongezi huyo muislam na kama si kwa hayo kuna data zingine zaidi ya hayo, basi ntaamuwa ntakapozipata.

ndugu yangu kwanini unatetea watenda dhambi tena ametenda kwa kiongozi wake -- huu ni utovu wa nidhamu hakustahili kufanya hivyo kuna sehemu za kutoa maoni yako kama hukubaliani na mawazo ya mwingine na sio vita
 
Hadi huyu jamaa anaenda High Table na kumfikia mzee wa watu kumzaba kibao ni udhaifu mkubwa kwa walinzi wake.

Hii imetokea kwa mzee wetu, next time tarajia hata Rais wetu atazabuliwa hivi. Au hata kibaya zaidi ya hiki!

Sintoruhusu mjadala huu uende kidini... Tuangalie athari za kitendo hiki kwa viongozi wa taifa letu na usalama wao na taifa kwa ujumla!
 
Kama kazabwa kibao kwenye sherehe ya kiIslam na yeye ni muIslam na kenda kuwaambia waIslam wenzake wavae kondom, wakati kama ni muIslam anatakiwa ajuwe kuwa uIslam hauruhusu kabisa ngono bila ndoa, iwe kwa kondom au bila kondom, basi hilo ni kosa, hata kama ni Rais hayuko juu ya uIslam, hawezi kuleta mafundisho mapya kwenye uIslam.

Kama ni kwa hayo niliyoyaeleza hapo juu, nampa pongezi huyo muIslam na kama si kwa hayo kuna data zingine zaidi ya hayo, basi ntaamuwa ntakapozipata.

Dar,

Argument yako inateleza pale unapofikiri kwamba condom zinatumika nje ya ndoa tu, condom zina matumizi mengi, ikiwapo uzazi wa mpango, ambapo hata ndani ya ndoa hutumika.

Swala la uislam ni gumu na linahitaji mjadala zaidi, kwa sababu vitabu vyenyewe vina tafsiri nyingi, kuna sehemu wanasema huwezi kukojoa ukielekeza utupu kibla, sehemu nyingine msomi wa dini akakutwa anakojoa huku utupu kauelekeza kibla akasema unaweza kukojoa ukiuelekeza utupu kibla kama kuna jengo au kitu kati yako na kibla, kwa hiyo kuna hadithi na tafsiri nyingi, kwa hiyo hatujui Mzee Ruksa alikuwa anaongelea katika context gani, na mpaka tukijua hilo, na kuangalia misahafu, tafsiri za hadithi na miongozo mingine ya masheikhs wasomi wa uislamu, ndipo tutajua.

Ona hapa, ukisoma utaona ukosefu wa elimu ya dini unaweza kusababisha mambo ya aibu kama hili la kumpiga kibao mzee wa watu, mzee aliyelitumika taifa kwa muda mrefu na ingawa mabaya mengi yametendeka chini yake, kuna mazuri mengi aliyafanya na mfano wake wa kuigwa wa kujiuzulu kwa integrity unawasuta ma fisadi wanaong'ang'ania madaraka katika scandals zote za leo.

Islam: Condom, sustenance, condoms

Question
As Salaam Walikum Sir
I am sorry to ask can i use condom with my wife because with the grace of ALLAH i have one child at present i dont want another so please tell me can i use or not?
And if not tell me what is the way not to have a child now because the frist child is not at complete one years aslo
please give me proper islamic way

Jazak ALLAH kahir
MOHAMMED

Answer
Yes, you may use temporary contraception, like condoms, to space yur children. Doing so isn't taking a child's life which what is condemned. 17:31 Kill not your children for fear of want: We shall provide sustenance for them as well as for you. Verily the killing of them is a great sin.
Also for the mother's health you may use condoms- there is no harming of oneself in Islam.
 
Hadi huyu jamaa anaenda High Table na kumfikia mzee wa watu kumzaba kibao ni udhaifu mkubwa kwa walinzi wake.

Hii imetokea kwa mzee wetu, next time tarajia hata Rais wetu atazabuliwa hivi. Au hata kibaya zaidi ya hiki!

Sintoruhusu mjadala huu uende kidini... Tuangalie athari za kitendo hiki kwa viongozi wa taifa letu na usalama wao na taifa kwa ujumla!

Nakuunga mkono pamoja na mguu wangu! Kitendo hiki kwa kweli kina implications nyingi tu kuanzia mambo ya jamii hadi ulinzi wa maraisi wetu wastaafu. Iachwe hapa hapa. Atakayeleta mambo yake ya udini maoni yake yafutwe.
 
Kitendo cha kumnasa Alhaji Mwinyi kibao ni kibaya sana, hata kama hukubaliana na hayo matumizi. Ukitaka kila kitu kiwe kama wewe unavyotaka utaishia kugombana na watu hata kama wewe umeiva kwenye imani, mengine inabidi uyaache yapite. Pole sana mzee wetu Mwinyi.
 
Nimeshuhudia kwa macho yangu tbc one mwinyi akilambwa kibao, ni kama ilikuwa sinema, kijana huyo alipanda jukwaani na kumlamba kibao, na wakati akishuka jukwaani ndipo alipobanwa na kuanza kushuhulikiwa, hata ahivyo mwinyi alikuwa mpole na kuhimiza hadhira ilyokuwa inamsikiliza kuendela na mdahalo, huku mbaya wake akishuhulikiwa chini ya miguu yake

akina mwinyi na viongozi wengine wa siasa , wanapaswa kutambua vizuri hadhira inayowazunguka, yeye kuhimiza matumizi ya kondomu ni sawa na kuwaambia waislamu wale nguruwe, yote ni haramu , yaani kujamiana kabla ya ndoa na kula nguruwe zote ni haramu, ni sawa pia ukikaribishwa vatican uanze kuhubiri kutoa mimba na hata kutumia kondomu.

Viongozi wa siasa watumie vizuri majukwaa yao, na wanapokuwa kwenye majukwaa ya kidini wawe macho. Mambo ya kidini ni very sensitive, huenda kijana aliyempa kibano tayari ana thawabu according to holy quaran

mfano mimi ni mkatoliki, nikifa kwa kukemea kutoa mimba tayari nimekufa kama shahidi wa kuitetea nchi yangu

pia, nawalaumu wanaozidi kumfuata mzee kama mwenye at his age of 80s, tayari amechoka kiakili
 
ndugu yangu kwanini unatetea watenda dhambi tena ametenda kwa kiongozi wake -- huu ni utovu wa nidhamu hakustahili kufanya hivyo kuna sehemu za kutoa maoni yako kama hukubaliani na mawazo ya mwingine na sio vita

Hapana uIslam hauna kuoneana haya kwenye makosa, kama mwinyi kafanya kosa kama hilo, anafaa aonywe na pengine huyo aliemzaba kibao ni wa rika lake, Jazba. Siku ingine atakuwa makini zaidi.
 
Nimeshuhudia kwa macho yangu tbc one mwinyi akilambwa kibao, ni kama ilikuwa sinema, kijana huyo alipanda jukwaani na kumlamba kibao, na wakati akishuka jukwaani ndipo alipobanwa na kuanza kushuhulikiwa, hata ahivyo mwinyi alikuwa mpole na kuhimiza hadhira ilyokuwa inamsikiliza kuendela na mdahalo, huku mbaya wake akishuhulikiwa chini ya miguu yake

akina mwinyi na viongozi wengine wa siasa , wanapaswa kutambua vizuri hadhira inayowazunguka, yeye kuhimiza matumizi ya kondomu ni sawa na kuwaambia waislamu wale nguruwe, yote ni haramu , yaani kujamiana kabla ya ndoa na kula nguruwe zote ni haramu, ni sawa pia ukikaribishwa vatican uanze kuhubiri kutoa mimba na hata kutumia kondomu.

Viongozi wa siasa watumie vizuri majukwaa yao, na wanapokuwa kwenye majukwaa ya kidini wawe macho. Mambo ya kidini ni very sensitive, huenda kijana aliyempa kibano tayari ana thawabu according to holy quaran

mfano mimi ni mkatoliki, nikifa kwa kukemea kutoa mimba tayari nimekufa kama shahidi wa kuitetea nchi yangu

pia, nawalaumu wanaozidi kumfuata mzee kama mwenye at his age of 80s, tayari amechoka kiakili

Mwikimbi,
Tuwekee kwenye you tube na sisi tuone.
 
Hapana uIslam hauna kuoneana haya kwenye makosa, kama mwinyi kafanya kosa kama hilo, anafaa aonywe na pengine huyo aliemzaba kibao ni wa rika lake, Jazba. Siku ingine atakuwa makini zaidi.
=====

Ndugu DSM

Kumbuka Mzee Mwinyi alikuwa anamwakilisha Rais Kikwete katika hafla hiyo.
Kikwete alialikwa kama Mkuu wa nchi lakini akawa na hudhuru na kumtuma Mzee Mwinyi. Hata kama wote wawili ni waislam, lakini kuwapo kwao pale waliwakilisha serikali kuonyesha mshikamano wa dini na serikali. Mchapaji kibao amechemsha, na ashukuru Mungu hakuwa JK kwani shaba ingewaka na labda jamaa sasa angekuwa "paradiso" na kupata thawabu yake aliyoahidiwa kwa kujitoa mhanga kumchapa kibao Mkuu wa nchi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom