Kisa cha Rais Ali Hassan Mwinyi kipigwa kibao akihutubia

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
43
Wadau,

Nimepata data muda si mrefu.
Inasikitisha ila habari ndiyo hiyo
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo jumanne pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam amelambwa kofi na Muumini kwa kile kinachoelezwa kama kutetea matumizi ya KONDOMU kwa waumini.

Alikuwa akizungumza katika baraza la Maulid lililofanyika jioni hii.

=====
UPDATES:

Kijana aliyemzaba kibao Rais Mwinyi afunguka

Machi 12, 2009

Wakati taasisi mbalimbali za kidini, wananchi wa kawaida na Kamati ya Bunge zikilaani kitendo cha Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, kupigwa kofi shavuni, muumini aliyefanya kitendo hicho, Ibrahim Said, ameeleza kuwa alifanya hivyo kupinga matumizi ya kondomu kwa waumini wa dini ya Kiislamu kwa madai kwamba, yanachochea vitendo vya zinaa.

Pia alisema alifanya kitendo hicho kupinga kuwapo kwa umoja kati ya Waislamu na Wakristo wakati wa kusherehekea sikukuu zao (Maulid, Idd, Krismas na Pasaka), uliozungumzwa na Mwinyi katika hotuba zake alizozitoa wakati wa mkesha Jumatatu usiku na kwenye Baraza la Maulid, jijini Dar es Salaam juzi.

Alisema hakuwa na nia ya kumdhuru Mwinyi na wala hamchukii, bali alikuwa na lengo la kufanya kituko chochote ili ujumbe wake uwafikie watu wengi.

Alitoa maelezo hayo alipohojiwa na polisi saa chache baada ya kufanya kitendo hicho wakati Mwinyi alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam juzi jioni.
 
Last edited by a moderator:
Raisi wa iran nae alishambuliwa kwa kiatu na mtu aliyefanya hivyo hawajamkamata

kweli watanzania wa leo sio wale wa jana na juzi , lakini kuchukuwa hatua mkononi ni kosa
 
Hata kama hukubaliani na msimamo wake, lakini ni vema kuuheshimu. Personally sikubaliani na vitu kama abortion lakini I always strive to respect other people`s point of views. Right to make a choice. No body is a sole custodian of the truth.

Thats why nakataa vitu kama kadhi`s court kuviweka kwenye katiba inayotuhusu WATANZANIA wote..maana ni issues ambazo wengi hatuwezi kukubaliana mpaka mwisho wa dunia. Hivyo ni bora tuu kila mtu akaachiwa uhuru wa kuamua. Ya dini yawe ya dini. Ya kisecular yawe hivyo hivyo. Hapo tutaishi kwa amani na upendo.

Pole sana Alhaji.
 
Masanja you are right kuna jinsi ya kupresent matters ikazungumzwa na kupatiwa ufumbuzi. Haikuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe hata kama huyo mtu hajakubaliana na suala la Kondomu zaidi kaonyesha utovu wa nidhamu kwa kiasi kikubwa. Kumpiga mtu kama Mwinyi hadharani, haipendezi kwakweli.

NB:Happy Maulid Day kwa wote!
 
Masanja you are right kuna jinsi ya kupresent matters ikazungumzwa na kupatiwa ufumbuzi. Haikuwa njia nzuri ya kufikisha ujumbe hata kama huyo mtu hajakubaliana na suala la Kondomu zaidi kaonyesha utovu wa nidhamu kwa kiasi kikubwa. Kumpiga mtu kama Mwinyi hadharani, haipendezi kwakweli.

NB:Happy Maulid Day kwa wote!

Na je mlinzi/walinzi wake walikuwa wapi? maana nina uhakika aliyempiga kofi hawezi kuwa alikuwa amekaa kwenye meza kuu!
 
..Moderator peleka hii kwenye ukumbi wa DINI-DINI.

Sipendi na sema tena sipendi mijadala ya u-dini lakini kama ni kweli imetokea hivyo hapa ni mahala pake maana huko kwenye udini watu wengine huwa hatutaki kuingia. Na kama imetokea kweli huyo jamaa afungwe maana hata kama Alhaji mwinyi angekuwa ni raia wakawaida sheria inazuia kumshambulia mtu bila sababu. Bila shaka mwendesha mashtaka atasema " tarehe ....bwana jazba bila halali yoyote alimshambulia rais mstaafu Ali mwinyi na kumsabibishia maumivu makali."
 
Jamani!!!!!
Imekuwaje wakati rais mstaafu anatakiwa awekewe ulinzi kama kiongozi?
Sasa Mwinyi amepigwa bodyguard wake akiwa wapi?

Sasa kama kapigwa kweli. Basi hii ni ishara kwamba sasa nchi imefikia hatua ya kutowaheshimu kabisa viongozi. Si tu walioko wastaafu bali hata wallioko madarakani.
 
Wadau...Nimepata data muda si mrefu...
Inasikitisha ila habari ndiyo hiyo
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo jumanne pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam amelambwa kofi na Muumini kwa kile kinachoelezwa kama kutetea matumizi ya KONDOMU kwa waumini. Alikuwa akizungumza katika baraza la Maulid lililofanyika jioni hii.

Kwa wale waliohudhuria, basi watupe data zaidi...

...
Sikuhudhuria, lakini kuna mdau alinitonya juu ya hili na alikuwa ndani ya ukumbi huo.

Wale wanaosema mjadala huu umekaa kidini nadhani tuvute subira, yawezekana ikawa si dini tu... Kuna zaidi. Tusubiri kuona vyombo vya habari vya nyumbani vitaandika vipi.
 
Hawa maraisi wastaafu wanakuwa wamepangiwa walinzi wangapi? Kama ni kweli hii takuwa ni uzembe wa hali ya juu waliouonyesha hao walinzi.
 
Halafu huyo Mwinyi ni tapeli,yeye ndie anamuandaa mwanawe eti akatawale Zanzibar ,ni kibaka kwa sababu ni mmoja alieamua CCM ishinde kwa vyovyote na ndie mmoja alieweka mkakati wa kutumia nguvu za kijeshi kuisimika Usultani wa CCm Zanzibar ni mtu mmbaya sana ambae kuuwa kwake ni rahisi sana kwa tamaa ya madaraka,ila ukimsikiliza ana maneno mazuri lakini ni mnafiki wa kutupwa hana ukweli anaitumia dini kama kivuli cha kujificha au anaitumia kama ukuta mkubwa uliozunguuka wacheza ngoma,hivyo huwezi kuwaona wanaocheza kwa jinsi ukuta ulivyo mkubwa.Ndivyo mheshimiwa huyo alivyojivika dini. Na watu wamemsitukia ndio moja ya sababu ya kuzabwa kibao
 
Kosa ni vile aliongelea Kondom ktk Ghafla ya Dini!

Waache wataalamu wa afya wayaongee haya!

Ila la kumwasha kofi..jamani mimi huyu mzee nampenda sana..basi tu wasingempiga!
 
Invisible,

..ALHAJI kashambuliwa kwenye shughuli ya KIDINI.

..halafu wachangiaji wameshaanza kuleta hoja za KADHI,BAKWATA, etc etc.

..hata huyo aliyemshambulia inawezekana kabisa amefanya hivyo kwasababu za KIDINI.

..moderator fanya kazi yako. peleka hii kwenye ukumbi wa DINI-DINI.
 
Halafu alivyo kibabu hivyo unamchapa kibao cha nini? Akizimika moja kwa moja je?Watu wengine bana wanajitafutia kesi za mauaji bure..
 
Hawa maraisi wastaafu wanakuwa wamepangiwa walinzi wangapi? Kama ni kweli hii takuwa ni uzembe wa hali ya juu waliouonyesha hao walinzi.
Nasikia hata TBC Taifa (Radio) wamegusia kitendo hiki. Hii itawafanya waone umuhimu wa topic ile ya "Walinzi wa viongozi Mbalimbali". Taarifa nilizopata ni kuwa UWT wamemshughulikia aliyehusika na kitendo hicho, sijajua ni kwa extent gani.
 
Wadau...Nimepata data muda si mrefu...
Inasikitisha ila habari ndiyo hiyo
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo jumanne pale katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam amelambwa kofi na Muumini kwa kile kinachoelezwa kama kutetea matumizi ya KONDOMU kwa waumini. Alikuwa akizungumza katika baraza la Maulid lililofanyika jioni hii.

Kwa wale waliohudhuria, basi watupe data zaidi...

...

Bado natafakari vipi kama angepigwa hayo makofi na Mkristu? Pole mzee ruksa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom