Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana...

WaTanzania kote nchini sasa tunasema tena kwa sauti kwamba waliomteka Dr Ulimboka WAMWACHIE MARA MOJA na akiwa hana jeraha lolote lile!

Hili lisipotekelezwa kwa haraka basi huenda kukafuatia mgomo mkubwa zaidi wa sehemu kubwa zaidi ya wananchi kila kona ya nchi wakati wowote tangu sasa!
 
WANAJF,
Kwanza natanguliza samahani kwa kuleta taarifa ambayo haijathibitishwa bado na familia ya muhusika Dr. Ulimboka, lkn kuna taarifa zinasema kwamba amekamatwa usiku wa leo kwasababu ya mgomo wa madaktari. Je, kuna mwana-JF yeyote mwenye taarifa hizi kama ni kweli au?
TELO.
 
Kwani chanzo cha mgomo ni mtu au ubovu wa system?? does having him arrested nullifying the existing facts???
 
Nimecheki na Rafiki yangu mmoja ni daktari wa Amana kuhusu Kazia hii,wao nao wanaamini kwamba Daktari Ulimboka ametekwa na watu ambao wametumwa na Serikali!!

Hii inazidi kuamsha hasira zao na Wamesema wanajipanga Kogoma zaidi,sio baridi tena,itakuwa Mgomo Moto!!
 
Sasa hii serikali dhaifu hapo ndipo inapokosea kumkamata ama kumteka huyu Ulimboka ndio kuchochea mgomo ni sawa na kuweka petroli kwenye moto unafifia kuzimika.

Hii sio kutatua tatizo bali ni kuongeza taizo kwani madaktari wanaweza kugoma kudai mwenzao arudishwe na hii itatuletea maafa zaidi ukiangalia wanajeshi wamegoma kutoa madaktari wao wakitaka serikali dhaifu imalizane na madaktari wake kuepusha maafa zaidi
 
Kipindi hiki ni cha mvutano wa madaktari na serikali pengine jamaa ameamua kuzima simu na kubadilisha makazi kwa hofu yake tu kisha tunasema katekwa ......

sioni sababu ya kusema sana kama hatuna uhakika na jambo hili
 
Angekamatwa ingejulikana ni kwa sababu zipi na amepelekwa wapi, unasema amekamatwa kwa mahojiano zaidi,unajua amekamatwa na nani na anahojiwa kuhusiana na nini?
Unajuwa ndani ya nchi kuna vyombo vingi vya usalama.vingine vinafanya kazi waziwazi na vinajulikana kwa watu.vingine vinafanya kazi kwa kificho na havitakiwi kujulikana na ofisi zao unaweza ukakuta ni mahandaki na vyote hivyo vinamiliki silaha kihalali na lengo lao ni moja.

Kwa hoja ya mleta taarifa kutekwa nineno zito sana halilingani na nguvu iliotumika kumchukuwa huyu dr.kutekwa lazima itumika nguvu kubwa.nguvu iliotumika hapa ni ya kawaida hivyo atakuwa amekamatwa na baadhi vyombo vya usalama ambavyo unaweza ukakuta hata vyenyewe havijuwani.

Kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea.
 
Sina hakika na ukweli wa habari hii!
Kwa uhusiano alionao na serikali hii, saa sita ya usiku anaenda kufanya 'reconciliation' na 'mtu' wa serikali? Tena peke yake bila viongozi wenzie? Atakuwa wa ajabu basi!

King'asti

Hii taarifa inaacha maswali mengi kuliko majibu!

Hivi nani anakumbuka ile story ya mbunge wa CUF Msabaha kutekwa na Serikali?! Nasikia siku hizi huyo Msabaha ni CCM damu damu!
 
Kuna thread ipo yenye hii habari, ila nayo bado ni unconfirmed.
 
Kwanini tunamuita KIONGOZI wa MGOMO badala ya Kumuita MTETEZI wa WANYONGE????????? Huyu ndie mtetezi wetu na sio vinginevyo hayo ya Viongozi wa mgomo yanaleta maana hasi kwa jamiii
 
Kama yuko tayari kufa kwa ajili ya taifa kutekwa ni moja ya silaha zinazoweza kutumiwa katika uwanja wa vita
 
katekwa kwenda wapi? nimezungumza na daktari rafiki wa karibu sana na Ulimboka anasema yuko salama tu
 
Risasi na kuteka watu ni mbinu za serikali iliyofilisika mawazo.

nadhani hata naibu mwanasheria wa serikali anahusika kwa sababu jana alinukuliwa na VOA akisema madaktari wasiporudi kazini kwa kutii amri ya mahakama. Watasikia kesho nadhani hii ni mojawapo ya uthibitisho wa kauli yake. sasa watatujua sisi ni kinanani na sasa ndiyo wamechokoza moto hata na kwenye mahalmashauri madaktari watagoma, solidarity forever bravo madaktari
 
Habari hizi zikithibitishwa ni za kweli na Ulimboka akipigiwa simu akawa hapatikani inabidi wananchi tuunge mkono madaktari na bila shaka hali itakuwa mbaya zaidi
 
Back
Top Bottom