Mzee Busara
Senior Member
- Feb 29, 2008
- 113
- 19
atakuwa hajatekwa bali kaingia mitini hataki kuongoza tena mgomo
Unajuwa ndani ya nchi kuna vyombo vingi vya usalama.vingine vinafanya kazi waziwazi na vinajulikana kwa watu.vingine vinafanya kazi kwa kificho na havitakiwi kujulikana na ofisi zao unaweza ukakuta ni mahandaki na vyote hivyo vinamiliki silaha kihalali na lengo lao ni moja.
Kwa hoja ya mleta taarifa kutekwa nineno zito sana halilingani na nguvu iliotumika kumchukuwa huyu dr.kutekwa lazima itumika nguvu kubwa.nguvu iliotumika hapa ni ya kawaida hivyo atakuwa amekamatwa na baadhi vyombo vya usalama ambavyo unaweza ukakuta hata vyenyewe havijuwani.
Kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea.
Akamatwe kwa kuvunja sheria ipi? Maana kugoma ni haki ya kila mtu, kama ingekuwa kudai haki yako ni kuvunja sheria basi tusingekuwa tunamsifu Nyerere, maana angekuwa ndo mhalifu kuwashinda wahalifu nchini Tanzania. Lets believe kwamba hawatamfanya kitu kibaya. Maana isije ikatokea kesho tukasikia mwili wake umekutwa kando kando ya barabara. Na kwa watz walivyo waoga, kila mtu atafyata mkia, halafu aliyekufa inakuwa ni hasara yake na familia yake.Watakuwa wapuuzi kweli wakimteka. Labda kukamatwa kwa kuvunja sheria. But does it help?
Nimepata nafasi ya kufuatilia suala la Dr. Ulimboka. Naweza kuthibitisha kuwa amepatikana baadaya kuwa kupigwa kwa takribani masaa matatu, kujeruhiwa na kupoteza damu nyingi. Sasa hivi anakimbizwa hospitali kuokoa maisha yake bila ya shaka katika kumtumia ujumbe wa aina yake kama kiongozi wa mgomo wa madaktari.
Hii ni aibu ya taifa!
Tumwombee anusurike lakini vile vile wengine watiwe moyo kuwa wapo mashujaa katika Tanzania!!
Viva Dr. Ulimboka!! - M. M. Mwanakijiji
mh! sidhani kama that can be the case, labda useme amekamatwa. kutekwa?