Mnayakumbuka ya Dkt. Ulimboka na Awamu ya Nne? Je, yupo wapi sasa?

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,171
Mwaka 2012 Dkt. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana.

Sababu kuu ya kutekwa ilikuwa ni kuongoza mgomo wa Madaktari nchi nzima waongezwe mshahara kutoka 950k hadi 3.5m. Aliitwa chemba apozwe asitishe mgomo, akagoma.

June 27, 2012 akiwa Leaders Club akatekwa, June 28 akaokotwa msitu wa Mabwepande akiwa hana baadhi ya meno na kucha.

Chanzo

Je yuko wapi kwa sasa Dr. Ulimboka?

Hii ndiyo ilikuwa hali yake baada ya kutekwa.

20230815_214706.jpg
20230815_214701.jpg
 
Aliamua akae kimya. Kwenye mambo ya nchi mengine unaona watu wanaongoza jambo fulani ukute ni mapandikizi I mean wamewekwa kwaajili hiyo na hautaona wanaguswa Sasa tokeza wewe from no where utajua hujui! It's better to play smart before you take any step,every shadow you see isn't something that can't harm you other shadows are very dangerous it's like you wear a clothes with snake in it!
 
Huu ni mwaka wa 8 tangu Jakaya kastaafu na hakuna Nyongeza ya Mshahara hata ya Tsh 10, mbona hawagomi tena?

Eti kima cha chini kifike 3.5 million?

umesahau kumalizia story yako kuwa alipotekwa akatupwa Mabwepande akapita 'mtu' akamuona yupo katikati ya Pori huyo mtu 'bahati nzuri' alikuwa na namba ya Dr Hellen Kijo kisimba akampigia nae akawapigia ITV wakaenda live kumuokota Dr Ulimboka

baadae Dr Hellen akakusanya watu pale Salender bridge wakampindue Jakaya kwa maandamano kama ya Arab Spring wakati huo…kama Kawaida yetu Watanzania tukapuuza upuuzi wa kuvuruga Taifa kwa movie za kutengenezwa

Damu ya wale wagonjwa waliogeuzwa Silaha ya kisiasa hadi wakapoteza maisha itawaandama wale wahuni mpaka siku wanaingia Makaburini.

"Mzee akatoswa na Chama chake 2015, akafadhiliwa Ubalozi kufika kule akakimbiwa na Muhaya wake aliempora kwa Meneja wa Bandari, Ghafla Tajiri aliempa Ubalozi akafa ghafla, nae akapoteza kazi, akarudi home akavamia hoja ya Katiba mpya, Mara akaparamia Hoja ya Bandari akajikuta katangaza uhaini akayakanyaga …" Dhambi za kutumia Wagonjwa kama Silaha ya kisiasa haitowaacha salama…yule Mama nae kapatwa na maradhi ya Wasiwasi

Dr Ulimboka baada ya kupona na kugundua kuwa nani alimuuza pale Leaders Club hadi sasa hataki hata mawasiliano nao Makamanda wenzie

JK kwmy sakata la Madaktari alionesha sifa moja kubwa sana ya kiungozi ambayo hatutopata Rais kama yule hadi mwisho wa Dunia
 
Sio kila jambo linapaswa kusuluhishwa kwa ubabe. Jifunze uongozi.
Wewe unatumia ubabe na ujeuri kupimana ubavu na Serikali unataka ifanyaje ?

Serikali ina deal na mtu kwa kadri yeye alivyo deal na Serikali, waliotangazia vurugu Serikali acha nao watangaziwe vurugu

Hayati Chiluba alikuwa na msemo wake style ya ku deal na adui ataichagua adui. wenyewe

ukitangaza kutumia nguvu dhidi ya Serikali usitegemee Serikali itumie hoja …itatumia style hiyo hiyo uliyotaka kutumia …Slaa alihisi Dola itamuogopa kutokana na hadhi yake
 
Aliamua akae kimya.. kwenye mambo ya nchi mengine unaona watu wanaongoza jambo fulani ukute ni mapandikizi I mean wamewekwa kwaajili hiyo na hautaona wanaguswa Sasa tokeza wewe from no where utajua hujui! It's better to play smart before you take any step,every shadow you see isn't something that can't harm you other shadows are very dangerous it's like you wear a clothes with snake in it!.
Yeye hakuwa muajiriwa wa serikali,kijana aliongea na mzee pinda kwa lugha za dharau,walichomfanya anajua yeye,aliamua kumuachia Mungu,usiombe Dola ikuangukie
 
Back
Top Bottom