Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,081
Ni 2017 nilikuwa nachati na wadau whatsapp mida ya saa tatu usiku, muda huo umeme ulikuwa umekatika, simu ikawa inakaribia kuisha chaji nikaona sio mbaya niweke status kabla simu haijazima.
Nikiwa nimeingia sehemu ya status kwenye gallery ghafla ni kama nilimis touch nikachagua video ya x (nilikuwa nimejoin group la connection) na ikajipost status, ebwana ee ukisikia siku ya nyani kufa miti inateleza basi ndio hiyo, yaani nikawa naona naenda kuua heshima yangu, Nilipaniki, kichwa hakikutulia yaani nikaanza kushikilia power button nizime simu ili niizuie, nikabadili maamuzi niweke airplane mode kuzuia data lakini naingia whatsapp naona ishaenda, nilidata zaidi nikaondoa airplane mode niwashe data niwahi kuifuta video lakini ghafla simu ikazima.
Tumbo lilizunguka kwa spidi ya ajabu akili iliniviriga nikawa nimedata nawaza itakuwaje sasa, bimkubwa anaeniona mimi mtoto pekee nilietulia atanichukuliaje? Wadogo zangu Je ? Majirani vp? Yani kiufupi watu tunaoheshimiana wakiiona nimekwisha... , Na hapo kumbuka umeme umekata mtaa mzima hakuna umeme.
Nilitoka nje kama nilivyovaa kikaptula, kivesti na kandambili, nikawahi sehemu ya boda boda nikaikuta moja tu nae kaniambia kuna mteja anamsubiri, kwakweli sikuweza kusubiri boda mwengine, nikamwambia ntampa elf 5 tena sehemu yenyewe ya karibu ni ofisi ya kamari / kubeti huwa wanawasha jenereta.
Yaani boda nikawa namkaripia aongeze mwendo maana naona kama pikipiki haiendi,
Tukiwa njiani nikakumbuka nilisahau chaja maweee!! nilienda duka la njiani niliambiwa chaja elf 10 wala siku fikiria mara mbili
Nafika ofisi za kubeti hawakunielewa kuchaji simu nikatoa hapo hapo elf 5 ambayo ilibidi iwe ya boda boda nikasema tutajuana mbele kwa mbele.
Yaani nikaingia WhatsApp nakuta kuna views kama 3 tayari ila kwa bahati nzuri zilikuwa za marafiki wa viwanjani, kwenye inbox wanaomba full clip.😂😂
Boda naye akanitwanga zaidi kwa kisingizio alikuwa na mteja mwengine nimevurugia ratiba.