kina kaka naombeni majibu....(hata kinadada changieni)

.,habari zenu wana jf. nauliza kina kaka mkiacha kuangalia tabia, muonekano nk. kwa msichana, je ufundi wa mapishi jikoni huwa mnatilia maanani? au mnatizama sura tu, makalio na guu la bia

Sura, makalio, miguu, umbo ni natural (ukiondoa vya mchina) na vinaonekana barabarani ndo mana tuna-concentrate kuviangalia. Ila kupika kunafundishika halafu hakuonekani barabarani, hiyo siyo ishu kwa wakaka wengi
 
Yaani mcihango ya hii sredi karibu yote nafurahisha kwa kweli.

Anyway, mtoa mada hivi, ili uwe mzuri lazima pua iwe nzuri? Na je pua peke yake inabeba uzuri wa mtu?


Ukijibu swali langu utakuwa umejijibu. Upishi kwa mwanamke ni kielementi kimoja tu kwenye mapenzi kama ilivyo pua kwenye kuchangia uzuri wa mtu
 
Kupika sikunafundishika bwana sio issue sana unaweza mfundisha au mpeleka korse ,kupika ni kama udereva bana

kuna food netwok....magazeti kibao....internet....etc....nini kupika bana.....
 
Mapishi.......yaani unatafuta msichana uanze kuonjaojna vyakula ili u-choose? Hii ngumu na sidhani kama imo. Ila inaweza kuwa 'added advantage' ya ku-cement relationship....au kubomoa if the viseversa of being a good cook is the case!
 
Kujua kupika na mapishi ni added advantage

hakuna mwanaume na akili zake atakayemtaka msichana ambaye haujui kupika kila siku kula nje hapana....

ila sijaelewa mnapozungumzia makalio ndo nini?

mi najua sana kuchoma nyama na kuchemsha trupa....
sasa wewe....nataka nikuchoree makalio....ngoja nilete penseli.....
 
halafu wewe.....leo uje pale Narok pub kambi ya fisi.....tuikung'ute hii baridi....

nakuja aise mana ahii baridi haitaki kuisha mji wetu huu
Yaani utafikiri aliyeko kule mlimani kila siku anaongeza kitufe ili baridi izidi
 
Kweli kila mtu anavutiwa na chake mwengine guu la bia,mwengine wowowo,mwengine sura nk,lakini baadaa ya yote hayo usafi na kupika muhimu Sanaa,kwanza mwanamme anajisikia raha au mapenzi yanaongezeka akija nyumbani chakula kizuri mkewe kampikia Leo kala hiki kesho kala kile,inamfanya hata akienda kula kwengine anaona dhiki anajua hakuna anaeweza kunipikia Vizuri Kama mkewangu,lakini Kama kazi yako kubwa ni chali chakula anapika mfanya kazi hailipi kwa ville atakwambia tuu sio neno hataki kukukeraa....lakini neon lipo...
 
Asikuambie mtu, Tunatilia maanani sana tu!
Kwa mfano umevutiwa na mdada kwa sura na umbo,mkaanzisha mahusiano baada ya muda unamzoea tu. Ila akiwa fundi kwenye majukumu ya kike na mapishi yakiwemo ngumu kuachika na kusahaulika...
Na tena tunavyopenda kula?

kumbeee....! thtz gud 2 hear.....! thnx petcash
 
.,habari zenu wana jf. nauliza kina kaka mkiacha kuangalia tabia, muonekano nk. kwa msichana, je ufundi wa mapishi jikoni huwa mnatilia maanani? au mnatizama sura tu, makalio na guu la bia

Mimi hlo kubwa kwangu,na ufundi wa 6 by 6
 
ah mwanamke mapishi...mwanamke kama hajui kupika hakai ndani na mimi its that simple..na navosema kupika sio apike chips mayai...namaanisha proper upishi, ndizi,wali, samaki chapati maandazi..eeh ndo manake
 
.,habari zenu wana jf. nauliza kina kaka mkiacha kuangalia tabia, muonekano nk. kwa msichana, je ufundi wa mapishi jikoni huwa mnatilia maanani? au mnatizama sura tu, makalio na guu la bia

mwanamke mapishi dada,ila kuna wadada weng hawajui kupika. hasa watoto wa kishua. me nina mfano hai, huyo mdada kwao wapo well-off na kasoma nje tangu akiwa mdogo mpk kamaliza university lakin hajui kaz yoyote ya kike zaid ya kufua pichu yake.hta akila chakula haez toa vyombo mezan
 
Ngoja nikusaidie Preta, hakuna mwanaume asiyependa kula mahanjumat. Zaidi ni kwamba huwa kuna hii hisia iliyojengeka kwa wanaume kuwa mwanamke aliyekamilika(mrembo) basi anapaswa kujua sana kupika.
Binafsi nimesoma nje ya nchi, na huko wanaume wa nchi nyingine(hasa zile za Kiafrika) walikuwa wanapenda sana kuhudhuria sherehe za kitanzania ili tu wagonge misosi mitamu ya kibongo na uzuri ni kuwa wadada wengi waliokua wanakorofisha hiyo misosi ni kutoka ukanda wa Pwani na Zanzibar.

..,asante watu8 kwa maelezo yako. sasa naomba unipe mtazamo wako binafsi kwenye issue hii....
 
Last edited by a moderator:
kujua kupika chakula kizuri ni moja ya vigezo muhimu ambavyo binti anapaswa kuwa navyo... naona wengine wanajipa matumaini tu hapa, ooh kuna internet sijui magazeti, ooh sijui inafundishika - yaani binti ushindwe kujifunza kupika nyumbani kwenu kama sehemu ya makuzi yako utegemee kufundishwa ukiolewa?
 
Napenda mwanamke makini, mwenye msimamo, asiye na tamaa ya mali bila kujua namna ya kuitafuta, mcha MUNGU, anayejiheshimu, mpole sio mcharuko, macho makubwa ya huruma.
All others, are added advantages.
 
katika moja ya sifa ninayopta toka kwa mume wangu ni kuhusu chakula ninachompikia huwa kinamfurahisha sana
 
.,habari zenu wana jf. nauliza kina kaka mkiacha kuangalia tabia, muonekano nk. kwa msichana, je ufundi wa mapishi jikoni huwa mnatilia maanani? au mnatizama sura tu, makalio na guu la bia


Mapishi ndo mpango mzima,unakula unashiba dunia yote unaiona ya kwako,sura kauze kwenu
 
upishi ni muhimu sana, ikiwa mi najua kupika kwanini yeye asijue?
Na siishi hapo tu, hata uwajibikaji wake ktk kazi nyingine kama kufua nk ni kigezo muhimu kwangu.
Sitaki mwanamke mvivu kabisaaa...
 
.,habari zenu wana jf. nauliza kina kaka mkiacha kuangalia tabia, muonekano nk. kwa msichana, je ufundi wa mapishi jikoni huwa mnatilia maanani? au mnatizama sura tu, makalio na guu la bia

Sidhani kama mwanamke mzuri wa kuoa eti lazima awe FUNDI kwenye kupika. Nadhani mradi anajua basics za kupika mengine yatajiset baadaye..Kama walivyosema wengine inaongeza kidogo sana upendo kama utakuwa FUNDI but kwa asiye fundi still she can learn and be a good cooker!
 
Swala la mapishi is very important na kama mwanamke haujui kupika cv yako inashuka sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom