Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Mida flan nilipita pale kuna jamaa yangu anauhusika na mambo ya feza pale ndan akanambia kuna vijana wanahojiwa,ila hakunipa majina ya vijana hao.
Pia sehemu ya parking magari ya vigogo ilikuwa na magar yao hii inaonesha kuna jambo kuukuu.

nipo hapa mjengoni naweka sawa mambo ili niwajuze kilichojili
 
Huyo Bananga kama anapumulia mashine vile.... Inaonekana upepo unawavumia vibaya mafisadi. Yetu macho!
Mkuu Alwatan sijakuelewa, anapumulia mashine kwanini? Maana yeye si kiongozi wa juu, au amerudi madarakani UVCCM? Ama ndio katika lile kundi lililosafirishwa kwenda Dodoma, au katika wale wanaoandaa maandamano Arusha kumpokea shujaa Lowassa atakapojivua gamba au kumpokea kama shujaa atakapoogopwa na wengine kama Nape, Sitta na kundi la kung'olewa? Na yeye kupokewa kishujaa kama aliyepona kwenye magamba.

Nchi hii ina mambo mengi sana na hili nalo jambo.
 
CCM hawatabiliki wanaweza mweka EL 2015 just like watavyouchuna kutowachukulia hatua CAG na Ngeleja pamoja na mikashfa hii lundo
 
Je, kundi la Lowassa limeshanusa hatari? Maana Nimekuta katika Facebook Ally Bananga wa Arusha, ambaye anafahamika sana kuwa mfuasi wa Lowassa akisema: "akikupiga ngumi ya jicho nawe mpige ya sikio, akiuliza umeonaje nawe mwambie unajisikiaje. hakuna nidhamu ya uoga sasa, hakuna kugeuzana mbuzi wa kafara, imetosha, TUMEDHALILISHWA SANA, TUMEONEWA SANA, tumeamua, tunaweza. TULIFURAHI PAMOJA, TUKAHUZUNIKA PAMOJA NA SASA TUNASUKUMA PUSH PAMOJA. Huu utabaki ukweli. naam mushi ni AZIMIO LA DODOMA 2011!!

Ally Bananga Mwatiga3:15pm Nov 20
wapenda haki wote, wanapenda kijani na njano wote, wanaoguswa na tatizo la ajira kwa vijana, wanaotambua thamani ya mtu ni kazi, wanaotambua adabu ya wa kiume ni kutenda na sio kuropoka, wanaoamini rais ajae ni mungu ndie anamjua na sio wale waliosema jakaya anamjua, wanaopuuza kanda zingine wakiamini yao ni bora, wanaoamini ktk maamuzi magumu, MKONO MMOJA WEKA JUUU, WEKA JUUU AAAAH AAAAH NI ISHARA YA USHINDI!"...

Anayedhani kuna heri anajidanganya, hali si shwari

Lakini hapo kwenye kafara si ni kweli katolewa kafara juu ya RICHOMD kuinusuru serikali nzima a ccm? Hawana shukrani hawa.

Ama JK kamgeuka?

Maana mara ya mwisho nakumbuka alisema ni "ajali ya kisiasa"

Sasa kamgeuka kumvua gamba na yeye naona anadai mboga anayo...Incase wameamuwa kumwaga ugali.

Hapo pa kwamba wako na JK pia bado pana ugumu wake,urahisi wake ni kama JK anaamini kuwa EL ataingia ikulu,if so,atahitaji mtu wa "kumwacha apumzike"
 
Huyo lowasa aking'oka atafute pengine pa kwenda. Mie ntamwomba Mungu asaidie asipate hata wazo la kuja chadema!
Kuhusu Sugu kuitwa rais wa mbeya kwani kuna shida gani? Kama watu wake wanamkubali kiasi hicho haina tatizo. Rais ni title tu hata TFF ina rais wake! Shida iko wapi?
We unasema TFF? masharobaro tu wanarais wao itakuwa Sugu kuwa rais wa Mbeya.
 
siku hizi wanaacha simu mlangoni kama us embassy na laptop haziruhusiwi.ni diary tu" na simu zao wanaprint activity log ya muda wite wa jikao
 
Vita vya panzi furaha kwa kunguru ccm endeleeni kugombana hivyo hivyo alafu nakuja kuwaonyesha
 
Ccm inatia huruma maana sasa hivi kuna wanachama wake wako upande wa upinzani;waanzilishi wote wa ccj na wafafhiliwa wa fedha za gadafi;membe hili kundi ndio litauwa ccm wala sio waliobatizwa mafisadi na watakiuwa kwa makusudi tukose wote,jk tumia busara yako
 
kama CCM wanataka kubaki na amani yao ni ku-compromise na waliowabatiza magamba, vinginevyo CCM ndio watakaoleta fujo nchi hii na wala si maandamano ya CDM!
 
Uko sahihi Mkuu, tunaweza kucheza ngoma yao, lakini kibaya zaidi ni kucheza ngoma ya kutetea mafisadi. Ni bora kama ngoma yao ni huko kugombana na kaka mazingira ya sasa Lowassa hawezi kupata umaarufu kwa kufukuzwa chama kwa ufisadi, angekua kama Sitta akifukuzwa kwa kupiga vita ufisadi, angepata umaarufu.

Mrema alipotoka CCM alikua na jina la mtu anayetetea wanyonge na mpiga vita ulanguzi na wezi, now Lowassa akitoka ama kufukuzwa anatoka kwa jina la wizi si utetezi, na ndio maana juzi aliibuka kujifanya anatetea ajira kwa vijana na hali ngumu ya maisha ili ajulikane kama mtetezi wa wanyonge.

Ratiba ni kwamba jana na leo Kamati ya Maadili inakaa na jana ndio iliwaita vijana kadhaa wa UVCCM na wote ni wale wa upande wa Lowassa, kesho ni Kamati Kuu kabla ya NEC, Jumanne na Jumatano.
Ngoma tunaicheza kwa viuno na mabega, sii ujaona kijiwe kilivyo noga!...Lowassa ni maarufu kuliko Sitta ndani ya chama na nje ya chama hilo usijidanganye. Leo hii EL ikisimama na Sitta atamtoa nje kwa sababu Sitta hana mbinu za ushindi.. Kumbuka tu kwamba hata Uspika alipigwa changa la macho na EL..

Hivi unafikiri nguvu kubwa unayofanyika kumdhalilisha JK ina lengo gani? yaani leo EL ana uchungu sana na nchi yetu inakokwenda kuliko alivyokuwa waziri na waziri mkuu..tena watu wako radhi kumsamehe wengine wakidai arudi madarakani. Halafu JK amekaa kimya hata kujitetea hana moja isipokuwa wasizungumze CDM...Uchaguzi ulopita viongozi karibu wote walimkimbia JK akabakia nani? - EL na familia ya JK! EL ndiye aliyechakachua majina ya wagombea na kadhalika, hawa kweli maadui jamani au mnajichanganya...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom