Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Hahahaa you make a good point, ingawa to me i can smell some undertones of sarcasm. Wapambanaji wa ufisadi CHADEMA wampokee S.I Unit(I like this) ya ufisadi!!!... But under the sun never say never.

By the way, sijui mkuu una ratiba ya series za vikao vya MAGAMBA vinavyoanza this weekend. Naomba nijue NEC
yenyewe wanakaa lini?
Ratiba ni kwamba jana na leo Kamati ya Maadili inakaa na jana ndio iliwaita vijana kadhaa wa UVCCM na wote ni wale wa upande wa Lowassa, kesho ni Kamati Kuu kabla ya NEC, Jumanne na Jumatano.
 
Leo mchana nikijadiliana na mbunge mmoja wa CCM kutoka mkoa wa Dar, aliniambia wazi kwamba, Lowassa hawezi kufukuzwa chamani, kwani ndiye anayeunganisha chama. Kabla ya EL kungo'lewa gamba, mwenyekiti atakuwa wa kwanza kwani matatizo lukuki ndani ya chama na taifa yametokea katika utawala wake. Amesema udini, ufisadi, umasikini, siasa ya makundi yameendelezwa na mwenyekiti wa chama na siyo Lowassa, kwa maana hiyo gamba kubwa ni Rais mwenyewe na siyo EL.

EL akingo'lewa basi tutaelekea kwenye uchaguzi mara moja na CCM itakufa kwa maana 70% ya wabunge CCM wanamuunga mkono EL. JK hawezi kumgusa EL na anajua hilo

Acha ndoto za kufikirika.kwanza wabunge wote si wajumbe wa NEC.Ushaambiwa mbele giza nyuma kaburi
 
Ingawa mi si muumini wa siasa za kikanda, lakini 2015 Rais lazima atoke kaskazini kama si Slaa atakuwa Lowasa, Dr. Slaa atachaguliwa kwa mapenzi ya walio wengi na CCM ikitaka kushindana vema na CDM lazima imsimamishe Lowasa, ile dhambi ya vijana wa Kikwete wa mkoa wa Pwani waliosema rais hawezi toka kaskazini itawatafuna
 
Mkuu si kama hawajui, kama ulivyosema wanafikiri kwa tumbo na wengine hawaoni mbele bila ya ENL na kwa kweli ni vipofu na wana upofu wa ajabu. Hawataki kukubali kwamba kwa sasa ukimsimamisha ENL umepoteza mvuto kama chama. Uongo mwingi unatengenezwa kuonyesha kwamba ana wafuasi wengi katika jamii. Uongo mtupu maana ENL ndiye 'SI Unit' ya Ufisadi nchini tutake tusitake.

du halisi hapo kwenye blue upo right kabisa mkuu. ENL ni kipimio cha ufisadi kwa lugha yetu ya kiswahili.
 
Sasa hivi tuna serikali mbili wala hili halina ubishi!. Moja inaongozwa na JK toka Magogoni, na nyingine EL from anywhere. Wakubwa hawa wanajuana vilivyo na kama mmojawao alivyosema 'wahakukutana barabarani'. Kila mmoja ana wabunge wa kutosha, mawaziri, wanachama katika jumuiya zote za chama na mbaya zaidi kila mmoja ana team nzuri kwenye usalama wa taifa.

Kauli kama ile ya Pinda bungeni kuwa nchi iko shwari sio kweli maana hata kwenye maandamano ya CHADEMA polisi wanapopiga watu na kuuwa si kwamba wanawapiga CHADEMA ila in their mind wanapambana na kundi pinzani la mkubwa wao! Maneno kama yale ya Wassira kwamba CHADEMA wanatumiwa ni kielelezo kwamba wanahofu kundi kundi liko nyuma ya CHADEMA.

Hii inanifanya nijiulize, hivi hii katiba mpya wanayong'ang'ania kusimamia kutengeneza itakuwa ni ya ccm ipi? CCM ya magogoni au ccm ya mtaani. Hata kama JK atasema kwa sasa yeye na upper hand lakini kwa historia yake (6yrs now) ni kweli anaweza kuzuisha ccm kutoingilia mchakato? Je, wananchi wa Tanzania wako wapi kwenye hili?

Lowassa anakimbilia Nigeria kuomba ushauri wakati Kikwete anakimbilia Bagamoyo sasa hapa Gamba litavuliwaje??
Nani mwenye makosa kati yenu???

Ndio maana tunataka katiba mpya ili wote mfungwe!
 
Jk na El si maadui,huu mnaouona ni "uadui" wa kutengenezwa!! Lengo lao ni moja! Kinachoshangaza hata wabunge wanaotumiwa hawaelewi!!
 
Natabiri
- Lowassa atang'oka. Kung'oka kwake kutaleta mpasuko mkubwa CHADEMA wengine wakitaka aalikwe CHADEMA na wengine wakiapa "over my dead body".
- Sitta atapewa karipio kali, na kwa kuwa ni ndumilakuwili ataufyata.
- Chenge is not as powerfull as those two, yeye ataondolewa kirahisi na haraka sana.
- Itapangwa mikakati mikali ya kuhakikisha SUGU anang'oka Mbeya kwa hali na mali, haswa baada ya kuitwa Rais wa Mbeya.
Kwani mtu kuitwa Rais ni jambo la kushangaza ?
 
Inatisha kweli, kwanza michango anayotoa kwenye harambee za ujenzi wa makanisa unatisha.

Haitishi chochote! Yeye anatafuta publicity na ni move yake ya kujisafisha! Mchango wa 11m kwa level ya EL si kitu kabisa! Hata kina Mengi wanachangia zaid ya hapo! CCM wakilogwa kumpa nafasi ya kugombea 2015, wamekwisha!
 
Tupeni mpya zaidi huko dom kwani wanaotakiwa kuvuliwa gamba nao watumia vijana kujikinga kuvuliwa ngozi...KAZI IPO VIJANA CCM leo mpaka kieleweke...
 
Tupeni mpya zaidi huko dom kwani wanaotakiwa kuvuliwa gamba nao watumia vijana kujikinga kuvuliwa ngozi...KAZI IPO VIJANA CCM leo mpaka kieleweke...

Mida flan nilipita pale kuna jamaa yangu anauhusika na mambo ya feza pale ndan akanambia kuna vijana wanahojiwa,ila hakunipa majina ya vijana hao.
Pia sehemu ya parking magari ya vigogo ilikuwa na magar yao hii inaonesha kuna jambo kuukuu.
 
Ratiba ni kwamba jana na leo Kamati ya Maadili inakaa na jana ndio iliwaita vijana kadhaa wa UVCCM na wote ni wale wa upande wa Lowassa, kesho ni Kamati Kuu kabla ya NEC, Jumanne na Jumatano.
Big up comred Halisi.Endelea kula nao sahani moja hadi mwisho. Endelea kutupasha kila uwezavyo.
 
We should give them benefit of doubt as long as they have a constitutional legitimacy to govern our country. At this stage of time we can not do anything to kick them out of system regardless of how angry we are about their blunders. However it is a matter of time before we decide to 'depose' them in a rather democratic manner i.e through 2015 poll.

keep on dreaming.it is good for your weak mind
 
Je, kundi la Lowassa limeshanusa hatari? Maana Nimekuta katika Facebook Ally Bananga wa Arusha, ambaye anafahamika sana kuwa mfuasi wa Lowassa akisema: "akikupiga ngumi ya jicho nawe mpige ya sikio, akiuliza umeonaje nawe mwambie unajisikiaje. hakuna nidhamu ya uoga sasa, hakuna kugeuzana mbuzi wa kafara, imetosha, TUMEDHALILISHWA SANA, TUMEONEWA SANA, tumeamua, tunaweza. TULIFURAHI PAMOJA, TUKAHUZUNIKA PAMOJA NA SASA TUNASUKUMA PUSH PAMOJA. Huu utabaki ukweli. naam mushi ni AZIMIO LA DODOMA 2011!!

Ally Bananga Mwatiga3:15pm Nov 20
wapenda haki wote, wanapenda kijani na njano wote, wanaoguswa na tatizo la ajira kwa vijana, wanaotambua thamani ya mtu ni kazi, wanaotambua adabu ya wa kiume ni kutenda na sio kuropoka, wanaoamini rais ajae ni mungu ndie anamjua na sio wale waliosema jakaya anamjua, wanaopuuza kanda zingine wakiamini yao ni bora, wanaoamini ktk maamuzi magumu, MKONO MMOJA WEKA JUUU, WEKA JUUU AAAAH AAAAH NI ISHARA YA USHINDI!"...

Anayedhani kuna heri anajidanganya, hali si shwari
 
Lowassa atahamia NCCR, Sugu atarudi CCM, Slaa atagombana na Mbowe, Halima Mdee atahamia CCM, Lema atakuwa Mwenyekiti wa Chadema.
Umetuambia kuwa umetoka hospitali leo, na mdomo bado mchungu. Sasa dozi haijaisha umeshaanza kunywa pombe?
 
EL anatumia pesa nyingi saana kutumia magazeti kumpamba, na hii kaianza miaka mingi saana, alikuwa anawanunua waandishi wa habari anawalipa posho waandamane naye safari popote ili kumpamba. Huyu jamaa si maarufu kama mnavyofikiria, na wale wote amewatuma hapa ruduni mkamwambie era na enzi yake katika CCM inafikia kikomo. CCM wakifanya makosa, watauumia zaidi ya sasa, hauziki kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom