Kilimo cha Nyanya: Aina za mbegu, mbinu za kulima na masoko yake

Ookay kwavile ni perishable ukizilima msimu wake ukakosa soko ehhh? Nilishamskia Kubota akiongea hii. Fafanua nawe zaidi tuelewe, nadhani wa sita uko iringa wanalima wengi basi soko litakuwa hamna au bei ya kutupa. Hebu wadau mtujuze msimu gani mzuri kulima nyanya?
Barikiwa sana bwana GEBA2013. Zao la nyanya linakanuni mbili tu, NYANYA ninyanyase & NYANYA ninyanyue!! ikiwa na maana kwamba ukilenga msimu mzuri wa nyanya utanufaika na soko, ila ukifail kutageti soko/msima utanyanyaswa na nyanya mpaka utachukia kilimo hiki.
 
Last edited by a moderator:
Haijarishi ni mkoa gani unaishi ila kuna miezi nyanya zinakuwa adimu kiasi cha kuuziwa nyanya moja sh 200. Uzoefu nilionao mimi miezi ya nov-april soko la nyanya ni zuri sana karibu maeneo mengi nchini.
Usilogwe kukutanisha mavuno na nyanya za magole/mateteni morogoro, debe wanauza sh1000. Hii ni miezi ya july,aug na sep. Wanauza kwa bei ya kutupa coz uzalishaji wao hauna gharama. Hawamwagilii maji na hutumia kiasi kidogo cha dawa na mbolea.
Nashauri mkulima survey hali soko kabla hujalima na kawaida nyanya huchukua miezi 4 kuanzi kitaruni mpaka kuvuna.
 
Asante sana hizi info za Moro ndo nilikuwa nahitaji maana ni washindani wakuu. Ningependa kuanza na eka chache Pwani nitapanda kwenye September au October ili nipishane nao. Thanks and blessings
Haijarishi ni mkoa gani unaishi ila kuna miezi nyanya zinakuwa adimu kiasi cha kuuziwa nyanya moja sh 200. Uzoefu nilionao mimi miezi ya nov-april soko la nyanya ni zuri sana karibu maeneo mengi nchini.
Usilogwe kukutanisha mavuno na nyanya za magole/mateteni morogoro, debe wanauza sh1000. Hii ni miezi ya july,aug na sep. Wanauza kwa bei ya kutupa coz uzalishaji wao hauna gharama. Hawamwagilii maji na hutumia kiasi kidogo cha dawa na mbolea.
Nashauri mkulima survey hali soko kabla hujalima na kawaida nyanya huchukua miezi 4 kuanzi kitaruni mpaka kuvuna.
 
HABARI WANA JAMII........
WAKUU NAOMBENI USHAURI NA MCHANGANUO ZAIDI KUHUSIANA NA KILIMO CHA NYANYA MAJI.NATAKA KULIMA ENEO LIPATALO EKARI MOJA TUU

.........NIPO WILAYA YA KILOMBERO.........

Ifakara.....
 
Wakuu naombeni ushauri na mchanganuo zaidi,nataka kulima kilimo cha nyanya maji kama ekari moja hivi.

nipo kilombero,ifakara

Asanteni.........
 
Mkuu sahz usilime nyanya mkuu utalichukia zao hili kama utakutana na nyanya za feri na mateteni.
Lima nyanya kuanzia sept au nov &dec utapga hela takatifu.!
 
Hapa Ifakara nyanya maji zinastawi sana ila zinakabiliwa na Bacterial wilt labda ulime eneo ambalo halijawahi kupandwa mazao aina ya solanaceae kwa muda wa miaka mitatu iliyo pita na kama utatumia kumwagilia maji ya mto Lumemo uwezekano wa nyanya kupata maambukizi ya Bacterial wilt utaongezeka kwakuwa unapita maeneo yanayo limwa mazao jamii ya solanaceae
 
Wadau naomba mwenye uzoefu wa kilimo hiki hasa kipindi cha masika. Nataka nianze mwezi wa kumi ili nivune kama mwezi wa kwanza kipindi mvua inapokuwa kali na nyanya kuwa adimu.

Shamba lipo Mbeya ukubwa wa hekari mbili. Mtaji nataka niweke maximum wa 3mil kwa hekari zote mbili.

Naomba mnisaidie challenge nitakazokutana nazo mbegu nitatumia anna f1.

cc: malila
 
Na mi nataka nilime hizo za kumwagilia na mvua mwz wa 11 pande za dom,,nasubiri majibu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom