Kilimo cha Nyanya: Aina za mbegu, mbinu za kulima na masoko yake

ahsante wakuu kwa michango yenu!
Binafsi napenda kujua kuhusu kilimo cha nyanya.......ila kwa mliyoyachangia hapa yanatosha,napenda tuu kuongezea swali dogo juu ya soko la nyanya,jee ni msimu wa kuanzia mwezi gani unafaa kwa kilimo cha nyanya?ili wakati wa mavuno uvunie ktk bei nzuri?na bei ya wakati huo huwa number bei gani kwa kilo ya nyanya(moneymaker)na vipi soko la hoho lipo?
 
Wapendwa wana JF, Happy New Year!
Jamani nina interest ya kulima nyanya kibiashara. Naomba ushauri juu ya utunzaji wa shamba, mimea hadi matunda pamoja na challenges. Nina imani nyanya zinaweza kunitoa, kwa muono wangu,
Wenye ujuzi naomba msaada.
Thanks in advance.
sijui kama ulishapata maelezo ya kutosha mkuu, ila nimeona maelezo mazuri kwenye hii blog MITIKI -KILIMO KWANZA jaribu kutembelea huenda yakakufaa
 
Pia jaribu Roma varieties (zipo nyingi) kama zile ambazo unaona zina spherical shape. Mimi huwa naona zinachelewa kuharibika. Muhimu, onana na wataalamu wa kilimo, ikiwa ni pamoja na mabwana/bibi shambas watakupa msaada mzuri tu.

Nimetembelea duka moja pale kariakoo linalouza mbegu na madawa ya kilimo wameniambia kuwa hizi jamii ya mbegu zinaweza kuzaa hadi tani arobaini kwa ekari. Ni kweli?
 
Nimetembelea duka moja pale kariakoo linalouza mbegu na madawa ya kilimo wameniambia kuwa hizi jamii ya mbegu zinaweza kuzaa hadi tani arobaini kwa ekari. Ni kweli?

Ngoja tuwasikilize wakuu waelimishaji wetu Malila, Mpevu, Nanren. Usipoweza kugundua fursa mbalimbali kupitia JF, basi ajira ndo njia sahihi kwako!
 
Last edited by a moderator:
Wakuu heshima kwenu kwa michango hapa nami nachangia kuhusu Aina za nyanya tu kidogo kadri ninavyozifahamu ili kuongezea akiba ya taarifa.

Money maker: Hii ni aina ya siku nyingi sana ni nyaya za kusimikia mti unabakiza shina moja au mawili mara nyingi zikifikia mikungu 5 au 6 unatakiwa ukate juu. Zinatabia ya kupasuka matunda zikipata maji mengi hasa wakati wa mvua shauri ya ganda laini, hazikai muda mrefu na hazistahimili misukosuko ya safari ndefu!

Roma: Ni nyaya zinazaa sana na ni aina ya mbegu ya enzi na enzi, zinangozi laini, hivyo hazikai muda mrefu mezani kwa mfanyabiashara na zinapondeka kirahisi zinaposafirishwa mbali. Roma ni nyanya tamu sana kwa kachumbari na zina mchuzi mzito lakini zinatabia ya kukauka kitako chake kirahisi sana zinapokabiriwa na ukame au udongo wenye chumvi.

Marglobe: Hii inahitaji kusimamishiwa kwa kufunga kwenye kijiti na mara nyingi hupunguziwa na kuachwa shina moja tu, matunda yake ni makubwa sana na machache nayo inangozi laini haistaimili misukosuko ya kusafirisha.

Tengeru (97?): Hii ni aina ya mbegu zilizozalishwa na watafiti wa kitanzania, inahitaji kusimamishiwa kwa kufunga kwenye kijiti na mara nyingi hupunguziwa na kuachwa shina moja, matunda yake ni makubwa sana na machache hii aina nyanya zake zinaganda gumu hustahimili kusafirishwa na huvumilia magonjwa ya mnyauko, mavuno yake makubwa.

Tanya: Hii ni aina ya mbegu zilizozalishwa na watafiti wa kitanzania, nikifupi cha Tanzania Nyanya. Aina hii haipunguziwi matawi. Ni nyanya nzuri sana zinazokidhi matakwa ya soko inaweza kusafirishwa mbali na inakaa muda mrefu mezani iwapo sokoni. Umbo lake ni matunda marefurefu mfano wa yai isipokuwa ncha zake ni bapa kidogo si mchongoko kama yai.

Ukibahatika kupata mbegu Original ya aina hii utaifurahia kwani matunda yake ni mengi, makubwa na yanavutia sana umbo lake! Angalizo ni kwamba makampuni mengi yanauza mbegu ya Tanya iliyochanganyika kiasi kwamba imefanya wakulima wengi kuichukia mbegu hii! Nimewahi kuilima ilipofikia mavuno nilichoona sikuamini! Ilikuwa ni mchangayiko wa Roma, Marglobe, vigorori na mtepeto, yaani wateja wangu walinikimbia! Ni mbegu nilizonunua kwenye makopo yaliyopakiwa na East African Seed Company, ndugu zangu muwe makini, makampuni ya kibongo yakiishiwa mbegu hukusanya nyanya kwa wakulima na kuzikamua tu! Kuweni macho ikibidi tunzeni mbegu zenu. Mbegu za makampuni ya Kikwetu ninaziogopa sana, utapeli ni mwingi tu na wenye pesa wako above the law!

Cal J: Aina hii haihitaji kupunguziwa matawi, inazaa sana. Ina ngozi ngumu na kwa kweli hustahimili hekaheka za usafirishaji yaani ni mawe, wengine huziita dumudumu, kuna wakati matunda pia hupasuka mvua ikizidi. Hii ni aina maarufu maeneo maarufu ya kilimo cha nyanya.

Rio Grande: Hii ni aina mpya ambayo imekuja kuuwa umaarufu wa Tanya huachwa kutambaa haihitaji kupunguziwa matawi. Aina hii ni aina ya kisasa zaidi inayojibu mahitaji ya soko kwa kuweza kustahimili kusafirishwa masafa na kukaa muda mrefu mezani sokoni (shelf life). Hii ni aina nzuri sana ya nyanya zenye umbo la yai, aina hii humwaga maua na matunda bila kelele, hutoa majani kiasi na inapokunya matunda shambani utaona shambani yanaonekana matunda tupu! Kama ningelima leo ningechangua mbegu hii.

Ornyx: Hii ni aina mpya ambayo imekuja kuuwa umaarufu wa Tanya. Aina hii haihitaji kupunguziwa matawi. Aina hii ni aina ya kisasa zaidi inayojibu mahitaji ya soko kwa kuweza kustahimili kusafirishwa masafa na kukaa muda mrefu mezani sokoni (shelf life).

Aina hii ina matunda makubwa na mengi kuliko Tanya. Matunda yake umbo ni mfano wa yai. Inafanana sana kama Rio Grande, ingawa haifikii uzazi wa Rio Grande. Kwa uzoefu wangu shambani Rio Grande iko juu zaidi ya Orynx.

Nimewahi kuona mbegu za Mkulima Seed Company kopo limewekewa label iliyosomeka 'Rio Grande (Orynx)' ! Inashangaza sana kwa vile hizo ni aina 2 tofauti! Nadhani ni kumpa picha mkulima aliezoea aina mojawapo aone ni ile ile! Yaani aliyezoea Oryx anunue na aliyezoea Rio Grande anunue, lakini huo ni wizi, ni utapeli hizo ni aina tofauti kabisa za nyanya japo zinafanana muonekano wa matunda yake!

Anna F1: Hii ni aina chotara, shina tawi moja au mawili husimamishwa kwa miti, hurefuka urefu zaidi ya mita tano, shina moja huzaa kuanzia kilo 25, ni aina maalum kwa green house ingawa huzalishwa pia nje, unavuna miezi zaidi ya 6, mbegu zake ni ghari sana. (Msifikiri ni hadithi nyingine ya machungwa 4000 kwa mti nina Hand book yake ukipenda niPM nikugawie).

NB: Kusimamishia miti!
Wakati wa masika au umwagiliaji ni lazima kusimamishia miti aina yoyote ya nyanya maana zinapogusana na udongo wenye unyevunyevu huoza.

Unapochagua aina ya nyanya za kupanda angalia soko lako linapenda aina gani ya nyanya ingawa huwa zikiadimika nyanya ni nyanya tu hakunaga kuchagua!

Samahani mimi nami sijuagi kuandika maelezo mafupi msinichoke mwee enh jamani!!
 
Anna F1: Hii ni aina chotara, shina tawi moja au mawili husimamishwa kwa miti, hurefuka urefu zaidi ya mita tano, shina moja huzaa kuanzia kilo 25, ni aina maalum kwa green house ingawa huzalishwa pia nje, unavuna miezi zaidi ya 6, mbegu zake ni ghari sana. (Msifikiri ni hadithi nyingine ya machungwa 4000 kwa mti nina Hand book yake ukipenda niPM nikugawie).

Mkuu ubarikiwe umemaliza kila kitu hapo kwenye red hamna utapeli kama kule kwenye Machungwa ni kweli hii mbegu inazaa sana na inalimwa sana huko Kenya
 
Hello,
Naomba wataalamu wa vitu hivi wanipatie mwongozo au ukweli kuhusu kilimo cha nyanya.

Nataka nilime ekari 1 ya nyanya aina ya TANYA
Kwa kutumia mtaalamu wa kilimo anipatie ushauri kuhusu namna ya kuandaa shamba hadi kuwa anatembelea shamba kwa ajili ya consultation kila wiki kuanzia kupanda hadi kuvuna.
Nitachimba kisima cha bore hole niwe napandisha kwa pump katika tank.

Nyanya zinakuwa tayari kwa kuuzwa baada ya muda gani
Ekari moja inatoa nyanya kilo ngapi au ndoo za ujazo wa lita 10 ngapi?

Naomba na miongozo mingine
 
naomba msaada kwa watu ambao tiyari wanafanya kilimo cha nyanya (hotculture) kwa kutumia material yanayopatikana locally. kisima ninacho kina maji mengi-naweza kupata angalau pipa 15-20 kwa siku. Eneo nililonalo ni kama 40mx25m. NATAFUTA WA KUNIPA UJUZI NA UZOEFU. PSE HELP.
 
Tafuta jukwaa hili hili kuna thread inaelezea mambo ya greenhhouse na kilimo hicho hapa dar utapata mengi
 
Wanajamvi naomba kuwakilisha ombi langu. Mimi nimelima nyanya maeneo ya Dumila. Naomba mwanajamvi mwenyefununu juu ya soko anijuze. Napatikana kwa namba 0767310750.
 
Wanajamvi naomba kuwakilisha ombi langu. Mimi nimelima nyanya maeneo ya Dumila. Naomba mwanajamvi mwenyefununu juu ya soko anijuze. Napatikana kwa namba 0767310750.

Mkuu una mzigo wenye ukubwa gani maana masoko yanatofautina! Ni nyanya aina gani? Kwani wewe ulipokuwa unaanza kulima ulilenga soko lipi?

Mkuu next time usianze kulima zao hujui utaliuzia wapi, mikakati ni muhimu sana kuliko kwenda tu kwa kutegemea bahati. Tunashauri wawekezaji mkianza kuwekeza anzieni kwanza kulijua soko, na kuwa na mawasiliano na soko. Ulipaswa uwe na contacts za wanunuzi mbali mbali Dodoma hadi Dar!

Kwa kawaida kipindi chote unachokuwa unaelekea kuvuna yakupasa uwe unamawasiliano na wanunuzi wako watarajiwa. Majira haya wanunuzi wengi wanakuja kununua hapo Dumila wakitokea pande mbalimbali inamaana hujapata mnunuzi kweli?

Kama huridhiki na wanunuzi hao unaonaje ukisafirisha mwenyewe mzigo huo kupeleka Dar?
 
Soko sijapata. Hii leo watu wananunua box kwa shs 2,000/= huko shamba. Nililenga soko la Dar lakini nyanya imafurika kiasi imefika 10,000/= kwa box ambayo hailipi. Nina wateja (madalali) watatu Mabibo, Stereo na Ilala. Tatizo ni bei, nasikia kuna watu wengi wamelima mwaka huu. Kwa kweli nilijitahidi kuandaa wanunuzi lakini bei inanikatisha tamaa. Ndiyo maana nikaona niombe msaada kwa wanajamvi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom