Kilimo cha Nyanya: Aina za mbegu, mbinu za kulima na masoko yake

MKuu Ohotaite Kintu, nashukuru kwa ufafanuzi wako. Nami ninauzoefu sana na Kilimo cha nyanya za majira haya! Kwa uzoefu wangu kutokana na maelezo yako hapo juu nakusihi hivi sasa pamoja na kutafuta bei nzuri usikatae bei inayopatikana hapo shambani! Umefanya vema kuomba msaada jukwaani ila usikatae kidogo kitakachofika shamba! Mkuu katika majira haya ya nyanya nyingi watu tumewahi kutoka kapa! Anakuja mnunuzi anakuta umechanganyikiwa anakuambia umuuzie mali kauli atakulipa mzigo ukifika sokoni, mkifika sokoni wanasema mzigo umefurika hakuna mnunuzi, unaanza kukumbuka 2000 ulizokataa shamba, maana ukiangalia pesa ya kulipia nauli ya gari huna unaamua kutoroka sokoni kimya kimya kurudi shamba. Mkuu endelea kutafuta soko lakini usiache kupokea hicho kinachokuja shamba hata kidogo pokea, nyanya za majira haya Kilosa wanaita "Nyanya ninyanyue nyanya ninyanyase".
 
Soko sijapata. Hii leo watu wananunua box kwa shs 2,000/= huko shamba. Nililenga soko la Dar lakini nyanya imafurika kiasi imefika 10,000/= kwa box ambayo hailipi. Nina wateja (madalali) watatu Mabibo, Stereo na Ilala. Tatizo ni bei, nasikia kuna watu wengi wamelima mwaka huu. Kwa kweli nilijitahidi kuandaa wanunuzi lakini bei inanikatisha tamaa. Ndiyo maana nikaona niombe msaada kwa wanajamvi.

Mkuu unajua kwa elimu yangu ya ndogo tu juu ya soko la nyanya,mara nyingi msimu huu kupata soko la maana inakua shida sana,maana nyanya zinazovunwa na kuuzwa kipindi hiki ni zile nyanya zinaitwa za wote ambazo watu wengi sana walizilima kwa kua wenyewe wanadai nyanya zinazovunwa sasa ni rahisi kidogo kuzilima kwa maana ya gharama!ila kuna kipindi nadhani kuanzia november mpaka april nyanya inakua ni lulu kupita kiasi,ila nyanya inayovunwa miezi hiyo nayo uwa ina kazi kidogo katika ulimaji
 
MKuu Ohotaite Kintu, nashukuru kwa ufafanuzi wako. Nami ninauzoefu sana na Kilimo cha nyanya za majira haya! Kwa uzoefu wangu kutokana na maelezo yako hapo juu nakusihi hivi sasa pamoja na kutafuta bei nzuri usikatae bei inayopatikana hapo shambani! Umefanya vema kuomba msaada jukwaani ila usikatae kidogo kitakachofika shamba! Mkuu katika majira haya ya nyanya nyingi watu tumewahi kutoka kapa! Anakuja mnunuzi anakuta umechanganyikiwa anakuambia umuuzie mali kauli atakulipa mzigo ukifika sokoni, mkifika sokoni wanasema mzigo umefurika hakuna mnunuzi, unaanza kukumbuka 2000 ulizokataa shamba, maana ukiangalia pesa ya kulipia nauli ya gari huna unaamua kutoroka sokoni kimya kimya kurudi shamba. Mkuu endelea kutafuta soko lakini usiache kupokea hicho kinachokuja shamba hata kidogo pokea, nyanya za majira haya Kilosa wanaita "Nyanya ninyanyue nyanya ninyanyase".

Ushauri mzuri sana mkuu Kubota
 
Moja ya Matatizo makubwa tulio nayo ni haya, Na kilimo kimekuwa Duni Tanzania kwa sababu mnunuzi ndo mpanga bei, wakati Nchi za watu huko Wakulima ni levo nyingine kabisa, na kwa chochote kile inapotokea hari kama hii ni lazima kuanza kuwaza nje ya box,

Unapo ingia Kulima, au kufuga ni lazima ujiulize je nikishindwa kuuza haya mazao yangu nitafanyaje? Cha kusikitisha hakuna mtu anaye taka kuweka hiyo optional ingawa ni muhimu sana, watu wamekuwa wanapata hasara kubwa sana kwa sababu tu wao walilima wakijua watauza bila kujalisha hao wanunuzi watatokea pande zipi, na hii ipo hata kwenye kufuga hasa kuku, mtu anafuga kuku kwa sababu jirani yake anafuga na wanapo fikia muda wa kuuza ndo ananza kutafuta wateja, na matokeo yake ni wa nunuzi kupanga bei wanayo taka,

Hivyo tunapo lima au Kufuga kabla hujaanza jiulize je ni kikosa wateja nii product yangu nitaifanyeje? na ni lazima uwe n optional kwamba ikitokea mazao yangu yakikosa wateja basi mimi nitafanya A B C itasaidia sana,

Huwa inauma sana watu kama Madalali wako town lakini wanakula sawa na mzalishaji tena some time kumzidi mzalishaji
 
Mkuu chasha hapo juu umenena nyanya zinahitaji timing ya hali ya juu sana ukiweza kuzilima kipindi cha mvua zinalipa sana cause huwa hazipatikani kipindi hicho
 
Mkuu chasha hapo juu umenena nyanya zinahitaji timing ya hali ya juu sana ukiweza kuzilima kipindi cha mvua zinalipa sana cause huwa hazipatikani kipindi hicho
Kwa wenye uwezo wa kumiliki Green house hapa ndiyo suluhisho wakati wa masika. Unakamua pesa hadi unahisi unawaibia watu.
 
Wadau naomba kujuzwa hasa kwa wale wenye uelewa juu ya zao la nyanya,nilikua napenda kujua changamoto kuu za kilimo cha nyanya kipindi cha kiangazi kama hiki!na je uhakika wa soko la nyanya za kiangazi uko vipi?natanguliza shukrani zangu
 
Mkuu hizi nyanya za kiangazi nasikia zina changamoto zake hasa katika madawa,ila ukifanikiwa kuvuna ni kua umepiga bao!ngoja waje kina Malila na Kubota watatoa shule ya uhakika hapa!
 
Mkuu hizi nyanya za kiangazi nasikia zina changamoto zake hasa katika madawa,ila ukifanikiwa kuvuna ni kua umepiga bao!ngoja waje kina Malila na Kubota watatoa shule ya uhakika hapa!

Poa mkuu
 
Kiangazi nyanya zinazaa kupitiliza mahitaji kwa mbali sana, magonjwa machache, kwakua miundo mbinu ya kuongeza thamani si ya kutosheleza, bei yake inadondoka kupita gharama za uzalishaji.
 
Kiangazi nyanya zinazaa kupitiliza mahitaji kwa mbali sana, magonjwa machache, kwakua miundo mbinu ya kuongeza thamani si ya kutosheleza, bei yake inadondoka kupita gharama za uzalishaji.

Asante mkuu!je hizi nyanya tunazokula sasa hivi ambazo ndoo ni 2000/= zililimwa kipindi gani?maana kuna mdau kanidokeza kua nyanya zinazolimwa kuanzia mwezi oktoba na kuendelea bei yake uwa inakua juu sana sababu ya ugumu katika uzalishaji wake!je ili linaukweli wowote?
 
Mkuu hizi nyanya za kiangazi nasikia zina changamoto zake hasa katika madawa,ila ukifanikiwa kuvuna ni kua umepiga bao!ngoja waje kina Malila na Kubota watatoa shule ya uhakika hapa!
Mkuu Nyamburi asante kutambua uwepo wangu, acha nianze kuchangia na wadau wengine wataendeleza nitakapoishia. Kuna thread moja ilianzishwa hapa kuna mdau alikwama kupata wanunuzi wa nyanya (Dakawa) Dumila Morogoro akaandika hapa kuomba msaada wa kuunganishiwa wanunuzi. Kuna mchango mwingi wa mawazo kule kwenye thread hiyo nadhani hapa ni suala linalojirudia.

NI hivi: 1) Nyanya za kiangazi hufanikishwa na kufaidiwa sana na wakulima wenye mitaji mikubwa ambao huwa wanalima kwa maeneo makubwa sana kuweza kujaza FUSO mwenyewe na kusafirisha masoko ya mbali. Ijapokuwa bei ni ndogo lakini kwa kuwa huwa wanamzigo mkubwa na gharama za uzalishaji ni ndogo sana huwa wanaingiza pesa kubwa sana. Kuna wakulima wengi sana aina hii ukifika msimu wa kilimo cha kiangazi huja kwa wingi sana mkoani Morogoro maeneo ya Dumila, Mbigiri na mabonde ya Kilosa na pia eneo la Doma kuelekea Mikumi. Wakulima hawa ni wenye mitaji mikubwa hasa toka Iringa na maeneo mengine, huja msimu wa kiangazi kulima nyanya hizi kwa wingi sana, na wao hata bei ikiwa ndogo husafirisha kupeleka masoko ya mbali ikiwamo Dar! Mkulima mdogo mdogo akilima msimu huu sana sana ndiyo huishia kuwauzia hao wenye uwezo wa kusafirisha na bei ambayo hupewa ni ya kutupa karibu na bure.

2) Kilimo cha nyanya za kiangazi ni kilimo kisichokuwa na changamoto ukilinganisha na nyanya za masika. Majira ya kiangazi kuna ubaridi na hewa kavu magonjwa hayashamiri sana na nyanya huzaa kwa uwezo mkubwa kuliko majira ya mvua. Nyanya huzaa mavuno makubwa sana kiangazi kuliko majira ya mvua ambako huwa kuna joto linalopukutisha maua na matunda.

3)Hata hivyo uzoefu wangu maeneo ya Morogoro kwa ujumla kwa mfano nyanya zisizokuwa na changamoto ni kuanzia mwishoni mwa mvua na kupitia kipindi chote cha baridi nyanya za mwisho zivunwe mwezi wa nane. Kuanzia mwezi wa tisa huwa kuna changamoto ya ukame ambapo umwagiliaji lazima uwe wa karibu karibu zaidi, pia hutokea wadudu ambao ni nuksi sana, wanaitwa red spider mites, ni kama utitiri mwekundu, hawa ni wabaya sana kuanzia majira ya joto kali yanapoanza. Hawa wadudu ndiyo hupausha majani na matunda yanapoiva kuwa kama rangi ya machungwa. Kuanzia mwezi wa kumi hadi kipindi chote cha joto kali mimea ya nyanya hupunguza sana uzaaji kwani maua huwa yanapukutika tu au hayarutubishwi kwa hiyo nyanya zinazozaliwa ni chache. Na pengine ni kipindi hiki nyanya huanza kuadimika na bei huanza kupanda juu.

Kwa hiyo nahitimisha kwa kusema kuwa kupindi cha kiangazi kina awamu mbili, awamu ya kiangazi baridi ambacho huishia mwezi wa nane na ndicho nyanya huzalishwa kwa wingi sana bila changamoto na awamu ya kiangazi joto kinachoanzia mwezi wa tisa hadi mvua zinapoanza, kipindi hiki ni cha wadudu nuksi, ukame mkali na uzaaji duni wa nyanya shauri ya joto kali linaloathiri uchavushaji na urutubishaji maua. Nawasilisha wakuu !!
 
Asante mkuu!je hizi nyanya tunazokula sasa hivi ambazo ndoo ni 2000/= zililimwa kipindi gani?maana kuna mdau kanidokeza kua nyanya zinazolimwa kuanzia mwezi oktoba na kuendelea bei yake uwa inakua juu sana sababu ya ugumu katika uzalishaji wake!je ili linaukweli wowote?
Mkuu 1800 nyanya zilizoko sokoni hivi sasa ni mpando wa mwezi June na July. Nimefafanua kwa ukamilifu kwenye jibu langu kwa Mkuu Nyamburi hapo juu. Ni kweli kipindi kuanzia October uzaaji wa nyanya hupungua sana na bei huanza kuja juu, anayeweza kukabiliana na changamoto za kipindi hiki hukutana na kabei katamu.
 
Mkuu wangu Kubota nashukuru sana kwa mchango wako,hakika hapa Jamiiforum kuna vichwa zaidi ya shule,ukiingia hapa hauwezi toka kapa!mkuu kwa kweli naona kilimo kina changamoto za hapa na pale ambapo kama wewe una moyo mdogo unaweza kata tamaha,lakini lazima tukumbuke hakuna mafanikio mepesi!kuna jamaha kule Msowelo alilima nyanya nadhani ilikua may akaanza kuvuna august,ukweli ni kua alikumbana na wingi wa nyanya sokoni na bei ya kutupwa mpaka akawa anakosa wateja na nyanya nyingine zikawa zinamuozea tu shambani,ndio maana mimi nikaona kabla ya kuzama huko nije kwanza humu nipate shule kwa wadau wenye uzoefu kama ndugu yetu Kubota,mimi target yangu ni kuweka kitalu kuanzia oktoba kwa mantiki ya kuvuna december/january,ila mtaji wangu ni bado wa kuunga unga,je kwa ushauri wako mkuu nitastahili kufanya mambo kwa kuanzia mwezi oktoba,au ndio nitakutana na bei ya kutupwa kipindi cha mavuno kiasi kwamba kimtaji changu kisije hata kurudi na nijute kuingia huko?natanguliza shukrani zangu mkuu
 
Naombeni nitoke nje ya mada mtanisamehe waungwana.

Hivi ni wapi mtu anaweza kupata mbegu bora hapa Dsm , mahala ambapo wana aina nyingi za mbegu kama vile Matikiti, nyanya nk?
 
Naombeni nitoke nje ya mada mtanisamehe waungwana.

Hivi ni wapi mtu anaweza kupata mbegu bora hapa Dsm , mahala ambapo wana aina nyingi za mbegu kama vile Matikiti, nyanya nk?

Mkuu nadhani kwenye maduka yote ya pembejeo unaweza pata mbegu,kikubwa ni kua ujue tu ni mbegu gani stahiki/bora kwa kile unachokusudia kuipanda na itakayokidhi makusudio yako
 
Zingatia yafuatayo,

1. Mbegu_ pendelea kupanda mbegu za hybrid km ana eden nuru nk ilimradi iwe hybrid.

2. Shamba liwe nzuri kwa rutuba km haina rutuba weka samadi napia tumia mbolea ya kisasa.

3. Dawa iwe muhimu sna kupiga marakwa mara kuanzia kwenye kitalu cha mbegu hadi shambani.

4. Mbolea unatakiwa kuweka mara2 au 3 kutoka rutuba ya shamba ikoje.

4. Nyanya unakiwa uweke vijiti kusapot kusimama ili isianguke nakuozesha matunda.

Ukizingatia hayo utafanikiwa kwenye kilimo chako cha nyanya.nb zao la nyanya inaweza ikakupa faida kubwa pale unapozingatia kanuni zake.
 
zingatia yafuatayo 1mbegu_ pendelea kupanda mbegu za hybrid km ana eden nuru nk ilimradi iwe hybrid.2.shamba liwe nzuri kwa rutuba km haina rutuba weka samadi napia tumia mbolea ya kisasa.3.dawa iwe muhimu sna kupiga marakwa mara kuanzia kwenye kitalu cha mbegu hadi shambani.4.mbolea unatakiwa kuweka mara2 au 3 kutoka rutuba ya shamba ikoje.4.nyanya unakiwa uweke vijiti kusapot kusimama ili isianguke nakuozesha matunda.ukizingatia hayo utafanikiwa kwenye kilimo chako cha nyanya.nb zao la nyanya inaweza ikakupa faida kubwa pale unapozingatia kanuni zake.

Asante kwa somo... nitajuaje kama ndo hybrid.!,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom