Kilimo cha Mapapai: Ushauri wa Kitaalamu, Changamoto na Masoko yake

Habari ndugu wanajamvi kwanza nibishe hodi kwasababu mimi ni mgeni umu,
baada ya salam ningependa kuomba msaada kwa wataalam au mtu yoyote mwenye uzoefu wa kilimo cha mapapai, mimi ni mwajiriwa ila nimetafakali sana nimeona niingie katika shuguli za kilimo ili nijiongezee kipato, nipo dar nimepata shamba maeneo ya mwanzo mgumu chanika.

nimevutiwa na kilimo iki kwa sababu nimepitiapita dondoo zake ktk mitandao umu, ila bado sijajitosheleza namna sahihi ya kulima zao ili, tatizo langu kuu jinsi ya kutunza, mbegu bora zenye soko zuri na masoko, asanteni sana naomba kuwasilisha.
 
uploadfromtaptalk1471637174269.jpg
 
shamba lako likiwa hivi wewe unakuna kitambi tu
umeona maiye, mimi nina ekari moja nataka nipande mapapai tu, iko sehemu nzuri nina kisima cha maji, ila tatizo langu mbegu bora ikiwezekana kama hizo na namna ya kuzitunza
 
umeona maiye, mimi nina ekari moja nataka nipande mapapai tu, iko sehemu nzuri nina kisima cha maji, ila tatizo langu mbegu bora ikiwezekana kama hizo na namna ya kuzitunza
Ukishajifunza matunzo na kila kitu nicheki nikupe connection ya mbegu nzuri ya hybrid fupi ya mmpapai
 
Ukishajifunza matunzo na kila kitu nicheki nikupe connection ya mbegu nzuri ya hybrid fupi ya mmpapai
Sawa kiongozi ila nishaanza kuandaa shamba kama uwezekano upo ni bora ukanipa hiyo connection, japo bado sijaivaa sana ila mwelekeo tayari nishaupata nikipata mbegu akili yangu itatulia
 
Karibu sana.
Nina uzoefu kidogo Wa hii kitu. Sio kusomea nimefanya mwenyewe. Leo tuongelee mbegu.

Nakushauri nunua mbegu dukani zina Faida zaidi ya kuchukua za waitikaji au kula Papai na kuchukua mbegu

Ukinunua ziweke ktk maji kwa siku tano lakini badili Maji kila siku. Baada ya siku hizo zifunge ktk kitambaa kwa siku tatu.

Ukimaliza weka kwenye viriba ndio utapata matokeo mazuri. Nilinunua red royale f1, muuzaji hakunipa maelekezo hayo haikuota hats moja!

Uzoefu wangu unaonyesha kuwa Miche inayouzwa kwenye vitalu vingi haina u ora lakini kubwa utapata madume 20- 30 katika miti 100. Hii ni hasara kubwa.
Nunua mbegu kwenye maduka ya pembejeo zinauzwa kuanzia she 5000 had 16000.
Karibu na jipange kufanya kazi sio kutumia simu kufanya Kilimo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom