Kikwete's 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania'

DSC01234.jpg
DSC01238.jpg
DSC01244.jpg
 
Jamani hizi sehemu za wapi tz? Hebu tupitishe bakuri wa tz tujichangishe hawa watoto ndiyo taifa la leo wapate hata madarasa na madawati. Shime watz hizi picha zinatisha ktk karne hii. Waandishi ndiyo wangefanya kuvumbua sehemu kama hizi ili tuchangie.
 
Tuchangie nini wakati wanaweza kusoma BURE HADI CHUO KIKUU tukimchagua SLAA kuwa RAISI.Hakuna haja ya michango.Ukiuza ndege ya raisi tu wote hawa wanasoma vema,hapo sijagusia madini!!.tubadilike,tubadili uongozi!!!eeeh sijui tusemeje watu waelewe
 
Hukutukiendelea kupigania huo uwezekano, hawa watoto wasaidiwe kwanza hii ni emergency hayo mengine tukiuza ndege mtarejeshewa na wataenedelea kupata faida za madini na elimu bure. tutoe huduma ya kwanza kwanzaaaa mkuu!
 
Hapa sio South Sudani kweli? Ama kweli CCM inastahili kupigiwa kura milele! Tuendelea kudanganyika....
 
Wewe nawe.. yaani bandiko katika blog yako shurti uje ulitangaze hapa?

Kibunango sasa ulitaka alibandike wapi kama sio hapa? Kama una picha za kuonesha mafanikio ya awamu ya kwanza ya muungwana weka hapa watu waone hata kama ikiwa picha ya MAXIMO; wasomaji watapembua mchele na pumba!!
 
Piga picha ya ofisi yako unayofanya kazi (itakuwa ya serikali anyway maana wanaofanya kazi kwenye private sector hawana muda wa kuvinjari kwenye ukumbi huu), picha ya nyumbani kwako unapolala na sebuleni halafu tuambie hayo yalikuwa mafanikio ya serikali gani iliyopata kutawala nchi hii.
 
WanaJF,
Kwa jinsi hali ya maisha inavyoendelea kuwa ngumu, ninashawishika kuhisi kuwa Kikwete na timu yake waliteleza ulimi wakati wa kampeni. Inawezekana walikuwa wanamaanisha MAISHA BORA LIENDE KWA KILA MTANZANIA.

Mnasemaje wazee.
 
Ndugu zangu,
Ki ukweli kama mambo yataendelea hivi katika mjengo huu wa Bunge lililojengwa kwa madhumuni ya kutetea maslai ya watanzania, ya kwamba wale watu wanaoonekana kutetea watanzania ili kubadili hali dhaifu ya kiuchumi inayopelekea asilimia kubwa ya watanzania kuwa na maisha duni, kuwa wao ndio wavunjifu wa amani, Basi ni nani atatetea Tanzania!

Tulitegemea Bunge letu na Uongozi wake (Hususani Spika wa Bunge Anna Makinda) watakuwa mstari wa mbele kutetea maslai ya Watanzania katika kujenga uchumi wa taifa hili kwa haki na badala yake imekuwa kinyume kabisa! Ebu tujiulize, Wanatupeleka wapi?

Kinacho nichosha ni kauli mbiu waliyonayo ya "Maisha Bora kwa KILA Mtanzania" ambayo ilianza pindi tu JK alipoanza kutawala; kwa muda wa miaka 5 iliyopita imegeuka na Kuwa "MAISHA BORA KWA KILA MBUNGE WA CCM" na kwa watanzania ambao ndio waliwaweka watu hawa madarakani imebadirika na kuwa "BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA". WAnafunzi wanalia, wafanyakazi, wakulima kuwa maisha ni magumu. Awamu hii tena alikuja kwa kauli mbi hiyo hiyo, Sasa tujiulize ni kweli hayo maisha bora yatakuja kwa mwenendo mzima wa Buge la sasa? Kama Mbunge anaweza kumzomea Mbunge anayesimamia haki ya watanzania, Ataweza kweli kuleta maisha Bora kwa kila Mtanzania aliyemchagua. Si kweli, Hii ni kutoka katika maisha Bora kwa kila mtanzania kwenda katika Bora maisha kwa kila mtanzanioa, kumekuchwa tunasubiri tena kukuche, lakini umasikini uko pale pale!

TUIOMBEE TANZANIA, TUSIMAME NA KUWATETEA WATANZANIA, NO MATTER WHAT!!!
 
......Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote..................................Rais Jakaya K. Kikwete

maneno ya mkulu hapo jana...

tafsiri yangu.....kikwete amekubali rasmi kushindwa na kwamba ile ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania ilikuwa ni porojo za kisiasa.

wale waliokuwa wakifikiria kuwa JK ni tofauti na watangulizi wake..wajiulize mara mbili

Nawasilisha.
 
[FONT=georgia, bookman old style, palatino linotype, book antiqua, palatino, trebuchet ms, helvetica, garamond, sans-serif, arial, verdana, avante garde, century gothic, comic sans ms, times, times new roman, serif]
Notice the difference between what happens when a man says to himself, "I have failed three times," and what happens when he says, "I am a failure." ~S.I. Hayakawa
[/FONT]
 
Kati ya watu ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kwa CCM kuanguka basi JK ametoa mchango mkubwa sana.
 
niaje wadau? Naomba kwa leo niwape kile nilichokikuta kwa soko mjini Tabora. Mchele kilo Tsh 1200-1500, sukari kilo 1700, unga kilo 800, mafuta ya taa litr ni sh 1600, mkaa gunia Tsh 1200, umeme kwh moja ni sh 147, mafuta ya kula lita moja na nusu ni sh 4500, maharage kilo ni sh 1200, dagaa kilo sh 3000, samaki kilo ni sh 5000, nyama kilo ni sh 3000, maji tulikuwa tunanunua dum sh 500 ingawa sasa hivi mvua zinanyesha tumepata nafuu kidogo. Kwa hali kama hii jamani mbona twafaaa??? Hivi kwa hii mishahara ya serikali isiyokutana tutafika?
 
ila gunia la mkaa bei rahisi.
Hali ngumu kila sehemu ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom