Kikwete's 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania'

Hayo ndio maisha bora yaliyoletwa na Kikwete na CCM yake. Tuywape miaka mingine tena ili yaimarishwe zaidi kwa Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi.
 
Hivi hawa wote wanaompigia CCM na JK debe humu ndani ni vipofu? Viziwi" Au nini? Au wamelogwa kwa kuuangalia Mwenge wa Uhuru kwa miaka mingi? Maana huo mwenge ni pumbazo kubwa la CCM mimi sijawahi maishani mwangu kupishana nao -- hua nakula kona ile mbaya!!

Watu wazima wanaona kiza eti ndiyo mwanga!!! ewe Mwenyezi Mungu -- awafungulie macho hawa Watz wenzetu ifikapo Oct 31.
 
Naona Naomi anawaonea huruma akina mama wajawazito wakiwa wamejikalia chini kwa kukosa vitanda mbaya zaidi such things happen at TEMEKE/AMANA/MWANANYAMALA sasa uko Nanjirinji,lupembe,pawaga
 
Haya ndiyo JK alitakiwa kuwaambia wananchi - yaani aliahidi nini, ametekeleza yapi, na atayaendeleza vipi ingawaje kwenye kuendeleza amesema 'kasi zaidi, ari zaidi, na nguvu zaidi'. Tutarajie picha mbaya na za kukera zaidi ya hizi!!
 
Mi kunabango linanikera limewekwa dar njia panda ya kigogo kunawanafunzi wanaonekana na jk wakiwa maabara, halafu limeandikwa elimu kwa vitendo Mi ntaling'oa na wacha ninunue kesi, anamaanisha hizi shule za kata au anamaanisha nini?? na vitendo vp?? wanachama wa ccm jamani tusishabikie kila kitu vingine tuchuje kidogo. kwa nini tunapenda kujiaibisha tunadhani ndo tutapata kura nyingi kwa uongo huo, walimu wetu wanaweza kusema ukweli kuhusu hili!
 
A friend of mine sent me this.......

LKIONGOZI BWM Vs JK
MWAKA 2000 -2004 Vs 2005-2009

Unga 460 Vs 1000 = 217%
Mchele 600 Vs 1200 = 200%
Sukari 760/kg Vs 1600/kg = 210%
Mkate 250 Vs 700 = 280%
Maharagwe 360/kg Vs 1000/kg = 277%
Mafuta ya taa 450/lt Vs 1050 = 233%
Mafuta ya uto 178/lt Vs 720/lt = 404%
Nazi 100 Vs 550 = 550%
Mchicha/tembele 50 Vs 150 = 300%

unalipwa 100,000/-kwa mwezi kwa jedwali la hapo juu kila siku lazima
ununue unga robo 400, mchele nusu 300, uto kibaba 125, mafta taa
kipimo 300, sabuni nusu kipande 50, sukari robo 400, maharagwe robo
250, mkaa nusu kisado 300, nauli go & return 500, maji ya kunywa 500,
hapo ni bachalor kwa siku ni 3,125 mara 30 = 93,750 kwa mwezi. Okay
kodi kwa mwezi 20,000/- umeme 6000 kwa mwezi =total kwa mwezi ni
120,000/- je hiyo 20,000/- ziada katoa wapi????? ndo hizo mwisho wa
siku zina wapeleka jela au kuwanaachishwa kazi. Je maisha bora hapo
atoe wapi? Na je angekuwa na mtoto wa shule au watoto wawili? hapo
hajaumwa, hajatembelewa na mgeni akamnunulia soda, hajanunua nguo
nyingine!!!! Huyu mnaempigia kura hayajui hayo na hatambui kama una
familia kijijini pia. wao wanatibiwa na serikali, mafuta ya magari
kwao ni sawa na kumuuliza bibi akupigie story ya sungura. wenzie
wakitaka ongezo la mshahara wanajadiliwa in 2Hrs jibu tayari ila
waalimu na wenzao.........! 3 years.

Yeye huyu JeyKey na hao wapambe wake na hao wanajipendekeza kama
Shigongo waulizeni watoto zao ni akinani? utaambiwa mbunge, mara yuko
BOT mara yule wa mwisho yuko ulaya kamtembelea shangazi yake, mara
yuko busy na tenda ya kusuply komputa Wizarani. Wewe je unae mpigia
kura tupe wasifu wako hata hao watoto wako na wategemezi wako. Hata
baiskeli kule kijijini huna wala wazazi wako ndo unakesha kuwaombea
wasiumwe kwa kuwa gharama za hospitali zitakuwa zako.

Muulize kesi za mafisadi vipi? Na je wanampango gani? utaambiwa yuko
busy na harakati ya kutafuta ulaji kwa mara ya pili.

Hao wapambe wake na mawaziri wanaendesha magari gani utaambiwa aah
wana tano tano kila wizara VBV8, uliza bei zake kila moja, inatumia
mafuta kiasi gani kwa mwezi, na majukumu yake ni yapi? Na je
zinakoenda akina RAV4, Suzuki, BMW ndogondogo hawafiki? Utaambiwa
wanawahi kuwasilisha agenda. KWEEELI?

Na je hizo gharama za uendeshaji fedha zinatoka wapi? Utajibiwa kwenye
mfuko wa serikali. Waulize serikali ina miradi gani ya kuweza
kuendesha hayo magari tu achana na posho zao na mengineyo? Jibu ni
KODI ZENU wananchi waungwana tulio na amani na utulivu kwetu. KWEELI
kwa mshahara wa laki mbili zangu/zako?

FUNGUENI MACHO NA AKILI ZENU WAUNGWANA. Wenzenu Zenji wameshaliona
hili wameamua kujichorea MIPAKA yao Mapema.

MTAENDELEA KUZUBAISHWA NA STORI ZA KUTUNGA NA UDAKU NA KUSHANGILIA
MISAFARA MIREFU YA KAMPENI INAYOUNDWA KWA KODI ZENU.


Yours Truly,?


Tuendelee kudanganyika kwa miaka mingine mitano.
 
Hapo afadhali ungemuwekea na pombe za kienyeji za 1000 kwa siku ili aweze kusahau matatizo na taabu za kukagawa hako ka laki anakolipwa kwa mwezi. Nakuhakikishia huyo jamaa mwenye hiyo bajeti hapo ataendelea kumchagua JK na sisiemu yake apewe Tshirt na Kofia manake sijaona bajeti ya nguo hapo!!!!!!
 
Inauma sana mazee, mbaya zaidi huyu bwana hajapiga bajeti ya maji dumu 300 hadi 400, chukulia kuwa atatumia dumu moja kila siku.
jumlisha na vocha ya 250 kila siku.
 
TAFAKARI, CHUKUA HATUA

:A S new: :help::help::help:!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
TUKO HIVYO
Hatuoni
Hatusikii
Tunadanganyika kirahisi
Tunafuata mkumbo
BAADAE TUNALALAMIKA

Ofisi zetu -taabani

Hii ndio hali ya barabara zetu ambazo aliahidi na anaahidi tena.......

Picture_050.jpg

MAKAZI YETU -ni kama mahame[sehemu ambazo watu walihama miaka mingi]

7976228.jpg



maggid2bc.jpg



aabb42bkopierahr0.jpg


shule zetu -
1:
ShulezaTanzania.bmp

2:
01_10_fyz0h9.jpg


Darasani kwa watoto wetu-viti ni ardhi tuliyopewa na mungu na hii sijui ndo geto la huyu ticha........

Shule+ya+msingi.jpg


Huko vijijini-Dispensary -i cant say

WAO WAKICHAGULIWA....

Ubalozi wa Tanzania Washington-more than the US embasy


Jengo+jipya+la+ubalozi+wa+Tanzania+mjini+Washington+DC.jpg


Ofisi zetu za Bunge-you cant believe if it is the same tz



Bunge+Dodoma.jpg


Kuna cha kuongeza?

Sasa tucheze na hesabu 6,900,000/= kwa mbunge mmoja,zidisha mara miezi 12 then zidisha kwa miaka 5 = 414,000,000/= jumlisha 50,000,000/= anayopewa mara baada ya kumaliza miaka 5 = 464,000,000/= kwa mbunge mmoja.

464,000,000/= siko tayari kuzidisha fedha hii mara wabunge wote kwa miaka 5,calculator yangu itachanganyikiwa alafu niingie gharama ya kununua nyingine.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom