Je, maisha bora ilikuwa kwa kila Mtanzania au kwa baadhi tu ya Watanzania?

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,473
21,953
Maisha bora kwa kila mtanzania ilikuwa 2005 hadi 2015.

Tulidanganywa hivyo kipindi hicho, tukadanganyika kwa miaka 10, baada ya hapo jomba akasepa akiwa na kitita cha kutosha kumpa maisha bora yeye tu na watu wake.

Hivi kwa nini huwa tunakubali kudanganywa kirahisi hivyo?

Sasa tupo na "kazi iendelee" bado tunakodoa macho tu, ila maisha bora yapo kwa vigogo na watu wao, hata wakistaafu wamekuwa wakijirudisha tena madarakani ili kuendeleza maisha bora kwao na jamaa zao tu.

Kuna watu waliahidiwa kuwezeshwa kupata ajira, bila shaka waliamua kuwa bodaboda baada ya kukosa ajira, bado hayo sio maisha bora.

Mungu tuondolee viongozi waongo na mafisadi.

1694495561392.jpg
 
Ilianza na Ari mpya nguvu mpya Kasi mpya ikaja Ari zaidi Kasi zaidi kumbe Kasi zaidi ya kujitajilisha na family zao pumbafu CCM
 
Back
Top Bottom