Mzee Kikwete anatakiwa kuelewa kuwa Dini ni Siasa na Siasa ni Dini

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
MHESHIMIWA KIKWETE SISI WATUMISHI WA MUNGU HATUWEZI KUTOFAUTISHA SIASA NA DINI KWA SABABU SIASA NI DINI NA DINI NI SIASA.

Na Mwandishi wetu Mzalendo Mtanganyika toka Ughaibuni.
20 August 2023. 16:30 pm

Watanganyika wenzangu someni andiko hili mtapata faida na maana kubwa acheni kuhadaiwa na viongozi wa kisiasa wanataka kuigeuza nchi yetu shamba la Bibi.

Kwanza kabisa napenda niwashukuru Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuuelewesha Umma. Kanisa Katoliki ni kanisa lenye sifa na heshima Duniani kwa kuwa na Uongozi uliokomaa na kusimikwa kuanzia ngazi ya familia Duniani.

Mheshimiwa Kikwete kama hujui acha tukujuze yafuatayo:-
  1. Dini hizi zote ni Imani tulizoletewa na wakoloni kwa kuwa Babu na Bibi zetu walikuwa na Imani zao ambazo walikuwa wanaamini kabla ya kuja ukoloni.
  2. Historia inaonyesha Dini zimeanza kuingia Barani Afrika miaka ya 1600 - 1700.
  3. Dini na siasa haviwezi kutenganishwa kwa sababu Dini ni serikali na serikali ni Dini. Ndio maana jifunze kabla ya kusema kwa muono uliouleta leo hii ili tukujuze.
Roman Catholic ni kanisa Mama Duniani ambapo kanisa hili makao makuu ya kanisa yako Vatican city na Mkuu wa Kanisa ni Papa ambaye hata wewe unamuheshimu na kumtukuza kama Mkuu wa Kanisa na Mkuu wa serikali ya Vatican city kama nchi.

Makao makuu ya kanisa la Anglican yako Uingereza ambapo Mkuu wa kanisa hilo ni Malkia au Mfalme wa Uingereza na Uingereza ni nchi.

Makao makuu ya kanisa la Rutheran yako Ujerumani na mkuu wa kanisa hilo ni Rais wa Ujerumani na Chancellor wa Ujerumani.

Makao makuu ya makanisa ya Pentecostal yako Marekani na hii ni baada ya Vita kuu ya kwanza ya Dunia Marekani walikuja kustuka ya kuwa ili upate uungwaji mkono wa mtu mweusi ni lazima uwapelekee Imani na Dini ili wapate kuamini hivyo wakaweka mkakati wa kuanzisha Imani na Dini katika Afrika

Imani zipo nyingi sana kwani historia zinaonyesha katika Imani hizo zipo nyingine zilianza hata BC na kusimamia imara mfano Krishna n.k

Uislamu ni Imani na Dini iliyoletwa kwetu na Waajemi na Historia inaonyesha waliingia nchini miaka ya 1700 kwa kisingizio cha wafanyabiashara wa pembe za ndovu na mazao ya kilimo, lakini baadaye wakawa wafanya biashara wa kuwauza watumwa kwa Wazungu.

Uisalma makao makuu yao yapo Saudia na katika Uislamu kumegawanyika katika makundi 73 kwa mujibu wa Quran. Na hapa naweza kukutajia machache tu ingawa wote wanaamini katika Muhimili mmoja wa Mtume Mohamed:-
Shia
Sun
Bohora
Ahamaddiya
Haya ni baadhi ya madhehebu ya Kiislamu ingawa yapo mengi sana na haya ni mfano wapo tu.

Hapo unawezaje kutofautisha Dini Imani na serikali ikiwa wakuu wa Imani na Dini ndio hao hao wakuu wa serikali hizo zinazotawala Nchi na Dunia?

MADA KUU.
Mheshimiwa Rais mstaafu wa awamu ya nne, kwanza katika hutoba yako tumesikia ukieleza namna ulivyotatua mgogoro wa kiimani Zanzibar. Ngoja tukueleze na kukukumbusha.

Mgogoro wa kiimani Zanzibar ulisababalishwa na Viongozi wa kisiasa ambao walianza kutamka wazi wazi nchi ya Zanzibar ni nchi ya Kiislamu na kupelekea wananchi wa Zanzibar kutengeneza chuki kwa wakristo na kuamua kuchoma makanisa Tukasahau hakuna Zanzibar nchi bila Tanganyika na sheria inasema Taifa letu halina Dini bali watu wake ndio wenye Dini.

Tunatambua wazi asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar ni waislamu ingawa wakristo wapo pia. Zanzibar haijawahi tawaliwa Rais mkristo tokea mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Vivyo hivyo Tanganyika Bara Kuna idadi kubwa ya Wakristo mara 2 au zaidi ya waislamu ingawa Tanganyika kumetawaliwa na Wakristo na Waislamu.

Maasi hayo na mgogoro huo kipindi yanatokea wewe ulikuwa Rais wa Tanzania mwenye Imani ya Uislamu na wakristo hawakurejesha kisasi wakiamini katika akupigaye shavu la kushoto mgeuzie la kulia. Je unawezaje kujisifia kwa jambo kama hilo?

Tanzania kiujumla, Ukristo umegawanyika katika madhebu tofauti tofauti lakini Imani yao wote ni wakristo wanaamini katika Kristo.

Kiimani na kielimu wakristo wamejikita katika Elimu Dunia na Elimu Akhera na ndio maana karibia Mapadree wote ni PhD holders na hata wachungaji na Maaskofu. Kwani katika msingi wa Imani ya Ukristo elimu zote zinaendana.

Katika nchi yetu ya Tanzania kwa bahati mbaya sana Tanganyika haina serikali tumesimama na kuishia kusema sisi ni Watanganyika na tukajiweka ndani ya koti la Utanzania.

Hivyo tukakubali kutawaliwa au kuongozwa na Wazanzibar na Watanganyika wenzetu kitu ambacho tuliamini katika Umoja.

Katika Uongozi, sisi tuko tayari kuongozwa na Wanzibar kwa kuanzia na viongozi wa ngazi ya mtaa, kata, wilaya, Mkoa na hata Taifa. Je Zanzibar kuna Mtanganyika ambaye ni kiongozi au anaruhusiwa kumiliki ardhi?

SISI WACHUNGAJI NA BARAZA LA MAASKOFU TURUDI KWENYE HOJA KUU NA MSINGI JUU YA IMANI ZETU, TUSICHANGANYE DINI NA SERIKALI.

Mheshimiwa Rais mstaafu hongera kwa kutoka hadharani na kutueleza hayo lakini tunakuomba upate kutoa ufafanuzi juu ya maswala yetu ambayo tunahitaji majibu juu ufisadi na upendeleo wa haya yanayoendelea nchini juu ya mkataba wa DP WORLD.

Baada ya Mkataba wa DP WORLD tumeshuhudia yafuatayo yakiendelea katika nchi yetu na upendeleo wa makundi na hata kutugawa
  1. Je uliwahi kutoka na kueleza kama Rais mstaafu mpaka uone BARAZA LA MAASKOFU likitoa msimamo wake nawe ndio utoke na kusema?
  2. Waislamu na Mashekhe walisimama na kumuunga mkono Mhe Rais Samia juu ya uwekezaji wa Bandari uliwahi kujitokeza na kusema wasichanganye Dini na serikali?
  3. CCM walitembea nchi nzima wakiusifia Mkataba na kutoa elimu ya uwekezaji wa Bandari, Uliwahi kutoka na kusema wasichanganye siasa na uongozi wa serikali?
  4. Machawa waliandamana nchi nzima wakiunga mkono uwekezaji wa DP WORLD uliwahi kujitokeza na kusema wasichanganye mahaba na utendaji wa serikali?
  5. Serikali imewabambikia kesi za uhaini watu wasio kuwa na uhusiano wa Majeshi je wewe kama Rais mstaafu uliwahi kujitokeza na kuwatetea kwa kuuelezea umma madhara ya kesi za namna hiyo?
Iweje leo Baraza la Maaskofu, watetezi wa mali za nchi, Mawakili wanaotaka kutetea rasilimali za nchi pamoja na watu wanaotaka haki na sheria vizingatiwe wawe wahujumu uchumi au waonekane wanakuwa wachochezi au wanachanganya Imani na serikali?

UFISADI UMEKITHIRI.
Mheshimiwa Kikwete nchi yetu kwa sasa haiko salama wala hakuna amani ni kutokana na uongozi wa Chama cha mapinduzi kutokuangalia umuhimu wa usawa na haki kwa Taifa.
  1. Kinachozungumzwa na Baraza la Maaskofu Tanzania sio kukataa Mkataba bali taratibu sheria na kanuni zifuatwe katika kutoa hiyo tenda kwa DP WORLD na sio vinginevyo.
  2. Sheria za ugawaji tenda zitangazwe mashirika yashindanishwe na atakaye shinda tenda birds apewe kulingana na makubaliano serikali itakayoingia na kuwa na mkataba makini na wenye tija kwa pande zote mbili.
  3. Nchi hii ni mali yetu sote kuwepo na haki katika pande zote yaani kwa wanahoji wapewe majibu na wanaotetea walete majibu.
  4. Bunge lisitumie nguvu kubwa katika kuunga mkono hoja za uuzwaji wa Bandari kwa kulazimiashia kuwa sehemu ya wananchi kwa uroho wa fedha na kupoteza utu wao.
  5. Bunge kwenda kupitisha sheria ya umiliki wa ardhi kwa wageni ni kosa kubwa sana bila muswada huo kupitia kwa wananchi ambapo tumeshatambua mchezo mchafu unaofanywa na kikundi cha watu wachache kuonekana wametoa maoni kwa niaba ya wananchi.
  6. Mheshimiwa Rais mstaafu wewe na kikundi cha baadhi ya familia za watu wachache katika nchi hii sio wasafi na tunajua unatoka hadharani kutetea ugali wako tunaomba uwe muwazi na mkweli.
  7. Takwimu zinaonyesha wewe ni sehemu ya mnufaika wa baadhi ya Ghati pale Bandarini ambapo ulikuwa ukivuna mapesa mengi kupitia TICTS na hata hapa unatetea ugali baada ya kuona mambo magumu na ikiwa kanisa litasimamia msimamo wake nawe utakosa.
  8. Katika uongozi wako ufisadi mwingi umetokea ukiwemo wa RICHMOND na Escrow je uliwahi kusema au kuomba radhi kwa wananchi.
Wewe sio msafi hata kidogo katika jambo hilo na huwezi kuwa msafi kwa kauli hii uliyoinena Leo.

Wewe ndio mchonganishi na mwenye kuingiza au kutaka kujimilikisha siasa na uongozi na kutugawa sisi kama wananchi.
Sisi kama viongozi wa Dini jukumu letu ni kusimamia amani na mshikamano kama vitabu vyetu vinavyotuongoza.

Mkataba wa DP WORLD hauna viashiria vya amani wala umoja kwa Taifa letu. Ikiwa Rais ni Mzanzibar, Waziri aliyeingia Mkataba ni Mzanzibar na Katibu mkuu wa wizara husika ni Mzanzibar.

Inaonyesha katika utendaji kazi wako unatuheshimu nasi tutakuheshimu kuwa mkweli na muwazi kwetu usiwe na kauli mbili.

Katika mambo ya Muungano Bandari sio jambo la Muungano iweje haya yatokee nankutendeka?

Nakushauri kuwa mshauri mwema na sio mtu wa mihemko na tamaa za mwili na akili kwa kutaka kuuza Tanganyika na mali zake. Mshauri Mama Samia vyema juu ya mkataba wa Bandari haufai hatuko tayari kuona tunakuja kuingiza kizazi chetu machafukoni na kwenye ulipaji wa madeni kwa DP WORLD.

Mbona ni mengi yametokea, Loliondo, KIA na hatujasikia umetoka kukemea au kuwakemea wahusika why hili?

Sisi tutasimama imara na tutasema kwa sababu kazi za kichungaji ni kutunza amani na kueleimisha jamii kimaadili.

Asante
Tuipende nchi yetu kama Taifa teule la Mungu.

Ni mimi Mzalendo toka Ughaibuni kunako Amani na Upendo.

JamiiForums681497641.jpg

Pia, Soma

Huyo mu west Africa ni mkweli sana mimi huwa ni mfuatiliaji wa hizo clip zake muda wote na huwa ninamuelewa.
Sasa hivi amejikita kwa Tinubu...Rais wa Nigeria kuhusiana na ECOWAS kutaka kutuma majeshi huko Niger ili kuuondoa utawala wa kijeshi uliochukua madaraka kwa njia ya Mapinduzi hivi karibuni.

Dogo anawaambia "ECOWAS"kwamba ni mawakala wa nchi za Magharibi sababu chanzo ni Madini ya "URANIUM" ambayo yanapatikana kwa wingi nchini Niger na sasa wanajeshi wamewatimua wazungu kwenye migodi yote waliyokuwa wakisomba "URANIUM".

Kwa hiyo nchi za magharibi zinaichochea "ECOWAS" kwa mlango wa nyuma ili ku-push agenda yao kuwaondoa wanajeshi na kumrudisha Yule Rais wa kiraia na bilionea mkubwa Niger.
Ili waendelee kuchota "URANIUM" kama awali

Jambo ambalo ndio ukweli sahihi.
 
Naamini Kikwete hatarudia tena kutamka yale maneno yake aliyoyazoea, kwasababu sasa anapewa mafundisho ya kila aina.
 
Naamini Kikwete hatarudia tena kutamka yale maneno yake aliyoyazoea, kwasababu sasa anapewa mafundisho ya kila aina.
Ni kweli na pia hata wenzie kwenye genge lake nako waelewe kuwa watanzania wa leo sio wale wa enzi za utawala wake.
 
Huyo Mzee akapumzike kwenye ikulu aliyojengewa kwa Kodi za wananchi. Kama inawezekana kuuza bandari halafu wananchi wasilipe Kodi yoyote sawa. Yaani nchi hii iwe tax heaven kama nchi tunazozisikia Ila kama tutaendelea kulipa Kodi basi iachwe hivo hivo

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Na Mwandishi wetu Mzalendo Mtanganyika toka Ughaibuni.
20 August 2023. 16:30 pm

Watanganyika wenzangu someni andiko hili mtapata faida na maana kubwa acheni kuhadaiwa na viongozi wa kisiasa wanataka kuigeuza nchi yetu shamba la Bibi.🩸🩸🩸

Kwanza kabisa napenda niwashukuru Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuuelewesha Umma. Kanisa Katoliki ni kanisa lenye sifa na heshima Duniani kwa kuwa na Uongozi uliokomaa na kusimikwa kuanzia ngazi ya familia Duniani.

Mheshimiwa Kikwete kama hujui acha tukujuze yafuatayo:-

Dini hizi zote ni Imani tulizoletewa na wakoloni kwa kuwa Babu na Bibi zetu walikuwa na Imani zao ambazo walikuwa wanaamini kabla ya kuja ukoloni.
Historia inaonyesha Dini zimeanza kuingia Barani Afrika miaka ya 1600 - 1700.

Dini na siasa haviwezi kutenganishwa kwa sababu Dini ni serikali na serikali ni Dini.

Ndio maana jifunze kabla ya kusema kwa muono uliouleta leo hii ili tukujuze.
🩸 Roman Catholic ni kanisa Mama Duniani ambapo kanisa hili makao makuu ya kanisa yako Vatican city na Mkuu wa Kanisa ni Papa ambaye hata wewe unamuheshimu na kumtukuza kama Mkuu wa Kanisa na Mkuu wa serikali ya Vatican city kama nchi.
🩸 Makao makuu ya kanisa la Anglican yako Uingereza ambapo Mkuu wa kanisa hilo ni Malkia au Mfalme wa Uingereza na Uingereza ni nchi.
🩸 Makao makuu ya kanisa la Rutheran yako Ujerumani na mkuu wa kanisa hilo ni Rais wa Ujerumani na Chancellor wa Ujerumani.
🩸 Makao makuu ya makanisa ya Pentecostal yako Marekani na hii ni baada ya Vita kuu ya kwanza ya Dunia Marekani walikuja kustuka ya kuwa ili upate uungwaji mkono wa mtu mweusi ni lazima uwapelekee Imani na Dini ili wapate kuamini hivyo wakaweka mkakati wa kuanzisha Imani na Dini katika Afrika
🩸Imani zipo nyingi sana kwani historia zinaonyesha katika Imani hizo zipo nyingine zilianza hata BC na kusimamia imara mfano Krishna n.k
🩸Uislamu ni Imani na Dini iliyoletwa kwetu na Waajemi na Historia inaonyesha waliingia nchini miaka ya 1700 kwa kisingizio cha wafanyabiashara wa pembe za ndovu na mazao ya kilimo, lakini baadaye wakawa wafanya biashara wa kuwauza watumwa kwa Wazungu.
🩸Uisalma makao makuu yao yapo Saudia na katika Uislamu kumegawanyika katika makundi 73 kwa mujibu wa Quran. Na hapa naweza kukutajia machache tu ingawa wote wanaamini katika Muhimili mmoja wa Mtume Mohamed:-
Shia
Sun
Bohora
Ahamaddiya
Haya ni baadhi ya madhehebu ya Kiislamu ingawa yapo mengi sana na haya ni mfano wapo tu.
🩸 Hapo unawezaje kutofautisha Dini Imani na serikali ikiwa wakuu wa Imani na Dini ndio hao hao wakuu wa serikali hizo zinazotawala Nchi na Dunia?

MADA KUU.

Mheshimiwa Rais mstaafu wa awamu ya nne, kwanza katika hutoba yako tumesikia ukieleza namna ulivyotatua mgogoro wa kiimani Zanzibar. Ngoja tukueleze na kukukumbusha.
Mgogoro wa kiimani Zanzibar ulisababalishwa na Viongozi wa kisiasa ambao walianza kutamka wazi wazi nchi ya Zanzibar ni nchi ya Kiislamu na kupelekea wananchi wa Zanzibar kutengeneza chuki kwa wakristo na kuamua kuchoma makanisa Tukasahau hakuna Zanzibar nchi bila Tanganyika na sheria inasema Taifa letu halina Dini bali watu wake ndio wenye Dini.
Tunatambua wazi asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar ni waislamu ingawa wakristo wapo pia. Zanzibar haijawahi tawaliwa Rais mkristo tokea mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Vivyo hivyo Tanganyika Bara Kuna idadi kubwa ya Wakristo mara 2 au zaidi ya waislamu ingawa Tanganyika kumetawaliwa na Wakristo na Waislamu.
Maasi hayo na mgogoro huo kipindi yanatokea wewe ulikuwa Rais wa Tanzania mwenye Imani ya Uislamu na wakristo hawakurejesha kisasi wakiamini katika akupigaye shavu la kushoto mgeuzie la kulia. Je unawezaje kujisifia kwa jambo kama hilo?
Tanzania kiujumla, Ukristo umegawanyika katika madhebu tofauti tofauti lakini Imani yao wote ni wakristo wanaamini katika Kristo.
Kiimani na kielimu wakristo wamejikita katika Elimu Dunia na Elimu Akhera na ndio maana karibia Mapadree wote ni PhD holders na hata wachungaji na Maaskofu. Kwani katika msingi wa Imani ya Ukristo elimu zote zinaendana.
Katika nchi yetu ya Tanzania kwa bahati mbaya sana Tanganyika haina serikali tumesimama na kuishia kusema sisi ni Watanganyika na tukajiweka ndani ya koti la Utanzania.
Hivyo tukakubali kutawaliwa au kuongozwa na Wazanzibar na Watanganyika wenzetu kitu ambacho tuliamini katika Umoja.
Katika Uongozi, sisi tuko tayari kuongozwa na Wanzibar kwa kuanzia na viongozi wa ngazi ya mtaa, kata, wilaya, Mkoa na hata Taifa. Je Zanzibar kuna Mtanganyika ambaye ni kiongozi au anaruhusiwa kumiliki ardhi?

SISI WACHUNGAJI NA BARAZA LA MAASKOFU TURUDI KWENYE HOJA KUU NA MSINGI JUU YA IMANI ZETU, TUSICHANGANYE DINI NA SERIKALI.

Mheshimiwa Rais mstaafu hongera kwa kutoka hadharani na kutueleza hayo lakini tunakuomba upate kutoa ufafanuzi juu ya maswala yetu ambayo tunahitaji majibu juu ufisadi na upendeleo wa haya yanayoendelea nchini juu ya mkataba wa DP WORLD.

Baada ya Mkataba wa DP WORLD tumeshuhudia yafuatayo yakiendelea katika nchi yetu na upendeleo wa makundi na hata kutugawa
Je uliwahi kutoka na kueleza kama Rais mstaafu mpaka uone BARAZA LA MAASKOFU likitoa msimamo wake nawe ndio utoke na kusema?

Waislamu na Mashekhe walisimama na kumuunga mkono Mhe Rais Samia juu ya uwekezaji wa Bandari uliwahi kujitokeza na kusema wasichanganye Dini na serikali?
CCM walitembea nchi nzima wakiusifia Mkataba na kutoa elimu ya uwekezaji wa Bandari, Uliwahi kutoka na kusema wasichanganye siasa na uongozi wa serikali?
Machawa waliandamana nchi nzima wakiunga mkono uwekezaji wa DP WORLD uliwahi kujitokeza na kusema wasichanganye mahaba na utendaji wa serikali?
Serikali imewabambikia kesi za uhaini watu wasio kuwa na uhusiano wa Majeshi je wewe kama Rais mstaafu uliwahi kujitokeza na kuwatetea kwa kuuelezea umma madhara ya kesi za namna hiyo?

🩸🩸 Iweje leo Baraza la Maaskofu, watetezi wa mali za nchi, Mawakili wanaotaka kutetea rasilimali za nchi pamoja na watu wanaotaka haki na sheria vizingatiwe wawe wahujumu uchumi au waonekane wanakuwa wachochezi au wanachanganya Imani na serikali?

UFISADI UMEKITHIRI.

Mheshimiwa Kikwete nchi yetu kwa sasa haiko salama wala hakuna amani ni kutokana na uongozi wa Chama cha mapinduzi kutokuangalia umuhimu wa usawa na haki kwa Taifa.

Kinachozungumzwa na Baraza la Maaskofu Tanzania sio kukataa Mkataba bali taratibu sheria na kanuni zifuatwe katika kutoa hiyo tenda kwa DP WORLD na sio vinginevyo.
Sheria za ugawaji tenda zitangazwe mashirika yashindanishwe na atakaye shinda tenda birds apewe kulingana na makubaliano serikali itakayoingia na kuwa na mkataba makini na wenye tija kwa pande zote mbili.
Nchi hii ni mali yetu sote kuwepo na haki katika pande zote yaani kwa wanahoji wapewe majibu na wanaotetea walete majibu.
Bunge lisitumie nguvu kubwa katika kuunga mkono hoja za uuzwaji wa Bandari kwa kulazimiashia kuwa sehemu ya wananchi kwa uroho wa fedha na kupoteza utu wao.
Bunge kwenda kupitisha sheria ya umiliki wa ardhi kwa wageni ni kosa kubwa sana bila muswada huo kupitia kwa wananchi ambapo tumeshatambua mchezo mchafu unaofanywa na kikundi cha watu wachache kuonekana wametoa maoni kwa niaba ya wananchi.

Mheshimiwa Rais mstaafu wewe na kikundi cha baadhi ya familia za watu wachache katika nchi hii sio wasafi na tunajua unatoka hadharani kutetea ugali wako tunaomba uwe muwazi na mkweli.
Takwimu zinaonyesha wewe ni sehemu ya mnufaika wa baadhi ya Ghati pale Bandarini ambapo ulikuwa ukivuna mapesa mengi kupitia TICTS na hata hapa unatetea ugali baada ya kuona mambo magumu na ikiwa kanisa litasimamia msimamo wake nawe utakosa.
Katika uongozi wako ufisadi mwingi umetokea ukiwemo wa RICHMOND na Escrow je uliwahi kusema au kuomba radhi kwa wananchi.

Wewe sio msafi hata kidogo katika jambo hilo na huwezi kuwa msafi kwa kauli hii uliyoinena Leo.

Wewe ndio mchonganishi na mwenye kuingiza au kutaka kujimilikisha siasa na uongozi na kutugawa sisi kama wananchi.
Sisi kama viongozi wa Dini jukumu letu ni kusimamia amani na mshikamano kama vitabu vyetu vinavyotuongoza.

Mkataba wa DP WORLD hauna viashiria vya amani wala umoja kwa Taifa letu. Ikiwa Rais ni Mzanzibar, Waziri aliyeingia Mkataba ni Mzanzibar na Katibu mkuu wa wizara husika ni Mzanzibar.

Inaonyesha katika utendaji kazi wako unatuheshimu nasi tutakuheshimu kuwa mkweli na muwazi kwetu usiwe na kauli mbili.

Katika mambo ya Muungano Bandari sio jambo la Muungano iweje haya yatokee nankutendeka?

Nakushauri kuwa mshauri mwema na sio mtu wa mihemko na tamaa za mwili na akili kwa kutaka kuuza Tanganyika na mali zake. Mshauri Mama Samia vyema juu ya mkataba wa Bandari haufai hatuko tayari kuona tunakuja kuingiza kizazi chetu machafukoni na kwenye ulipaji wa madeni kwa DP WORLD.

Mbona ni mengi yametokea, Loliondo, KIA na hatujasikia umetoka kukemea au kuwakemea wahusika why hili?

Sisi tutasimama imara na tutasema kwa sababu kazi za kichungaji ni kutunza amani na kueleimisha jamii kimaadili.

Asante
Tuipende nchi yetu kama Taifa teule la Mungu
Ni mimi Mzalendo toka Ughaibuni kunako Amani na Upendo.
JamiiForums1315008447.jpg
 
JK alitumwa apime upepo, Mama mwenyewe hata kuongelea DP World hataki, hii kitu bila shaka imewashangaza hata CCM wenyewe, huu muunganiko wa Watanzania kukataa hii kitu kwa umoja hivi sidhani kama ishawahi tokea huko nyuma.
Bila shaka majibu ya Dr. Shoo yamemfikia.
 
Ukweli ni kwamba wanapigwa za uso kila kona wanayoelekea.

Mzee Shoo alieleza kiusomi na kifalsafa ya hali ya juu sana.

Na nilimuona Rais wetu alivyokuwa kwenye wakati mgumu ndani ya lile kanisa wakati akipewa za uso na Askofu Shoo.
 
Hivi vitu hata Yesu alishindwa kuvvitenganisha...Mafarisayo na Masadukayo waliamua kumuuwa shauri alikuwa hawavumilii.

Alifikia hata kupindua meza za wakusanya kodi kwenye masunagogi.

Sembuse hawa maaskofu?
Herode alitaka kumuuwa Yesu
 
viongozi wa dini ya kiislamu Wana shida kubwa zaidi kuliko viongozi wa dini nyingine.

#ccm
#2023
 
Back
Top Bottom