Kikwete to USA (May 2009)

Matunda yapo, unataka tuanze kuzitaja?
1. Safari ya Bush TZ na Millenium.....
2. Kupata Misaada (soma MIKOPO)
3.
4
5.....

Aaah Kikwete nae kazidi kujifanya celebrity, basi anaona raha hii kutembea na kukutana na viongozi wa nchi matajiri na kupiga picha nao tu, nafikiri hakuna kiongozi wa Afrika anaemshinda kwa hizi safari za nje. Mwamsheni kuwa yeye ni raisi wa nchi masikini hiyo misaada kwa sasa anaweza kuiombea kwa simu tu viongozi wote wa nchi tajiri na hao watoa misaada na wawekezaji si ameishakutana nao mara nyingi tu na weshamjua tayari sasa kuna umuhimu gani tena wa hizi safari au anazipenda tu?, kama ni hivyo ajilipie mwenyewe asituletee ufisadi wa kiaina.
 
FMES,
Mimi nina wasiwasi na mahala pa kuwapeleka hawa Magaidi..Hizi habari za Muslims na kumtaja Kikwete kusaidia wala sidhani (kamba) kwa sababu hana sifa hizo wala sii Ulamaa wa kusikilizwa. Kuna kitu...Mtakuja nambia..
 
FMES,
Mimi nina wasiwasi na mahala pa kuwapeleka hawa Magaidi..Hizi habari za Muslims na kumtaja Kikwete kusaidia wala sidhani (kamba) kwa sababu hana sifa hizo wala sii Ulamaa wa kusikilizwa. Kuna kitu...Mtakuja nambia..

- Bob you are right on the money bro, hapa something is up!

FMES!
 
Leokweli,
Binafsi sii mtu wa upande wa kushoto na sipendi kabisa mbinu zao ktk maendeleo ya mtu maskini kwani siku zote tunawajaza matapeli nchini.. Strong leadership kwa nchi maskini hutokana na msimamo unaowekeza kwa wananchi wake kuunda jamii ambayo itaendesha uchumi wetu kwa karne zijazo na sii kutegemea wageni wasiweza hata kupata uraia wa nchi mbili..meaning at one point ni lazima wajikate!
Ukisoma kwa makini mawazo ya Jasusi ni mawazo ya kila Conservative, kwamba siku zote kizuri hujiuza na mwanamke anayejipenda mara nyingi hupata wachumba lakini sio umalaya kama huu unaofanyika.
Na siamini kabisa kazi ya rais kutembea na wafanyabiashara kwa sababu rais ni mtu anakwenda kufunga mkataba wa kibiashara na kukaribisha uwekezaji ktk sekta ambazo ni muhimu kwetu ktk kupata soko la nje..

Mara nyingi tunasahau kwamba Wageni wanapokuwa nchini iwe Saudia kulima mpunga nchini kinachohesabika ni kwamba mchele huo ni made in Tanzania na tunasafirisha nje.. Kodi yetu haiwezi kubadilika kama atakuwa Mtanzania au Mgeni na uwezo wa serikali kukusanya zaidi utatokana na soko tutakalo pata nje..Lakini kama Watanzania wenyewe wana uwezo wa kulima na kinachowashinda ni zana za kilimo nashindwa kabisa kuelewa kwa nini serikali ipo radhi kununua mashangingi na misafara kama hii kutafuta waarabu kuja kulima mpunga ktk eneo ambalo sisi wenyewe tunaweza kabisa kulima na kutosheleza soko la Saudia..
Kwa nini JK asiweke mkataba na Saudia ktk ununuzi wa mchele toka Tanzania na sisi tukajipanga kuweza ku supply demand yao!..Navyofahamu mimi ktk ubepari viongozi wa nchi huweka mikataba kama hakika ya mwanzo ya mauzo ushirikiano wa Kibiashara na sio kutembea na wafanyabiashara wadogo wanaotembea na sample mikononi kutafuta soko nje..Kwa mfano Prime minister wetu alikwenda UK, China na US kuweka mkataba wa kuuza mbao zetu huko jambo ambalo limekuwa likipigwa vita sana na wananchi wa nchi hizo..Lakini sikuona Priminister wetu akiandamana na wanamisitu au wwenyeji kujipanga na wanunuzi ktk zikao vyote.. Prime Minister alijua uwezo wetu ktk kusupply na wao walijua ni kiasi gani cha mbao zetu wanazihitaji ukiondoa supplier wengine..
Hivyo kazi inabakia kwa wakulima (wanamisitu) kuweza kuzalisha kiwango kinachotakiwa na kama ikitokea wamezalisha Zaidi au Pungufu serikali huwapa wakulima subsidy kutokana na hesabu zinavyo fahamika lakini sii kwetu..

Zamani enzi za mwalimu Tanzania ilijulikana duniani kwa mass production ya Sisal, Cotton, Coffee beans, Korosho na kadhalika hivyo hapakuwa na haja kabisa yetu sisi kujitangaza isipokuwa tulipeleka mali zetu sokoni. Utamaduni huo ulikufa baada tu ya Ujamaa kufa na hasa pale bei za bidhaa hizo ilipoporomoka.. Leo hii hatuna bidhaa yoyote ambayo tunaweza kujivunia au kuitangaza nje.. na sidhani kama JK anaweza kutafuta soko la kitu chochote wakati hana uhakika wa uzalishaji wake nchini.

Mimi nashindwa kuelewa kwa nini tumeacha Kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wetu. Sioni ndani kabisa kama alivyosema Jasusi..Unless Muungwana anataka kunambia hata kufua umeme, kusambaza gas yetu tunahitaji msaada au mwekezaji toka nje. Ni kitu gani hasa anacho shop nashindwa kuelewa kwani hao kina Johnson ni wababishaji tu biashara zao za Kariakoo - zinafanyika South East ya miji mingi ya US..
Til now, can't stop wondering kuna kitu gani ambacho sikifahamu kitatokana na misafara hii!..

Nakubaliana na mambo mengi unayoyasema. Kwenye maswala ya Kilimo ninadhani sera za mikopo mingi ambazo nchi masikini tunapewa haziruhusu subsidy kwenye kilimo. Kwahiyo unakuta conditionality nyingi ziko against maendeleo ya sekta ya kilimo which in large inachangia kutokua kwa hiyo sekta. Bado hakuna invesment za kutosha katika kilimo, maana kilimo bora sio trecta na mbolea tu, it need irrigation Technology , Utunzaji, Ukoboaji nk

I think sio wazo zuri sana kuwauzia wasaudi ardhi but nadhani hiyo ndio inaweza ikawa turning point ya kilimo Tanzania, kama tunaweza kuwa na negotiator wazuri katika meza amabpo watalazimisha wasaudi wafanye technolgy sharing/ subcontracting kwa wakulima wa nyumbani , I think that will be very good kwa wakulima wa local.

Pili kama investment ya dola billioni 3.5 kwenye kilimo itakuja Tanzania ina maana competation itaongezeka katika wauzaji pembejeo na kuzifanya zipatikane kwa bei nafuu sana.

Sisi tunaweza kulima lakini hakuna mtu anaweza kukukopesha Dola billioni tatu uwekeze kwenye kilimo, Is too risky business.

Chamuhimu ninadahni ni vizuri tufanye kama proction sharing zinazofanywa nchi kama botwana kwenye madini, maana yake ni kwamba tunakuwa na shares katika hiyo kampuni ya wasaudi which means we get Tax and devidend
 
Msemaji wa Obama alisema hivi kabla ya mkutano
WASHINGTON (AFP).

Before the meeting, Obama's spokesman Robert Gibbs said the two leaders would discuss regional security and terrorism.

"I think regional concerns like economic development and health will also be on the agenda," Gibbs said.

"I think the president obviously will continue his outreach in the lead-up to his speech in Cairo with continued outreach to elected Muslim leaders like the president."


Obama, who traces part of his ancestry to Kenya, will also concentrate on sub-Saharan Africa during a stop in Ghana in July, but has not yet fleshed out his administration's policy towards the continent in detail.

The US president is due to give a major speech to the Muslim world in Egypt on June 4, and has been attempting to engage Muslim leaders and their populations since taking office.

Politico wanaripoti kilichozungumzwa,
The President and President Kikwete met this afternoon and had a valuable discussion on a range of issues. President Obama expressed his appreciation for the close bilateral relationship the United States shares with Tanzania.

President Kikwete and the President exchanged views on approaches to enhancing the U.S.-Tanzanian partnership, improving development policy in the fields of health, education, and agriculture, and working with other partners in the region to solve some of the most pressing conflicts on the African continent.

President Obama and President Kikwete expressed a desire to work together to solve common problems in the future. This was the first African Head of State to visit President Obama at the White House
 
Hiyo picha inaonyesha JK na list yake sijui ilikuwa na misaada mingapi inayoombwa!!

Yaani ninauhakika kabisa safari ya week nzima marekani iliyojumuisha mkutano wa dakika 5 na Obama ni hasara kubwa mno kwa nchi yetu. Nina uhakika zaidi ya $1.5 million zimetumika ambazo zingeweza kabisa kujenga zahanati kwenye wilaya 20 nchini.

Mungu tubariki na hizi ziara za kutembelea viNGO nchi za nje.
 
Disclaimer ya WhiteHouse iko vipi:

This official White House photograph is being made available for publication by news organizations and/or for personal use printing by the subject(s) of the photograph. The photograph may not be manipulated in any way or used in materials, advertisements, products, or promotions that in any way suggest approval or endorsement of the President, the First Family, or the White House.
 
nawao wanatuomba tusiwape iran uranium. Nyie mbona mnapenda kudharau nchi yenu kiivyo..lol
 
Nilikuwa najiliza jk ataonmgea nini na obama...maana ni vichwa viwili vinapishan sana kifikra na ki IQ..angalieni hapa JK ana desa aliloandaliwa na akian Salva....hata maongezo ya kawaida ana desa...alafu Obama anamshangaa tu....
attachment.php
 

Attachments

  • pres.jpg
    pres.jpg
    71 KB · Views: 135
Nimesoma na kuona kule kwa michuzi Vasco anaendelea kuvumbua whit House. Ila nimecheka sana baadaye kuhuzunika na kufedheheka sana. Kajamaa DESA NJENJE sijui kaandikiwa nini cha kuongea na Obama ama alikuwa antoa speech kwa Obama. au alikuwa darasani anakopi mambo mihimu sasa sijui akilia yake mkuu imechoka hata mazungumzo ya watu wawili tu still kabrasha la MADESA!!
 
Ghailani,Mimi nadhani JK amewekwa kwenye "schedule" ya kukutana na rais Obama whishono kwasababu ya issue ya huyo mTanzania atakayefikishwa mahakamani.

Kumbukeni kwawmba, JK anatafuta nchi za kuwapeleka hawa ma"detainees" ili afunge Guantanamo.

Kwahiyo JK anaweza akaombwa amchukue huyo "detainee" aje amalizie kifungo chake Tanzania.




Ili i'sound vizuri, nadhani hapo kwenye bluu ulimaanisha OBAMA.

Nadhani kimsingi kwenye hoja yako kuna ukweli mkubwa.
 
Kwa mujibu ya matangazo ya bbc idhaa ya kiswahili yanayosikika hapa dar es salam,

jk atakutana na obama ikulu ya marekani, ambapo watazungumzia maswala mbalimbali yanayohusu nchi zetu

kikwete anakuwa rais wa kwanza wa afrika kusini mwa jangwa la sahara kukutana na obama

Anathibitisha kuwa yeye ni Vasco da Gama mvumbuzi wa karne ya 21. Pili anaongoza kww UMATONYA UGHAIBUNI. na anajivunia hilo. Ona ana list kibao ameandika request kibao mpaka kamchanganya Obama kabakia ameduaaa What a president!!! (picha ya kukutana kwake na Obama)
 
People relaaax!,

Prez Obama just posed na anasikiliza, si kama anamshangaa, kah!. Although, it'll be interesting to know what's in that paper Prez Kikwete is holding.
 
Nimesikitishwa na prezidaa kudesa hata katika light talks na Obama, wadanganyika tuliliona hili, wengine tulimwambia Prezidaa wetu ajiandae vizuri anapoenda kukutana na Obama, kile ni kichwa kizuri, hakuna ubabaishaji na hafla zisizo na tija pale.

Haya sasa hayo ndiyo matokeo yake. Next time do your home work braza!!!
 
Wakuu mimi nikimuangalia vizuri Obama nikama anamshangaa sana Da gama! Nikama ana ona maajabu Huyu kweli Raisi!! mbona hamna kitu! anajaribu kutafuta cha angalau kuweza kumuelewa waapi! hebu angalieni kwa makini jamani... ni kweli!
 
mi huwa namshangaa sana huyu jamaa.( presidaa wetu)

unajua kwa wabongo wengi tunaona dili sana kwa vasco kukutana na obama,
kwanza alipokelewa na mayor,
leo obama aje hapa bongo yule mayor wetu anaweza kwenda kumpokea na kikwete yupo bizy na KAZI?
tutake tusitake huyu wetu ana upe mdogo wa kufikiri. huwezi kwenda nje kutembea wakati kwako kuna matatizo. sawa hatukatai safari lakini awe na mipango na nchi yake, leo yuko marekani akirud hapa hamalizi wiki mtasikia huyooo kachomoka!!
ANAMCHOSHA SANA SHENI KILA SIKU SHENI ANAMSINDIKIZA AIR PORT!!
 
dailyhabari

Michuzi kaweka transcript ya maongeazi.. BO kamsifia sana JK na serikali yake na alikua anataka kujua atasaidiaje Africa kiuchumi na kuondoa conflicts... Amemuagiza Hillary afuatilie na ameomba JK atoe recomendations and that is what he did and will continue to do since its an on goin process. Kasema yeye amekuwa wakwanza kumuona kwasababu ya utawala bora.. (many here disagree) lakini compare with the rest of this continent and then ongea tena..! Katika nchi zaidi ya 50 I'm sure tuko top 5 kwa 'good governance' so its not such a bad thing. Mimi nashangaa mmemuattack sana.. JK on this, eti Vasco... that made my day though,too funny.. JF.. nakupenda

Truly URs K.
 
dailyhabari

Michuzi kaweka transcript ya maongeazi.. BO kamsifia sana JK na serikali yake na alikua anataka kujua atasaidiaje Africa kiuchumi na kuondoa conflicts... Amemuagiza Hillary afuatilie na ameomba JK atoe recomendations and that is what he did and will continue to do since its an on goin process. Kasema yeye amekuwa wakwanza kumuona kwasababu ya utawala bora.. (many here disagree) lakini compare with the rest of this continent and then ongea tena..! Katika nchi zaidi ya 50 I'm sure tuko top 5 kwa 'good governance' so its not such a bad thing. Mimi nashangaa mmemuattack sana.. JK on this, eti Vasco... that made my day though,too funny.. JF.. nakupenda

Truly URs K.

Tatizo kubwa la Watanzania walio wengi wana mawazo kama yako Kinyambiss..........Na hapo ndipo tunapogundua kwamba bado tuna safari ndefu sana!
 
Back
Top Bottom