Uchaguzi wa USA Leo

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
TAREHE 8/11/2016 NI SIKU YA KUAMUA NANI AWE RAIS WA MAREKANI KATI YA HILLARY CRINTON NA DORNALD TRUMP.

•Na ujue mfumo wa electoral college unaoamua nani atakaye hudumu white house.. Kama raisi wa USA (next Potus to white house at Washington D.C)

Na: COMRED MBWANA ALLYAMTU

Siku ya Jumanne Novemba itakuwa ni tarehe 8/11/2016 ni siku ambao dunia nzima itageuza masikio na macho yake kuangazia taifa kubwa duniani la marekani ambao litakuwa linatimiza wajibu wake wa kikatiba wa upigaji kura wa kumtafuta mrithi wa Obama. Katika katiba ya marekani iliyopitishwa mwaka 1789 huko Philadelphia imelibainisha shughuri Hii inayofanyika leo huko marekani katika katiba sehemu ya II sura ya Tatu.... Katika uchaguzi huyu unatazamwa kama uchaguzi muhimu katika duru za siasa duniani kutokana na nafasi ya ushawishi wa marekani katika sayari ya dunia.

Baada ya muhula wa Rais kumalizika nchini Marekani ndio siku Wamarekani huitumia kuchagua na baadae kuamua nani awe Rais wa Taifa hilo lenye nguvu kubwa kijeshi na kiuchumi Duniani. Hivyo ndio maana Tarehe 08 Novemba, 2016 siku ya Jumanne Wamarekani karibu milioni 120 wanaitumia kumiminika katika vituo vya kupiga kura kutimiza wajibu wao wa kikatiba ili kumpata Rais wa Taifa lao ambayo kimsingi ndio kiongozi wa Juu kabisa katika taifa hilo kubwa kiuchumi na kijeshi duniani. Wamarekani wanachagua Rais wao wa 45 tangu kuasisiwa kwa Taifa hilo mwaka 1776 na kuwa jamuhuri rasmi mwaka 1789 pale George Adam Washington alipo chaguliwa na kongamano kuu la taifa (National Electoral college) kuwa raisi wa kwanza wa taifa hilo.MAREKANI ni taifa lenye umri wa takribani miaka 239 tangu ipate uhuru wake toka kwa Mwingereza mwaka 30/6/1776. Na kuwa jamuhuri rasm mwaka 1789 chini ya rais wa kwanza Georg Adam Washington kijana msomi kutoka katika jimbo la Viginia.

Pamoja na ukomavu huo wa kisiasa nchi hiyo imekuwa ikipokezana vijiti katika uongozi bila kuwepo na kashi kashi yoyote kwa mda huo wote.siasa ya vyama ilianza mwaka 1801 wakati wa utawala wa Thomass Jeffason ambaye alijuwa Rais wa 3(tatu) wa Marekani. Toka hapo Kumeapishwa marais 43, na kumekuwa na marais 44, kwa sababu aliyekuwa rais Grover Cleveland alihudumu mihula miwili isiyofuatana, na kwa hivyo anahesabiwa mara mbili, kama rais nambari 22 na nambari 24. Marais wanne walifariki kawaida wakiwa mamlakani ambao ni William Henry Harrison, Zachary Taylor, Warren G. Harding na Franklin D. Roosevelt mmoja akajiuzulu ambaye ni Richard Nixon na wengine wanne wakauawa ambao ni Abraham Lincoln, James A. Garfield, William McKinley na John F. Kennedy. Rais wa kwanza wa Marekani alikuwa George Washington, aliyeapishwa 1789 bada ya kupigiwa kura na wajumbe wote katika kongamano. Na William Henry Harrison alihudumu kwa muda wa siku 31 pekee, mwaka 1841 na ndiye raisi aliyeudumu kipindi kifupi zaidi nchini marekani naye Franklin D. Roosevelt akahudumu kwa muda mrefu zaidi kuliko wote, kwa karibu miaka 12. Rais wa sasa in Barack Obama, aliyeapishwa 20 Januari 2009.


Toka mwaka 1789 kumekuwa na utaratibu wa kumpata raisi Wao kwa njia za kidemokrasia kwa mda mrefu sasa Katika uchaguzi huu Mshindi ndie ambaye atapokea mikoba ya uongozi kutoka kwa Rais wa 44 anayemaliza muda wake January mwaka 2017 Barack Hussein Obama anayemaliza utawala wake wa miaka nane. Kama ilivyo kawaida kwa chaguzi za Marekani wagombea kutoka vyama viwili vikubwa gani Democratic na Republican huchuana vikali kwani hivi ndio vyama vikubwa vyenye ushawishi katika siasa ya marekani Karibu miaka 100 sasa. Katika upande wa wagombea kuna mwana Mama Hillary Rodham Clinton mwenye umri wa miaka 69 wa chama cha Democrat anachuana vikali kabisa na Bilionea Donald John Trump mwenye umri wa miaka 70 wa chama cha Republican.

Kama ilivyotokea wakati anachaguliwa Rais wa sasa anayeondoka Barack Hussein Obama ambapo historia iliandikwa kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa kwanza mweusi vivo hivyo mwaka huu inatarajiwa kuandikwa historia nyingine ambapo kama Hillary Clinton ataibuka mshindi basi atakuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kuchaguliwa kama Rais wa taifa hilo kubwa na lenye ushawishi Duniani. Uchaguzi huu una mvuto wa aina yake kwa wafuatiliaji wa siasa za Marekani na hasa ukichagizwa na misimamo binafsi ya wagombea pamoja na mitazamo yao kuhusu Mahusiano ya Marekani na mataifa mengine Duniani, Sera za kigeni, Ulinzi, Ugaidi, Suala la Uhamiaji, Ubaguzi, masrahi ya taifa na Maadili. Haya yamewagusa na kuwavutia wengi ndani na nje ya Marekani kwa ama kuyaunga mkono ama kuyapinga.

Wachambuzi wa siasa za Marekani wanautaja uchaguzi huu kuwa ni uchaguzi baina ya mwanasiasa bobezi na mwanadiplomasia mahiri wakimaanisha Mama Hillary Rodham Clinton ambaye aliwahi kuhudumu kama kiongozi wa taifa hilo katika nafasi ya waziri wa kigeni, dhidi ya Mfanyabiashara mkubwa na Bilionea mashuhuri wakimlenga Donald Trump. Wagombea hawa wawili ndio mashuhuri zaidi duniani katika siasa za uchaguzi kwa takribani miaka 5 kwenye uchaguzi huu kutokana na jadi ya Marekani ambapo vyama viwili vya Democrat na Republican huchuana vikali. Mpaka leo asubuhi Kura za maoni zimeonesha kwa kiasi fulani wagombea hawa wamekaribiana ingawa Hillary Clinton anaongoza kwa asilimia 4 na anapewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika uchaguzi huu. Japo Bado hali ni ngumu katika uchaguzi huu.

katika siasa ya marekani leo takribani wapiga kura milioni 120 watapiga kura kitu kitakachopelekea Mmoja wapo kati ya wagombea wawili Hili litatokea tu pale mmoja wapo atakapo pata ungwaji mkubwa kutoka kwenye wajumbe 538 wanaoamua nani awe Raisi wa taifa hilo.
1478610167498.jpg


TUANGAZIE MFUMO WA UCHAGUZI NCHINI MAREKANI.

Ni namna gani wajumbe maalumu 538 ndio wanaamua nani awe Raisi wa marekani?......

Uchaguzi nchini Marekani ni tofauti na chaguzi za nchi nyingine nyingi Duniani. Japokuwa marekani imekuwa taifa linalojinasibisha na mfumo wa demokrasia ya maamuzi kutoka kwa raia wengi lakini marekani imekuwa sivyo hivyo kwani marekani Mshindi wa uchaguzi wa Marekani hapatikani kwa wingi wa kura za wananchi yani (popular votes) bali huamuliwa na wajumbe teule 538 ambao hawa ndio baada ya wananchi kuchagua wao huamua nani awe raisi wa taifa hilo. Utaratibu huu huitwa kura za wawakilishi wa majimbo yani (Electoral College). Electoral College ndio huamua nani awe Rais wa Marekani.

Je mfumo huu wa Electoral College ni nini? Inapatikanaje na inafanyaje kazi kwa mfumo upi?...

•Electoral college ni nini?.... Hi ni jukwaa maalumu la wateule ambao limetajwa kikatiba katika katiba ya marekani "ibara ya Pili sehemu ya kwanza."... Kimsingi wateule Hawa ni wajumbe ambao hutokana na idadi maalumu ya kila jimbo kati ya majimbo 51 yanayounda taifa la marekani katika nchi hiyo ambayo kiujumla wake ni wajumbe 538. Wajumbe Hawa ni waamuzi wa nani anayetakiwa kuwa mtawala wa taifa hilo yani (Potus state )... Na idadi ya wajumbe hutokana na kutegemea Idadi ya wakazi wa eneo husika (electoral population status) mfano jimbo la California lina idadi tofauti na jimbo la Maryland.... Pia wajumbe hao wateule hutegemaidadi ya wabunge ambao kura yao ni 435 maseneta 100 na Washington D.C kura 3 ambazo ukijumuisha unapata (538) Kama nitakavyo eleza Namna ya kuwapata wajumbe hao pia ndio waamuzi wanaoitwa wafia nchini..(wafia taifa)....

Tofauti na uchaguzi wa Magavana wa Majimbo 51 ya marekani yani (State Governors), au wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (Members of US House of Representatives) ama Wajumbe wa Baraza la Maseneta (US Senate) ambapo wananchi hupiga kura moja kwa moja kwa mgombea kwa kuwachagua katika utalatibu wa kawaida gani (direct vote) lakini kwenye nafasi ya Urais wa Marekani wapiga kura hawapigi kura moja kwa moja kwa mgombea wa uraisi wa nchini yao bali hupiga kura ambazo zitapelekea kupata wateule 538 kisha wateule hao ndio uhusika na shughuri nzima za kuchagua nani anaekuwa raisi wa marekani. Hivyo wajumbe wa kura za majimbo (Electoral College) ambao hao ndio chombo cha kikatiba kinachoamua nani awe Rais wa Marekani.Utaratibu wa kura za Majimbo (Electoral College) ni wa jadi na umekuwepo tangu 1787 na umeelezwa katika (Ibara ya Pili sehemu ya Kwanza ya Katiba ya Marekani.)

Zipo sababu kadhaa ambazo zinatajwa kwamba ndio zilisababisha waasisi wa Taifa la Marekani katika kongamano la uhuru na badae la katiba ( Philadelphia convention 1785) kuweka utaratibu huo lakini kubwa zaidi inaelezwa kuwa ni kuzuia uungaji mkono wa udikteta wa kigeni na pia kuzuia kuibuka kwa viongozi pandikizi kutoka kwa mataifa maadui. Pia waliami mfumo huu ni bora kupata kiongozi mwenye kuheshimu masrahi ya taifa lao... kwani Wao huamini....kuwa "Sio kila MTU anaweza kufanya maamuzi ya taifa hata hivyo maamuzi ya taifa ni fursa ya watu wachache"

Katika utaratibu huu kila jimbo katika majimbo yote 51 yanayounda United States of America (USA) na Wilaya ya Columbia (District of Columbia) ambayo ni eneo muhumu kiutawawala nchini marekani, katika kila jimbo huwa na idadi fulani ya wajumbe wanaoliwakilisha jimbo katika kuunda wajumbe maalumu wateule (Electoral College) jumla ya wajumbe wote ni 538 wanaoamua nani awe Rais wa Marekani. Kati yao wajumbe 435 hutokana na kura zinazotokana na Baraza la Wawakilishi (US House of Representatives), wajumbe 100 hutokana na kura za Baraza la Maseneta (US Senate Congress) na wajumbe 3 hutokea Wilaya ya Columbia yani District of Columbia (D.C). Ili mgombea yeyote aweze kushinda nafasi ya Urais wa Marekani ni lazima upate kura za wajumbe 270 wa Electoral College ambazo ni sawa na (50% plus 1) ya idadi jumla ya wajumbe 538 wanaoamua nani awe Rais wa Marekani.

Ndio maana tunasema; katika watu milioni 120 watakao piga kura leo tarehe 8/11/2016 leo Wamarekani huchagua kwa kupiga kura ya popular vote (kura ya jumla) lakini ni watu 538 pekee tu kutoka kwa wateule maalum (National electoral college) ndio watakao amua nani atakuwa raisi wa USA (next potus).... Kimsingi Unaweza kupata kura nyingi za wananchi (popular votes) lakini usipopata kura 270 za wajumbe wa kura za majimbo (Electoral College) huwezi kuwa Rais wa Marekani. Kwani jopo hilo ndio Wanaoamua nani awe Rais wa taifa lao. Ni kwa muktadha huo ndio unaona wakati wa kampeni za lala salama wagombea wote wa Democrat na Republican walikuwa wakichuana zaidi na kupigana vikumbo kufanya kampeni kwenye majimbo yale yenye wajumbe wengi wa electoral college ili kuweza kujiongezea ushindi katika kinyanganyiro hicho. Majimbo kama California, Texas, Florida, New York, Pennyslvania, Ohio, Michigan, North Carolina ambayo yana wajumbe wengi wa electoral college ndio yamekuwa yakilengwa zaidi na wagombea wa Democrat na Republican ili kupata idadi ya kutosha ya kura 270 ya wajumbe maalumu 538 Ili waweze kupata kura zinazohitajika kushinda Urais wa Marekani.

Mgombea atakae ongoza kwenye jimbo husika basi hupata kura zote za wajumbe wa electoral college wa jimbo hilo na ikiwa atapata kula nyingi katika majimbo Mengi Basi atakuwa na wajumbe wengi wateule wa (Electoral College) kitu kitakacho muhkikishia ushindi mwembamba katika kongamano maalumu la taifa gani ( national delegate council) hivyo ni lazima wapiga kura wapige kura kwanza wajitokeze kwa wingi na kupiga kura kwa wagombea hao kwani kura za raia ndio zitakazo pelekea kupata idadi ya wajumbe wateule. Mfano ikiwa mgombea moja wapo atapata kura nyingi kutoka kwa wananchi Basi atakuwa na idadi kubwa ya wajumbe wateule wa (electoral college) hivyo na kumfanya kushinda kiurahisi.

Katika kinyanganyiro hichi chochote kinaweza kutoka japokuwa bibi HILLARY Clinton amekuwa akiongoza kutokana na matokeo ya asali ya kura za maoni. Pamoja na yote Bado msuguano ni mkali sana kwa wagombea wote waili na msuguano huyu unaonesha bibi Hillary Clinton akimuacha Dornarld Trump
Kwa Karibu asilimia 4%... Hivyo dunia yote sasa macho yako Washington kutazama nani ni mrithi wa Obama

Kila la kheri Wamarekani katika uchaguzi huu na kila la kheri wajumbe 538 wa Electoral College mtakaoamua nani awe Rais wa 45 wa Marekani. Nawatakiwa upigaji kura Salama na kuwaombea muhitimishe Salama.....

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu

copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
1478610137347.jpg
1478610149518.jpg
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.

Leo ndo leo na asiye na mwana aeleke jiwe.

Leo ndo siku pekee ambapo dunia nzima husimama kuzunguka kwenye mhimili wake hadi hapo uchaguzi wa taifa bora kabisa katika historia ya uhai.

Hata wale wanaojifanya kuiponda USA leo wataacha kufanya yao yote na kutega masikio na macho yao kusikilizia na kuona nani atachinjwa na vichinjio vya Wamarekani.

USA ndo dunia na dunia ndo USA. Hilo halina mjadala.

USA baby
upload_2016-11-8_8-14-20.png
upload_2016-11-8_8-14-22.png
upload_2016-11-8_8-14-23.png
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.

Leo ndo leo na asiye na mwana aeleke jiwe.

Leo ndo siku pekee ambapo dunia nzima husimama kuzunguka kwenye mhimili hadi hapo uchaguzi wa taifa bora kabisa katika historia ya uhai.

Hata wale wanaojifanya kuiponda USA leo wataacha kufanya yao yote na kutega masikio na macho yao kusikilizia na kuona nani atachinjwa na vichinjio vya Wamarekani.

USA ndo dunia na dunia ndo USA. Hilo halina mjadala.

USA baby View attachment 430983 View attachment 430984 View attachment 430985
piga kura ukimaliza utupe maendeleo ya uchaguzi
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.

Leo ndo leo na asiye na mwana aeleke jiwe.

Leo ndo siku pekee ambapo dunia nzima husimama kuzunguka kwenye mhimili wake hadi hapo uchaguzi wa taifa bora kabisa katika historia ya uhai.

Hata wale wanaojifanya kuiponda USA leo wataacha kufanya yao yote na kutega masikio na macho yao kusikilizia na kuona nani atachinjwa na vichinjio vya Wamarekani.

USA ndo dunia na dunia ndo USA. Hilo halina mjadala.

USA baby View attachment 430983 View attachment 430984 View attachment 430985
bado tu?
 
Back
Top Bottom