Jason Bourne
JF-Expert Member
- May 11, 2011
- 200
- 438
Mtakumbuka wiki tatu zilizopita niliwaambia kuwa USA na Ulaya zimetoa karipio na kuagiza hatua zichukuliwe dhidi ya wizi huu, Rais JK aliahidi kulishughulikia, akiwa njia alifanya mabadiliko ya ghafla kwa mwendesha mashtaka na wakuu wengine wa idara,
Someni nilichowaambia.
Sasa leo, rais anawasili USA, pamoja na mambo mengine ya kiserikali rais atakutana na Wakuu wa kanda ya Afrika wa USA na Ulaya na kuwaambia hatua aliyofikia kushughulikia mgogoro huu unaoelekea kuiangusha serikali yake.
Kabla ya mtu, kulikuwa na mtu, na baada ya mtu kuna mtu.
Hutaki, Unaacha!
===================================
Someni nilichowaambia.
Kufuatia hali ya ufisadi nchini kushamiri tangu enzi za serikali ya BWM na serika ya JK kuingizwa madarakani kwa nguvu ya ufisadi kitendo kinachoifanya serikali ya jk kutoonyesha uwajibikaji wowote juu ya ufisadi nchini,
Washington na Ulaya walimuweka kitako jk majuzi baada tu ya kufika USA, Wakuu wa kanda ya Afrika wa USA na Ulaya walionyesha kukerwa na hali ya mambo nchi Tz huku kukiwa hakuna juhudi zozote za kupambana na ufisa,
Mabadiliko yaliyofanywa pccb na dpp ni pressure ya Ulaya na US kwa JK kuhusu vita ya ufisadi
USA ilikuwa ikitambua kuwa felishi ameonekana akilinda ufisadi tangu epa kaondolewa
Sahivi Hossea atakuwa amefurahi, maana wabaya wake ndani ya DPP na PCCB wote wametolewa
Sasa leo, rais anawasili USA, pamoja na mambo mengine ya kiserikali rais atakutana na Wakuu wa kanda ya Afrika wa USA na Ulaya na kuwaambia hatua aliyofikia kushughulikia mgogoro huu unaoelekea kuiangusha serikali yake.
Kabla ya mtu, kulikuwa na mtu, na baada ya mtu kuna mtu.
Hutaki, Unaacha!
===================================
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameondoka Jumatatu usiku kwenda Marekani kuanza ziara ya wiki mbili nchini humo.
Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu, ilisema Rais atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York pamoja na kuhudhuria mikutano muhimu Washington, D.C.
Akiwa Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 iliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi Oktoba Mosi. Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia baraza hilo.
Septemba 25. Pia atakuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu mazingira (CAHOSC) ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon.
Chanzo: Mwananchi