Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Mtanzania unachoongea naona ni nadharia tu, kwenye topic hii na kule kwa makala ya Ngurumo.

Unajua kwa nini CCM na JK wake walishinda kwa kishindo? JK ni sifa zake binafsi: handsome boy and easy-going. CCM inatumia mtandao wa dola uliopo nchi nzima kwa faida yake. Pia usisahau wananchi wanavyoiogopa dola. Wamesahau au hawajui kama dola inatakiwa iwatumikie wao (owner of an organisation vs manager of the organisation).

Wenye nchi wana nguvu kubwa mikononi mwao ila hawajui kuitumia ipasavyo. Nguvu hiyo ni kura.

Uongozi ni mfano. Mimi sijui wewe unafanya nini in real life. Ila nitashangaa kama utasema manager mkuu kazini kwako ni mwizi wa kutupwa; ila ninyi subordinates ndio wachapa kazi hodari wa kupigiwa mfano.
 
Mwafrika wa Kike,

Hapo ndipo tunapotofautiana, wengine tunaamini kwamba ni lazima tutimize wajibu wetu kabla hata ya kuangalia kama mtu mwingine anatimiza wajibu wake.

Fisadi anaiba mamilioni kwasababu anaona mshahara wake hautoshi, daktari naye anaiba malaki kwasababu anaona mshahara wake hautoshi, nurse naye anamwacha mama mja mzito anakufa kwasababu mshahara wake hautoshi. Wote hawa ni kitu kimoja, hawana tofauti yoyote. Hata yesu alisema toa kibanzi kwenye jicho lako kwanza kabla hata ya kuthubutu kuangalia jiko la mwingine.

Kitu nilichojifunza kwa nguvu zote huku nje ni umuhimu wa kutimiza wajibu wangu, kisha kujua kutetea haki yangu mpaka dakika ya mwisho. Je nina haki gani ya kutetea haki yangu huku mimi mwenyewe nimenyang'anya haki ya mtu mwingine?

Sisi tunaona akina Karamangi, JK, Lowassa ndio mafisadi lakini kwa mama mjamzito anayekufa kitandani kwasababu tu ameshindwa kutoa rushwa kwa Mkunga, huyu Mkunga ndio fisadi namba moja. Kwa
msichana wa mlimani ambaye anafelishwa kwasababu tu ameshindwa kutoa mwili wake ili mwalimu achezee, huyo mwalimu ndio fisadi namba moja, kwa mfanyabiashara anayefilisiwa kwasababu tu kakataa kumpa hongo mtu wa TRA, huyu TRA ndiye fisadi.

Sawa haya mapambano yanaweza kuharakishwa kama utawala wa juu utatimiza wajibu wao, lakini mapambano haya yatafanikiwa zaidi kama Watanzania tutabadilika na kuthamini haki ya mtu mwingine. haki ambayo inatakiwe umpe mbaya wako sawa na kipenzi chako. Kama tutajenga culture ya kuthamini kazi badala ya bla bla nyingi. Culture ya kujua kwamba ukiiba elfu kumi ni sawa tu na kuiba milioni kumi, wote ni wizi na inatakiwa ulaaniwe. Kinyume chake wote sisi tutakuwa mafisadi tu.

No Mtanzania,

Hapa ndipo tunakubaliana mimi nawewe.

1. Nakubaliana nawe kwa sababu wewe unataka kila mtu afanye nafasi yake na sio kupiga kelele kulaumu viongozi tu.

2. Nakubaliana nawe kuwa ufisadi ni ufisadi tu hata kama umefanywa na nesi au waziri wa afya.

3. Nakubaliana nawewe kuwa tunaopiga kelele hapa JF tukipata nafasi serikali tufanye vizuri na wala sio kurudia yaleyale wanayofanya tunaowapigia kelele.

4. Nakubaliana nawe kuwa inabidi nitimize wajibu wangu kabla ya kumwambia mwenzangu atimize wakwake

5. Nakubaliana nawe kuwa ufisadi uitwe ufisadi either ukiwa sisiemu au upinzani.

6. Nakubaliana nawe.... oh kuna mengi sana tunakubaliana nawe.

......

1. Natofautiana tu nawe kwa madai yako kuwa yanayofanyika all over the country sio matokeo ya uongozi mbovu wa serikali ya juu (Kikwete). Mlengwa wa mapambano yangu kwa sasa ni serikali ya juu ya Kikwete na hayo mengine yatafanywa na watanzania ktk level zote nchini.

Nafurahi kuona kuwa tunakubaliana zaidi ya tunavyotofautiana
 
we mwanamama wewe.. umenikumbusha mjadala kati ya George Bernard Shaw na G. K Chesterton
 
1. Kama huamini kwamba viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe subiri ifikapo 2010. Mtanikumbuka!

Viongozi wetu ni reflection za character zetu wenyewe yaani wananchi wa bongo, mabaya yote ya Muungwana kama yanavyosemwa hapa forum, ninataka kuamini kuwa, yalisemwa kwenye uchaguzi mdogo kule Tunduru, lakini matokeo yakawa CCM 63%... Chadema 3%!

Majuzi tumeona wananchi wakimpokea Muungwana Airport, tena kwa wingi sana, Mpaka huko majuu, tumeona wananchi wanavyomuhangaikia, wengine tumeona kwenye picha za Michuzi Line, eti wameenda kumpa mpira wa miguu, lini Muungwana aliwahi kucheza mpira? Tumeona majuu huko wananchi wakijikusanya na kujiita wawakilishi wa wabongo, ili tu wapige picha na Muungwana, huyu huyu ambaye tunaambiwa hapa hafai?

Tunamlaumu rais weee, lakini never sisi wenyewe wasanii wa dunia, wakuu tumpe nafasi rais ajipange, katika mabaya mengi tunayoyaona, pia kuna mazuri mengi ambayo hatuyaoni, tujitahidi kumpa ushirikiano rais wetu, badala ya kumshambulia tuu, mimi nimeona mashambulizi toka siku ya kwanza alipoapishwa,

Sawa tunaelewa kuwa kazi kubwa na muhimu ya upinzani, ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani kwa kila njia, lakini sio hata wananchi wakimpokea basi wamelipwa, hapana wakuu, tuwe na heshima kidogo kwa rais, wananchi ambao ni sisi wenyewe tumempa kura zetu, hiyo sio siri, alishinda kihalali kuwa rais kwa miaka mitano ijayo, katika uchaguzi uliopita upinzani walisema mabaya yote ya CCM, tena mpaka kwa helikopta, lakini wananchi ambao ni sisi wenyewe, tukaichagua CCM na Muungwana,

Leo mgeni akija hapa forum, atashangaa kuwa he! Hii CCM na Muungwana, waliingiaje madarakani kama wananchi wanalia namna hii? Hawezi amini kuwa walipigiwa kura na kushinda, kama vile wabunge Zitto na Dr. Slaa, walivyoshinda kwenye majimbo yao na si kweli kwamba hawa wabunge waiwili wa upinzani waliiba kura! NO!

Political Analysis, yoyote duniani leo, inatakiwa iangalie pande mbili za any ishu, ndio inaweza kukubalika na wenye akili timamu, ama sivyo inakuwa ni cheap analysis, ambayo sio worthy kuwa-diggested na politicians, maana sasa ninaanza kuamini huenda Chadema inapata matatizo kwenye uchaguzi kutokana na kuchukua sana mawazo toka hapa forum, maana haya mawazo huwezi hata yaita one sided, bali hayana hata juice ya reality za pande zote mbili za siasa,

I mean my point sio spinning, au kampeni au unazi, lakini guys kuna serikali Tanzania, ndio maana tunayo nchi bado ya kujivunia, matatizo ya orodha ya ufisadi ni kweli ni mazito, tena sana, lakini look how long it took kina Butiku and the likes, kusimama na kusema something? Almost a month, WHY? Ni kwa sababu hatujawahi kukumbana na mambo mazito kiasi hicho, na wala hatuna mwongozo na unaweza kukuta hata sheria zake hatuna!

Kwa hiyo ninataka kukubaliana na mkuu Ngabu, kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe wananchi, na tumnewachagua wenyewe kwa hiari yetu, upinzani tunaowategemea bado hawajatupa sababu ya kuwachagua, ingawa finally, ndio wanaonekana kuanza kuamka lakini bado sana, Roma, haikujengwa kwa siku moja, wasianze kuamini kuwa orodha ya mafisadi basi itawapa uongozi, hapana it will takes more than that, na pia wajifunze kukubali na mazuri ya CCM pia, ndio siasa za kisasa, na pia tatizo letu kubwa bongo ni katiba yetu ni mbovu, bado tunaongozwa na katiba iliyokuwa made kwa ajili ya chama kimoja CCM, mpaka itakapobadilishwa upepo wa siasa utaendelea kuwa-favor CCM, ambao ndio hasa katiba iliyopo ilianzishiwa for,

Na sisi wana-forum tusaidie kampeni za kuwaamsha wananchi usingizini, kwa manufaa ya taifa na sio ya vyama, maana kufukua maovu ya serikali iliyopo madarakani, sio tatizo ni kuongoza, na kufukua maovu ya seriklai sio dhana ya kuaminika, maana ingekuwa Ukraine sasa hivi wasingekuwa walipo, yaani kwenye kumtoa kiongozi wa upinzani waliyemlalia macho kumuweka, ya Kenya tuinayasikia, jinsi Kibaki na wenziwe ambavyoi wananchi hawa waamini to the point wamewakatalia hata referendum ya kubadili katiba, maana wanawaaogopa kuwa watawaibia tu!

But oh well....we deserve the people we elect, who happened to be us!
 
Mie bado nasubiri hiyo makala gazetini kesho...........narudia ombi langu, tuwekewe hapa kopi ambayo haijabadilishwa mambo mawili matatu.
 
Mkuu MMJ,

Heshima mbele mkuu, binafsi bado sijafikia kumuweka rais wa sasa Muungwana, kwenye listi ya wafisadi au wezi, na viongozi wabovu wa taifa letu,

Urais ni kazi nzito sana, inayohitaji kutumia busara kabla ya kufanya maamuzi muhimu ya taifa, ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza kwa makini washauri wake wa kuitawala na kisiasa, pamoja na kisheria, mambo ya kukurupuka yalituponza taifa tukawalipa mamillioni lukuki watu fulani wa benki kuu, enzi zile za Mkapa, tumewalipa mamillioni lukuki ndugu wa Kombe, kutokana na kurupu kurupu,

Mkataba wa IPTL, tuliletewa na Lowassa, akishirikiana na Kolimba, Radar tuliletewa na Mramba, kwa kushinikizwa na marafiki wa Mkapa, kuwa na hisa kwenye kampuni tumekubaliana hapa forum kuwa sio tatizo, tatizo ni kama walizipata hisa hizo kwa haki, na wanaendelea kuzimiliki kwa haki na kufuata sheria zote zetu za nchi kuhusiana na hizo hisa,

Tuhuma zilizotolewa ni nzito, hilo halina ubishi, rais amesema serikali inachunguza mdai hayo, pia tumeambiwa na Spika kuwa yeye binafsi ameyafikisha malalamiko ya kina Slaa kwa mwanasheria mkuu, naye anasubiri majibu, recentlty tumeambiwa na waliotuhumiwa kuwa, wanajitayarisha kwenda mahakamani, na sasa hivi tunawasikia viongozi wengi wa CCM, hata Kingunge, wakijitokeza kuwa majibu yanatakiwa,

Kumbuka hii ni mara ya kwanza Tanzania kama taifa tumejikuta na ishu nzito kama hii, so far ni vyema kuwa na subira, binafsi siamini bado kuwa Muungwana, ni mchafu au si safi kama ulivyosema, ninaamini kuwa kinachomsumbua ni lack of experience na urais, na siasa za taifa kwa ujumla, he was good kwenye kampeni, lakini kwenye urais bado kunamtatiza kidogo,

Lakini kwamba yeye ni mchafu, hapana hilo labda kuwepo na ushaidi zaidi ya uliokwishatolewa tayari, Muuungwana hana mali za kutisha, hana majumba, wala mahekalu, hana magari wala mashamba, I mean mnyonge mnyongeni the man is poor kwa standards za marais wengine wa Afrika, au hata mstaafu wetu,

Binafsi bado niko radhi kusubiri, na sijafikia hatua ya kuamini kuwa Muungwana ni mchafu, just because hasikilizi mob justice, hapana urais una maadili yake na miiko yake, na busara zake tofauti kabisa na busara za kuwa upinzani kwenye siasa za taifa, au hii forum,

Mkuu sawa ni haki yetu wananchi kuonyesha outrage zetu kuhusiana na tuhuma za mafisadi, lakini bado ninampa benefit of the doubt rais Muungwana, maana hii hukumu na charges ulizozitoa ni nzito mno kwa mkuu wa nchi na kisiaa pia, ambaye amekuwa madarakani for only 23 months.

Aahsante Mkuu, na Wakuuu Wote Waliochangia Hiii Topic!

sasa kwanini asichague wasiidizi wanaofaa, i.e ambo ni competent kufanya hizo kazi na wasio na tuhuma.
Eg Chuo kikuu kuna watu wengi tu wazuri ambao wanaweza kuwa washauri wake wazuri katika mambo mengi, kuanzia ya kisheria mpaka ya kiuchumi.
Akifanya hivyo ataonekana yuko Serious, lakini so far Nchi imekuwa like a dancing Hall, kila mtu na lwake, mwenye ku-dance Blues sawa, Ngwasuma Haya, za Kizaire, taarab imo etc
 
Ukiwasha moto huwezi kuuzima haraka hadi uteketeze kwanza, na hapo ndipo tumefika.
 
FMES, wananchi walioenda kumpokea kikwete watu walisema kwamba walikodishwa eti, kwa kifupi wanasema kwamba kikwete hapendwi na mtu yoyote ! teh teh ! wamenikuna nami ntawakuna !

pia vile vile huwezi kufanya kampeni ya kuwaamsha wananchi iwapo watu/wapinzani watatumia chuki na upuuzi kusmear viongozi ili mradi wanufaike wao ! that being said, ndio maana ........................ !!
 
1. ....
Majuzi tumeona wananchi wakimpokea Muungwana Airport, tena kwa wingi sana, Mpaka huko majuu, tumeona wananchi wanavyomuhangaikia, wengine tumeona kwenye picha za Michuzi Line, eti wameenda kumpa mpira wa miguu, lini Muungwana aliwahi kucheza mpira? Tumeona majuu huko wananchi wakijikusanya na kujiita wawakilishi wa wabongo, ili tu wapige picha na Muungwana, huyu huyu ambaye tunaambiwa hapa hafai?

Umesahau kuwa hata Bush hupata umati mkubwa sana kwenye mikutano yake ya hadhara?

Tunamlaumu rais weee, lakini never sisi wenyewe wasanii wa dunia, wakuu tumpe nafasi rais ajipange, katika mabaya mengi tunayoyaona, pia kuna mazuri mengi ambayo hatuyaoni, tujitahidi kumpa ushirikiano rais wetu, badala ya kumshambulia tuu, mimi nimeona mashambulizi toka siku ya kwanza alipoapishwa,

Sawa tunaelewa kuwa kazi kubwa na muhimu ya upinzani, ni kuikosoa serikali iliyoko madarakani kwa kila njia, lakini sio hata wananchi wakimpokea basi wamelipwa, hapana wakuu, tuwe na heshima kidogo kwa rais, wananchi ambao ni sisi wenyewe tumempa kura zetu, hiyo sio siri, alishinda kihalali kuwa rais kwa miaka mitano ijayo, katika uchaguzi uliopita upinzani walisema mabaya yote ya CCM, tena mpaka kwa helikopta, lakini wananchi ambao ni sisi wenyewe, tukaichagua CCM na Muungwana,

Soma alichoandika Dar si Lamu kuhusu kiongozi mzuri. It is all about the present and the future.

Leo mgeni akija hapa forum, atashangaa kuwa he! Hii CCM na Muungwana, waliingiaje madarakani kama wananchi wanalia namna hii? Hawezi amini kuwa walipigiwa kura na kushinda, kama vile wabunge Zitto na Dr. Slaa, walivyoshinda kwenye majimbo yao na si kweli kwamba hawa wabunge waiwili wa upinzani waliiba kura! NO!

Political Analysis, yoyote duniani leo, inatakiwa iangalie pande mbili za any ishu, ndio inaweza kukubalika na wenye akili timamu, ama sivyo inakuwa ni cheap analysis, ambayo sio worthy kuwa-diggested na politicians, maana sasa ninaanza kuamini huenda Chadema inapata matatizo kwenye uchaguzi kutokana na kuchukua sana mawazo toka hapa forum, maana haya mawazo huwezi hata yaita one sided, bali hayana hata juice ya reality za pande zote mbili za siasa,

Huo upande wa pili ndio inabidi uuweke hapa ili watu wauone maana labda mie sijaouona bado!

I mean my point sio spinning, au kampeni au unazi, lakini guys kuna serikali Tanzania, ndio maana tunayo nchi bado ya kujivunia, matatizo ya orodha ya ufisadi ni kweli ni mazito, tena sana, lakini look how long it took kina Butiku and the likes, kusimama na kusema something? Almost a month, WHY? Ni kwa sababu hatujawahi kukumbana na mambo mazito kiasi hicho, na wala hatuna mwongozo na unaweza kukuta hata sheria zake hatuna!

Kwa hiyo ninataka kukubaliana na mkuu Ngabu, kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe wananchi, na tumnewachagua wenyewe kwa hiari yetu, upinzani tunaowategemea bado hawajatupa sababu ya kuwachagua, ingawa finally, ndio wanaonekana kuanza kuamka

Ningependa viongozi waamke mapema kabla nchi haijauzwa yote kwa wakoloni!

lakini bado sana, Roma, haikujengwa kwa siku moja,

Unajua nimekuwa naona hii term inatumika sana hapa forum bila ya wanaoitumia kusema pia wakati Roma inajengwa kulikuwa hakuna viongozi wa Roma walokuwa wanaiba pesa za nchi na kuziweka kwenye mabenki ya nje.\

Wakati Roma inajengwa, kulikuwa hakuna watu walokuwa wanauza migodi ya dhahabu ya thamani ya mabilioni kwa sents 26.

Tukiendelea kusubiri hii Roma ijengwe, tutajikuta tumetawaliwa tena kwa mara ya pili na wazungu, wachina na waarabu.

wasianze kuamini kuwa orodha ya mafisadi basi itawapa uongozi, hapana it will takes more than that, na pia wajifunze kukubali na mazuri ya CCM pia, ndio siasa za kisasa, na pia tatizo letu kubwa bongo ni katiba yetu ni mbovu, bado tunaongozwa na katiba iliyokuwa made kwa ajili ya chama kimoja CCM, mpaka itakapobadilishwa upepo wa siasa utaendelea kuwa-favor CCM, ambao ndio hasa katiba iliyopo ilianzishiwa for,

Na sisi wana-forum tusaidie kampeni za kuwaamsha wananchi usingizini, kwa manufaa ya taifa na sio ya vyama, maana kufukua maovu ya serikali iliyopo madarakani, sio tatizo ni kuongoza, na kufukua maovu ya seriklai sio dhana ya kuaminika, maana ingekuwa Ukraine sasa hivi wasingekuwa walipo, yaani kwenye kumtoa kiongozi wa upinzani waliyemlalia macho kumuweka, ya Kenya tuinayasikia, jinsi Kibaki na wenziwe ambavyoi wananchi hawa waamini to the point wamewakatalia hata referendum ya kubadili katiba, maana wanawaaogopa kuwa watawaibia tu!

But oh well....we deserve the people we elect, who happened to be us!

so far hii mikataba iliyopo hapa na ile ambayo tunayo ila hatujaiweka hapa inashuhudia kuwa JF imeamka na imeanza kufanya kazi!
 
Wooooh people, kabla hatujaenda mbali sana lazima tufanye mambo kama hospitalini..........mgonjwa anapimwa na kuja na diagosis, ugonjwa wa tanzania ni chronic metastazied cancer....prognosis ni nzuri tu kama kutafanyika emergency radical surgery ya kuondoa cancerous cells hizo. Lakini mgonjwa huyu(Tanzania na Watz) ana matatizo ya knowledge deficit na non compliance ya medical regimen so teaching and close monitoring is very important for better results.
Tunajua tatizo la Tanzania labda ni serikali mbovu ya ccm, kwa bahati nzuri/mbaya kikwete ndio ana-run show. Watu wamekuja na solns zote hapa za nini cha kufanya, ambazo ni nzuri tu, lakini wanasahau kwamba matatizo ya watanzania na tanzania ni WATANZANIA wenyewe x 5. Kama ukishindwa kuwaelimisha watz juu ya matatizo yao/yetu na kila mtu akawa responsible kama vile mgonjwa wa kansa hapo juu, tutakuwa tunapoteza muda tu kwani mchezo huo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. kwikwikwikwi i hope sijapoteza muda wangu kupost hii kitu!!!!!!!!!!1.
 
sasa kwanini asichague wasiidizi wanaofaa, i.e ambo ni competent kufanya hizo kazi na wasio na tuhuma.
Eg Chuo kikuu kuna watu wengi tu wazuri ambao wanaweza kuwa washauri wake wazuri katika mambo mengi, kuanzia ya kisheria mpaka ya kiuchumi.
Akifanya hivyo ataonekana yuko Serious, lakini so far Nchi imekuwa like a dancing Hall, kila mtu na lwake, mwenye ku-dance Blues sawa, Ngwasuma Haya, za Kizaire, taarab imo etc

Mkuu wangu hao watu wa chuo, si ndio waliotuambia kwenye polls kuwa Muungwana, anakubalika kuliko wote, na ata-make a good president, kweli mkuu untaka tuongozwe na kina Prof. Mkandalla?

Urais siku zote ni learning on the job, unless uwe kwenye nchi kama USA, ambako kuna CIA, State Department, FBI, Congress, Judicial, ambao kazi yao ni pmaoja na kuiangalaia executive branch inafanya nini kila siku, lakini bongo inabidi wakampigie magoti Kigoda, ndio maana Muungwana majuzi alikuwa mklai kweli aliposikia kuwa Makamba, alikuwa akimpiga vita Kigoda kwa jina lake,

Kwenye kampeni za urais uliyopita, tuliambiwa na wananchi wengi kuwa tunataka vijana, haya vijana ndio wanaoongoza sasa hivi, sasa tukubali tu kuwa tulikosea, maana ukweli ni kwamba hatujawahi kuwa na serikali ya wasomi kama this time na vijana pia, lakini angalia yaliyotukuta, maana yake ni moja tu nayo ni kwamba kuanzia wananchi wa Tanzania, yaani sisi hatuelewi cha kufanya inapokuja kwenye uongozi, sasa wote turudi tujipange upya tuangalie tulikosea wapi, badala ya kuwalaumu tu walioko, maana kama ni Mlimani, Prof. Mbilinyi aliyekula hela za minofu ya samaki alitoke wapi Mkuu? Prof. Malima alitokea wapi?

Invincible Mkuu FMES

We are in the process of significant change; and for a better course.

Mkuu wangu Invicible,

Heshima mbele, unayosema ni kweli kabisaa, lakini bado hatuja-address matatizo yetu ya character, kutokana na kutokuwa na maadili ya uongozi, ambayo yataanzia kwenye level ya sisi wananchi pia kuwa na maadili ya kijamii, otherwise sisi wananchi haya mabadiliko hayatatusaidia kitu, bali viongozi wachache, maana hata kuanzishwa kwa vyma vingi walionufaika ni kina Mreema na Mtei, sio sisi wananchi, bila wanachi kuamshwa tutaishia kama Visiwani, wananchi wanamuaminia Seif tuu, mpaka sasa amenunuliwa hawaelewi cha kufanya maana kila kitu kilikuwa Seif tu,

Kama tusipokazana kuwaamsha wananchi, hata yanayoendelea sasa yataishia kuwanufaisha wachache tu, na sisi tutaendelea kupiga kelele tu hapa!

Lakini heshima kwa maneno yako mazito mkuu!
 
sasa kwanini asichague wasiidizi wanaofaa, i.e ambo ni competent kufanya hizo kazi na wasio na tuhuma.
Eg Chuo kikuu kuna watu wengi tu wazuri ambao wanaweza kuwa washauri wake wazuri katika mambo mengi, kuanzia ya kisheria mpaka ya kiuchumi.
Akifanya hivyo ataonekana yuko Serious, lakini so far Nchi imekuwa like a dancing Hall, kila mtu na lwake, mwenye ku-dance Blues sawa, Ngwasuma Haya, za Kizaire, taarab imo etc

Msee,
wewe mwenyewe hapo you can make a good presidential advisor bwana alaa, mbona wajiweka nyuma!!!!.
 
Ukiwasha moto huwezi kuuzima haraka hadi uteketeze kwanza, na hapo ndipo tumefika.

Dua,

labda uwaambie wewe. Watu wamezoea sana status quo na hawakubali kuona nchi inavyobadilika haraka hivi.

Kila mara nasoma kuwa tuvute subira, subira wakati baada ya miaka 25 Barrick watakuwa wamekomba gold yote ya Buzwagi!
 
so far hii mikataba iliyopo hapa na ile ambayo tunayo ila hatujaiweka hapa inashuhudia kuwa JF imeamka na imeanza kufanya kazi!

Mkuu ndiyo ninayosema, tuendelee kuwaelimisha wananchi waamke maana kuamka kwetu haisaidii kitu, na uchaguzi uliopita ndiuo ushahidi tosha kuwa kuamka JF peke yake haitoshi kuwapata viongozi safi wa taifa letu,

Sasa tukazane kuwaamsha wananchi ndio njia pekee itakayotusaidia na yanayotukuta, lakini tusikwepe lawama ya kuwa sisi hatuhusiki na viongozi tulionao sasa hivi, hapana ni chaguo letu wenyewe, tumekosea sasa tukubali na tuanze upya, lakini lazima tukubali kwanza kuwa tumekosea, na sababu za msingi tuzitoe hapa, badala ya kulaumu tu, hapana hawa viongozi wetu hawakushushwa toka mbinguni, tuliwachagua wenyewe au tuliwachagua kwa kutopiga kura, lakini tusilaumu wananchi,

Kwenye uchaguzi mmoja majuzi hapa bongo, nilikuwa ninamsiadia mawazo kiongozi mmoja kwenye kuingia NEC, ambaye alishinda pamoja na kuwa underdog tena 50-1, unajua mkuu alishindaje, nilimuambia kuwa utashinda kwa sababu wananchi wengi wanaamini kuwa mpinzani wako ni maarufu sana kwa hiyo hawataenda kupiga kura wakiamini kuwa atashinda tu, maana amekuwa kwenye nafasi kwa muda mrefu, exactly what happened, wananchi wengi wanaomuunga mkono yule mpinzai hawakuenda kupiga kura, wakiamini kuwa amezoea kushinda tu,

It sound like hapa forum, wakuu tusiposhirki wataendelea kushinda tu, huku tukishangaa nani amewachagua hawa? Viongozi wabovu hupenda sana wananchi wasiopiga kura maana wengi wao hawawezi kuwapigia anyways, na hivyo kuwachagua anyways!
 
Mkuu wangu hao watu wa chuo, si ndio waliotuambia kwenye polls kuwa Muungwana, anakubalika kuliko wote, na ata-make a good president, kweli mkuu untaka tuongozwe na kina Prof. Mkandalla?

Urais siku zote ni learning on the job, unless uwe kwenye nchi kama USA, ambako kuna CIA, State Department, FBI, Congress, Judicial, ambao kazi yao ni pmaoja na kuiangalaia executive branch inafanya nini kila siku, lakini bongo inabidi wakampigie magoti Kigoda, ndio maana Muungwana majuzi alikuwa mklai kweli aliposikia kuwa Makamba, alikuwa akimpiga vita Kigoda kwa jina lake,

Kwenye kampeni za urais uliyopita, tuliambiwa na wananchi wengi kuwa tunataka vijana, haya vijana ndio wanaoongoza sasa hivi, sasa tukubali tu kuwa tulikosea, maana ukweli ni kwamba hatujawahi kuwa na serikali ya wasomi kama this time na vijana pia, lakini angalia yaliyotukuta, maana yake ni moja tu nayo ni kwamba kuanzia wananchi wa Tanzania, yaani sisi hatuelewi cha kufanya inapokuja kwenye uongozi, sasa wote turudi tujipange upya tuangalie tulikosea wapi, badala ya kuwalaumu tu walioko, maana kama ni Mlimani, Prof. Mbilinyi aliyekula hela za minofu ya samaki alitoke wapi Mkuu? Prof. Malima alitokea wapi?

...dah, Mkuu FMES hapo umekata mzizi wa fitna kikweli kweli, ama kweli 'mtoto akilia wembe mpe', mnh!!!
 
Back
Top Bottom