Umeanza tena! naona hujipendi. Waache wale wala wali wale wali wao!
Bi. Senti 50;
Umerudi tena,unatafutwa kujibu tuhuma nzito hapa;
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6202
Umeanza tena! naona hujipendi. Waache wale wala wali wale wali wao!
Hapa kuna ukweli lakini yeye ameshakuwa kwenye hiyo nafasi kama amiri jeshi mkuu kwa takribani miaka miwili,Hivyo kama ni uchunguzi na kuweza kujiridhisha ktk ishu mbali mbali amepata muda wakutosha na imefikia wakati wa kuyatolea maamuzi na kuyasimamia maamuzi yake kwa manufaa ya taifa na si kwa manufaa ya kundi lake au wanaojiita wafadhili au wawekezaji.Urais ni kazi nzito sana, inayohitaji kutumia busara kabla ya kufanya maamuzi muhimu ya taifa, ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza kwa makini washauri wake wa kuitawala na kisiasa, pamoja na kisheria, mambo ya kukurupuka yalituponza taifa tukawalipa mamillioni lukuki watu fulani wa benki kuu, enzi zile za Mkapa, tumewalipa mamillioni lukuki ndugu wa Kombe, kutokana na kurupu kurupu!
Ni kweli Urais una maadili yake Lakini yeye ameonyesha mengi kutoyafuata,Kuna mambo yanahitaji maelezo ya haraka kutoka kwa watendaji wako ili waonyeshe uwajibikaji na wanaposhindwa kuyatolea maelezo na wananchi wakarithika huna budi kuwawajibisha hata kwa kuwaambia waachie ngazi Lakini kuendelea kuwakingia kifua kunamfanya na yeye kuingia moja kwa moja kwenye kundi hilo kwa kutoonyesha uwajibikaji pia kama amiri jeshi mkuu na kutofanya maamuzi sahihi.Binafsi bado niko radhi kusubiri, na sijafikia hatua ya kuamini kuwa Muungwana ni mchafu, just because hasikilizi mob justice, hapana urais una maadili yake na miiko yake, na busara zake tofauti kabisa na busara za kuwa upinzani kwenye siasa za taifa, au hii forum,
We mwanakijiji hulali?
Je JK ni fisadi? Mimi kwasasa nitakuwa NEUTRAL juu ya dai hili, sijawa convinced na vigezo vinavyotumika kumhukumu lakini pia sijafurahishwa na ukimya wake.
Kikwete ni fisadi tu..
richmonduli, buzwagi, nk vyote vimefanyika chini yake na anahusika moja kwa moja kama rais. Mikataba mingine ya madini yote "inayorekebishwa" Kikwete anahusika na sofar guys mnaona mikataba "iliyorekebishwa" ilivyo...
Kashfa zake akiwa madini zilimhusu yeye moja kwa moja. Miezi sita ya kwanza ya Kikwete ikulu, taarifa ya mkaguzi wa hesabu iligundua matumizi ya karibu billion moja yasiyothibitishwa kwa receipts au authorizations( kwa lugha rahisi - bilioni ziliibwa).
Huu usafi wa Kikwete uko wapi?
Documentation za mambo yake ni nyingi ila mengine yanatunzwa tu hapa yasiweke hadharani na lawyers wake wakajiandaa na utetezi. Huyu Kikwete lazima atasimama mahakamani siku moja kujibu!
Sasa mtu mchafu inakuwakuwaje akachaguliwa kuwa raisi kwa asilimia zote hizo? Si mambo kama haya (uchafu) ndio yalitakiwa yazungumzwe kwenye kampeni. Na kama yalizungumzwa na watu bado wakamchagua, hiyo inasema nini kuhusu watu hao?
Sasa mtu mchafu inakuwakuwaje akachaguliwa kuwa raisi kwa asilimia zote hizo? Si mambo kama haya (uchafu) ndio yalitakiwa yazungumzwe kwenye kampeni. Na kama yalizungumzwa na watu bado wakamchagua, hiyo inasema nini kuhusu watu hao?
Hii inasema kuwa hao watu wanahitaji kufanyiwa mental evaluation kama kweli walimchagua huyu Kikwete. Au sivyo inawezekana hawa watu hawakuelezwa ukweli halisi kuhusu huyu guy ukichukulia media kampeni ya Rostam Aziz.
Kama viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe, I am afraid soon nitaanza kukubaliana na arguments zako kuwa kuna tatizo na sisi watanzania na waafrika kwa ujumla!
Kama huamini kwamba viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe subiri ifikapo 2010. Mtanikumbuka! Ila kwangu mimi binafsi sioni haja ya kusubiri hadi 2010. Nilishaliona hilo toka zamaaaaani na ndio maana sikuona chochote alichokuwa nacho huyo Kikwete zaidi ya personality. Kwa kweli ningefurahi kama Salim Ahmed Salim angekuwa raisi. But oh well....we deserve the people we elect.