Kikwete: Hata Nyerere alishindwa ingawa tunamsifu sana

Mh! Simple execuse, shame

Kama Jakaya mwenyewe anakili kuwa ameshindwa kutatua kero zinazowakabili wananchi, ni jambo la bisara kuachia ngazi na kuona kama mwananchi mwingine anaweza kuisaidia nchi kufikia level nyingine. Sio siri kuwa Rais wetu ni mgonjwa hivyo basi muda wake mwingi anautumia kufikirai maradhi yanayomsibu kuliko kujali matatizo ya nchi; na ndiyo maana hafanyi maamuzi muhimu ya nchi kama vile kujaza nafasi zilizo wazi za watedaji na kuwabadilisha watendaji wabovu!! Afya za viongozi wa juu wa nchi lazima iwe hoja ya kujadiliwa kwa kina katika katiba mpya itakayoandikwa kwani madhara yake tunayaona hivi sasa.
 
Leo katika hotuba yake ya siku ya kuzaliwa CCM, kuna kauli nyingi za kikwete ambozo kama rais hakustahili kuzisema, mojawapo ya ,ni kauli yake ya kwamba pamoja na kumsifu sana Nyerere lakini alishindwa kutatua changamoto nyingi katika utawala wake na hivyo hivyo kwa marais wengine waliomtangulia, sembuse mimi (Kikwete). Alisema hayo akijitetea kwamba yeye sio wa kwanza kushindwa kuondoa matatizo ya watanzania.

Mimi nimeichukulia kauli hii kama simple/cheap excuse ya kikwete kwa jinsi alivyoshindwa kutatua matatizo ya watanzania. Sio tu kikwete ameshindwa kutatua matatizo bali ameyaongeza na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu zaidi. Anaweza kutuambia yeye kama rais am-achiave nini, wenzake wote wana vitu vya kujivunia.

Nyerere alijenga umoja wa kitaifa na kufanya watanzania kuwa wamoja na kuwepo kwa amani ambayo kikwete anajivunia leo, lakini pia mzee huyu alijenga uwajibikaji kwa watumishi wa umma kitu ambacho kikwete ameshindwa.

Mzee Ruksa aliruhusu uchumi wa soko ambao ulisaidi kufanya upatikanaji wa bidhaa muhimu ambazo mwanzo zilionekana kama anasa.

Mzee Mkapa akajitahidi kujenga uchumi imara bila kusahau miundo mbinu na kurudisha heshima ya wafanyakazi.

Pamoja na mapungufu yao viongozi waliopita wanayo ya kujivunia.

Akaja kikwete
1) akaharibu kabisa umoja wa kitaifa kwa kuanza na makundi ndani ya CCM (kwa kuanzisha mtandao wake uliowavuruga wengine) na baadae kuharibu umoja taifa zima kwa kuchochea ajenda zake za udini na ukabila.
2) Akabomoa kabisa uchumi alioujenga mzee Mkapa kwa kuendekeza anasa, matumizi makubwa serikalini, kusafiri kwenda kubembea na kuendekeza ununuaji wa magari ya kifahari yasiyo na tija, gharama za maisha zimepanda mno, thamani ya shilingi imeshuka sana, mfumuko wa bei hauelezeki.
3) Ametengeneza mitandao ya wizi kwa kuwatumia marafiki zake kama RA, ED kwa kutaja wachache.
4) Akaharibu kabisa mfumo wa elimu kwa kuanzisha kisiasa shule za kata zisizo na walimu wala vifaa, ukiangalia wanafunzi wanaofeli ni heri hata tungebaki na shule chache bora,maana waliofeli wanabaki kuwa darasa la saba hawawezi kusema wana elimu ya form IV.
Ni mengi jamani yanayoonyesha tofauti ya utendaji kazi wa kikwete na watangulizi wake, naomba niishie hapa.

Lakini Kikwete please dont look for cheap excuses, just admit that ur the most failure president we ever had.

Mkuu naona hii statement ya Kikwete imepokelewa kwa hisia tofauti
1. Kwanza kwa nini amesema hivi? is it excuse?? if is excuse then this is wrong
2. Kazungumza kama vile ana-recall historia ili atupeleke mahali pazuri au kasema hili naye a-fail??

All in all ukiondoa statement hii kuwa kaisema Kikwete, ukweli matatizo mengi sana nchi hii source yake ni Nyerere, Nyerere alishindwa kwa vingi na vile vichache alivyofanikiwa vimekuwa landmark.

Kwa udhaifu au failure za Nyerere rais pekee ambaye ngekuja kujenga alipoharibu Nyerere ni yule ambaye angekuwa visionary kama Nyerere, yaani baada ya Nyerere marais waliokuja wote walikuwa vilaza akwemo huyu JK. afadhali mkapa sana and may be is second to Nyerere.

Kushindwa kwa Nyerere sio chuki, angalia siasa yake, katiba, kuondoa vyama vingi, maamuzi ya wananchi, uchumi, n.k although he failed he is still the best president ever... i mean he failed but he had good intentions and righ reasons, etc HII NDIO HASA quality of leadership. JK kafeli kabisa hana hata good intention wala good reasons...
 
after failure .... a well said farewell speech

JK ameanza kuaga rasmi
 
Waberoya, kushindwa kuongoza baada ya kupewe nafasi zote anazozipata Jakaya ni aina ya LAANA fulani hivi; kiongozi makini hawezi kwenda nchi za nje hata kama kuna mkutano wa aina gani wakati nchi yake iko gizani!! Jamaa anachezea shilingi chooni.!
 
sawa lakini hajalaaniwa na Nyerere!
 
Kama alijua hawezi sasa kimbelembele cha kuutaka urais kilitoka wapi na ahadi hewa zisizotekelezeka za kutegemea wanaume wenzie akina Obama wamtekelezee ahadi zake, hua sipendi umbea!
 
huwezi kumlinganisha kikwete na waliomtangulia kwa uzalendo mkubwa aliouonyesha kwa nchi ya tanzania, amefanya mengi katika uchumi, katokomeza ujambazi n.k nenda kisekta utaona ni yepi ameuyafanya katkika utawala wake, na kwa taarifa yako ameshajenga km nyingi za lami kuliko marais wote waliomtamgulia, n akwa mara ya kwanza tokea uhuru mikoa ya pembezoni k.m kigoma ndio kwanza inaanza kuelewa kuwa nayo ipo tanzania

mafanikio ya kutafutwa kwa microscope siyo ya kujivunia kiihivyo. ukiangalia kisekta utakuta kuwa quantity imeongezeka but quality imeshuka mf. kwenye elimu shule nyingi za sekondari na 50% ya wanafunzi wamefeli, afya: majengo ya vituo vya afya vingi lakini havina miundo mbinu ya kitaalamu ya kutosha, barabara:km nyingi zinajengwa kwa gharama kubwa kuliko wastani na bado hazidumu mfano barabara ya kilwa,ajira: muda wa kukaa nyumbani kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo umeongezeka na wanaopata hizo ajira zinakuwa sio katika fani waliyosomea, viwanda: viwanda vikubwa vya uzalishaji hamna n.k

kwa hiyo ndugu usitulazimishe kuumiza macho yetu kuangalia vitu kwa Microscope ili tuje kumsifia mtu. mafanikio ya akina nyerere na mwinyi na mkapa hayahitaji kutafutwa kwa Mikcroscope ili kuyaona.
 
Basi kama anakubali na kulijua hilo, aache majivuno na ahadi zake za mbingu wakati anatupa jehanamu
 
dos santos sio uzalendo matusi -manake wote tupo hapa bongo, unajidanganya kudhani kwamba watu hawajui unayemhusudu alivyomchafu kitandani, usipende kukimbilia hoja za kitandani manake kurasa za unaowahusudu zinatia kinyaaaa huwezi kulinganisha na dr slaa, kuna watu wameliwa tigo wakapewa uongozi, kuna watu wananyea debe kwa kuchangia tigo za machangu na unaowahusudu-kwa hiyo mimi nadhani tuwe wazalendo mambo ya vitandani tuyaache huko. Tujadili maada kama waungwana bila kumvunjia mtu heshima.

Mwanangu asante.
Mwanadamu yeyote mwenye mwili na akili tafakari; Ataelimika kwenye jukwaa hili.
Kinyume cha hapo atabaki na upenzi, ushabiki, ukereketwa, wazimu, ushetani, ujinga ima na mambo yafananayo na hayo.
UKWELI UTADUMU.
 
mafanikio ya kutafutwa kwa microscope siyo ya kujivunia kiihivyo. ukiangalia kisekta utakuta kuwa quantity imeongezeka but quality imeshuka mf. kwenye elimu shule nyingi za sekondari na 50% ya wanafunzi wamefeli, afya: majengo ya vituo vya afya vingi lakini havina miundo mbinu ya kitaalamu ya kutosha, barabara:km nyingi zinajengwa kwa gharama kubwa kuliko wastani na bado hazidumu mfano barabara ya kilwa,ajira: muda wa kukaa nyumbani kwa vijana wengi wanaomaliza vyuo umeongezeka na wanaopata hizo ajira zinakuwa sio katika fani waliyosomea, viwanda: viwanda vikubwa vya uzalishaji hamna n.k

kwa hiyo ndugu usitulazimishe kuumiza macho yetu kuangalia vitu kwa Microscope ili tuje kumsifia mtu. mafanikio ya akina nyerere na mwinyi na mkapa hayahitaji kutafutwa kwa Mikcroscope ili kuyaona.
Unachekesha,badala ya kuelimisha,Tofautisha zama na nama
 
Ebu jamani acheni ku-show up a very big level of ignorance kwenye leadership, hivi kuna watu mmemuona Nyerere mtume?? Nyerere alishindwa vitu VINGI SANA NCHI HII NA ALIFANIKIWA KWNYE VITU VINGI SANA PIA.... this is reality, japo asilimia 99 ya Kikwete ni mbovu bado ana asilimia yake moja ya mazuri.........

Swala la Nyerere kushindwa halijaanza na Kikwete, wasomi, papers, books, articles nyingi zinaandika hayo HUO NDIO UKUBWA NA DEMOKRASIA-VITU VINGI LEO HAVIENDI SOURCE NI NYERERE!!! katiba hii mnaoililia source ni Nyerere he failed!!!!. Cha kujiuliza ni Kikwete kasema kwa mazingira gani?? kasema kwa kebehi kame vile anafabya makusudi kutoongoza nchi vizuri?? kwa nini hasa kasema hivyo??

Lakini hawezi kupata laana kwa kusema hivyo cammon Nyerere ni mtu, siyo mtume, siyo jini, siyo ghost ni mtu, aliishi akafa!!!! haya ya laana is justa nother nonsense ...kwa hiyo tulivyosema Mkapa kaiba, Mwinyi karuhusu Rushwa tutapata laana??? ebu futa thread

unapokuwa kiongozi , ajenda yako haiwezi kuwa unataka kufanya vizuri zaidi ya fulani, ajenda yako inapaswa kuwa unataka kufanya vizuri, full stop! unapoanza kufanya mlinganisho kati yako na mtu mwingine unawafanya unaowaongoza wajiulize kama umekata tamaa au umeamua kuweka ukomo katika kiwango cha uzuri unachotakiwa kukifanya au haukuwa na ajenda kabisa.

mtoto akifanya kosa ukimuadhibu anaweza kujitetea kwa usema mbona fulani naye alifanya hivyo hivyo. utetezi wa namna hii kwa mtoto unaweza kukubalika kwa misingi kwamba bado uwezo wake wa kupambanua mambo ni mdogo lakini unapotolewa na mtu mzima inabidi tujiulize kuhusu uwezo wa kufikiri wa mtu huyu maana tunajua ya kuwa kama ulishaona fulani kakosea sehemu fulani wewe ulitakiwa kutokurudia kosa basi kujirekebisha ili makosa hayo yasikutokee na wewe.

uongozi wa taifa ni endelevu kwa maana ya kuwa taifa litaendelea kuwepo hata baada ya sisi wote tuliopo sasa hivi kuwa tumekufa na kwahiyo hatuwezi kutegemea kutokea kiongozi ambaye atakuja kutatua matatizo yote yanayokuwepo katika taifa letu kwa wakati mmoja lakini ni haki yetu kutegemea kupata kiongozi ambaye atakuwa na ajenda chache ambazo atazisimamia na kuzikamilisha katika kipindi chake cha uongozi.

kwa mfano Nyerere alianzisha na kusimamia ajenda ya kuwa na taifa moja lenye watu wa namna mbalimbali lakini lenye umoja na amani. Mwinyi alisimamia ajenda ya kuufanya uchumi wetu kuwa uchumi wa soko huria na lenye ushindani.
Mkapa alisimamia ajenda ya utandawazi na kuimarisha miundo mbinu ya barabara zetu. mambo haya ndiyo tunayoyahusisha na utawala wa marais waliotutangulia, je ajenda ya rais kikwete ni ipi?
 
Hii ni ya chini Mno.

Hamuwezi kutafuta chanzo cha matatizo yenu kwa kiongozi aliyeongoza nchi mara ya Mwisho miaka 26 iliyopita! Miaka 26 inatosha kabisa kuibadili nchi. Hawa apologists wa Kikwete na Kikwete mwenyewe wanakera watanzania na hasa wanatia kichefu chefu wanapojaribu kuhalalisha kushindwa kwao kwa kumtumia kiongozi aliyetoka madarakani miaka 26 iliyopita. Jamani hamuoni aibu??

Nyerere si malaika, hata yeye alisema hakuwa malaika. Wote tulioishi enzi zake tunajua hakuwa malaika. Tulitarajia wale waliomfuata waanzie pale alipoishia. Bahati mbaya sana waliomfuata wamevuruga hata pale alipoishia. Sasa wanalalama eti yeye ndo chanzo cha matatizo, ebu oneni aibu. Miaka 26 tangu aondoke Nyerere mmeshindwa kurekebisha katiba na miaka 12 tangu aondoke duniani, bado mnalalamika eti katiba mbaya yeye ndo aliyeiacha, halafu mnatarajia tuwaone mna akili.

Shame on CCM, Shame on Kikwete administration. Kama heshima anayopata Nyerere inawachefua, jiulizeni kwa nini watanzania tunamheshimu. Hatuwezi kuwaheshimu wezi na Majambazi. Katika viongozi waliostaafu, Mzee Mwinyi anaheshima zaidi, pamoja na kuwa kwenye utawala wake rushwa ilitamalaki, bado Mwinyi aliondoka madarakani mwaka 1995. Leo hii 2010 tungeshoiondoa rushwa hiyo kama kweli tungekuwa na nia njema. Sioni haja hata ya kumlaumu Mwinyi aliyeongoza miaka 16 iliyopita. Hiki bado ni kipindi kirefu mno kufanya mapinduzi makubwa na kuibadili Nchi. Kwa hiyo failure za Kikwete haziwezi kuelekezwa kwa kiongozi mwingine yeyote aliyetangulia ni kwake mwenyewe!

Mwaka 2005 wakati tunamshangilia Kikwete tulijua kuwa huko nyuma kulikuwa na matatizo. Tulicho tarajia ni yeye kurekebisha mambo si kuendeleza wizi ulioanzishwa wakati wa mkapa. Kibaya zaidi Kikwete analigawa taifa hili kwa misingi ya udini. Hilo hatalikwepa na historia itamkumbuka kwa hilo, kati ya viongozi waliomtangulia ni nani aliyeegemea kwenye dini yake kama si Kikwete. Asijidanganye, kadri mnavyomsakama Slaa eti ni Mdini, watanzania tunawaangalia ninyi mlioko madarakani.

CCM imekufa na Kikwete hawezi kumlalamikia yeyote kwa kuiua CCM. CCM inakufa kwa sababu uongozi umeacha majukumu yake ya kuhakikisha kuwa chama kinasimamia misingi yake. Chama kimegeuzwa gulio la walanguzi na matapeli waliokubuhu. Wananchi tunawaona, unaweza ukamlaumu kiongozi yeyote kwa tabia ya Kikwete kuwakumbatia kina Lowassa, Kina Rostam Aziz, Kina Chenge, Kina Mramba, n.k. Ni viongozi wangapi wakati wa Nyerere walifukuzwa na kutiwa Lupango? Kikwete alitaka Nyerere aje kumsaidia kuisafisha CCM? Nyerere hakusema Lowassa hafai kuwa kiongozi? Ni nani alimlazimisha Kikwete kumfanya Lowassa waziri mkuu??

Acheni unafiki, ... Acheni uongo, .... Acheni uzushi. Kama heshima anayopewa Nyerere inawatia kichefu chefu, jitieni vidole mtapike. Nyerere anaheshimiwa kwa sababu ya aliyoyafanya. Hata kama hakufanikiwa sana, Watanzania wanamjua Nyerere kama mwenzao. Hawana haja ya kuambiwa.

Watanzania hao hao wanamjua Kikwete. Kikwete huyo huyo anayesema Richmond ni Kampuni hewa, halafu anasema Dowans wametupa umeme kwa miezi tisa. Watanzania tunajua jinsi Rostam alivyompeleka Kikwete ikulu akiwa amempandisha kwenye toroli, halafu yeye Rostam akilisukuma hilo toroli. Rostam huyo anayeapa kuwa hajui chochote kuhusu Dowans, Lakini akiwa na mikataba inayoonesha kuwa yeye ndiye anayeendesha shughuli zote za Dowans.

Mbona Rostam hajaja kwenye vyombo vya habari kukanusha yaliyoandikwa na Gazeti la East African. Ikiwa hayo hayakanushikii Kikwete uko wapi, wakati aliyekupeleka ikulu amechafuka hivyo. Unataka watanzania tukuheshimu kama Nyerere? ..... Wivu unakukereketa?
 
Unachekesha,badala ya kuelimisha,Tofautisha zama na nama

faraji, nimekuchekesha kwa lipi hapo kaka? kama unajaribu kuijibu hoja yangu naomba uainishe maeneo unayoyaona kuwa yana mapungufu, hapo ndio utakuwa umenisaidia na kunielimisha siyo kutoa ka sentensi kamoja ambako hakaoneshi msingi wake ni upi.
karibu sana kwenye jukwaa kaka.
 
ilovef.jpg
Kwa kauli hii Kikwete anatakiwa kwenda Mwitongo kwenye kaburi la Nyerere na kutubu. kwani hakumtendea haki Mwalimu Nyerere
 
Ebu jamani acheni ku-show up a very big level of ignorance kwenye leadership, hivi kuna watu mmemuona Nyerere mtume?? Nyerere alishindwa vitu VINGI SANA NCHI HII NA ALIFANIKIWA KWNYE VITU VINGI SANA PIA.... this is reality, japo asilimia 99 ya Kikwete ni mbovu bado ana asilimia yake moja ya mazuri.........

Swala la Nyerere kushindwa halijaanza na Kikwete, wasomi, papers, books, articles nyingi zinaandika hayo HUO NDIO UKUBWA NA DEMOKRASIA-VITU VINGI LEO HAVIENDI SOURCE NI NYERERE!!! katiba hii mnaoililia source ni Nyerere he failed!!!!. Cha kujiuliza ni Kikwete kasema kwa mazingira gani?? kasema kwa kebehi kame vile anafabya makusudi kutoongoza nchi vizuri?? kwa nini hasa kasema hivyo??

Lakini hawezi kupata laana kwa kusema hivyo cammon Nyerere ni mtu, siyo mtume, siyo jini, siyo ghost ni mtu, aliishi akafa!!!! haya ya laana is justa nother nonsense ...kwa hiyo tulivyosema Mkapa kaiba, Mwinyi karuhusu Rushwa tutapata laana??? ebu futa thread

Una ukweli ndani yako. Labda nikukumbushe kitu hiki,: mchambuzi yeyote anayeweza kutoa tathimini yenye hoja zilizosimama ni yule ambaye aghalabu unbiased!. Mimi binafsi namtaza mwl Nyere na uongozi wake,mapungufu yake na mafanikio yake ktk angle hii:-1. Wakati anaichukua tanganyika,wasomi ambao angekaa nao kuweka mikakati ya kimfumo na utawala miongoni mwa watanganyika walikuwa wakihesabika..Sina kumbukumbu vizuri iliwahi kusemwa alianza akiwa na mainjia wasiozidi watano(naweza kusahihishwa).
2..katika mazingira duni,wasomi wakuhesabika,miundombinu isiyopitika,uchumi mbovu, nk ,mwl alijitahidi kwakweli kwa asilimia 100% (KWA WACHAMBUZI WANAOANGALIA MAZINGIRA YA TANGANYIKA 1961 kama nilivyoanisha hapo juu) kujenga Nchi yenye kuheshimiana,usawa,na ustaarabu. Kumbuka misingi na fikra zake juu ya Arusha declaration.,kufanikiwa au kutofanikiwa ni jambo lingine but dhamira na uthubutu unapambanua Mwl ni kiongozi wa aina gani..
Anyway,ninayomengi mno kutetea misingi na utukufu wa mwl in leadership. Huwezi kulinginsha wanariadha tamati zao bila kugusia muda na startng point zao. Lets say,mmoja aanze saa moja asubuhi poitia A, na mwingine aanze zaa tatu asubuhi point B ahed of opint A,then useme wote at the same contant speed wafike point C at ttime, huo ni uwendawazimu.
Mkuu Waberoya,nakuheshim sana,but kwa wenye hekima,kumsema mwl mapungufu yake kwa misingi ya kujitetea,au kuhalalisha upuuzi wao, ni UPUNGUANI. SI KWASABABU HAKUKOSEA,HAPANA,BALI KWA AINA NA UWAJIBIKAJI WA SERIKALI YAKE,ALIYOIONGOZA KWA KUANZIA NA WASOMI WATAALAM KIDUCHU,NA UMASKIN WA NCHI,UCHUMI AT ZERO,MIUNDOMBINU ZORO, THEN ULINGANISHE KIKWETE NA WASOMI WASHAURI KIBAO,ANAAMUA KWA MAKUSUDI KUCHAGUA MATAPEL BADALA YA WAZALENDO WASOMI,THEN UTETEE, NOOO!!! n
 
Alipokuwa akiongea hayo maneno, washabiki wa CCM walishangilia, au walikuwa wakimtazama tuuu!!
 
Alipokuwa akiongea hayo maneno, washabiki wa CCM walishangilia, au walikuwa wakimtazama tuuu!!

teh teh teh... hata hao washabiki walishindwa kushangilia jana, nadhani walikuwa wamepigwa na butwaa wakiwa hawaamini wanachokisikia....
 
Mkuu naona hii statement ya Kikwete imepokelewa kwa hisia tofauti
1. Kwanza kwa nini amesema hivi? is it excuse?? if is excuse then this is wrong
2. Kazungumza kama vile ana-recall historia ili atupeleke mahali pazuri au kasema hili naye a-fail??

All in all ukiondoa statement hii kuwa kaisema Kikwete, ukweli matatizo mengi sana nchi hii source yake ni Nyerere, Nyerere alishindwa kwa vingi na vile vichache alivyofanikiwa vimekuwa landmark.

Kwa udhaifu au failure za Nyerere rais pekee ambaye ngekuja kujenga alipoharibu Nyerere ni yule ambaye angekuwa visionary kama Nyerere, yaani baada ya Nyerere marais waliokuja wote walikuwa vilaza akwemo huyu JK. afadhali mkapa sana and may be is second to Nyerere.

Kushindwa kwa Nyerere sio chuki, angalia siasa yake, katiba, kuondoa vyama vingi, maamuzi ya wananchi, uchumi, n.k although he failed he is still the best president ever... i mean he failed but he had good intentions and righ reasons, etc HII NDIO HASA quality of leadership. JK kafeli kabisa hana hata good intention wala good reasons...

Waberoya,

Wakati wengi tuna amini kwamba Nyerere kuna mengi alishindwa, jambo moja tutakubaliana kwamba Nyerere alikuwa na maono ya wapi anataka kupeleka Tanzania.
Lakini pia Nyerere hakuweza kutimiza malengo kwa sababu nchi ilikuwa changa, hakuna wasomi wakutosha wala uchumi wenye nguvu.

Viongozi wanaofuatia hawapaswi kujifariji kwa vile tu aliyetangulia hakufanya vema. Wanasema makosa mawili hayafanyi jambo kuwa sawa. Hii wala sio cheap excuse bali ni LAME EXCUSE.

Nimepata kusema kabla kwamba JK aliutaka sana urais wa URT lakini hakuwa na hana maono ya nini alitaka kufanya akipata urais.
Watu waliom-support kupata kiti hicho ni wachafu pasi mfano ni kiongozi asiye maono tu angeweza kuwafanya kuwa timu yake ya Ushindi.

Angalia kina nani walikuwa timu ya S. Ahmed (2005) na wale walokuwa ama wako timu ya JK (2005-2010).

JK can be a good man BUT have failed to make a good leader!

Ili tutoke hapa tulipo we need a RADICAL PRESIDENT bila kujali anatoka wapi so long as ni mtanzania mwenye DIRA.
 
Back
Top Bottom