Kikwete: Hata Nyerere alishindwa ingawa tunamsifu sana

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,214
Leo katika hotuba yake ya siku ya kuzaliwa CCM, kuna kauli nyingi za Kikwete ambazo kama Rais hakustahili kuzisema, mojawapo ni kauli yake ya kwamba pamoja na kumsifu sana Nyerere lakini alishindwa kutatua changamoto nyingi katika utawala wake na hivyo hivyo kwa marais wengine waliomtangulia, sembuse mimi (Kikwete). Alisema hayo akijitetea kwamba yeye sio wa kwanza kushindwa kuondoa matatizo ya watanzania.

Mimi nimeichukulia kauli hii kama simple/cheap excuse ya Kikwete kwa jinsi alivyoshindwa kutatua matatizo ya watanzania. Sio tu Kikwete ameshindwa kutatua matatizo bali ameyaongeza na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu zaidi. Anaweza kutuambia yeye kama Rais ame-achiave nini, wenzake wote wana vitu vya kujivunia.

Nyerere alijenga umoja wa kitaifa na kufanya watanzania kuwa wamoja na kuwepo kwa amani ambayo kikwete anajivunia leo, lakini pia mzee huyu alijenga uwajibikaji kwa watumishi wa umma kitu ambacho kikwete ameshindwa.

Mzee Ruksa aliruhusu uchumi wa soko ambao ulisaidi kufanya upatikanaji wa bidhaa muhimu ambazo mwanzo zilionekana kama anasa.

Mzee Mkapa akajitahidi kujenga uchumi imara bila kusahau miundo mbinu na kurudisha heshima ya wafanyakazi.

Pamoja na mapungufu yao viongozi waliopita wanayo ya kujivunia.

Akaja Kikwete
1) Akaharibu kabisa umoja wa kitaifa kwa kuanza na makundi ndani ya CCM (kwa kuanzisha mtandao wake uliowavuruga wengine) na baadae kuharibu umoja taifa zima kwa kuchochea ajenda zake za udini na ukabila.
2) Akabomoa kabisa uchumi alioujenga mzee Mkapa kwa kuendekeza anasa, matumizi makubwa serikalini, kusafiri kwenda kubembea na kuendekeza ununuaji wa magari ya kifahari yasiyo na tija, gharama za maisha zimepanda mno, thamani ya shilingi imeshuka sana, mfumuko wa bei hauelezeki.
3) Ametengeneza mitandao ya wizi kwa kuwatumia marafiki zake kama RA, ED kwa kutaja wachache.
4) Akaharibu kabisa mfumo wa elimu kwa kuanzisha kisiasa shule za kata zisizo na walimu wala vifaa, ukiangalia wanafunzi wanaofeli ni heri hata tungebaki na shule chache bora,maana waliofeli wanabaki kuwa darasa la saba hawawezi kusema wana elimu ya form IV.
Ni mengi jamani yanayoonyesha tofauti ya utendaji kazi wa kikwete na watangulizi wake, naomba niishie hapa.

Lakini Kikwete please dont look for cheap excuses, just admit that ur the most failure president we ever had.
 
Pia anatumia udini kama kivuli chake kutishia wananchi, na sasa ameshauleta udini. Slow learner yule
 
the guy is a terrible failure! mimi tangia 2005 nilisema salim ndie ulistahili urais na kwamba huyu jk ni bogus watu wakabisha, udhaifu wake hauna kificho tena!
 
Binafsi, naamini sasa kuwa usomi wa kikwete uko kwenye vyeti kama alivyowahi kudokeza Dr Slaa siku chache zilizopita.
 
JK anatia huruma. Pamoja na kujua na kukiri kuwa ana weakness bado anashindwa kuchukua hatua. Aibu sana kwa huyu check bob!
 
leo katika hotuba yake ya siku ya kuzaliwa ccm, kuna kauli nyingi za kikwete ambozo kama rais hakustahili kuzisema, mojawapo ya ,ni kauli yake ya kwamba pamoja na kumsifu sana nyerere lakini alishindwa kutatua changamoto nyingi katika utawala wake na hivyo hivyo kwa marais wengine waliomtangulia, sembuse mimi (kikwete). Alisema hayo akijitetea kwamba yeye sio wa kwanza kushindwa kuondoa matatizo ya watanzania.

Mimi nimeichukulia kauli hii kama simple/cheap excuse ya kikwete kwa jinsi alivyoshindwa kutatua matatizo ya watanzania. Sio tu kikwete ameshindwa kutatua matatizo bali ameyaongeza na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu zaidi. Anaweza kutuambia yeye kama rais am-achiave nini, wenzake wote wana vitu vya kujivunia.
sio kweli, ana mengi ya kujivunia, tusingeyafahamu ya epa, na ufisadi woote kama sio kuiachia democracy ifanye kazi yake, uhuru wa kweli, uwazi ukweli na uwajibikaji wake!
nyerere alijenga umoja wa kitaifa na kufanya watanzania kuwa wamoja na kuwepo kwa amani ambayo kikwete anajivunia leo, lakini pia mzee huyu alijenga uwajibikaji kwa watumishi wa umma kitu ambacho kikwete ameshindwa.
sio kweli, nyerere alikuza tabaka lililokuwepo la wasiothaminiwa na watawala wa kikoloni waliojitahidi kila kona kutafuta uhuru yaani waislamu na wakristo ambao aliendelea kuwapendelea bila kificho na kwa kufuata kwa unyenyekevu kabisa maagizo ya maaskofu katika masuala mbalimbali ya utawala wa nchi, refea kisa cha padr wa kikatoliki kumuita nyerere na kumfokea pindi akiteleza kufuata maagizo yake, kaasisi kwa ustadi mkubwa mfumo kristo utakaiingiza nchi hii katika machafuko kama watawala watajifanya hawauoni! Mfumo ambao una madhila makubwa kwa waislamu ambao ni majority, na ambao umepelekea serikali kuwa na mou ya kusaidia makanisa wakati huo huo hoja ya kujiunga na oic , na mahakama z ya kadhi zikionekana za kidini zaidi!
mzee ruksa aliruhusu uchumi wa soko ambao ulisaidi kufanya upatikanaji wa bidhaa muhimu ambazo mwanzo zilionekana kama anasa.

hii ni kweli lakini naye ana mapungufu pengine ni kuzidiwa na mfumo kristo maana mou iliandaliwa kipindi chake na kutiwa saini na edwad luwasa hatujui kama alikuwa na habari au alishtukia mfumo kristo ulioasisiwa na nyerere umeshafaya kazi yake.
mzee mkapa akajitahidi kujenga uchumi imara bila kusahau miundo mbinu na kurudisha heshima ya wafanyakazi.
huyu yeye uchumi alioujenga ni sawa na kuuza rasilimali za nchi kwa bei ya kutupa halafu ukajaza mapesa yasiyo endelevu na hatimae unaondoka madarakani kuuza vimeisha! Amesifika kwa kuutumia ujambazi kujinufaisha akiwa na mahita, aidh ni raisi wa kwanza kuifisadi nchi yeye mwenyewe kwa mkono wake hivyo asingeweza kumkemea fisadi yeyote katika utawala wake, wakati huo vinara wa leo wa ufisadi akina mengi walikuwea wanafisadi chinichini hivyo wasingethubutu kuongea kitu!
pamoja na mapungufu yao viongozi waliopita wanayo ya kujivunia.

Akaja kikwete
1) akaharibu kabisa umoja wa kitaifa kwa kuanza na makundi ndani ya ccm (kwa kuanzisha mtandao wake uliowavuruga wengine) na baadae kuharibu umoja taifa zima kwa kuchochea ajenda zake za udini na ukabila. makundi aliundiwa na aliowashinda ambao hawakukubali ashinde, uungwana aliouonesha yeye alivyonyanganywa urais na nyerere huku akiwa amemshinda mkapa haukutosha wapinzani wake kumkubali baada ya yeye kuwa rais, makundi hakuunda ila hilo lilikuwa zengwe ili aonekane kaunda makundi, tunajua!
2) akabomoa kabisa uchumi alioujenga mzee mkapa kwa kuendekeza anasa, matumizi makubwa serikalini, kusafiri kwenda kubembea na kuendekeza ununuaji wa magari ya kifahari yasiyo na tija, gharama za maisha zimepanda mno, thamani ya shilingi imeshuka sana, mfumuko wa bei hauelezeki.wastani wa ukusanyaji mapato ulisha double ule wa mkapa changamoto za kiuchumi alizokutana nazo amezisolve silently bila kuathiri sana uchumi wa mtu mmojamoja, pamoja na uchumi uliokuwepo wakati wa mkapa bado hali ya mwanachi wa kawaida ilikuwa mbaya sana na biashara za wajasiriamali wengi zilikufa wakati huo
3) ametengeneza mitandao ya wizi kwa kuwatumia marafiki zake kama ra, ed kwa kutaja wachache. ametokomeza ujambazi karibu unakwisha kabisa
4) akaharibu kabisa mfumo wa elimu kwa kuanzisha kisiasa shule za kata zisizo na walimu wala vifaa, ukiangalia wanafunzi wanaofeli ni heri hata tungebaki na shule chache bora,maana waliofeli wanabaki kuwa darasa la saba hawawezi kusema wana elimu ya form iv.
ywatoto wengi wa walalahoi wameiona sekondari, changamoto kama za kufeli kwa kukosa walimu zinatatulika na zimeanza kushughulikiwa tatizo lenu mlitaka tabaka la ninyi watoto wa kota mnaosomea shule za misheni tu ndo muitwe mmefika sekondari na vyuo , wenzenu wa uswahilini hata sekondari iwe ni mtihani kwao, sikitikeni tu maana mmepunguziwa mahousegirl mnaowabaka kila siku majumbani mwenu kwa ajili ya uwepo wa shule za kata
ni mengi jamani yanayoonyesha tofauti ya utendaji kazi wa kikwete na watangulizi wake, naomba niishie hapa.huna lolote ni chuki tu zinakusumbua, ni yeye ndo ameruhusu muendelee kumchafua humu na kujifurahisha ili kupanua demokrasia na uhuru wa habari!


lakini kikwete please dont look for cheap excuses, just admit that ur the most failure president we ever had.

huwezi kumlinganisha kikwete na waliomtangulia kwa uzalendo mkubwa aliouonyesha kwa nchi ya tanzania, amefanya mengi katika uchumi, katokomeza ujambazi n.k nenda kisekta utaona ni yepi ameuyafanya katkika utawala wake, na kwa taarifa yako ameshajenga km nyingi za lami kuliko marais wote waliomtamgulia, n akwa mara ya kwanza tokea uhuru mikoa ya pembezoni k.m kigoma ndio kwanza inaanza kuelewa kuwa nayo ipo tanzania
 
Binafsi sikuwahi kumtambua kama rais kutokana na jinsi kambi yake ilivyomzulia Salim A.Salim ili tu yeye apate urais. Lakini kama kweli amesema hivyo, siyo tu kwamba ni kilaza bali pia hana adabu kabisa... Hivi kweli anaweza kutwambia ni wapi ambapo watangulizi wake walifeli yeye amerekebisha? Jamani! Kamateni huyo mtu mkampime akili... wallah nawaambia akili yake haiko sawa.
 
huwezi kumlinganisha kikwete na waliomtangulia kwa uzalendo mkubwa aliouonyesha kwa nchi ya tanzania, amefanya mengi katika uchumi, katokomeza ujambazi n.k nenda kisekta utaona ni yepi ameuyafanya katkika utawala wake, na kwa taarifa yako ameshajenga km nyingi za lami kuliko marais wote waliomtamgulia, n akwa mara ya kwanza tokea uhuru mikoa ya pembezoni k.m kigoma ndio kwanza inaanza kuelewa kuwa nayo ipo tanzania

Ndugu taratibu!
haya ya EPA angeweza kuyazuia yasijulikane angefanya hivyo kwa sababu na yeye yupo kwenye hizo dili kwani ndizo zimemweka madarakani, kuna wazalendo walivujisha siri na ushahidi ukawepo asingeweza kukwepa. Hizo Km alizojenga ziko hewani, naona kama anakarabati alizojenga mkapa.

Uchumi gani alodhibiti wakati watu mmoja mmoja ndio wako hoi kiuchumi, tembelea vijijini lakini hata mijini maisha ya watu ni magumu mno.

Halafu hakuna mwenye chuki na kikwete, mimi ni kati ya watu waliomshabikia sana mwanzoni lakini jinsi alivyoshindwa kufanya niliyoyategemea nadhani he is a failure and u should also admit that.

Hana uwezo wa kuzuia watu kusema tena sio kwamba anaruhusu.
 
hakuna hoja ya maana,zaidi ya chuki ndo imewatawala. Nyinyi mkisema maneno ya hovyo ok,sisi no. Tatizo JF imeingia ushabiki wa dini na vyama. Nasi twaenda kwa style iliyopo. Kwahiyo tuvumiliane
 
Ndugu wana JF, leo katika hotuba ya kijani ya JK, nimemsikia akijaribu kutolea mfano ambao hauendani na wakati, eti serikali haiwezi kufanya vitu vizuri vyote kwasiku moja, eti ndomana hata Nyerere hakuvimaliza vyote. Hivi ukilinganisha mambo aliyoyafanya Nyerere mzee wetu katika nchi hii anaweza kujilinganisha nae kweli? Jamani si kumvunjia heshima Mzee wa watu? Au ndo laana zenyewe zinaanza kumwingia huyu mtu?
 
Kamwe asijifananishe kushindwa kwake na kushindwa kwa Nyerere. Mwalimu kuna mengi sana aliyoyafanya ndani ya nchi yetu ambayo matunda yake hadi hii leo bado tunayaona pamoja na kupigwa vita sana na nchi za magharibi kwa kuamua kufuata siasa ya ujamaa na kujitegemea. Yeye hakuna hata kimoja alichokifanya zaidi ya uVDG na kuwakingia kifua mafisadi wenzie.
 
the guy is a terrible failure! mimi tangia 2005 nilisema salim ndie ulistahili urais na kwamba huyu jk ni bogus watu wakabisha, udhaifu wake hauna kificho tena!

Wakamuandalia zengwe Salimu sio mtanzania...leo mambo yanawashinda wanasingizia wanaonewa kwasababu ni dini tofauti. DuuH! Wengine hatifikirii mbali zaidi ya urefu wa macho yetu.
 
The biggest difference btn him na Nyerere ni kwamba JK is completely out of touch........ pamoja na kujipigisha piacha na walemavu, wanakijiji, maskini but he doesn't have a clue as to how it means by being one of those. Na hiii yote imesababishwa na ulimbukeni.
 
hakuna hoja ya maana,zaidi ya chuki ndo imewatawala. Nyinyi mkisema maneno ya hovyo ok,sisi no. Tatizo JF imeingia ushabiki wa dini na vyama. Nasi twaenda kwa style iliyopo. Kwahiyo tuvumiliane

Nani ni Nyinyi na Nani ni sisi, Mkuu ? nani ameongelea udini hapa ?,
Mkuu wewe ndio umeporomosha matusi kwenye hii post..,
Kumbuka Respect works both ways.. you have to give one to receive one...
 
hakuna hoja ya maana,zaidi ya chuki ndo imewatawala. Nyinyi mkisema maneno ya hovyo ok,sisi no. Tatizo jf imeingia ushabiki wa dini na vyama. Nasi twaenda kwa style iliyopo. Kwahiyo tuvumiliane

dos santos sio uzalendo matusi -manake wote tupo hapa bongo, unajidanganya kudhani kwamba watu hawajui unayemhusudu alivyomchafu kitandani, usipende kukimbilia hoja za kitandani manake kurasa za unaowahusudu zinatia kinyaaaa huwezi kulinganisha na dr slaa, kuna watu wameliwa tigo wakapewa uongozi, kuna watu wananyea debe kwa kuchangia tigo za machangu na unaowahusudu-kwa hiyo mimi nadhani tuwe wazalendo mambo ya vitandani tuyaache huko. Tujadili maada kama waungwana bila kumvunjia mtu heshima.
 
Back
Top Bottom