Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Mambo mengi yamesemwa humu ndani kuhusu uhusiano wa Lowassa na Jakaya Kikwete na ile hoja kwamba wawili hawa hawakukutana barabarani inajulikana na kila mmoja wetu. Lakini Historia inaonyesha kwamba ni Lowassa ndiye aliyemtengeneza Kikwete kuwa "Presidential material" na wala si Kikwete aliyemtengeneza Lowassa. Kwa maana nyingine Kikwete ni zao la Lowassa.
Hata timu za ushindi na jinsi ya kukusanya fedha na kuteka nyara vyombo vya habari likuwa ni kazi ya Lowassa. Ukiangalia kwa undani bila ya makengeza ya ushabiki utagundua kwamba Kikwete "aliwekwa" na wanamtandao na wanamtandao ni kazi ya mikono ya Lowassa.
Walipoingia madarakani ni Lowassa ndiye aliyekuwa anaonyesha njia ni wapi wanaelekea, shule za kata na hata kuhimili serikali za mitaa ilikuwa ni kazi ya Lowassa. Lakini tangu Lowassa alipopata "ajali ya kisiasa" na "kuachia ngazi" serikali ya Kikwete imepata myumbo mkubwa sana na hakuna dalili kwamba itatoka huko iliko na badala yake siku hadi siku inapoteza uhalali wa kutuongoza watanzania.
Lakini swali langu linalohitaji kujadiliwa ni kama Kikwete amepoteza Mwelekeo kutokana na Lowassa kujiondoa kwenye serikali yake au tangu mwanzo wakiwa na Lowassa tayari walishapoteza mwelekeo?