PayGod
JF-Expert Member
- Mar 4, 2008
- 1,259
- 57
- Thread starter
- #21
Wadau, nimeona niwakumbushe , kuhusu huyu mgombea wa ubunge ,kupitia CCM EMAMANUEL LUHAHULA, huyu ni yule mbunge ambaye mwaka jana alivamiwa na majambazi na kupolwa bastola na majambazi, kwa kushindwa kuitumia.
Mbunge Luhahula acharangwa mapanga
• Avamiwa na majambazi, aporwa bastola
na Stella Ibengwe, Shinyanga
KUNDI la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamemvamia Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Luhahula, pamoja na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Mberito Magova, na kuwajeruhi vibaya kwa mapanga na marungu.
Licha ya kuwajeruhi vibaya, majambazi hayo yalifanikiwa kupora bastola na vitu vingine walivyokuwa navyo mbunge huyo na katibu huyo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Nasikukulu wilayani Bukombe mkoani hapa, majira ya saa 4 za usiku wakati mbunge huyo akitoka Kahama kuelekea nyumbani kwake Bukombe.
Luhahula alikuwa akitumia gari yake aina ya Toyota Cresta yenye namba za usajili T 510 ANV. Akakumbana na tukio hilo akiwa amebakiza kilomita 20 kufika eneo la Ushirimbo ambako ni nyumbani kwake.
Alipofika katika kijiji hicho, alikuta mawe makubwa yamepangwa barabarani na ghafla alivamiwa na kundi la watu waliokuwa wamejificha vichakani na kuanza kuwashambulia.
Habari zaidi zinasema, mbunge huyo alifika Kahama usiku na kulazimika kutafuta dereva ili amsaidie kuendesha gari kuelekea jimboni kwake.
Habari zaidi zinasema, mbunge huyo aliokolewa na wananchi waliofika eneo la tukio hali iliyosababisha majambazi hayo kukimbia.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Sospiter Boyyoh, alisema Luhahula alijeruhiwa vibaya sehemu za kichwa; ameshonwa kwenye majeraha yake matatu.
Alisema mbali ya kuumia kichwani, pia alitokwa na damu nyingi hali iliyosababisha kuwekwa chumba maalumu cha uangalizi ili kuokoa maisha yake, tofauti na ilivyokuwa wakati anafikishwa hospitalini hapo.
Alisema mbunge huyo alijeruhiwa mkono wake wa kulia na kukatwa na panga kichwani na kuporwa simu yake ya mkononi na fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu, Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Magova, alisema katika tukio hilo, alifanikiwa kukimbia baada ya kuvamiwa ingawa tayari alikuwa amekwishajeruhiwa kichwani kwa kukatwa na panga.
Alisema hadi jana mbunge huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya na kwamba hali ya mbunge huyo haikuwa nzuri.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Daudi Siasi, alithibitisha kutokea kwa tukio na kwamba hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa.
"Nimemwagiza mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) kufuatilia suala hilo kwa makini ili kubaini wahusika ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Kamanda Siasa.