Changamoto ya maji wilaya ya Handeni mkoani Tanga ulikuwa mtaji wa kisiasa. Mradi wa htm ni taa ya giza la muda mrefu

Almalik mokiwa

Senior Member
Jun 5, 2020
147
157
Anaandika Almaliki Mokiwa
Februari 28, 2024.

Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga ni eneo lenye 6,534 km² lililopakana na Wilaya ya Kilindi upande wa Magharibi, Wilaya ya Korogwe na mkoa wa Kilimanjaro kwa upande wa Kaskazini huku likipakana na wilaya ya Pangani kwa Upande wa Mashariki na Mkoa wa Pwani kwa upande wa Magharibi.
download (1).png

Shughuli kubwa ya kiuchumi katika wilaya hii ni Kilimo, hasa kilimo cha Mihogo pamoja na shughuli nyingine za kibiashara.

Ni wilaya iliyobarikiwa Siasa Tulivu zisizo na ukakasi. Itakuhitaji kuwa na Sera nzuri na uwezo wako mkubwa wa ushawishi kuwafanya wananchi wa wilaya ya Handeni kuwa upande wako.

Wananchi wa Wilaya ya Handeni wamekuwa wakinywa na kupikia tope (maji yasio safi na Salama) tangu Uhuru 1961. Wawakilishi wa wananchi Bungeni, ambao ni sauti ya wananchi wasiopungua 384,353 wamekuwa wakitumia Changamoto hiyo kujinufaisha kisiasa kila ifikapo nyakati za Uchaguzi mkuu. Ahadi za kuwaletea wanaHandeni maji zimekuwa zikiwashwa wakati wa kampeni na kuzimwa kama mshumaa mara baada ya Uchaguzi kuisha, utekelezaji Zero. Maelezo?. Hakuna. na wakati mwingine baadhi ya wabunge waligeuka kuwa mabubu wanapokuwepo kwenye ukumbi wa Bunge, utadhani wamenyweshwa uji wa gundi, wakijisahau kuwa wametumwa wakalete Maji na kuboresha shughuli za kimaendeleo.
download (17).jpeg


Mwaka 1974, Mzee Mussa Masomo akiwa Mbunge wa wilaya ya Handeni aliusemea mradi wa HTM kuletwa wilayani Handeni ili kupunguza kero ya ukosekanaji wa maji na kunyonya kiwango kikubwa cha ukame kinacho wabagaza wananchi wa wilaya hii ya kibiashara. Mradi ule ulikuwa ni mpango wa miaka 20, ukilenga kuwanufaisha wananchi wapatao Elfu Ishirini ikiwa makadirio ya idadi ya watu kwa wakati huo haikuwa ikipungua Elfu tisini. Maazimio ya uboreshwaji wa mradi huo muda baada ya Muda uliegemezwa kuoanisha baina ya Ongezeko la watu na mahitaji ya lita za maji kwa wakati huo. Ilipofika mwaka 1994, mradi ule ukaisha muda wake, wakina mama wakarudisha ndoo kichwani kufata maji zaidi ya Kilometa 10.

download (18).jpeg


Katika kutafakari juu ya uwepo wa adha hii ya UKAME na kukosekana mtu sahihi wa kuwasemea Bungeni, wananchi wa Handeni walikubali kuigeuza Changamoto ya ukosekanaji wa maji safi na Salama kama sehemu ya maisha yao na kuziridhisha nyoyo zao kuwa, Handeni bila maji Inawezekana na utatuzi wa Changamoto ya maji ni jambo lisilowezekakana. Wakaendelea kuchapa kazi na kumwachia MUNGU kwasababu, matatizo ni Mtazamo. Namna unavyoliona tatizo wengine wataona Fursa, na ndio maana Franklin D. Roosevelt Rais wa 32 wa nchi ya Marekani, alipoona mataifa ya Ulaya na Dunia yanaingia Vitani Septemba 1, 1939 yeye aliona Soko la kuvuna mabilioni kupitia uuzaji wa Silaha, huku dunia ikiona damu, vifo na ufilisi wa mali.

download (19).jpeg


Mwaka 2020 wakati wa kampeni za Uchaguzi, likaamka jembe kutoka upande wa rangi ya mazao, akatia nia na kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge jimbo la Handeni mjini. Mheshimiwa Kwagilwa Samtagwa Mamba Lwaigwanani Longishu (Kwagilwa Ruben Nhamanilo) ambaye alikuwa Katibu Myeka wa naibu katibu mkuu CCM bara mwaka 2012 (Dr Mwigulu Lameck Madelu Nchemba) na Mjumbe wa Kamati ya Bajeti Bungeni, akaja na Hotuba iliyoitwa "Kura yako kesho". Tuliozizoea siasa za wabunge wengi Handeni, ambao ni watamu wa maneno na wachungu katika utekelezaji, tulikaza mafuvu kuielewa hotuba ile ambayo kwa asili ya siasa za wilaya yetu tuliona ugumu katika utendaji na utekelezaji.
download (20).jpeg


Jamaa liliahidi mambo mengi ikiwemo uboreshwaji wa huduma za Afya, Elimu, barabara, umeme na MAJI. Aliyo ahidi mengi aliyasemea na matokeo yamekuja tumeyapokea tukisubiri ukamilifu wa baadhi ya miradi hiyo. Kwakuwa lengo la makala hii ni kuudadavua mradi wa HTM ambao umelenga kuleta mageuzi ya kuigeuza Handeni kutoka kuwa Jangwa na kuwa ardhi oevu nitajielekeza zaidi kwenye hoja ya Maji kwani ndio kilio kikubwa cha wana Handeni.

Mradi wa HTM ni mradi uliokadiriwa kudumu kwa miaka 50 ijayo, uliotengewa bajeti ya Shilingi 171 Bilioni, uliyolenga kuinufaisha miji 28 ikiwemo Korogwe, Pangani, Muheza na HANDENI kupitia uzikwaji wa mabomba makubwa ya maji ikiwa ni pamoja na kusafirisha maji kutoka Mto Pangani mpaka Wilayani Handeni, mradi huu umelenga kuzalisha na kusambaza lita za maji zisizopungua milioni 52 utakao wanufaisha wananchi wasiopungua 384,353 ikiwa ni pamoja na Tarafa 6, kata 21, Vijiji 91, na vitongoji 770.

Tarehe 2 Agosti 2023 meli kubwa ya kwanza ya mizigo ilitua Bandari ya Tanga kutoka India, ikiwa imebeba mabomba makubwa na Vifaa vingine kwaajili ujenzi wa mradi mkubwa wa HTM, na tarehe 25 Agosti 2023 vifaa hivyo vya mradi vilipokelewa Na wananchi wilayani Handeni. Hapo ndipo Imani ya uwezekano wa Handeni kuwa tepe tepe ikarejea. Baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Screenshot_20240228_015332.jpg



Safari hii ya kuusimika mradi huu mkubwa, utakao mtua mwanamke wa Handeni ndoo kichwani, imeanza ambapo ujenzi wa kuukaribia kujengwa kwa Tanki kubwa la lita milioni mbili za maji kijijini Bongi, umeshika hatamu. Vilevile, line ya kijiji cha Kwamatuku itatumika kusukuma maji kuelekea Handeni mjini katika mlima wa Samhandeni ambako Tenki la lita milioni mbili nyingine litajengwa mlimani. Hii inatoa picha ya uwepo wa matanki mawili ya lita 2000 ikiwa Tanki la mlimani Handeni litatawanya maji kwenye mitaa isiyopungua 60 na kata 12. Na changamoto ya maji ikalala Chali Wilayani Handeni.
download (21).jpeg


Mimi sio mzuri wa Siasa za Mapambio, lakini nitoe pongezi kwa Mbunge wa wilaya ya Handeni mjini, kwa kutembelea sera zake alizonadi wakati wa mkutano wa Uchaguzi 2020, vile vile kuwa mfatiliaji mzuri wa Miradi. Nakumbuka aliungana na madiwani kumkataa Mkandarasi wa Civil Loaths baada ya kuchelewesha Mradi mdogo wa ujenzi wa Bwawa la maji uliogharimu shilingi Bilioni 1.9, uliolenga kuwanufaisha watu 96,364.
download (22).jpeg


Pia, kutafuta ufadhili wa mradi wa bwawa la maji kutoka kwa Serengeti Breweries ambao walidhamini ujenzi wa bwawa hilo kata ya Kideleko uliogharimu zaidi ya milioni 380 kwa asilimia 90% na usimamizi wa miradi mingine ya maji.

Kwakuwa, Wilaya ya Handeni haina Chanzo chochote cha maji isipokuwa Mvua na mabwawa, uendelezaji wa ujenzi na uchimbaji wa mabwawa ni jitihada za kuifanya kero ya maji Handeni kuwa historia. Huku tukiendelea kusubiri kukamilika kwa mradi huu mkubwa wa HTM.

Ni matumaini yetu kuwa, tumefika mwisho wa kusubiri.
 
Nimezaliwa na sasa ni mtu mzima nasikia kitu kinaitwa HANDENI TRUNK MAIN. Kuna watu nawajua walikuwa katika mradi huo kutoka Idara ya maji Dar enzi hizo.... na vijana wengi (miakaya 70s). Leo bado mradi huo haujawahi toa maji ya uhakika kwa watu wa Hndeni
 
Back
Top Bottom