Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

Nchi nyingi hasa za ulaya mashariki zilizotupa ujamaa/ukoministi mara nyingi wawekezaji hawatoi kodi ni 0% ila wanachoambiwa tu mfano waajiri watu atleast 200 bila kupungua ndani ya miaka 10.

Sema kwetu balaa tu ni kwenye madini maana wanakuja kuchukua chetu, yani hawazalishi chochote bali wanachukua.Lakini mtu wa kampuni ya simu hata asipolipa kodi sawa tu tena poa tu.

Kama ameajiri watu 1000 ni mpuuzi tu atakayesema kwamba hawalipi kodi.
 
Tatizo siyo UJAMAA kama anavyotaka tuamini, Tatizo ni Viongozi pamoja na yeye wanaingiza nchi katika mikataba inayonyonya watanzania na kutufanya tuwe maskini zaidi wakati nchi imejaa utajiri. Viongozi wanaangalia maslahi yao binafsi katika mikataba ya hao wanaoitwa eti wawekezaji.

Kwa mtizamo wangu naona JK anapotuambia kukubali ufisadi, ulafi kupindukia wa viongozi wa serikali, na kunyonywa kunakofanywa na wawekezaji bandia ni sawa kusema Mgeni uchwara aje nyumbani kwako halafu wewe umpishe akalale chumbani kwako na mkeo, halafu wewe na watoto muwe mnalala nje ya nyumba wala si sebureni eti huo ndiyo ukarimu.

Jamani simwelewi kabisa - Ujamaa has nothing to do with uozo wa serikali
 
je ujamaa wa scandinavia nao utasemaje.....siasa zote ni noma muhimu ni watendaji wanatafsiri vipi kiuntendaji

Unajua watu wengi wanatazama mambo kijuu juu, tu. Uchumi wa ujerumani ya mashariki haukuwa mbaya kwasababu za sera za kijamaa, badala yake ni kwa sababu ya mambo mengi yaliyohusishwa na vita baridi. Hata wakati huo, zilikuwepo nchi ambazo zilikuwa zinafuata ubepari na uchumi wao ulikuwa mdogo kuliko wa hiyo ujerumani mashariki. Nchi za magharibi walifanikiwa wakati ule kwa propaganda (na mpaka leo kuna watu wanaamini hivyo) kuwa matatizo yoyote katika nchi zilizokuwa zinafuata usoshalist yalitokana na usoshalist wenyewe. Lakini cha kujiuliza ni je hata hapa Africa, nchi kama malawi, zaire, kenya, na zinginezo, zilikuwa zinafuata ubepari, je leo hii wako wapi? njaa tupu! Kenya wamebaki kuwa mgonjwa mwenye nafuu. Malawi nafikiri hata tz tumewazidi kwa sasa.

Ukiangalia nchi kama Cuba, Vietnam na North Korea, Venezuela, China, zote hizo zimekuwa zikifuata usoshalisti/ukomunist na pamoja na kwamba maendeleo yao hayajaifikia marekani au uingereza au Japan au ujerumani, bado, maendeleo yao yapo juu kuliko nchi nyingi tu ambazo zimekuwa zikifuata huo ubepari kwa muda mrefu.

Kwa hiyo, suala sio ujamaa au ubepari, suala ni SERIKALI inayojua KUTAWALA na wakati huo inajali watu wake, na watu wanaheshimu serikali yao na kuipenda nchi yao. Hapo bongo we unategemea nini, hata ukibadilishw mfumo wowote ule, hii hali ya ubinafsi tuliyonayo, hatuwezi kuendelea kamwe. Karibu kila mtu ni mwizi mwizi, na yupo tayari kuuza nchi kwa manufaa binafsi. Uzalendo una-approach zero.
 
Hapa Kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha Mwalimu Nyerere?.<br />
<br />
Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.
<br />
<br />
Ndugu upo sahihi kabisa. Kikwete huwa anasema ukweli na kwa wengi ni vigumu saana kuumeza. Nchi zote zilizoendelea sekta binafsi ndio injini kuu ya uchumi. Lakini ukifika Tanzania watu wanawaona wawekezaji kama wezi vile. Wale wanaofanyakazi serikalini wao wanaamini ndio wenye stahili kuu. Ipo mifano wazi ya athari za kijamaa. Angalia Cuba inavyodondoka taratibu. Juzi fulani nilifika Cuba nikawa ninataka kufanya kaji transaction kadogo saana lakini watu kama wanane walihusika na ilichukua siku 3 kumaliza hiyo. Na huu ndio utendaji wa Kitanzania ambao umejaa mfumo wa kijamaa. Ukienda mahotelini au sehem zote za biashara angalia Watanzania wenzetu wanavyofanya kazi! Mfumo ni mbovu saana na ndio maana kila linalotokea hata yaliyo ndani ya uwezo wetu tunalaumu serikali.
 
Mwanatanu

Nimatumaini yangu umemaliza kuona list ya nchi za kikominist/ujamaa ,sasa rudi tujadili zaidi. Unajua nini, nchi walioamua kwa dhati na moyo mkujufu na kwa akili yao yote kuutupa ukoministi/ujamaa wanapiga hatua sana. Tatizo ni akili ya watanzania bado inaamini ktk ujamaa.

Kuna mdau hapo pembeni, eti anasema ujerumani mashariki walikuwa ktk vita baridi. ha ha ha ha ha ha. Kwani hiyo vita ilikuwa ina hasara tu kwa upande wa kikoministi na upande wa pili ilikua haiathiri?

Ha ha ha leo simba imeifunga yanga kwa sababu jua kali, kwani simba wao walikuwa wanayafunga hayo mabao wakiwa nje ya uwanja?

Mkitaka kuona ukoministi/ujamaa ni nomaa angalieni tena KOREA ilikua nchi moja lakini baaada ya kaskazini kufuata ujamaa wao kawaangalieni wamechoka vibaya balaaa, wananchi mlo mmoja ni wa kubahatisha kule korea kaskazini.
 
Watafute wajamaa wenzako wa korea kaskazini, kumbuka nchi hii ilikuwa moja wakaamua kutengana

20 Richest Asian Countries (GNP per capita*)

Hong Kong (pop. 6,940,432) ... $31,560
Japan (pop. 127,463,611) ... $29,810
Singapore (pop. 4,492,150) ... $27,370
South Korea (pop. 48,846,823) ... $20,530
Malaysia (pop. 24,385,858) ... $9,720
Russia (pop. 142,893,540) ... $9,680
Thailand (pop. 64,631,595) ... $7,930
Turkey (pop. 70,413,958) ... $7,720
Kazakhastan (pop. 15,233,244) ... $6,930
China (pop. 1,313,973,713) ... $5,890
Philippines (pop. 89,468,677) ... $4,950
Sri Lanka (pop. 20,222,240) ... $4,210
Armenia (pop. 2,976,372) ... $4,160
Azerbaijan (pop. 7,961,619) ... $3,810
Indonesia (pop. 245,452,739) ... $3,480
India (pop. 1,095,351,995) ... $3,120
Georgia (pop. 4,661,473) ... $2,900
Vietnam (pop. 84,402,966) ... $2,700
Cambodia (pop. 13,881,427) ... $2,310
Pakistan (pop. 165,803,560) ... $2,170

Read more at Suite101: Richest Asian Countries: Top 20 Wealthiest Asian Nations (GNP) | Suite101.com Richest Asian Countries: Top 20 Wealthiest Asian Nations (GNP) | Suite101.com
 
Sudan 2,200 2010 est.
153 Mauritania 2,100 2010 est.
154 Tajikistan 2,000 2010 est.
155 Cambodia 2,000 2010 est.
156 Gambia, The 1,900 2010 est.
157 Senegal 1,900 2010 est.
158 Chad 1,800 2010 est.
159 Côte d'Ivoire 1,800 2010 est.
160 São Tomé and Príncipe 1,800 2010 est.
161 Korea, North 1,800 2009 est.
162 Bangladesh 1,700 2010 est.
163 Lesotho 1,700 2010 est.
164 Benin 1,600 2010 est.
165 Ghana 1,600 2010 est.
166 Kenya 1,600 2010 est.
167 Tuvalu 1,600 2002 est.
168 Tanzania 1,500 2010 est.

Angalia North korea wajamaa na Tanzania wajamaa wanavyovutana mashati. Teh teh teh,
 
nafikiri mkamap na wenzake wanaongelea zaidi ujamaa kushindwa bila kuelewa concept ya uchumi, concept ya uchumi ya kwanza ni ku-mobilise resource kirahisi rahisi tutasema mtaji, sasa wewe na wenzako katika kufuata huo ubepari wenyewe, kuna nani tanzania mwenye uwezo wa kuwekeza kwenye reli? hao wazee wa darisalama wanaojifanya tanzania ni yao wanaweza, kasma sio kuwa matarishi wa watu wa nje? kwenye umeme tokea hiyo iptl na mkataba mbovu kuna muwekezaji wowote wa kweli umemuona kawekeza kwenye hii kitu? ok hiyo biashara huria tumeanza lini ? over 20 years je wameshindwa kweli hawa hawa wanao kaa ikulu na cabinet wanazo chagua wenyewe kumvutia mtu kuwekeza kwenye stigle gorge? kwanini mambo hayo ya msingi haya jafanyika? kama sio uongozi mbovu? je huyu aliye ikulu nae siasa za kijamaa ambazo ana zipinga au anaziona kikwanzo zemu muathiri? kama ni hivyo kwanini asijiuzulu?
uingereza na ujanja wao wa ubepari masuala ya reli wame privatise hivi karibuni baada ya kustabilise uchumi wao kwa kuvi miliki hivi vyombo, na mikataba yao ni 5 na usipofanya vizuri faini na mkataba unafutwa, lakini angali wetu na rites ni kama leo tumejiuzaa wholesale, kwenye umeme hivyo hivyo, lakini wewe na wenzako unataka kutuaminisha kwamba ujamaa ndio tatizo.
sasa tukirudi kwenye concept ya uchumi ya ku-pull resource together utaona tanzania ili kabiliwa na uhaba wa mitaji kutoka kwa locals? hao wana darisalaam wenzangu wanaodai bila wao uhuru usinge patikana, je walikuwa na uwezo huo? kenya unayo iona locals wengi walikuwa hawana uwezo huo, bali baada ya kula rushwa nk ndio unaona akina karanja nk na hiyo ni baada ya mzee kenyata kuwaambia ok dhambi ya rushwa mnayo , lakini kufanya la maana ni kuwekeza hizo fedha nchini otherwise kenya ilikuwa ya muingereza na wadosi, na sasa hivi wasomali ndio wana kuja juu. sasa katika kukabiliana na hilo tatizo la mtaji nyerere aliona au hata wewe mwenyewe ni kwa serikali kuwekeza na mashirika haya yaki stabilise ndio individuals tuuziwe hiyo mitaji na serikali ijiondoe. na huo ubepari unaosema kuhusu poland, ni kwamba baada ya kujiunga kuna mfuko wa pesa wanapewa na european union ambo ni mtaji? halafu kwanini ureno au ugiriki wana hitaji bail out kama ubepari ni mzuri? wakati cost of production kwenye nchi hizo ni ndogo ukilinganisha na uingereza. unapo laumu kitu usiangalie dalili, bali tafuta chanzo, mfano hapo tanzania kutokana na tatizo la malaria mtu akiumwa kitu cha kwanza ni dawa za malaria, kumbe mtu ana menengitis au typhoid nk nk
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Sudan 2,200 2010 est.
153 Mauritania 2,100 2010 est.
154 Tajikistan 2,000 2010 est.
155 Cambodia 2,000 2010 est.
156 Gambia, The 1,900 2010 est.
157 Senegal 1,900 2010 est.
158 Chad 1,800 2010 est.
159 Côte d'Ivoire 1,800 2010 est.
160 São Tomé and Príncipe 1,800 2010 est.
161 Korea, North 1,800 2009 est.
162 Bangladesh 1,700 2010 est.
163 Lesotho 1,700 2010 est.
164 Benin 1,600 2010 est.
165 Ghana 1,600 2010 est.
166 Kenya 1,600 2010 est.
167 Tuvalu 1,600 2002 est.
168 Tanzania 1,500 2010 est.

Angalia North korea wajamaa na Tanzania wajamaa wanavyovutana mashati. Teh teh teh,

Asante, mkuu kwa kutupakulia kutoka wikipedia.
Je unaweza kutunyambulishia, utueleze zipi kati ya nchi hizo zenye uchumi/maendeleo duni zilikuwa zinafuata ujamaa au ubepari?
 
Leo ndo Kikwete anatambua kuwa kuna ujamaa? Alikuwa wapi tangu 2006 alipo ruhusu swahiba wake apitishe Richmond. Amakweli kakurupukia blanket wakati kumekucha. Lazima kieleweke. Koo 7 haziwezi kuburuza watu milion 42
 
Angalia hapa chini list ya nchi za kijamaa harafu unitajie nchi ya scandinavia. Ndo tujadili

List of socialist countries - Wikipedia, the free encyclopedia

Tatizo wewe unataka watu wa pratice theory blindly wenzako wameweka socialism kwenye context yao na kuja na kitu ambacho kina leta welfare kwa watu wengi. I was trained in scandinavia tena kwenye issue za New Institutional Economics na policy analysis I know what the guy mean. Hata Israel wana special kind ya socialism kinachofanyika ni kitu kina itwa definition of bundles of rights and entitlements. Scandinavia ndiyo waanzilishi wa mambo ya sustainable development concept ambapo waziri wao Mkuu wa nchi mojawapo wakati huo Brutland ndiyo ali kuja na standard definition inayokubalika na wengi duniani. Tena Scandinavia ndiyo watu wakwanza kui challenge neo-classical economic theories ambazo hasa ndiyo imeleta matatizo ya valuation kwenye goods and services. Kwahiyo what the guy is saying is very correct. I appreciate Scandinavians maana model yao ndiyo sasa iko relevant sasa duniani hasa baada ya issue ya global warming na climate change.

Wakati nasoma tulikuwa tunatahadharishwa kuhusu poliy za America na tulikuwa tunafanya critical analysis na kuona how welfare is impacted na hizo Us policies. tatizo la nchi zetu hatujui ku transfer knowledge na kui apply kwenye context ya nchi zetu. Ostrom ameonyesha jinsi institutions za Africa zilivyo relevant katika ku manage common pool resources lakini sisi tunashindwa ku up date economic theories zetu ambazo ziko cultural embeded na kuleta proper allocation of resources. Theorist wetu ni Nyerere na hizo theory ukizi update ni bomba kuliko zingine zote kwani zimezingatia culture na context ya nchi yetu. Ilitakiwa wasomi wetu wa uchumi wamsaidie Nyerere kuboresha siasa yake ya ujamaa na kujitegemea na kuitoa katika listing or context ya either capitalism ama socialism na kuifanya ikawa theory yetu watanzania jinsi iwezavyo kutufaa kama walivyo fanya Scandinavians kwenye sustainable development theories ambazo huwezi kuziita capitalism ama socialism perse.
 
Sudan 2,200 2010 est.
153 Mauritania 2,100 2010 est.
154 Tajikistan 2,000 2010 est.
155 Cambodia 2,000 2010 est.
156 Gambia, The 1,900 2010 est.
157 Senegal 1,900 2010 est.
158 Chad 1,800 2010 est.
159 Côte d'Ivoire 1,800 2010 est.
160 São Tomé and Príncipe 1,800 2010 est.
161 Korea, North 1,800 2009 est.
162 Bangladesh 1,700 2010 est.
163 Lesotho 1,700 2010 est.
164 Benin 1,600 2010 est.
165 Ghana 1,600 2010 est.
166 Kenya 1,600 2010 est.
167 Tuvalu 1,600 2002 est.
168 Tanzania 1,500 2010 est.

Angalia North korea wajamaa na Tanzania wajamaa wanavyovutana mashati. Teh teh teh,

Ungekuwa unajua theory za development Economics usinge base arguments zako kwenye hizo per capita pekee kuna indicator nyingi sana za kuqualify uchumi na social welfare ya nchi. Nchi yaweza kuwa na percapita income kubwa lakini hiyo inategemea how that is distributed na what are the levels of investments kwenye public social welfare. Hizo statistics za kinadharia ndiyo illiyopelekea Tanzania kuzaa mambo shule za kata lengo likuwa kuwaridhisha mabwana kwenye enrolement bila kujali dro outs; wanapomaliza kama wanajua kusoma na kuandika. Hizo japo ni criteria mhimu lakini ukiingiza siasa na kutupa principals za development zinabakia tu kuwa poetic. Wenzetu wanafanya zaidi ya kuridhisha watu kwakuwa objective wakati sisi tunazitumia ili tuendelee kuonekana tu viranja wazuri na hivyo tuendelee kujaziwa bakuli letu la msaada.
 
Per Capita ni stat ambazo zinakuonyesha hali halisi ya maisha kwa kifupi. Also, you can use those facts kuweka argument za positive au negative kwenye uchumi wa nchi.
 
Tatizo wewe unataka watu wa pratice theory blindly wenzako wameweka socialism kwenye context yao na kuja na kitu ambacho kina leta welfare kwa watu wengi. I was trained in scandinavia tena kwenye issue za New Institutional Economics na policy analysis I know what the guy mean. Hata Israel wana special kind ya socialism kinachofanyika ni kitu kina itwa definition of bundles of rights and entitlements. Scandinavia ndiyo waanzilishi wa mambo ya sustainable development concept ambapo waziri wao Mkuu wa nchi mojawapo wakati huo Brutland ndiyo ali kuja na standard definition inayokubalika na wengi duniani. Tena Scandinavia ndiyo watu wakwanza kui challenge neo-classical economic theories ambazo hasa ndiyo imeleta matatizo ya valuation kwenye goods and services. Kwahiyo what the guy is saying is very correct. I appreciate Scandinavians maana model yao ndiyo sasa iko relevant sasa duniani hasa baada ya issue ya global warming na climate change.

Wakati nasoma tulikuwa tunatahadharishwa kuhusu poliy za America na tulikuwa tunafanya critical analysis na kuona how welfare is impacted na hizo Us policies. tatizo la nchi zetu hatujui ku transfer knowledge na kui apply kwenye context ya nchi zetu. Ostrom ameonyesha jinsi institutions za Africa zilivyo relevant katika ku manage common pool resources lakini sisi tunashindwa ku up date economic theories zetu ambazo ziko cultural embeded na kuleta proper allocation of resources. Theorist wetu ni Nyerere na hizo theory ukizi update ni bomba kuliko zingine zote kwani zimezingatia culture na context ya nchi yetu. Ilitakiwa wasomi wetu wa uchumi wamsaidie Nyerere kuboresha siasa yake ya ujamaa na kujitegemea na kuitoa katika listing or context ya either capitalism ama socialism na kuifanya ikawa theory yetu watanzania jinsi iwezavyo kutufaa kama walivyo fanya Scandinavians kwenye sustainable development theories ambazo huwezi kuziita capitalism ama socialism perse.

Unaweka argument kumtetea Nyerere wakati idea za Nyerere za Ujamaa zilishindwa kabisa. Hata Warusi walikuwa na modeli yao ya Ucommonist na walifeli kabisa.
 
Unaweka argument kumtetea Nyerere wakati idea za Nyerere za Ujamaa zilishindwa kabisa. Hata Warusi walikuwa na modeli yao ya Ucommonist na walifeli kabisa.
jk wa sasa ak juma kaseja alwahi kusema kwamba angependa kuona hizo statistic za uchumi nk zina onyesha maisha wa mtz, nyerere aliweza kureflect hizo idea zake na maisha ya mtz, kwani tuliona ajira zaidi za watz, nyumba bora kwa ajili ya watz, kama nhc, bhesco, hosco, nbc, crdb, thb, bora , tcc nk nk, sasa wewe na theory zako je waweza kutuonyesha, impact ya theory za sasa ktk maisha ya watz?
 
Kosa kubwa la Nyerere siyo Ujamaa, tatizo lake kubwa ni lile la kulea wanafiki. Angekuwa na utaratibu mzuri wa kuchuja wanafiki, basi wakati anaondoka madarakani angerithiwa na watu ambao wangerekebisha makosa yake na kuendeleza mazuri yake. Lakini alikuwa na wanafiki ambao walikuwa hawajui Nyerere anataka kufikia lengo lipi. Kwa hiyo baada ya Nyerere kuondoka kila mtu akaja na la kwake; nchi ikawa derailed kabisa.
 
Tatizo sio ujamaa,kama tatizo lingekuwa ni fikra za kijamaa naamini mambo yangekuwa mazuri kihuduma maofisini.Tatizo ni rushwa,watoa huduma wengi maofisini ni wala rushwa wakubwa, bila kutoa rushwa vikwazo ni vingi balaa.Pili kwa hao wawekezaji shida kubwa ni kwamba hasa wa kigeni wana-image mbaya kwa watz,kwa kuwa mpaka sasa ukiweka faida na hasara ya wawekezaji tz kwenye mizani faida itakuwa upande wa juu wa mizani kwamba ni ndogo na hasara itakuwa upande wa chini wa mizani kwamba hasara ni kubwa.Wawekezaji wametokea kuwa wezi wakubwa wa rasilimali zetu,wanawadhulumu wananchi ardhi zao bila fidia au fidia ndogo sana,hawawathamini wananchi wanawaona kama nyani tu, wanaharibu mazingira nk.Hebu watz tujiulize kitu kidogo tu sheraton hotel kwa nini kila baada ya miaka mitano inabadili jina mpaka sasa inaitwa moven pick kama bado haijabadilisha, kwanini? jibu lake ni wizi tu kukwepa kodi tax-holiday, mbona tukitembea nchi za watu tunaikuta sheraton? kwanini tz inakuwa kinyonga? hiyo ni sehemu moja.Nenda kwenye madini huko ndiyo balaa, mchanga wa madini unabebwa kinyemela kupelekwa nje, wizi huo, nenda kwenye hifadhi zetu wamejimilikisha hifadhi zetu na kusafirisha wanyama wetu hai kwao.Ktika mazingira kama haya hawa wawekezaji hata mimi wakinikuta ofisini lazima niwe mzito kuwapa huduma stahili.
 
Hakuna chochote, Rais analaumu ujamaa wakati tatizo kubwa la leadership yake ni "lack of priorities"...jana nilikuwa nasikiliza hotuba ya First lady wetu akiwa kwenye mission trip ya kutembeza bakuli kule Arizona, akawa anataja matatizo yanayosababisha mortality kwa watoto wanaozaliwa na akina mama wanaojifungua..oooh lack of this, lack of that....ili mradi blah blah....nikaanza kukumbuka zile zima moto zilizotolewa Dodoma juzi juzi za matairi matatu. What a fricking joke...nikaanza kukumbuka wanafunzi wasio na madawati. Nikakumbuka rafiki yangu mmoja Mmarekani aliyekuwa anakuja Tanzania kwa mara ya kwanza na ndege ya KLM ikalazimika kwenda kutua Nairobi kwa sababu uwanja wa KIA ulikuwa hauna umeme na mambo mengine mengi mengi tu. Hai make sense kujenga nyumba ya governor wa bank kuu na wasaidizi wake kwa mabilioni ya shilingi na kuwanunulia watendaji wa juu wa Serikali luxury vehicles (ma V-8) yanayokunywa mafuta ya Premium wakati hatuna barabara, wakati huo huo first lady na Rais wa nchi wanatembeza bakuli kwa donors kutoa visingizio lukuki vya shida tulizo nazo.
ukosefu wa priorities za kiutendaji, lack of good leadership ndio matatizo yetu sisi Watanzania. Kwenye good leadership kuna accountability na transparency...Obama anafile tax kila mwaka..wananchi wa Marekani wanajua Raisi wao ana kipato gani na amelipa kodi kiasi gani na source ya hiyo income...wa kwetu..mambo ya siri siri tu...sijui Africa tuna laana gani.

Until we fix these things huyu Raisi akae kimya maana kazi ilishamshinda.
 
Tatizo wewe unataka watu wa pratice theory blindly wenzako wameweka socialism kwenye context yao na kuja na kitu ambacho kina leta welfare kwa watu wengi. I was trained in scandinavia tena kwenye issue za New Institutional Economics na policy analysis I know what the guy mean. Hata Israel wana special kind ya socialism kinachofanyika ni kitu kina itwa definition of bundles of rights and entitlements. Scandinavia ndiyo waanzilishi wa mambo ya sustainable development concept ambapo waziri wao Mkuu wa nchi mojawapo wakati huo Brutland ndiyo ali kuja na standard definition inayokubalika na wengi duniani. Tena Scandinavia ndiyo watu wakwanza kui challenge neo-classical economic theories ambazo hasa ndiyo imeleta matatizo ya valuation kwenye goods and services. Kwahiyo what the guy is saying is very correct. I appreciate Scandinavians maana model yao ndiyo sasa iko relevant sasa duniani hasa baada ya issue ya global warming na climate change.

Wakati nasoma tulikuwa tunatahadharishwa kuhusu poliy za America na tulikuwa tunafanya critical analysis na kuona how welfare is impacted na hizo Us policies. tatizo la nchi zetu hatujui ku transfer knowledge na kui apply kwenye context ya nchi zetu. Ostrom ameonyesha jinsi institutions za Africa zilivyo relevant katika ku manage common pool resources lakini sisi tunashindwa ku up date economic theories zetu ambazo ziko cultural embeded na kuleta proper allocation of resources. Theorist wetu ni Nyerere na hizo theory ukizi update ni bomba kuliko zingine zote kwani zimezingatia culture na context ya nchi yetu. Ilitakiwa wasomi wetu wa uchumi wamsaidie Nyerere kuboresha siasa yake ya ujamaa na kujitegemea na kuitoa katika listing or context ya either capitalism ama socialism na kuifanya ikawa theory yetu watanzania jinsi iwezavyo kutufaa kama walivyo fanya Scandinavians kwenye sustainable development theories ambazo huwezi kuziita capitalism ama socialism perse.

Tatizo la ujamaa ndo hilo kupenda kuongea sana, nimewawekea list za nchi za ujamaa bado unaleta theory.

weka reference yako kudhibitisha unachosema. Nchi zingine ambazo zina practice uchumi wake usio kuwa wa kibepari mnakimbilia ni ujamaa. Ha ha ha. Backbone ya uchumi ya ujamaa ni kutojilimbikizia mali, kutonunua na kusaza lazima ununue na kukutumia.
 
Back
Top Bottom