Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

CCM bwana!!!

Ukweli ni kwamba hii yote ni dalili ya Chama Cha Magamba na Mafisadi kufilia mbali.
CCM wanatapatapa! Mara oh TUJIVUE MAGAMBA, mara oh MAFISADI wamepunguza umaarufu wa Chama,mara oh UDINI unachochea vurugu,mara oh,WAPINZANI wanataka kupindua nchi,mara oh,SIASA YA UJAMAA ndiyo tatizo n.k,na n.k. Yote longolongo tu!

CCM kweli maji yako shingoni. Safari hii lazima mtumbwi unazama na nahodha wao Kiwete.

CCM kamwe hawawezi kusingizia UJAMAA Ndiyo tatizo la kuboronga na kushindwa au kupoteza umaarufu kwa CCM. Je,Kiwete anaweza kutushawishi Wa-tz kuwa UJAMAA ndiyo umeleta UFISADI NCHINI???That is absolutely BIG NO!

Wakti wa Nyerere hakukuwa na UFISADI huu tunaoushuhudia kwa sasa ndani ya CCM. Nyerere(RIP) ameondoka akiikiacha chama na nguvu,mvuto na mshikamano kwa Watz. Mzee Mwinyi ndiye aliyeanza kupoteza mwelekeo na MKAPA alipoingia tu ndiyo AKAFUNGULIA MBWA WA UFISADI.

UFISADI uliokubuhu umeanzia wakti wa MKAPA. EPA imeanzia kwa njomba NKAPA. UGENISHAJI,UBINAFSI(shaji),na MIKATABA BOMU YA KUUZA MASHIRIKA na KUUZA MIGODI YETU ulishamiri wakti wa MKAPA. Hapo ndipo RUSHWA ilipochochewa moto na kushika kasi ya ajabu na kutufikisha hapa tulipo leo.

Kwa hiyo CCM msidanganye watu,UJAMAA siyo source ya UFISADI baali ni WANA-CCM wenyewe!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom