Kikao gani kiliamua Nyerere awe 'Baba wa Taifa'?

Kikao gani cha serikali na chama walikaa na kuamua kumwita Mwl.Nyerere kuwa aitwe baba wa taifa? Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge mmoja simkumbuki jina alisema"kwakuwa Nyerere anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa apewe mh.Mkapa!" akaongeza "kwakuwa utawala wa Mkapa ulikuwa mzuri basi napendekeza bunge liridhie tubadili katiba ili mkapa agombee tena ili aweze kutawala kwa miaka 10 mingine?".

Mytake:
Huu ni mlolongo wa sintofahamu ndani ya Tanzania ambazo zimepaliliwa tangu enzi! Kwani Nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi kuchanganya dini na siasa?

Naomba tujadili hoja hii nyeti kwa ueledi nasio matusi na kejeli.
​unawashwa.
 
Ndugu Bornvilla,

Pasipo kuangalia dhumuni na lengo nyuma ya swali lako wala kurejea mwenendo wa mada zako ndani ya JF, napenda kujibu kuwa; Mwalimu Julius Kambarage Nyerere si yeye peke yake bali pia na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume walitunukiwa heshima ya Ubaba wa Taifa kupitia Sheria ya Kuwaenzi Waasisi wa Taifa namba 18 ya mwaka 2004. Kwa msaada zaidi nimeiambatanisha hapa Founders of the Nation Act No. 18 of 2004.pdf

Kwa mtazamo wangu swali lako lingepata hoja yenye mashiko zaidi walau kama ungeuliza kwa nini sheria hii inafunga mwanya wa kuwatambua na kuwaenzi waasisi wengine? Hili swali ni hai, mjadala wake unaweza kuwa mpana na ukatoa msaada wa historia za waasisi walioshiriki ukombozi wa Tanganyika na Zanzibar ambazo zimevulugwa yamkini kwa maksudi.

Wakatabahu
View attachment Founders of the Nation Act No. 18 of 2004.pdf
 
Ndugu yangu BORNVILLA naomba mambo mengine kabla hujayatoa JAMVINI hebu jaribu kuuliza watu pembeni maana maswali kama haya YANAKUDHALILISHA na kuonyesha kuwa ni MTUPU KICHWANI
Hivi unajua ni kwa vipi mtu anaitwa BABA WA TAIFA? or FOUNDING FATHER OF THE NATION? ungeuliza kwanza wajinga wenzio huko nje kabla ya kuleta UPUMBAVU wako BARAZANI
 
Jiulize, ni nan alimtuma Nyerere kuacha kaz na kwenda kuimalisha Chama? Nan alimtuma Nyerere kwenda Uingereza kuongea Uk congres kuhusu uhuru? Nan alimtuma Nyerere awe mwenyekt wa chama na badae Urais? Babu yako na Babu yangu wote wanahusika, hasa hasa babu yako na wazee wenzake wa Kiislam wa Dar kipind hicho na ndio waliompa heshima hiyo wala sio wakatolic. Achen udin fanyen kaz na somen sana ndg zangu, kuuchukia Ukristo hautawasaidia..!
 
Kikao kilifanyika nyumbani kwako, mbele ya baba yako na mama yako....baada ya kukubaliana wakakutuma wewe
kuutangazia umma pale barazani kwenu kwa kutumia vuvuzela kama zile za kwenye world cup SA. Je, unalingine?

Acha matusi, ameuliza hajafanya kosa lolote. Ametumia lugha nzuri tu
 
Mswali Mengine ni ya kipuuzi kweli kweli; nadhani Tanzania tunanza kuwa na upungufu wa mawazo iwapo baadhi yetu wanaweza kukaa na kufikiria swali la namna hii, na kisha kuchukua muda kukaa mbele ya computer na kuliandika!
 
Baba yako wewe aliteuliwa na kikao gani?

Kama huyajui aliyoyafanya Nyerere si basi. Kama unadhani ni rahisi mbona wasimuite baba yako wewe bab wa taifa?
 
Kama wewe una mke na watoto je ni nani alikuchagua wewe pimbi kuwa BABA JINGA!
 
Kikao gani cha serikali na chama walikaa na kuamua kumwita Mwl.Nyerere kuwa aitwe baba wa taifa? Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge mmoja simkumbuki jina alisema"kwakuwa Nyerere anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa apewe mh.Mkapa!" akaongeza "kwakuwa utawala wa Mkapa ulikuwa mzuri basi napendekeza bunge liridhie tubadili katiba ili mkapa agombee tena ili aweze kutawala kwa miaka 10 mingine?".

Mytake:
Huu ni mlolongo wa sintofahamu ndani ya Tanzania ambazo zimepaliliwa tangu enzi! Kwani Nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi kuchanganya dini na siasa?

Naomba tujadili hoja hii nyeti kwa ueledi nasio matusi na kejeli.

Bornvilla, naona umechanganya mambo. Unahoji mambo ya kanisa katoliki hapo hapo unahoji mambo ya serikali.
Kuhusu baba wa taifa - hebu tupe ukarasa unaongelea taratibu/sheria zinazotakiwa kufuatwa hapa Tanzania kabla ya kumuita mtu baba wa taifa. Ukiweza kuweka hizo taratibu /sheria ndio mtu anaweza kusema ni wapi kulikosewa.

Na kuhusu kanisa katoliki na utakatifu - what do you know about the catholic church?
 
Niwajinga wachache wanaojaribu kupingana na uwezo wakitu wasichokijua wala kutambua uwezo wa mwalim.

Mwisho watapata majibu ya kushindwa na kuweweseka.
 
Tatizo ni shule,wewe Bornivilla soma uwe mwelewa nchi kibao waasisi wanaitwa baba wa taifa Angola n.k acha kusoma yale maandishi kutoka kulia kwenda kushoto utakuwa na mawazo ya kigaidi gaidi na kujitoa muhanga,humjui vizuri Nyerere alikuwa kipaji cha taifa toka kwa Mungu.
 
Waliochangia wametoa hoja mbalimbali pia maelezo ya kwa nini wanaamini Mwl jk nyerere kuwa baba wa Taifa mimi nachangia kuhusu UKATOLIKI ndg kama wewe si mbwa huwezi wala hutajakaa ujue lugha ya mbwa hadi pale utakapokuwa mbwa hivyo basi waache wakatoliki na ukatoliki wao. Wana taratibu zao na kanuni zao. Kuanza kumzungumzia Mwl na kanisa Katoliki kumfanya mwenye heri pia kuwa baba wa Taifa ni vitu viwili tofauti. Watafute wakatoliki nao watakueleza ni kwa nini wanafanya hivyo. Pia jaribu kuweka mbali siasa na dini
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sawa dini haichanganywi na siasa ila haimnyimi mtu kuwa na imani yake! Sasa huyu anahoji ***** gani? Unaleta udini jenga hoja ya msingi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom