Kikao gani kiliamua Nyerere awe 'Baba wa Taifa'?

kikao gani kilikaa mpaka baba yako akaamua kukuzaa kichwa maji kama wewe??


wanasemaga eti?
Ukiwa unaoga mwenda wazim akichukuwa nguo zako usimkimbize na wewe utakuwa mwenda wazim kama siyo kichaa. Me ninapita tu simo
 
POA TU KWANI NINI BWANA KUNA UBAYA GANI NGOJA NA MIMI NI MWIETE MKAPA MKURUGEZI WA TAIFA ,MZALENDO, MTOTO WA TANZANIA, Namuongezea na Sir B Mkapa. NIMALIZIYE MUTU YA WATU PAPAA MKAPA MUZEE YA CHAIN GR 1,000
 
hebu nijaribu kujibu swala la mleta mada kama ifuatavyo.

Suala la mwl. Nyerere kupewa hadhi ya ubaba wa taifa halikuja hivi hivi bali lilikuwa azimio la bunge la jamuhuri ya muungano wakati mwl. Anastaafu kutoka kiti cha raisi mwaka 1985. Hoja ya azimio hili ilipelekwa bungeni na hayati mzee thabiti kombo, wakati huo akiwa mbunge toka zanzbar, hoja hii ilisomwa kwa niaba yake na ndg. E.d maokola majogo, mbunge wa nachingwea tarehe 29.07.1985.

Bunge liliridhia hoja hii na hivyo kuazimia mwl. Nyerere atambulike kama baba wa taifa, na picha zenye sura yake ziendelee kubaki kwenye ofisi za chama/vyama na serikali, sarafu na mojawapo ya noti za fedha za tanzania.

Azimio hili lilizingatia mchango wa dhati wa mwl. Nyerere katika mambo mengi, nitaandika machache kati ya mengi:
1.kuanzisha tanu 1954, 2. Kuacha kazi ya ualimu 1955 ili kuongoza harakati za kudai uhuru. 3.kushiriki kuunda pafmeca 1958. 4.aliweka msimamo ktk jumuia ya madola kuhusu ubaguzi wa rangi, msimamo huo uliitoa afrika ya kusini nje ya jumuia ya madola hadi mwanzoni mwa myaka ya 90. 5.kuongoza tanganyika kupata uhuru 1961. 6.kujiuzuru uwaziri mkuu ili kuimarisha tanu, 1962.kushiriki kuunda oau 1963. 7. Kushirikiana na karume kuunganisha tanganyika na zanzbar 1964. 8.mwaka 1965 alivunja uhusiano na uingereza kufuatia mgogoro wa uhuru wa rhodesia.

Kwa kweli mlolongo wa matukio muhimu kabisa na ya kihistoria, yanambainisha mwl. Kama mtu wa pekee kwa tanzania, mtu mwenye msimamo usoyumba, mtetezi wa haki na zaidi ya yote mtu mwenye kipaji cha kushawishi kwa hoja. Viongozi wa mataifa makubwa walimuheshimu mwl. Kwa busara na hekima zake bila kujali itikadi yake ya ujamaa mfano jimmy carter nk nk. Kung'atuka ktk uraisi, ikumbukwe mwl aliacha kazi ya uraisi kabla ya muda wake kwisha. Azma hii alikuwa nayo muda mrefu na alikuwa amenuia kung'atuka mwaka 1980 kama isingetokea watu kumshauri aendelee kuongoza, lakini hili zaidi lilitokana na madhara ya vita ya amini 1978-1979. Mwl, aling'atuka kwenye uongozi wa ccm mwaka 1992 lakini kabla ya hapo alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mfumo wa vyama vingi unaanzishwa. Wakati ule hoja ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi ilipingwa vikali na viongozi wa ccm na hata watanzania wenyewe.

Bila shaka, sifa hizi za kipekee ndizo zilizo fanya bunge likaazimia aitwe "baba wa taifa". Kuhusu kanisa katoliki kuanzisha mchakato wa kutafiti endapo aliishi maisha ya mfano wa utakatifu, hili pia linatokana na maisha yake binafsi. Nielezee kidogo.

Mwl. Alibatizwa mwaka 1942 huko nyegina musoma, alifunga ndoa mwaka 1953 na mama maria nyerere. Mwaka 1955 alipoacha kazi ya ualimu huko pugu-dsm, alirejea musoma alipofanya kazi na shirika la wamisionari wa merynoll. Baadhi ya kazi alizozifanya ni pamoja na kutafsiri maandiko matakatifu ya biblia na katekesmu katoliki kwenda lugha ya kizanaki. Kadhalika, alikuwa muumini mzingativu (practising christian) ktk masuala ya kiimani. Katika hili, yapo mambo mengi yaliyojificha ambayo si tu wakatoliki hawayajui bali pia watanzania na ulimwengu hauyafahamu kuhusu mwl. Nyerere. Mimi pia siyajui kiivyo.

Mfano, wakati flani mwl. Nyerere aliwahi kusema "mimi katika handbag yangu daima siachi vitu viwili, biblia na kijitabu cha azimio la arusha......................' kwa mantiki hii, huenda kanisa katoliki limeona elements za maisha ya upekee ya kiroho ya mzee huyu. Mchakato hata ivyo, ni mrefu na wakati mwingine huchukua hata karne nzima kutafiti maisha ya utakatifu wa mtu ili hatimaye kumtangaza mtakatifu. Huko ulaya, marekani zote, asia, mashariki za mbali hata afrika watakatifu wapo. Uganda wapo, sudani yupo nk nk. Kwa hivi, hili lisitusumbue mana vizazi vyetu pengine ndio watakao shuhudia utakatifu wa mwl julius kambarage nyerere (1922-1999).

Ikumbukwe pia, mwl nyerere pammoja na kuongoza nchi kwa zaidi ya miaka 20, alistaafu akiwa hajajilimbikizia mali yoyote, aliishi maisha ya kawaida, alipenda kukosoa hadharari maamuzi mabovu ya serikali na wakati wote, nasema wakati wote, viongozi wa chama cha ccm na serikali yake hawakumpenda mwl kwa sababu ya msimamo wake dhidi ya ubinafsi, kiburi, rushwa, fitina na unafiki.

Wakati mwingine si rahisi kutoa majibu ya kuweza kumridhisha kila mtu, lakini ni vizuri kujitahidi kutoa maelezo mazuri kwa upole bila jazba. "watu wengine wameshindwa kumtambua mungu ktk maisha yao kwa sababu waalimu wa dini hawajitahidi kutoa maelezo mazuri kuhusu mungu, na zaidi ya yote.....wanashindwa kuishi kwa vitendo mafundisho wanayo wafundisha waumini wao". ............................. Huenda hizi sababu chache zinatosha kumfanya mwl. Kuwa baba wa taifa? Hapana, zipo nyingi, hata tukiacha kumuita baba wa taifa, tutamuita mwalimu km yeye mwenyewe alivyopendelea kuitwa, na pengine jina mwl. Linamstahili zaidi? Sijui!
i believe the function of education is to teach one to think intensively and to think critically.
Intelligence plus character that is the goal of true educational .sikujuwi ila wazazi wako hawakupoteza pesa kukupeka shule 100% wengi wame fail.
Ingekuwa ni mtihani basi wame fail kama ndugu zetu wa darasa 7 ila elimu haina mwisho kesho wana weza kufaulu
 
Tukiacha udini mleta uzi ana hoja nzuri sana... kwanin karume hakumbukwi kama baba wa Zanzibar? amewajengea zanzibar nzuri yenye kupendeza mpka vijijini... Kikao kilichompitisha Nyerere kuitwa baba wa Taifa ndicho kilicho bariki Mwinyi kuitwa baba wa Demokrasia? same kikao kiliamua Kawawa kuitwa Simba wa Vita? ...
 
Tukiacha udini mleta uzi ana hoja nzuri sana... kwanin karume hakumbukwi kama baba wa Zanzibar? amewajengea zanzibar nzuri yenye kupendeza mpka vijijini... Kikao kilichompitisha Nyerere kuitwa baba wa Taifa ndicho kilicho bariki Mwinyi kuitwa baba wa Demokrasia? same kikao kiliamua Kawawa kuitwa Simba wa Vita? ...
Mkuu ilboru 1995, 1998...ulikuwepo??
 
Back
Top Bottom