Kikao gani kiliamua Nyerere awe 'Baba wa Taifa'?

Kila mtu anao uhuru wa kujiamulia idikadi yake bila kusukukwa na mtu yoyote,vivyo hivyo hata watu nao wanaweza kujiamulia idikadi zao bila ya kulazimishwa,so mtoa mada kwa wakati ule naye pia alihusika kwa namna moja au nyingine hayati j.k nyerere kutangazwa baba wa taifa.sema tu labda kwa sasa kapevuka na kusahau mazuri yalioanzishwa.
 
Maswali mengine jamani watu mnataka tufungiwe hapa kwa madai tunawatukana lakini iunashangaza sana kuona Wadanganyika mnafikia kuwa question vitu vya ajabu ajabu.. Kaa huelewi maan ya Baba wa Taifa sema... na hadhi hii haipotoshi lolote zaidi ya kwamba ndiye rais wetu wa Kwanza ktk uzawa wa taifa letu huru la Tanganyika na Tanzania - Hutaki unaacha!.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa Vyote alivyovifanya kwa NCHI HII MAZURI NA MABAYA; Mazuri yanazidi Mabaya bado UNAHITAJI VIKAO

Kumjadili kumuita BABA WA TAIFA? SIJAONA MKIWEKA VIKAO KUJADILI VIONGOZI WENU WALIVYOPEANA

MAPESA HADI USWISI... AU NI PER DM HIZO?

* Mnataka kuona Kila kitu Sasa Imekua Azimio la Arusha?
 
Kikao kilifanyika nyumbani kwako, mbele ya baba yako na mama yako....baada ya kukubaliana wakakutuma wewe
kuutangazia umma pale barazani kwenu kwa kutumia vuvuzela kama zile za kwenye world cup SA. Je, unalingine?
mmh!kweli wewe mshika chuma.nimecheka sana.
 
Kikao gani cha serikali na chama walikaa na kuamua kumwita Mwl.Nyerere kuwa aitwe baba wa taifa? Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge alisema"kwakuwa Nyerere anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa apewe mh.Mkapa!"
Kwani Nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi kuchanganya dini na siasa?

Mkuu, Kuitwa baba wa kitu fulani au jamii fulani maana yake ni sifa kubwa sana anayopewa mtu kwa heshima ya mchango wake mkubwa ambao unafananishwa na baba katika familia au jamii husika. Baba huwa ni mlinxi au kiongozi shupavu ambaye huwa tayari kuitetea familia yake hadi ikiwezekana kutoa uhai wake kwa ajili ya familia.

Kwa wanaoijua historia ya Tanganyika na Tanzania wanaelewa kwa nini Mwl. Nyerere anaitwa Baba wa Taifa. Sina kumbukumbu sahihi kwamba kulikuwa na kikao rasmi cha kumpachika jina hilo na sijui ni nani aliyalianzisha, ila naweza tu kusema kwa uhakika lilikubalika kwa wa TZ wengi.

Kuhusu kutaka kutangazwa mtakatifu ni machakato mrefu sana wa Kanisa Katoliki, na si kwa sababu kalifanyia nini kanisa la hasha, bali alimcha vipi Mwenyezi Mungu katika uhai wake. Hiyo huhusisha pia miujiza endelevu ya kimungu iliyopata kuwatokea watu (mashuhuda) kwa jina lake na kuthibitishwa na watu pasi na shaka. Hata hivyo utakatifu ni hatua ya mwisho kabisa baada ya kutangazwa mwenye heri.

Kwa wanaomjua hawana shaka na ucha mungu wake. Hebu fuatilia speeches zake na uwe mkweli, wewe huoni kwamba kuna unabii fulani ndani yake? Sikulazimishi, ni maoni yangu tu mkuu.
 
Bornvilla kwa maelezo yako nahisi umesukumwa na wivu+udini Nyerere kuitwa Baba wa Taifa.Kama ni hivyo kuanzia sasa Baba wa Taifa ni Marehemu Shehe Yahaya.:israel:
 
Last edited by a moderator:
kwa maelezo yako nahisi umesukumwa na wivu+udini Nyerere kuitwa Baba wa Taifa.Kama ni hivyo kuanzia sasa Baba wa Taifa ni Marehemu Shehe Yahaya.:israel:

Hapana mkuu, usifanye hasira.
Jaribu tu kumuelimisha labda ataelewa. Yawezekana tatizo siyo wivu wala udini bali ni umri.
 
Saint nyerere

Saint kwa nani sasa? Maana mambo ya imani ya kanisa katoliki hayana uhusiano wowote na imani ya mtu mwingine mkatoliki. saesa kila siku hadithi ni hiyo hiyo tu...wakati tunajua pili pili usiyoila haiwezi kukuwasha. Nashangaa watu wanashupalia mambo yasiyo wahusu kabisa na kufanya kama kuna hoja ya maana. Naamini Nyerere hakujipa jina la baba wa Taifa. Na kama kuna mtu anaona linamsumbua sana apendekeze jina hilo anyang'anywe na apewe yoyote yule. Mwisho wa siku yeye alipenda alitwe mwalimu....hilo nalo sijui mtaweza kumpora?
 
Nyerere chanzo cha umaskini wa nchi hii. Chanzo cha jinamizi la muungano wa kiinimacho kati ya tanganyika na zanzibar. Vita dhidi ya idi amin ambayo haikuwa na ulazima wowote iliyopelekea kuyumba kwa uchumi wa nchi.
 
Muulize ben anajua alikompeleka na sababu za kusema aitwe baba wa taifa anazijua yeye nkapd.
 
Kikao gani cha serikali na chama walikaa na kuamua kumwita Mwl.Nyerere kuwa aitwe baba wa taifa? Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge mmoja simkumbuki jina alisema"kwakuwa Nyerere anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa apewe mh.Mkapa!" akaongeza "kwakuwa utawala wa Mkapa ulikuwa mzuri basi napendekeza bunge liridhie tubadili katiba ili mkapa agombee tena ili aweze kutawala kwa miaka 10 mingine?".

Mytake:
Huu ni mlolongo wa sintofahamu ndani ya Tanzania ambazo zimepaliliwa tangu enzi! Kwani Nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi kuchanganya dini na siasa?

Naomba tujadili hoja hii nyeti kwa ueledi nasio matusi na kejeli.

Kwani wewe, kikao gani kilichoamua baba yako mzazi awe baba yako. Dharau zako huko huko kwenu!
 
Kilifanyika Usiku wa Manane na MAMA YAKO MZAZI ALIKUWEPO MUULIZE, TENA BABU ALINIAMBIA MAMA YAKO ALIULIZA KIKAO KINGINE KAMA HIKI KITAFANYIKA LINI, AKAJIBIWA NA BABU KUWA UTAJULISHWA, NYANG'AU MKUBWA WEYE
 
Kikao gani cha serikali
na chama walikaa na kuamua kumwita Mwl.Nyerere kuwa aitwe baba wa taifa?
Kikao hicho kilifanyika wapi na tarehe ngapi? Tangazo la jina hilo
lilitolewa na nani na katika chombo kipi halali cha serikali?
Kuna wakati mbunge mmoja simkumbuki jina alisema"kwakuwa Nyerere
anaingia kwenye mchakato wa utakatifu basi heshima ya ubaba wa taifa
apewe mh.Mkapa!" akaongeza "kwakuwa utawala wa Mkapa ulikuwa mzuri basi
napendekeza bunge liridhie tubadili katiba ili mkapa agombee tena ili
aweze kutawala kwa miaka 10 mingine?".

Mytake:
Huu ni mlolongo wa sintofahamu ndani ya Tanzania ambazo zimepaliliwa
tangu enzi! Kwani Nyerere alilifanyia nini kanisa katoliki hadi limpe
hadhi ya utakatifu wakati yeye mwenyewe alidai ni haramu/dhambi
kuchanganya dini na siasa?

Naomba tujadili hoja hii nyeti kwa ueledi nasio matusi na
kejeli.

Kwanini unaidharau dini yako kiasi hiki! Au umegundua ni ya uongo!

Ya wakatoli wewe yanakunyima usingizi! Unaupenda kuliko dini yako!
 
jk 'dhaifu', ccm “magamba” ,a.chenge “vijisenti” ,naddir haroub 'kanavallo'jamhuri kiweru 'julio' je na hawa nao ni kikao gani kilikaa kuwapa hizi aka stahiki
 
Nyerere anastahili Kuitwa baba wa taifa akiwa kama mwasisi wa taifa aliyepigania uhuru na kama RAIS WA KWANZA WA TAIFA HILI..Hiki ndicho Mwalimu anachostahili..Hakuna kikao kinahitajika kukaa kwani ktk Tanzania nzima hakuna na hatatokea mtu anayestahili kuwa baba wa taifa kama nyerere.Full Stop
 
Back
Top Bottom