Zogwale
JF-Expert Member
- Jul 10, 2008
- 15,287
- 10,842
- Thread starter
- #61
Na wale wanaume wanaoa wanawake sawa na binti zao wa mwisho au mjukuu na mume wakipita wote anaamkiwa shikamoo babu inakuwaje? Na mke anaamkiwa mambo vipi na vijana wadogo. Masuala ya kuishi watu wawili kama mke na mume ni zaidi ya umri!!! Hvi kwa Tz hakuna mwanamke ameolewa na kijana say amempita miaka hata 10 na wanaishi vizuri? Nina mfano mmoja kuna mama amemzidi mke kwa miaka 8 na wanishi vizuri mno!!!! Inabidi wakati mwigine tubadilike na tusikilize kwanza feelings za watu. Ni kwa sababu hii sikutaka kumpa majibu ya haraka nikataka nipate mawazo hapa jamvini na nimeyapata ninashukuru mno kila mtu kwa mtizamo wake.Aisee wewe jamaa elewa mke si kwa ajili ya kumgalagaza tu, mke ni zaidi ya ngono, na kuna watu wanaowana na hawahitaji watoto. pamoja na sifa zote mke ni lazima muendane mnapokwenda sehemu na siyo yeye anaamkiwa na wewe unaambiwa mambo vipi!