Kijana miaka 38 amempenda mwanamke wa miaka 44 leta maoni ya busara

Wengine wanaona pouwa kwa kuwa hayawahusu...

Ngoja mabinti na vijana wao wawaletee vikongwe tuone kama hawajaleta uzi humu...

Inapendeza mtu aoe na kuolewa na age mate wake..

Chukulia huo mfano wa Khadija Kopa kuna taharabu ameimba mpaka niliuliza what's wrong kumbe ana wasiwasi kiserengeti kitachukuliwa na wa umri wake. Pressure tupu...Na siwaombei mabaya;ila its too early to conclude kuwa amepata mume alotulia au mume maslahi. Uzuri kina Shigongo hawatakawia kutupa taharifa.
What if is virce versa???? bintiyo au kijana wako ndo akawa kikongwe? Maisha huwa hayana formula...Je utaleta uzi humu??? Omba sana Mungu.
 
Wewe wasema kutawala...mimi naita descipline...siwezi kuwa na watoto wanaojiamulia kila watakalo kama kondoo wasio na mchungaji...\nilivyolelewa mimi ndivyo ntakavyolea wanangu.


Sounds like wale kina mama mkwe wenye matatizo wanaotawala watoto wao wa kiume...Utashangaa unawapata micharuko ...utakomaje!!!
 
Huu tunahita sijuhi uhuru ndio utafanya soon mtoto wa kiume akuletee dume mwenzie eti mchumba...ndio tunakoelekea; si uhuru bana.
Watu mnataka kuiga mabo ya kizungu hata yaso na maana.
 
Hiyo teknolojia inasaidia kupata mtoto tu au na kupata mtoto asiye na ulemavu wa akili??? Maana nimesoma juzi kati yahoo wakizungumzia ulemavu wa akili wa watoto waki connect na mama kuwa more than 45.

Age ain't nothing,is just a number. Ss hv hata uwe 50 utazaa tu, thanx to the devt in medical technology!
 
Hiyo teknolojia inasaidia kupata mtoto tu au na kupata mtoto asiye na ulemavu wa akili??? Maana nimesoma juzi kati yahoo wakizungumzia ulemavu wa akili wa watoto waki connect na mama kuwa more than 45.

Of course sio issue ya ku-conceive tu ni lazima ujue na kuilea hyo hyo mimba kwa kupata some hormonal tabs and all that. Yet the kid could be healthy!
 
Kipenda roho!
hula nyama mbici. Mimi naona waoane ingawa sababu alizotoa assuredly4 ni nzito, lakini naona kupendana kwao ni kuzito pia, na ingawa tumezoea wanaume wakubwa kuoa wanawake wadogo hii isiwe shida labda kama mwanamme ana wasiwasi
 
Mwenzako kampenda, wala mambo ya kuachika au kutoachika hayamuumizi kichwa na si suala lililoletwa hapa, kilicholetwa hapa ni suala la umri, mshauri kutokana na kilicholetwa hapa

Binafsi sioni kama kuna shida ukizingatia hao wote ni watu wazima let them go ahead

NIngependa kujua kama huyo mama yeye alishawahi kuolewa,ana mtoto au hajawahi kuolewa na hana mtoto.kama alikwisha kwa nn aliachana na mume wake wa kwanza na kama hajawahi kwa nn mpaka anatimiza 44? ni mambo ya msingi kuyaangalia ayo nayo.
 
Wanajamvi ninachukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa michango yenu mizuri kwa huyu ndugu. Kila mchango wa mtu nimeuchukua kuwa ni sahihi na kwa hakika nitajaribu kumpa huyu ndugu pande zote mbili za ushauri (positive and negative) ila maamuzi ya mwisho ni juu yake na mpenzi wake huyo. Nimapanga kuonana naye weekend hii na ninaamini atapata ukweli wote. Nataka tu niweke sawa kuwa huyu ndugu yangu si aina ya kina Mario, ni mtu ana uwezo wake sana kifedha na biashara zake (naye ni msomi aliyeamua kujiajiri). Mwanamke naye ni msomi, ameajiriwa na kazi nzuri tu. Kwa mantiki hii hakuna anayesema anataka aolewe na mwenzie kwa sababu ya mali au pesa. Nilichokuja kufahamu baadaye ni kuwa wawili hawa wana mahusiano ya kirafiki kwa miaka minne iliyopita!!! Again wote sana nawashukuru ila za pekee zimfikie EMT, Zomba, Zion Daughter, Matola kwa ushauri wao wa kina sana. They took the matter as theirs with critical minds. Thank you guys.

Kama michango ipo kwa wengine karibuni maana bado ninao muda wa kupitia na kuweka pamoja. Long Live JF. Kuna weledi wa mambo mengi.
 
This thinking is medieval, just medieval.

I bet mwanamme wa miaka 44 akitoka na mwanamke wa miaka 38 - wait, msichana wa miaka 18- itakuwa sawa tu, right?
 
Si mbaya kwa kuwa kijana ni 38; keshaponda maisha mpaka kashindwa kuchagua...imagine kijana wa miaka 24 aoe binti miaka 30????

Mkuu Nyumba ndogo kijana wa miaka 24 kweli ni mdogo na pengine hajapevuka akili sana. Lakini zee la miaka 38 nalo unalilinganisha na kijana wa miaka 24? Wote hawa mwanamke wa 44 na mwanaume 38 ni watu wazima mno, kwa Tanzania tayari hawa wanaitwa baba na mama!! Tena kwa sasa kuzaa watoto 2-3 unakuta na kufunga kuzaa wamefunga. Issue ni kuwa wote hawa wawili walipitia life tests almost same kwa kutendewa vibaya na watu wao wa awali. Kumbuka ndugu yangu alikatishwa tamaa kabisa kuoa alipokuwa na miaka 31-32 hivi baada ya mchumba aliyezaa naye kumtenda!!! Na huyu mwanamke hivyo hivyo!! So mambo mengine ni magumu zaidi tunavyofikiria sisi.
 
Back
Top Bottom