Kifo cha CCM kimetimia

Ndugu wajumbe, nimekuwa nikifuatalia kwa karibu mwenendo wa siasa za nchi yetu kwa ukaribu sana. Mambo yanayotokea sasa yananishangaza na sikutarajia kama yangeweza kuja kutokea katika nchi yetu nzuri ya Tanzania. Kutokana na mambo hayo ningependa mnijulishe hasa wale waliosoma historia na sayansi ya siasa, je? yawezekana haya yanayotokea ni dalili za chama tawala kupoteza madaraka na ni mambo gani mengine tuyatarajie katika mlolongo huu wa mambo ya ovyo yanayotokea nchini?
 
Ndugu wajumbe, nimekuwa nikifuatalia kwa karibu mwenendo wa siasa za nchi yetu kwa ukaribu sana. Mambo yanayotokea sasa yananishangaza na sikutarajia kama yangeweza kuja kutokea katika nchi yetu nzuri ya Tanzania. Kutokana na mambo hayo ningependa mnijulishe hasa wale waliosoma historia na sayansi ya siasa, je? yawezekana haya yanayotokea ni dalili za chama tawala kupoteza madaraka na ni mambo gani mengine tuyatarajie katika mlolongo huu wa mambo ya ovyo yanayotokea nchini?


Dalili ya mgonjwa ambaye kamwe haponi bali atafariki ni,
1. Huwa hawezi kuwaangalia uso kwa uso wale wanaokuja kumuona. CCM inaona hata aibu kutoa ahadi zao zimetekelezwa vipi maana imeshindwa kutekeleza.
2. Huwa ana hasira. Mgonjwa ambaye ni mahututi hudhani wanaokwenda kumuona wameenda kumsanifu hivyo huwa ana hasira nyingi sana. CCM imekuwa na hasira kila wakifanya vikao watu wanaoenda kuhudhuria vikao vyao ni wachache sana. Jazba zimewapanda sana kwani tayari wamehisi anguko limekaribia.
3. Huwa hawawezi kukumbuka muda wa kula au kwenda haja. Siku akila ndiyo siku ya kufa. CCM wanasahau kwamba wanaowaua ni wapiga kura wao ikiwa wangewatendea mema kwa sera zao.
 
Ni jambo la kusikitisha sana kuona leo CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimebadilisha sana namna ya kuendesha siasa, badala ya kutangaza sera,Kiburi cha kutawala muda mrefu na matusi majukwaani ndio zimekubalika kuwa sera halali za chama Tawala. Sasa sio jambo mbaya wala geni mahali walipo CCM wakiendesha mikutano yao ya kampeni kuwasikia watu kama Mwigulu Nchemba(MAKAMU KATIBU MKUU CCM),Livingstone Lusinde(MBUNGE-Mtera) na Nape M.Nnauye(KATIBU ITIKADI NA UENEZI-CCM) wakiporomosha matusi kwa CHADEMA na vitisho kwa wananchi. Siasa safi na Uongozi bora kwa CCM na Serikali yake vimekuwa ni bidhaa Adhimu saaana. Ndio maana wanawakumbatia watu wabovu kama Mwigulu Nchemba mtu standi wa kubuni clips feki na kuwabambikiza Akina Rwakatare, HUYU kijana sio mtu mzuri hata kidogo. JK usiposhtuka utajikuta Nchi imedumbukizwa kwenye machafuko na vurugu za kutisha, Huenda Mwigulu akikutana na JK anajaribu kumtumainisha kila wanalolipanga ni zuri na litazaa matunda ya kukisaidia CCM kubakia madarakani,NATAMKA MAPEMA KABLA HAYAJATUKIO MAMBAYA ZAIDI ya tuliyoshuhudia;Mwigulu Nchemba ni kijana ambaye asipoonywa, kudhibitiwa,kuzuiliwa,kurekebishwa na kupata maongozi mazuri na sahihi TUTAKUJA KUJUTA. Baadhi ya Viongozi wa ngazi za juu wa Serikali ya CCM wakiwemo maafisa wa Idara ya Usalama,kama hamtakuwa na njia mbadala ya makusudi ya kuwazuia Wale wanaom-remote Mwigulu ama Mwigulu kuendelea kuwa-remote ili kuweza kuikabili au kuiua CHADEMA AMANI ya Nchi yetu itabakia kuwa Hadithi . TANZANIA HAITAKUWA KISIWA CHA AMANI TENA,TUTAJIKUTA KWENYE GIZA NENE LA MAUAJI YA HALAIKI.Na kwa kauli aliyoitoa M.Nchemba kata ya Kimandolu Arusha kwamba kama WANANCHI hawataichagua CCM Watakufa. HUKO NI KUDHIHIRISHA NI JINSI GANI MWIGULU NCHEMBA NDIYE MVURUGAJI NA MTOWESHAJI WA AMANI YA TAIFA LETU.CHUNGENI SANA HII NAMBA NI HATARI KULIKO TUNAVYOAANDIKA NA KUSIMULIANA. TANZANIA NI ZAIDI YA MWIGULU NCHEMBA.
 
tegemea vurugu zaidi zitakazosababishwa na kung'ang'ania kutawala! Aidha Dalili nyingine ya angiuko ni kutosikiliza lolote linalo tahadharisha, ni kupuuza, kukejeli, kutisha kila anayetahadharisha lolote!
 
Ndungu watanzania wenzangu nianze kwa kuwapa pole wananchi wenzangu wote waliokumbwa na mauaji na wale ambao ni majeruhi kutokana na uratibu uliofanywa na CCM. Naamini wengi wetu tumeguzwa kwa namna moja au nyingine kwa kuondokewa na ndugu zetu na wale ambao ni majeruhi. Kama mtakumbuka ni hivi karibuni na katika chaguzi zilizopita baadhi ya vyombo vya habari viliripoti jinsi CCM ilivyokuwa inajiandaa kwa kuanzisha jeshi lake na kuonyesha kutoliamini jeshi linalosimamiwa na serikali yake kwa kuanzisha GREEN GUARD chini ya uratibu wa Mwingilu Chemba. Hatimaye matunda ya Jeshi la CCM limeanza kuonyesha wazi kuwa sasa kumbe CCM inajiandaa kuwa kundi la kigaidi na la mauaji baada ya kuona imezidiwa kisiasa. Hawapo tayari kuwa chama cha upinzani kama vyama vingine vilivyovumilia chini ya utawala wake gandamizi kwa karibu miaka 20 na sasa wananchi wameanza kuelewa umuhimu wa kuifanya CCM chama cha upinzani. Badala yake kinakasirika na wanachi waliowachia madara miaka zaidi ya 50. Sasa kinachoshangaza zaidi ni pale wanachi wa Tanzania wanapofanywa punguani na wale wanasimama bungeni na kujifanya kuwa wanawaonea huruma na wanauchungu na wanachi waliowawa chini ya uratibu wao wenyewe na hata kuahidi fedha za umma kumpa zawadi atakayewatambua wahusika ilihali wakijua wao wenyewe ndio wahusika. Sasa cha kujiuliza aliyewaua ndugu zako na kujeruhi wengine umpe taarifa wewe ndio uliyefanya hivyo, si ndio anataka wanaomtambua ili awamalize kabisa!!!???.. Au ndio baadaye iletwe ile picha ya Mkenya na Dr.Ulimboka na Mahakama mjadala uishie hapo!!??. Au Mwangosi na askari mtuhumiwa kama sadaka na mahakama ifunge mjadala. Hayo mamilioni ya zawadi ya fedha za umma siapewe Mwingulu Nchemba agawie Jeshi la Chama Chake na baadhi askari wanashirikiana nao kwa kutii amri zisizokuwa na utu za mauaji ili wajipongeze kwa kufanikisha yote yaliyotokea na yatakayoendelea kutokea. Sasa tunaletewa mambo kutufanya watanzania hatunazo zote. Eti CHADEMA ndio imefanya mpango huo, hivi hili linaingia akilini kweli!!!! kama ndivyo wanavyotuambia sisi ambao hatunazo hivi kweli hata mjinga wa aina gani utamwaminisha sehemu ambako wapinzani wananguvu za kiasasa ndio wajiletee vurugu. Au ndio yaleyale ya propaganda kuwa ukichagua upinzani ni vita na mauaji. Hilo watanzania wengi wanalijua kwa sasa, Mnawaua mnawajeruhi ili muonekane nyie ni mnabii. CCM kwa mtu moja moja hukumu hii ipo mbele yenu. Watanzania si majuha kiasi hicho. Nyie mnaotaka kujipatia umaarufu kule mlikoshindwa kiasasa mnajipendekeza kupeleka majeruhi mahospitalini. Kumbukeni hizo si fadhili hizo ni fedha za umma na hayo wanajua mmeyapanga wenyewe. Wananchi wanajua kabisa hiyo ni namna ya danga toto kujifanya mna huruma na wao.
 
Kuna mifano mingi tu ya vyama vikubwa vya siasa ambayo muda wake ulipofika vilikufa, natural death ingawa kwa mikiki lakini vilikufa. Kama Nazi ikikomaa lazima ianguke.

CCM ni kama papai lililoiva na muda wake wa kuanguka umekaribia, kinachofanyika hivi sasa mi popo wameanza kulila likiwa bado mtini.

Kinacjosubiriwa ni lini Hilo papai litaanguka, hatuwezi kuzuia limeshaiva hilo.
Nawakilisha
 
Katika kuonesha kuwa sasa uwezo wao wa kufikiri umefika mwisho na pia uongozi wa nchi umewashinda, CCM wanatumia vyombo vya usalama kujihalalishia kuwapo kwao madarakani. Yaliyotokea wakati wa chaguzi ndogo za madiwani hivi karibuni, imedhihirisha pasipo shaka kuwa CCM siasa wameishindwa na pasipo kutumia jeshi la polisi (japo kwa sasa) basi wanang'olewa madarakani. Kilichofanyika Serengeti katika kata ya Manchira ni mfano wa wazi na licha ya kushinda kwa "margin" ndogo, ni ukweli uisopingika kuwa ushindi wa MACCM ilichagizwa ka kazi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda ambaye anakaimu wilaya ya serengeti kwa sasa pamoja na utumikaji wa jeshi la polisi. Kuwafungia vijana zaidi ya 100 ili kuwazuia wasipige kura na kuja kuwaachia baada ya muda wa kupiga kura kuisha kuliisaidia ccm kuishinda Kata hiyo,la sivyo ni kwenda na maji.

Wakati hayo yakitokea, wanajisahau kuwa vitendo vyao vya kinyama vinazidi kuongeza chuki kutoka kwa jamii na jamii inaendelea kushikamana ili kuing'oa madarakani. Wanasahau usemi wa wahenga kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha.
 

Attachments

  • 2013-02-16 17.51.10.jpg
    2013-02-16 17.51.10.jpg
    409.4 KB · Views: 163
  • 2013-02-16 17.58.26.jpg
    2013-02-16 17.58.26.jpg
    268.4 KB · Views: 134
  • 2013-05-11 16.31.32.jpg
    2013-05-11 16.31.32.jpg
    282.1 KB · Views: 131
  • 2013-05-11 16.31.38.jpg
    2013-05-11 16.31.38.jpg
    281.6 KB · Views: 123
  • 2013-05-11 16.31.44.jpg
    2013-05-11 16.31.44.jpg
    282.7 KB · Views: 136
  • 2013-05-11 17.35.00.jpg
    2013-05-11 17.35.00.jpg
    174.9 KB · Views: 120
lameck Madelu alipodai ana ushahidi wa ugaidi wa Lwakatare, Polisi hawakutoka mipovu na kumtaka awapelekee huo ushahidi huo . Lakini, Mbowe alipodai kuwa na ushahidi wa aliyetupa bomu arusha, polisi siyo tu wanamtaka awapelekee huo ushahidi bali wametoa vitisho dhidi yake. Je, hii siyo double au triple standard? Na je, Polisi wameenda Arusha kuchunguza au kutoa vitisho?
 
Huo ujanjaujanja wenu CHADEMA wa kuwaua wananchi kwa makusudi halafu mnakimbilia kusema ni polisi ili wananchi waichukie serikali yao wananchi wameshaugundua.

Eti aliyerusha bomu alikuwa amevaa sare za polisi, mara oooh! risasi zilizotumika ni za jeshi la polisi, WTF?! Ni watu wangapi wanaomiliki sare za jeshi na silaha kinyume cha sheria?
 
Ni kweli tunaziona dalili zote za extinction kwa ccm. Imekuwa ikiringa kutokana na ukubwa wake lakini hakuna lisilo na mwisho
 
....huwa najiuliza ccm watakimbilia wapi zanzibar hawatakiwi,huku bara ndo kabsaaaa hata kuwasikia kinyaaa, labda waende komoro...
 
Kufa kwa CCM ni swala ambalo hata walioko ndani ya CCM wenyewe wanajua kama siku za kufa zinakalibia na ndio maana kila kukicha hawaishi hila, na kuzusha mambo kila leo hiyo ni katika hali ya kutapa tapa, na kwa msingi huo wanaanza kutumia udikteta katika utawala na kuanza kuuwa raia ambao hawana hatia.

Hata watumie polisi kiasi gani hawawezi kutunyamazisha katika harakati za kulikomboa taifa letu kutoka katika mikono yao ya kifisadi.

kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo watanzania wanavyozidi kujiamini katika kutete nchi yao na kudai haki zao za msingi

WATANZANIA WOGA WETU NDIO UMASIKINI WETU
 
Enzi hizo chama tawala nnchini kenya KANU kilipo karibia kuanguka kilikua kikifanya kama yanayofanywa na ccm sasa waliuwa sana wanaharakati, wasemakweli, mapadri n.k, vilevile enzi hizo Rais Arap Toroitich Moi aliwahi kumcheka Rais Kenes Kaunda wa zambia "hahahaha serikali yako, jeshi lako, polisi wakwako unaachia vp madaraka?" haya mambo yanayoendele TZ ya mabomu, kucha,mbaroni na meno wananchi tunaona na kusikia na tunajua yanafanywa na ccm adhabu inakuja 2015.
 
Kiukweli hata ukimuliza mtoto mdogo atakuambia ccm wamechoka. Kwa sababu ya matukio wanayofanya. Moja ya mambo yanayoonesha ccm imekufa na sio inakufa ni KUWATISHA WANANCHI katika nchi yeyote ile pale chama tawala kinapoona kuwa kinapopoteza matumaini na wananchi kinatumia nguvu za dolar kama polis kuwatisha wananchi. Kama yanayotekea kanda ya kaskazini ni dhahiri kuwa ni mbinu ya ccm kuwapa uoga wananchi ili waone bora waendelee kuwakumbatia mafisadi ccm NATOA USHAURI KWA WANACHADEMA WOTE KUWA WASIOGOPE YANAYOTOKEA NI ISHARA YA USHINDI MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI CHADEMA
 
Kwa mtanzania mwenye busara na akili timamu atakubaliana nami kuwa serikali ya ccm imeshindwa kabisa kuongoza.
Tanzania imejaliwa maliasili nyingi na Mwenyezi Mungu lakini hazi tunufaishi vilivyo bali kundi la watu wachache.
Tumeshuhudia madudu mengi ya hii serikali yenye dhuluma kuu na uvunjifu wa haki za binadamu yakitendwa na serikali hii dhalimu; Lakini wanajitetea kwa kutumia vyombo vya dola kuhalalisha dhuluma hizi. Angalia kama haya ya Arusha!
Hivyo wanachama wa ccm na viongozi wa serikali yao na chama wapo hapo kwa ajiri ya haya:-
1. Kujipatia Mali na fedha kwa dhuluma na magendo.
2. Kulinda biashara zao haramu.
3. Uchu wa madaraka na vyeo.
4. Waliofukuzwa vyama vingine kwa utovu wa nidhamu.
5. Waliokosa na ambao elimu ya uraia na ukombozi haija wafikia hasa vijijini.
Ndio maana ccm wanatumia na wataendelea kutumia nguvu ya mtutu kulazimisha wazalendo wawakubali yaani heshima ya mabavu.
Niaminivyo mimi dola makini hupata heshima kwa matendo yake mema,kutenda haki, utu, usawa na wajibu kwa viongozi wake na watu wake wataheshimu dola.
Hadi hapa tulipo dola la ccm limeshindwa; Hivyo naomba vyama makini vya upinzani mjikite vijijini kutoa elimu ya uraia na kuelezea madhambi ya ccm ambayo yametapakaa kama mchanga wa bahari.
 
Wane loose legitimate ya kuongoza kama Bashar Asaad wa Syria ndio ukaona kina Punda Mizengwe wakaanza kuhalalisha vyombo vya dola kutumia mabavu ili waendelee kutawala
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom