Nimeona kadi hii ya Christmas yenye picha ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Makamu wake William Rutto.
Lakini ukiangalia vizuri kwenye background ya picha hiyo utauoana mlima Kilimanjaro,
Nimejiuliza sana; Kwanini wakenya wanapenda kusafiria nyota zetu?
Huu mlima waliuweka kwenye ndege zao za Kenya Airways, wakaona haitoshi.
Sasa wameuweka tena kwenye kadi za Christmas ili kuendelea kuiaminisha dunia kuwa Upo kwao, hivyo kukuza sekta ya utalii kwa ulaghai wa namna hii.
Utakumbuka pia binti wa Raila Odinga akiwa anahutubia umoja wa mataifa aliwahi kusema bonde la Olduvai lipo Kenya japo alikuja kukanusha lakini nina hakika watanzania Tungekaa Kimya bado dunia ingeaminishwa bonde hii hili lipo Kenya.
Wakuu tabia Hii ya Kenya kusafiria nyota ya Tanzania Mpaka lini?
Sisi hatuna tabia ya kutangaza vitu vyetu
Alianza baba sasa mtoto anatujaribu japo anatujaribu wakati tuna rais genius.
[HASHTAG]#Tell[/HASHTAG] Uhuru to stop using Mt Kilimanjaro on his fotos background
Haaaah wazee wa fulsa ujanja ujanja,Chezeeni tu utalii kwa ma vat mtaleta feedback mwakani June
Kuna mlima gani kenya juu una barafu?Shule mlienda kusomea ujinga?Mbona hakuna sehemu wameandika huo ni mlima kilimanjaro?What if wanamaanisha mlima mwingine uliopo Kenya..Tunajistukia tu...