Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza mchakato wa kufanyia mabadiliko ya noti mpya ya Sh500, ili iwe ya sarafu baada ya kujiridhisha kuwa inachakaa kwa haraka zaidi.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Arusha, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, alisema mchakato kuifanyia mabadiliko na noti hiyo ili iwe katika sarafu, inazingatia ukweli kwamba fedha iliyoko katika mzunguko mkubwa katika jamii.
Profesa Ndulu alisema noti ya Sh500 inatumika kwa kiasi kikubwa na wananchi wengi, jambo linalosababisha kuchakaa haraka kabla ya wakati uliopangwa.
"Tunafanya mchakato wa mabadiliko ya noti hizi zinazochakaa kwa haraka kwa sababu zenyewe zinatumika zaidi," alisema Profesa Ndulu.
Alisema hatua hiyo haitaathiri mzunguko wa fedha na kwamba sarafu ya Sh500 itakapoanza kutumika, noti hiyo itaondoka polepole. Alisema sarafu hiyo ya Sh 500 itaanza kupatikana katika kipindi kifupi kijacho na kuwawezesha wananchi kuitumia.
"Watanzania wasishituke mabadiliko hayo ya noti za Sh500 kwenda sarafu maana hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watoa chenji," alisema.
Maoni yangu
Nimekuwa nikifwatilia sana kauli za Governor wetu Benno Ndulu binafsi nimegundua anatoaga kauli nying sana za kibabaishaji kama sio za kuhadaa umma wa watanzania. Katika toleo la noti mpya ambazo zipo sasa hivi kwenye mzunguku ikiwemo hii mia tano inayotaka kufanywa Sarafu, Benno Ndulu alituambia ina ubora wa hali ya juu, kauli hii ilikuja baada ya wananchi kuhoji ubora wake. Wananchi walisema noti hizo mpya kuwa zinachuja rangi, Benk kuu ikasema ukiona zinachuja basi ndo ujue zipo bomba yaani ni original na sio fake mana ujio wa noti hizi uliambatana na hela fake nyingi sana ambazo zilishabihiana sana na noti halali.
Governor keshasahau kauli yake na leo hii anasema kuwa noti hiyo inachakaa haraka zaidi kwa kuwa tsh 500 zinatumika zaidi, hii ni sababu ya kibabaishaji. Hii kauli kwa kweli toka uhuru haijawahi kusikika. Tulishakuwaga na tsh 10, 20, 50, 100 etc za noti, noti hizi zilishikwa sana tu, lakin sababu mbovu kama hii haikutolewa. Fedha zile zilibadilishwa kuwa sarafu baada ya dhamani yake kupungua na sio kuwa zilishikwa sana. Kimsingi anachomaanisha Governor hapa ni kwamba hela huwa inabadilishwa kutoka kwenye noti kuwa sarafu kwa ajili ya kushikwa sana na kutumika zaidi ya nyingine.
Huu utafiti kaufanya lini kujua kuwa 500 inazunguka zaid?????Anataka kusema ikitokea siku 10,000 ikawa inashikwa/inazunguka zaidi ya 5,000 atabadilisha noti ya 10,000 kuwa coin kabla ya kubadilisha noti ya 5,000 ambayo haishikwi sana kuwa coin????Mbona hawazifanyi sarafu za tsh 1, 5, 10, 20 kuwa noti???si hatuzishiki sana??? Kwanini anaficha ukweli kuwa mabadiliko hayo yanatokana na either kushuka kwa thamani ya fedha za Tanzania au poor quality ya noti zetu???
Kauli hizi binafsi naziclasify kama zakibabaishaji hasa kwa kuwa zimetolewa na Prof. ambaye pia ni mtendaji mkuu wa Central Bank ya Tanzania. Wataalam wa mambo ya uchumi tusaidieni, kuna ukweli wa maneno ya huyu mzee??? USA wanatumia $ 1 ya noti, $ 5 ya noti wao hizi hazipo kwenye mzunguko mkubwa??? Mbona hawahangaiki nazo kuzifanya sarafu??