Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
1. Je, Mhe Wakili Msomi, Ng'wasi Damas Kamani, anadhani kuchapisha Noti mpyani sawa na kwenda kutoa kopi "Stationary"?
2. Je, Mhe Kamani anajua Mkwanja mrefu sana unatumika kuchapisha noti mpya?
3. Je, kwakuwa WAHENGA walinena kuwa "Kupanga ni Kuchagua"; kipi cha muhimu kati ya Noti mpya zenye picha ya Rais Samia kama kumbukumbu ya Rais wa kwanza mwanamke au fedha hizo kutumika kutatua matatizo rundo yanayowakabili wananchi wengi walio kwenye rindi kubwa la ufukara?
4. Je, Mhe Kamani Ancona Rais JK & Dkt. JPM walikosea walipofuata nyayo za Rais Ben Mkapa ambaye aliita waandishi wa habari Novemba 23, 1995 na kueleza bayana kuwa haoni mantiki ya fedha nyingi kutumika kutengeneza noti mpya ili tu kuwekwa picha yake wakati nchi haina fedha na haikopesheki na hali za wananchi ni mbaya?
5. Je, na rai ya yule mbunge mwingine April 23, 2021 eti "Noti za Tanzania zibadilishwe na kuwekwa picha ya marehemu Rais Dkt. John Magufuli ili kuenzi makubwa aliyoyafanya kwa Taifa hili", haikufanyiwa kazi?
6. Je, huu si mwendelezo wa "Chawacracy" uliotamalaki kwenye "Medula oblangata" za viongozi wengi nchini?
7. Je, Mhe Kamani anajua kuwa nchi ya Marekani imekuwa na Marais 46 hadi sasa lakini noti zake zina picha George Washington tu ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo?
8. Je, umefika wakati sasa wa Sheria ya Benki Kuu 2006 ikarekebishwa ili kuingizwa kifungu kipya kama Kifungu cha 21 cha Sheria ya Benki Kuu ya Uganda, 2000 kilatazacho picha ya mtu yeyote aliye hai au alama yoyote ya kisiasa kwenye noti? Kifungu hicho kiliwekwa baada ya "Chawa" kuanza chokochoko kuwa Picha ya Rais Museveni iwekwe kwenye noti mpya za nchi hiyo.