Kauli hizi za Governor wa Benki Kuu zinadhalilisha taaluma yake na kuhadaa wananchi

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza mchakato wa kufanyia mabadiliko ya noti mpya ya Sh500, ili iwe ya sarafu baada ya kujiridhisha kuwa inachakaa kwa haraka zaidi.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Arusha, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, alisema mchakato kuifanyia mabadiliko na noti hiyo ili iwe katika sarafu, inazingatia ukweli kwamba fedha iliyoko katika mzunguko mkubwa katika jamii.

Profesa Ndulu alisema noti ya Sh500 inatumika kwa kiasi kikubwa na wananchi wengi, jambo linalosababisha kuchakaa haraka kabla ya wakati uliopangwa.

"Tunafanya mchakato wa mabadiliko ya noti hizi zinazochakaa kwa haraka kwa sababu zenyewe zinatumika zaidi," alisema Profesa Ndulu.

Alisema hatua hiyo haitaathiri mzunguko wa fedha na kwamba sarafu ya Sh500 itakapoanza kutumika, noti hiyo itaondoka polepole. Alisema sarafu hiyo ya Sh 500 itaanza kupatikana katika kipindi kifupi kijacho na kuwawezesha wananchi kuitumia.

"Watanzania wasishituke mabadiliko hayo ya noti za Sh500 kwenda sarafu maana hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watoa chenji," alisema.

Maoni yangu

Nimekuwa nikifwatilia sana kauli za Governor wetu Benno Ndulu binafsi nimegundua anatoaga kauli nying sana za kibabaishaji kama sio za kuhadaa umma wa watanzania. Katika toleo la noti mpya ambazo zipo sasa hivi kwenye mzunguku ikiwemo hii mia tano inayotaka kufanywa Sarafu, Benno Ndulu alituambia ina ubora wa hali ya juu, kauli hii ilikuja baada ya wananchi kuhoji ubora wake. Wananchi walisema noti hizo mpya kuwa zinachuja rangi, Benk kuu ikasema ukiona zinachuja basi ndo ujue zipo bomba yaani ni original na sio fake mana ujio wa noti hizi uliambatana na hela fake nyingi sana ambazo zilishabihiana sana na noti halali.

Governor keshasahau kauli yake na leo hii anasema kuwa noti hiyo inachakaa haraka zaidi kwa kuwa tsh 500 zinatumika zaidi, hii ni sababu ya kibabaishaji. Hii kauli kwa kweli toka uhuru haijawahi kusikika. Tulishakuwaga na tsh 10, 20, 50, 100 etc za noti, noti hizi zilishikwa sana tu, lakin sababu mbovu kama hii haikutolewa. Fedha zile zilibadilishwa kuwa sarafu baada ya dhamani yake kupungua na sio kuwa zilishikwa sana. Kimsingi anachomaanisha Governor hapa ni kwamba hela huwa inabadilishwa kutoka kwenye noti kuwa sarafu kwa ajili ya kushikwa sana na kutumika zaidi ya nyingine.

Huu utafiti kaufanya lini kujua kuwa 500 inazunguka zaid?????Anataka kusema ikitokea siku 10,000 ikawa inashikwa/inazunguka zaidi ya 5,000 atabadilisha noti ya 10,000 kuwa coin kabla ya kubadilisha noti ya 5,000 ambayo haishikwi sana kuwa coin????Mbona hawazifanyi sarafu za tsh 1, 5, 10, 20 kuwa noti???si hatuzishiki sana??? Kwanini anaficha ukweli kuwa mabadiliko hayo yanatokana na either kushuka kwa thamani ya fedha za Tanzania au poor quality ya noti zetu???

Kauli hizi binafsi naziclasify kama zakibabaishaji hasa kwa kuwa zimetolewa na Prof. ambaye pia ni mtendaji mkuu wa Central Bank ya Tanzania. Wataalam wa mambo ya uchumi tusaidieni, kuna ukweli wa maneno ya huyu mzee??? USA wanatumia $ 1 ya noti, $ 5 ya noti wao hizi hazipo kwenye mzunguko mkubwa??? Mbona hawahangaiki nazo kuzifanya sarafu??
 
Na ile noti ya sh elfu hamsini iliishia wapi?
Tatizo sio hela inazunguka sana bali material waliyotengenezea ni very poor quality!!wasitafute sababu zingine!!!
 
Noti hata ikiwa vipi lazima itachakaa esp hiyo ya denomination ya chini ambayo kila mtu anaishika. Kumbuka pia hizo 500 hazipiti sana BOT.Ni utaratibu wa kawaida kutoa noti chafu kuingiza safi.sasa sijui ubabaishaji umetoka wapi?
 
Mkuu,

Sioni ubaya wa hoja yake.
Ubaya wa hoja yake ni kwamba hii hoja imechelewa. hivi ni vitu ambavyo walitakiwa ku-consider wakati wanataka kutoa noti mpya ambazo sijui hata mwaka kama umeisha noti zinachakaa.

Ni kitu kiko wazi kabisa kuwa noti ya shs 500 inazunguka sana kwa sababu ndiyo inayotumiwa na raia wengi ambao kipato chao ni cha chini sana. kitu walichotakiwa hapo mwanzo hawa Bot kilikuwa ni kutengeneza noti ya shs 500 yenye ubora mzuri au kutengeneza sarafu from the begining.

Hizi tabia ni za kifisadi kabisa,mtu ana skip facts wakati wa decision fulani ili kuacha room kwa ajili ya kubuni activity nyingine lengo ni kuwa na opportunities nyingi za kupiga hela. Hivyo ndio serikali yetu inavyofanya kazi.

Mbona bado unaboronga tu. Noti siku zote zinakuwa kwenye circulation kwa muda fulani. Vilevile uchapishaji unaendeshwa na benk ambayo hiyo ni biashara yake. Hivyo hakuna ufisadi wowote ule.

Kwani kiwanda cha soda kikibadilisha kutumia chupa za kioo na kuanza kutumia plastiki, mlaji anapata hasara gani?
 
  • Thanks
Reactions: Tom
Noti hata ikiwa vipi lazima itachakaa esp hiyo ya denomination ya chini ambayo kila mtu anaishika. Kumbuka pia hizo 500 hazipiti sana BOT.Ni utaratibu wa kawaida kutoa noti chafu kuingiza safi.sasa sijui ubabaishaji umetoka wapi?

Vilevile hali ya hewa ya Tanzania. Watu wana mikono ya jasho na hawatumii waleti.
 
Hao watumiaji wa sh 500 wameongezeka lini?
Hapo kuna dili la waziwazi la kutafuna hela hela za wala ugali na chumvi kwenye mchakato wa kuifyatua sarafu mpya

Kwa taarifa yako life span ya sarafu ni kubwa kuliko noti. Hivyo gharama za uzalishaji za benk kuu zinapungua ukitumia sarafu.
 
Hata jk akimaliza kipindi cha ubabaishaji wake, bac nusu ya watz watakuwa mental dis-order kutokana na kauli na matendo ya hovyo ever zinazotolewa na sirkali hii. Ni vema Serikali ijayo lazma ifanye uchunguzi wa 'mental defection' kwa watanzania iliyosababishwa na maamuzi ya ajabu 'grand shocks' ya serikali ya jk, haiwezekani kila uchao tunasikia kauli tata tuuu utadhani zinatoka mirembe!
 
Noti hata ikiwa vipi lazima itachakaa esp hiyo ya denomination ya chini ambayo kila mtu anaishika. Kumbuka pia hizo 500 hazipiti sana BOT.Ni utaratibu wa kawaida kutoa noti chafu kuingiza safi.sasa sijui ubabaishaji umetoka wapi?

Ubabaishaji ni pale anapotaka kuhalalisha ubora wa hizi noti mpya kwa kisingizio cha noti kushikwa sana! Ukweli hizi noti ni bomu, basi na 1000 nayo waifanye iwe sarafu maana nayo imechakaa! Ni aibu kwa Prof. mzima kuwa mbabaishaji kiasi hicho
 
Mkuu,

Sioni ubaya wa hoja yake.

Naamini GAVANA ana nia nzuri na angependa ubora wa noti ungekua wa hali ya juu, lakini kama alivyo JK na uongozi wa CCM, gavana hajui afanyeje ili ubora wa noti uwe wa hali ya juu. Ubora ni jambo ambalo lilitakiwa walizingatie hata kabla ya hizo noti kuchapwa maana wanajua noti zipi zinatumika sana.
Kama utaratibu wa tenda usipokua madhubuti, hata sarafu hatitakua na ubora.
 
Mbona bado unaboronga tu. Noti siku zote zinakuwa kwenye circulation kwa muda fulani. Vilevile uchapishaji unaendeshwa na benk ambayo hiyo ni biashara yake. Hivyo hakuna ufisadi wowote ule.

Kwani kiwanda cha soda kikibadilisha kutumia chupa za kioo na kuanza kutumia plastiki, mlaji anapata hasara gani?

athari kubwa ya sarafu za mia 5 ni mzgo ukiwa mfukoni,itatutobolea mifuko ya vibwende vyetu bhana,
 
Back
Top Bottom