Kauli hizi za Governor wa Benki Kuu zinadhalilisha taaluma yake na kuhadaa wananchi

Noti hata ikiwa vipi lazima itachakaa esp hiyo ya denomination ya chini ambayo kila mtu anaishika. Kumbuka pia hizo 500 hazipiti sana BOT.Ni utaratibu wa kawaida kutoa noti chafu kuingiza safi.sasa sijui ubabaishaji umetoka wapi?
Hajausisha hoja ya kisayansi kama Prof. mbona hakuna noti ya Tsh 5??Maana tsh 5 hatuzishiki sana so hakuna haja ya kuzifanya sarafu. Ukweli ni kwamba thamani ya noti hiyo imepungua na hivyo kuitengeneza in form ya noti ni bei juu kuliko thaman ya noti yenyewe. Labda uniambie kuwa ni ile sera ya PRINT MORE MONEY.
 
Hakuna kitu hapo Gavana Benno Ndulu, ungesema tu ukweli kwa wananchi kuwa noti za mia tano hazina ubora unaotakiwa.

China kuna noti nyingi sana wanazitumia na ndio wapo wengi kuzidi sisi.

Lakini hawajawahi kusema kuwa watumie sarafu kwa sababu noti zao zipo kwenye mzunguko zinatumiwa na watu wengi zinachakaa.

Ilo ndio tatizo la Tanzania uchumi kutumikia siasa.
 
Mbona bado unaboronga tu. Noti siku zote zinakuwa kwenye circulation kwa muda fulani. Vilevile uchapishaji unaendeshwa na benk ambayo hiyo ni biashara yake. Hivyo hakuna ufisadi wowote ule.

Kwani kiwanda cha soda kikibadilisha kutumia chupa za kioo na kuanza kutumia plastiki, mlaji anapata hasara gani?
Kwa Tanzania yetu hapo hapakosi ufisadi, kuna suala la kuongeza idadi ya noti zinazotakiwa kuchapishwa, au umeshasahau huu ni mchezo wa kawaida wa BOT inapotokea uchapishwaji wa noti????? Kuna kuongeza bei halisi ya uchapishaji wa fedha hizo etc. Yapo mambo mengi sana dubious hapo kwenye huo mchakato.
 
Coin za 50 na 100 hazikai muda mrefu kabla ya kuharibika hiyo ya 500 itakuwaje?
 
Bank kuu ni bank inayojitegemea. Na moja biashara yake ni kutoa pesa. sasa nyinyi msio fanya hiyo biashara mnataka benki ifanye mnavyofikiria.
Yeye angechapisha tu zikija ndo atutangazie kuwa kuna mali mpya imeingia sokoni. Kinachokera ni kutufanya wote wa jinga na kutupa sababu za kibabaishaji as if wote hatujaenda shule. Naimani wenye mtazamo kama Ndulu wapo wengi, naomba kutofautiana nao mana sababu zao naziona hazina mashiko kutolewa na watu wazima.
 
Noti hata ikiwa vipi lazima itachakaa esp hiyo ya denomination ya chini ambayo kila mtu anaishika. Kumbuka pia hizo 500 hazipiti sana BOT.Ni utaratibu wa kawaida kutoa noti chafu kuingiza safi.sasa sijui ubabaishaji umetoka wapi?
Ni kweli ni utaratibu wa kawaida kutoa noti chafu kuingiza noti mpya, ila sio kawaida kutoa noti chafu kuleta coins badala ya noti mana hapo kuna kuandaa design ya hiyo coin na kutoa noti za 500 kwenye mzunguko na kuziteketeza. Ujue hizi zote ni cost na walipaji wa cost hizo ni sisi wananchi, kuna haja gani kubadilisha hiyo noti sasa hivi wakati uchumi wenyewe umetandikika????Kwann maamuzi hayo yasingefanywa wakati ule wanatoa toleo jipya la tsh 500???

Akiri ubora haukuzingatiwa, thamani ya pesa hiyo imepotea na hivyo inalazimu ibadilishwe na kuwa coin na sio kuwa inashikwa na watanzania wengi. Mbona nchi za wenzetu nao wana noti zinazoshikwa sana kuliko hata hizi zetu lakin hawafanyi maamuzi ya kibabaishaji kama haya???So ikitokea siku 10,000 ikawa inashikwa zaidi ya 5,000 atabadilisha noti ya 10,000 kuwa coin kabla ya kubadilisha noti ya 5,000 kuwa coin????After all ni uchunguzi gani aliufanya kujua 500 ndo inashkwa sana kuliko 1000 au 10,000???awe mkweli tu sababu aliyoitoa ni ya kibabaishaji hasa kutolewa na Prof, labda kama ni uProf maji marefu au uProf wa heshima.
 
I have discredited Governor Ndulu for a long time he is letting us down especially his students by the way he is abusing his academic credentials. Professor anakuwa sawa na mwanasiasa wa darasa la 7 mwe Tanzania kuna vituko!!!!!
 
Nategemea kuwa wabunge makini watalihoji jambo hili bungeni kwani ni muda mfupi tangu kuchapishwa noti mpya-je kitengo cha research hakifanyi kazi pale bot au benk haina planning system, au ni wizi?
 
“Watanzania wasishituke mabadiliko hayo ya noti za Sh500 kwenda sarafu maana hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watoa chenji,”alisema.

Mimi nimefurahishwa na hii sentensi..ati itawasaidia watanzania kwenye chenji..hivi profesa wa uchumi unaweza ukatoa sababu ya kijinga kama hii,wakati unapotaka kufanya mabadiliko makubwa na yanayogusa uchumi wa nchi? Hili ni tatizo la kuchanganya taaluma na siasa,ifike kipindi wataalamu wetu watambue kuwa kuchangamana na siasa na wanasiasa hakutawasaidia,zaidi watazidi kuonekana kama vituko mbele ya jamii....
 
Wewe unayesema noti ni bomu unatumia kigezo gani? Au kwakuwa huwa unapewa 500 chafu kutoka kwa muuza mkaa? Acheni kulaumu kusiko na msingi. Gov ameongea jambo la msingi alete 500 ya coin itatusaidia kupunguza gharama.
 
atanzania tusiwe wabishi wakati mwingine kwa mambo mengine ambayo yako wazi. Hivi unaweza linganisha 'hali' ya noti za Tsh. 10,000 na sh.500 zilizo kwenye mzunguko?? Zipi zimechakaa sana kuliko nyingine?? kwanini?? je zinatofautiana sana materials zilizotumika kuzitengeneza?? Tena ukiangalia kwa makini utakuta kadiri noti zinavopishana thamani ndo zinavoongezeka kwa rate ya uchakavu (Hii inatokana na urefu wa kukaa kwenye mzunguko na frequency ya matumizi)

Ingia benki yeyote fanya research uone watu wanapokuja kudiposit hua wanadeposit noti za kiasi gani kwa wingi. Kauli ya Ndullu ina mashiko, shilingi miatano zinakaa sana mikononi ukilinganisha na 10,000 au 5000 (tena kipindi hiki cha mfumuko wa bei). Tena ukienda ma-wilayani huko ambako kuna tawi moja tu la NMB noti ndo zimechakaa usipime, kwanini?? Jibu ni kwamba Zinachukua muda kufika benki kuu ili kubadilishwa. In a nutshell ni kwamba Governor yupo sahihi kabisa esp kama unaifahamu vizuri sector ya fedha wala hutabisha sana.
 
Mbona bado unaboronga tu. Noti siku zote zinakuwa kwenye circulation kwa muda fulani. Vilevile uchapishaji unaendeshwa na benk ambayo hiyo ni biashara yake. Hivyo hakuna ufisadi wowote ule.

Hivi kweli Zakumi unaongea kwa ukweli wa mambo ulivyo au wewe ni mmojawapo wa wenye maslahi na BOT? Siamini argument zako hapa kama kweli unashindwa kuelewa point anazotoa mwanzilishi wa hii thread. Unajua noti za US zinakuwa kwenye circulation kwa muda gani lakini? Sasa iweje baada ya kuwahakikishiwa Watanzania kwamba noti zilizochapishwa ni high quality leo tuseme unajua zinachakaa haraka! Hivi hujui kutengeneza sarafu maana yake tenda nyingine hiyo, ambayo ni kodi anayolipa mwananchi?

Jamani, hebu kuweni wa kweli. Tunajua humu ndani tupo wachukia ufisadi na wafaidikaji na ufisadi, lakini vitu vingine vya kifisadi ni aibu hata kuvitetea.
 
Ni wazi kuwa noti hizi mpya kiwango cha ubora kiko chini sana na hakuna duniani nchi yenye noti za kiwango cha chini kama hizi, tatizo Prof. Ndulu alishakula rushwa na kutoa zabuni kwa kampuni kutengeneza noti feki ambazo hazijawahi kutengenezwa na nchi hii toka tuanze kutumia noti
 
Mnataka kunambia thamani ya kutengeneza sh 10 au 20 ni ndogo ukiloinganisha na thamani ya pesa yenyewe?
 
Ni kweli ni utaratibu wa kawaida kutoa noti chafu kuingiza noti mpya, ila sio kawaida kutoa noti chafu kuleta coins badala ya noti mana hapo kuna kuandaa design ya hiyo coin na kutoa noti za 500 kwenye mzunguko na kuziteketeza. Ujue hizi zote ni cost na walipaji wa cost hizo ni sisi wananchi, kuna haja gani kubadilisha hiyo noti sasa hivi wakati uchumi wenyewe umetandikika????Kwann maamuzi hayo yasingefanywa wakati ule wanatoa toleo jipya la tsh 500???

Akiri ubora haukuzingatiwa, thamani ya pesa hiyo imepotea na hivyo inalazimu ibadilishwe na kuwa coin na sio kuwa inashikwa na watanzania wengi. Mbona nchi za wenzetu nao wana noti zinazoshikwa sana kuliko hata hizi zetu lakin hawafanyi maamuzi ya kibabaishaji kama haya???So ikitokea siku 10,000 ikawa inashikwa zaidi ya 5,000 atabadilisha noti ya 10,000 kuwa coin kabla ya kubadilisha noti ya 5,000 kuwa coin????After all ni uchunguzi gani aliufanya kujua 500 ndo inashkwa sana kuliko 1000 au 10,000???awe mkweli tu sababu aliyoitoa ni ya kibabaishaji hasa kutolewa na Prof, labda kama ni uProf maji marefu au uProf wa heshima.

Ndugu Patriote,

Hizo nchi unazozitaja siku hizi watu wachache sana wanabeba pesa cash, watu huko ni mwendo wa ku swipe card na kununua vitu amazon kama sio kuhamisha pesa kwa mtandao , internet and telephone banking. Pia, mazingira yao na maisha yao tofauti si kama huku kwetu kwahiyo still viehal vyetu hivi especially denomination za chini zitaendelea kuchafuka haraka namuunga mkono Prof.

Na nchi na nchi zipo tofauti, huku kwetu watu wanaopeleka benki ku deposit denomination za 500 ni wachache mkubwa.
 
I have discredited Governor Ndulu for a long time he is letting us down especially his students by the way he is abusing his academic credentials. Professor anakuwa sawa na mwanasiasa wa darasa la 7 mwe Tanzania kuna vituko!!!!!

Kwani Ndullu ni profesa sampuli ya akina Lipumba au sampuli ya akina Vulata na Maji marefu? Maana naona hatuna gavana wa BOT kwa muda mrefh
 
Kwani zile noti za 500 za zamani mbona hazikuwa zinachakaa?

Zamani 500 ilikua ina thamani, ilikua inaenda benki. Siku hizi 500 benki HAIFIKI!!asubuhi unalipa nauli, konda anaunulia maji ya kunywa, muuza maji anaipeleka kwa mama ntilie mchana, mama ntilie anarudisha chenji kwa mchuuzi, mchuuzi anapandia daladala jioni kurudi home kwake, konda anakurudishia chenji kwenye basi wakati unatoka kazini!!Kesho mzunguko unaanza tena. Hii ni tofauti na zamani wakati nauli ilikua sh.100,andazi sh.20, maji ya kiloba-AZAM sh.50, petrol lita sh. 420!!Sasa hapo sh.500 itachakaaje!!?

Ukibisha na hili basi tena
 
Back
Top Bottom