brainiac89
Member
- Dec 3, 2011
- 35
- 29
Nayasema haya nikiwa na uchungu na masikitiko makubwa kwa hiki ambacho madaktari wanachoendelea kututendea waTanzania! kuna machache wacha niyaseme ili moyo wangu utulie!
1. kama sikosei mgomo wa madaktari wa mwaka 2004, madaktari walikua wanadai ongezeko la mishahara, ambapo kwa kipindi hicho mshahara wa daktari anayeanza kazi ulikua ni mkubwa zaidi ya mshahara wa mwalimu aliyemaliza madaraja yote ya ualimu (nikimaanisha mwalimu aliyeitumikia serikali zaidi ya miaka 35).
2. daktari anayeanza kazi sasa analipwa 950,000 wakati mwalimu mwenye 'degree' anayeanza kazi analipwa si zaidi ya 500,000.
3. tukumbuke katika kada za utumishi wa serikali ni madaktari pekee ndio wanaruhusiwa kutumia utaalamu wao nje ya ofisi zao mf. kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri katika ofisi tofauti (najua kunawatakao uliza kuhusu walimu kufundisha tuisheni na kufanya katika shule binafsi, lakini kiukweli ni kwamba walimu hao wanakiuka mkataba wa kazi wa mwajiri wao 'serikali').
4. tukumbuke pia madaktari ndio watumishi pekee walioruhusiwa kulipwa au kupewa chochote kutoka kwa mtu waliyemuhudumia kwa issue kama consultancy na isihesabike kama rushwa, ndio maana unakuta kuna kibao kimeandikwa KUMUONA DAKTARI NI TSH.****. wakati kwenye kada nyingine hilo ni jambo lenye utata na inahesabika moja kwa moja kama ni rushwa! (ushawahi kuona mwanafunzi kamuuliza swali mwalimu halafu mwalimu akadai pesa???)
5. Pia tusisahau kwamba madaktari 'Medical Doctors' ndio taaluma pekee ambayo wanaposoma katika chuo kama Muhimbili wanapewa ada na matumizi mengine for free lakini taaluma nyingine wanalipa hiyo mikopo pindi watakapoanza kazi!
mimi nadhani imefika kipindi madaktari wasifanye vitu kwa utashi wao na kusahau kuwa ni Mungu tu ndiye aliyewapa utaalamu huo na kuwawezesha wafike hapo! tumrudie Mwenye enzi ili atutakase katika hili! kugoma kwenu madaktari mnasababisha vifo vya watu ambao hawana hatia, watu ambao wanategemea vipawa vyenu mlivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu ili muwahudumie wagonjwa. hebu jaribuni kuangalia mnapotupeleka, hivi kweli katika hili Mungu atabariki kazi za mikono yenu???? KWELI KATIKA HILI MADAKTARI HAMTUTENDEI HAKI WATANZANIA!