Katika hili Madaktari hamtutendei haki wa-Tanzania

asante
sana
mkuu, hawa madr we2 wameshakua hopeless, eti watagoma mpk mponda
na nkya wajiuzulu. Pia ni wabinafsi tu, kama mishahara yao ni midogo,
bila shaka ya sekta nyingne ni midogo pia. So km wana uzalendo,
wangeweka ubinafsi wao pembeni na kama wanagoma basi wagome kwa maslah
ya kada zote. Mimi binafsi siwaungi mkono hata kdg. Kama ni mazingira
magumu ya kazi, hebu waseme mwalimu aliyepangiwa kufundisha shule ya
kata wilaya ya kibondo vijijini huko kigoma ana mazingira rahisi ya
kazi? Wasituzingue sisi, wachape kazi na wadai maslah yao kwa mpango
sio kuwapa tabu watanzania.
nadhani kaka wasipokusikia wewe watakua ni wapumbavu! Hawa jamaa wanadai
mazingra magumu ya kazi kila m2 anamazingira magumu! Hawajawah
kujiuliza walgmu wa chemistry wanavyocheza na zile chemicals maabara
kuwafanya wao wajenge msingi wa hapo walipofikia! Hawa jamaa wamekua
hopeless kbs
 
Unajitahidi kujenga hoja za UONGO kiasi mtu hasipokuwa makini anaweza kukuamini...hongera kwa hilo. Acha tu tuaninshe ukweli wa baadhi ya uliyodanganya hapo:

2. Ni ukweli kuwa kada hazilipwi sawa kwa kiwango kimoja cha elimu kama mshahara wa kuanzia. Na hata benefit zinatofautiana..hilo lipo kisheria. Mshahara wa kuandia wa mwalimu mwenye degree, si sawa na mshahara wa kuanzia wa daktari mwenye degree, na si sawa na mshahara wa kuanzia wa mwanasheria, mchumi, mhasibu etc..Kila fani ina jukumu la kuamua thamani yake, na maDakatari hawawezi kuamulia fani nyingine thamani yao, kama mwalimu ameridhika na 500,000 na hadai zaidi, wakati kuna taasisi za serikali mtu mwenye diploma tu analipwa mamilioni...hiyo ni shauri yao! Hata muda wa kusomea degree ya udakatari na ile ya ualimu ni tofauti sana, na kuna sababu ya kufanya iwe tofauti. Daktari akidai anachodhani ni thamani yake, we usipodai ukakalia kubeza juhudi zaker, ni shauri yako!

3. Huo ni uongo wa mchana kweupee...mfano wa haraka haraka, wanaSheria kutumia utaalamu wao nje ya ofisi. wapo wanasheria wengi wa taasisi za kiserikali wanawakilisha watu binafsi mahakamani. Madaktari si fani pekee inayofanya hili.

4. Huo ni uongo dhahiri pia...narudia mfano wa wanaSheria ambao nao wanatumia utaalamu wao nje ya ofisi kutoa ushuri wa kisheria pamoja na huduma nyingine (mafano certification ya documents, mihuri etc). Na wanajitangaza, na consultation fee yao wanajipangia wenyewe..madaktari si fani pekee inayofanya hili.

5. Huo ni uongo wa kipuuzi kabisa...HESLB mwezi uliopita ilitoa list ya wadaiwa sugu...madaktari wapo kweny hiyo list (inapatikana online, itafute kwa faida yako). Mimi nalipa deni langu tangu mwaka 2009, na uthibitisho mwengine ni kuwa iliandikwa mpaka kwenye magazeti watoto wa rais JK nao ni wadaiwa sugu (Ridhiwani na Salama), Salama Kikwete ni daktari amesoma Muhimbili na anadaiwa. Kwa hiyo madaktari wanakopeshwa na wanalipa/wanapaswa walipe deni lao HESLB kama wadaiwa waliosoma fani nyingine.

Kama unataka kuweka hoja..tumia facts kufanya hoja yako iwe na mashiko, na sio kulazimisha ionekane na mashiko kwa kubandika uongo hapa!
Pamoja na mawazo yako bado haiingii akilini kuona daktari, yule ambaye kwa miaka mingi tulidhani ni wa kuaminiwa kutunza uhai wa binaadamu, leo hii anageuka kuwa mwanaharakati anyeweka rehani roho za wagonjwa ili kushinikiza apate marupurupu yake manono!
 
Mwanao anapokimbia masomo ya Kemia,Biolojia na Fizikia nawewe ukakenua meno unategemea daktari atatoka wapi?
Na km si walimu wako, kuanzia chekechea, shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu hawakujifunga kibwebwe kukujuza yaliyopaswa ufahamu huo udaktari ungeupataje....
 
Wapendwa madaktari, kesho mtadai waziri wa afya, Naibu wake na Katibu mkuu wawe na degree ya M.D. Ni hatari!!!! inawezekana waziri akawa na tatizo kidogo, lakini hatuendi hivyo. Mbona nyinyi mlipokosea magoti na kichwa hatukuwanyanganya vyeti? Fikiria tena jamani wapendwa
 
Ndugu acha upotoshaji wewe, sasa tumefikia wakati wa kuwajibishana tu ili nchi yetu isonge mbele, kama daktari, waziri, dc, rc nk anakosea lazima awajibishwe. Tukifanya hivi miaka 10 ijayo nchi yetu itasonga mbele hadi kuzipita nchi kama Thailand, Taiwan nk.
 
Uko sawa mkuu lakini madaktari wanadai hali bora katika sekta ya afya ila wamekamata kichwa cha Dr. Mponda na Dr. Nkya kama turufu yao; kwa maana hiyo ni kwamba Dr. Mponda na Dr. Nkya wakitoka hali katika sekta ya afya itakuwa nzuri?
 
Sawa kuwajibishana ni lazima inapobidi na ni hatua safi sana,sio kwa mtindo huu. kesho watadai mkuu wa majeshi, rais, waziri mkuu nk.......Yangu macho. Nawaunga mkono kwa madai ya hali bora ya kazi zao, mshahara, marupurupu, hili la sasa nina mashaka na uhalali wake. Sawa, waziri, naibu wake wana makosa???? tutumie vyombo vilivyopo eg bunge liwawajibishe kama Kikwete hataki, lakini mtindo wa kila kikundi kudai vyake sio utawala bora
 
Rais gani atakubali masharti ya aims hiyo? Leo madakitari wanaamrisha rais fukuza waziri anafukuza.kesho watasema fukuza waziri mkuu anafukuza, kesho kutwa itakuwa zamu ya rais kufukuzwa, uliona wapi Hali hiyo ikaleta maendeleo ya haraka? acheni ubabaishaji!
 
Uko sawa mkuu lakini madaktari wanadai hali bora katika sekta ya afya ila wamekamata kichwa cha Dr. Mponda na Dr. Nkya kama turufu yao; kwa maana hiyo ni kwamba Dr. Mponda na Dr. Nkya wakitoka hali katika sekta ya afya itakuwa nzuri?

Bila shaka sasa huu mgogoro umekuwa wa kisiasa..na unapaswa kutatuliwa kisiasa tena hasaa
 
Nayasema haya nikiwa na uchungu na masikitiko makubwa kwa hiki ambacho madaktari wanachoendelea kututendea waTanzania! kuna machache wacha niyaseme ili moyo wangu utulie!
1. kama sikosei mgomo wa madaktari wa mwaka 2004, madaktari walikua wanadai ongezeko la mishahara, ambapo kwa kipindi hicho mshahara wa daktari anayeanza kazi ulikua ni mkubwa zaidi ya mshahara wa mwalimu aliyemaliza madaraja yote ya ualimu (nikimaanisha mwalimu aliyeitumikia serikali zaidi ya miaka 35).
2. daktari anayeanza kazi sasa analipwa 950,000 wakati mwalimu mwenye 'degree' anayeanza kazi analipwa si zaidi ya 500,000.
3. tukumbuke katika kada za utumishi wa serikali ni madaktari pekee ndio wanaruhusiwa kutumia utaalamu wao nje ya ofisi zao mf. kufanya kazi ya kuajiriwa au kujiajiri katika ofisi tofauti (najua kunawatakao uliza kuhusu walimu kufundisha tuisheni na kufanya katika shule binafsi, lakini kiukweli ni kwamba walimu hao wanakiuka mkataba wa kazi wa mwajiri wao 'serikali').
4. tukumbuke pia madaktari ndio watumishi pekee walioruhusiwa kulipwa au kupewa chochote kutoka kwa mtu waliyemuhudumia kwa issue kama consultancy na isihesabike kama rushwa, ndio maana unakuta kuna kibao kimeandikwa KUMUONA DAKTARI NI TSH.****. wakati kwenye kada nyingine hilo ni jambo lenye utata na inahesabika moja kwa moja kama ni rushwa! (ushawahi kuona mwanafunzi kamuuliza swali mwalimu halafu mwalimu akadai pesa???)
5. Pia tusisahau kwamba madaktari 'Medical Doctors' ndio taaluma pekee ambayo wanaposoma katika chuo kama Muhimbili wanapewa ada na matumizi mengine for free lakini taaluma nyingine wanalipa hiyo mikopo pindi watakapoanza kazi!
mimi nadhani imefika kipindi madaktari wasifanye vitu kwa utashi wao na kusahau kuwa ni Mungu tu ndiye aliyewapa utaalamu huo na kuwawezesha wafike hapo! tumrudie Mwenye enzi ili atutakase katika hili! kugoma kwenu madaktari mnasababisha vifo vya watu ambao hawana hatia, watu ambao wanategemea vipawa vyenu mlivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu ili muwahudumie wagonjwa. hebu jaribuni kuangalia mnapotupeleka, hivi kweli katika hili Mungu atabariki kazi za mikono yenu???? KWELI KATIKA HILI MADAKTARI HAMTUTENDEI HAKI WATANZANIA!

Aliyeamua walimu walipwe 500,000 na madaktari 950,000 si ni serikali au unataka tuaminije. Serikali ndio inapanga mishahara sasa kama wao hawaioni hiyo tofauti unataka nani aseme. Hii nchi imeoza kila idara, inahitaji kufumuliwa vipande vipande tuanze upya.
 
MOB PSYCHOLOGY INAWAPONZA MADAKTARI WETU. HAWAJIJUI KUWA LABDA WANATUMIWA!! MOB PSYCHOLOGY NI MBAYA SANA HASA MNAPOKUTANA WATU WA TAALUMA ZINAZOELEKEANA KAMA MADOKTA, MAINJINIA N.K. MNAWEZA KUJIKUTA MAAMUZI YENU YAKO SAHIHI LAKINI KUMBE SIO SAHIHI KWA KUPOTOSHWA AU KWA KUWA HAKUNA WAKUWAPINGA. NASHAURI KILA DR. ATAFAKARI YEYE BINAFSI AMEGOMA KWA AJILI YA NINI? MPONDA NA NKYA? AU MASLAHI.

NA WATU WANAOWAUNGA MKONO HAWANA-UBINADAMU.

NA NAKUMBUSHIA TU:
The Declaration of Geneva, as currently amended, reads
At the time of being admitted as a member of the medical profession:
  • I solemnly pledge to consecrate my life to the service of humanity;
  • I will give to my teachers the respect and gratitude that is their due;
  • I will practice my profession with conscience and dignity;
  • The health of my patient will be my first consideration;
  • I will respect the secrets that are confided in me, even after the patient has died;
  • I will maintain by all the means in my power, the honor and the noble traditions of the medical profession;
  • My colleagues will be my sisters and brothers;
  • I will not permit considerations of age, disease or disability, creed, ethnic origin, gender, nationality, political affiliation, race, sexual orientation, social standing or any other factor to intervene between my duty and my patient;
  • I will maintain the utmost respect for human life;
  • I will not use my medical knowledge to violate human rights and civil liberties, even under threat;
  • I make these promises solemnly, freely and upon my honor.
 
Nasema MADAKTARI WA TANZANIA HAWAFAI na WAMEKAA KISIASA SIYO KITAALUMA. Kama wanataka Urais si wakaingie CHADEMA wagombee ili kuwawajibisha Waziri na Naibu wake!!!Hawafai...
 
pinda aliahidi kama kadanganya alitegemea na madaktari wadanganye?

huo ni upuuzi kuua watu wasio na hatia kwa sababu ya kubishana nani zaidi, wanakuwa kama hawajasoma bwana. Kama wako serious kweli wa-resign uone kama wata resign wote, sio kugoma. Ni mob psychology tu hiyo hawajitambui.
 
Wakuu ifikie wakati tuwe tunajadili mambo wa kuyaangalia vizuri,madaktari wana hoja ya msingi,hali katika sekta ya afya hairidhishi,ni dhahiri mabadiliko yanahitahika
Lakini,hebu tuangalie tena kama madokta leo hii hawatajadili lolote mpka mawaziri husika wawajibishwe,vp walimu nao wakaja na hitaji la viongozi wengine kuondolewa,mana tukumbuke zipo sekta nyingi na zinaweza opt hyo kama njia kama sahihi
Nadhani mgogoro huu upo ksiasa zaidi

Tafakari
 
Rais akimfukuza waziri kwa tatizo ili (inshu ya madaktari) huo utakuwa uwamuzi utakao leta madhala makubwa sana kwenye anga la serikali ya watanzania na watu wake.Utakuwa ugonjwa uliokosa dawa na kukuwa kwa haraka bila ya tiba uku ukiacha mamimia yakipukutika ndugi zangu lioneni hili kiundani na kiumakini sana.....

Ikiwa waziri mwenyewe kwa hiyari yake atajiuzulu hilo litakuwa somo la shujaa aliepambana mpaka tone lake la mwisho kwisha kuamua kubaki pembeni na kuwapisha wenye nguvu zaidi na wasio na majeraha kusonga mbele kwa hali yoyote itakayojitokeza kushinda au kushindwa bila lawama

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE INSHALLAH
 
Nasema MADAKTARI WA TANZANIA HAWAFAI na WAMEKAA KISIASA SIYO KITAALUMA. Kama wanataka Urais si wakaingie CHADEMA wagombee ili kuwawajibisha Waziri na Naibu wake!!!Hawafai...

KWELI NDUGU YANGU, JANA NILI POST THREAD HUMU KUHUSU MOB PSYCHOLOGY KUWA IME WA AFFECT MADAKTARI WETU, LAKINI NILIPINGWA VIKALI. hAWAJIJUI KUWA WANATUMIWA. HAWANA HURUMA KABISA HAWA MADAKTARI WETU. HAYA MAWAZIRI WATAJIUZURU IS OK!! JE MATATIZO YAO YATAISHA?? NA WATARUDISHA UHAI WA WALIO KUFA. KAMA WAKO SERIOUS WA-RESIGN ILA SIO KUGOMA.
 
rais akimfukuza waziri kwa tatizo ili (inshu ya madaktari) huo utakuwa uwamuzi utakao leta madhala makubwa sana kwenye anga la serikali ya watanzania na watu wake.utakuwa ugonjwa uliokosa dawa na kukuwa kwa haraka bila ya tiba uku ukiacha mamimia yakipukutika ndugi zangu lioneni hili kiundani na kiumakini sana.....

Ikiwa waziri mwenyewe kwa hiyari yake atajiuzulu hilo litakuwa somo la shujaa aliepambana mpaka tone lake la mwisho kwisha kuamua kubaki pembeni na kuwapisha wenye nguvu zaidi na wasio na majeraha kusonga mbele kwa hali yoyote itakayojitokeza kushinda au kushindwa bila lawama

mungu ibariki tanzania na watu wake inshallah

na tumesikia tazara wanataka waziri nundu awajibishwe, kesho utasikia walimu, kesho kutwa ......
 
Back
Top Bottom