Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
- Thread starter
- #61
Mkuu TM, thanks kwa background!.Pasco na wakuu wengine
Ni kweli jamaa...Abeli E. Ruanda, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro kajiuzulu. Ofcourse press conference kafanya leo, lakini ameandika barua tangu Agosti 21, 2012, kwa Katibu Mkuu.
Amepima joto la M4C, ameliotea kwa mbali, lakini kasikia 'makali' yake, ameamua kujisalimisha mapema mwenyewe. Mfano mdogo tu wa uzembe wa huyo bwana; majuzi amekaguliwa na timu ya advance, inayoongozwa na Mwita Waitara Mwikabe, ameshindwa kuonesha faili za ofisi yake, maana yake hana, hivyo hata kumbukumbu za ofisi hana au hatunzi kabisa.
Ameshagombana na watu wa fedha makao makuu na viongozi wa majimbo ya Morogoro Mashariki na Kusini Mashariki mara kadhaa kwa kukwamisha ruzuku isiende katika majimbo hayo.
Kwa sababu mbali ya kuwa Katibu wa Mkoa wa Morogoro, pia alikuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro Vijijini, yenye majimbo mawili...katika nafasi hiyo amekwamisha majimbo hayo yasifungue akaunti benki, hivyo hawapokei fedha za ruzuku kutoka makao makuu kama inavyotakiwa. Kazi za chama katika maeneo hayo zimevia kabisa na yeye yupo kama Mwenyekiti na kama katibu!
Chama kilikuwa kimedumaa, hata kama kulikuwa hakujafanyika operesheni serious kama ya sasa katika Mkoa wa Morogoro, bado uongozi wa mkoa unawajibika kuhakikisha mambo katika ngazi za chini yanakwenda na chama kinakuwa hai, hakufanya hivyo katika nafasi yake.
Hatoi taarifa kwa ngazi za chini zinazotoka makao makuu, mara kadhaa amewa-misinform au kuwa wa-mislead for the interests best known to him. Wanachama wengi wanalalamika na kudai kuwa amekuwa aki-block ukuaji na ueneaji wa chama mkoani hapa katika nafasi yake kama mtendaji mkuu mkoani.
Mtu ambaye anaweza kukaguliwa na asiwe na nyaraka au taarifa zozote za chama zilizokuwa filed ni vigumu sana kuamini kuwa mko naye katika safari moja na anajua kweli anachotakiwa kukifanya. Kwa joto lililoko katika operesheni hii amepima mwenyewe...lakini pia kwa kasi ambayo CHADEMA inahitaji viongozi wake waende nayo katika kutimiza principle ya 'supply and demand', katika kuwatumikia watu na kukidhi matumaini makubwa waliyonayo katika mapambano haya, amepima mwenyewe na kuona maji ni marefu mno kwake.
Bila shaka atakuwa amesaidia vyombo vya maamuzi katika kuchukua hatua. Hakuna mwanachama makini angeweza kuvumilia uzembe wa kiuongozi kama wa Ruanda.
Nakumbuka wakati wa ziara ya kutembelea mikoa mitano mwezi Aprili, Katibu Mkuu, Dkt. Slaa alikuwa akisema mara kadhaa, uzembe wa aina yoyote hautavumiliwa, wala mtu yeyote ambaye anaona hawezi kuendana na kasi inayotakiwa kuwatumikia watu ajipime haraka...huyo ni miongoni mwa walioamua kujipima haraka na kuona hawawezi.
Kuna mahali Pasco umeandika ukweli ambao tayari hapa Morogoro unajulikana vyema na kila mtu makini anayetakia heri mapambano haya. Asisingizie M4C, malengo yanajulikana wazi. Hakuna siri katika hilo.