Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro Aachia Ngazi and Soon to Defect to ....

Of coz dirisha la usajili linafungwa mwisho wa mwezi huu, so achangamkie ulaji wa magamba asaini kule.

Lazima ktk safari hii ndefu na ngumu pawepo na wasaliti na wenye kugeuka nyuma (kutoka ngazi na kada mbalimbali).

Asante kwa taarifa, if confirmed anyway
 
Wanabodi,

Hii nimeipata ikiwa bado ya moto, na mimi nimeileta hivyo hivyo ikiwa bado inachemka, ili JF iwe the first to break this news!.

Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, ameachia ngazi!.

Katibu huyo, (jina litafuatia), ameachia ngazi rasmi kwa kuitisha press conference iliyomalizika soon mjini Morogoro!.

Katibu huyo ametoa sababu kuu za kuachia ngazi, ni sintofahamu kati yake na Mwenyekiti wake, Mhe. Susan Kiwanga kuhusiana na lengo la M4C!.

Kwa mujibu wa mtoa habari wangu, Katibu huyo ameanza rasmi ubomoaji wa Chadema kwa aliyoyazungumza
na nimeona sii bora kusema alichosema, bali nitawawekea hapa soon!.

MY Take.
Huyu jamaa anaweza kuwa anatumiwa, na naombeni mvute kidogo tuu subira, very soon ata defect kuelekea rasmi kule kwa walio mtuma!.

Pasco.

Pasco na wakuu wengine

Ni kweli jamaa...Abeli E. Ruanda, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro kajiuzulu. Ofcourse press conference kafanya leo, lakini ameandika barua tangu Agosti 21, 2012, kwa Katibu Mkuu.

Amepima joto la M4C, ameliotea kwa mbali, lakini kasikia 'makali' yake, ameamua kujisalimisha mapema mwenyewe. Mfano mdogo tu wa uzembe wa huyo bwana; majuzi amekaguliwa na timu ya advance, inayoongozwa na Mwita Waitara Mwikabe, ameshindwa kuonesha faili za ofisi yake, maana yake hana, hivyo hata kumbukumbu za ofisi hana au hatunzi kabisa.

Ameshagombana na watu wa fedha makao makuu na viongozi wa majimbo ya Morogoro Mashariki na Kusini Mashariki mara kadhaa kwa kukwamisha ruzuku isiende katika majimbo hayo.

Kwa sababu mbali ya kuwa Katibu wa Mkoa wa Morogoro, pia alikuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro Vijijini, yenye majimbo mawili...katika nafasi hiyo amekwamisha majimbo hayo yasifungue akaunti benki, hivyo hawapokei fedha za ruzuku kutoka makao makuu kama inavyotakiwa. Kazi za chama katika maeneo hayo zimevia kabisa na yeye yupo kama Mwenyekiti na kama katibu!

Chama kilikuwa kimedumaa, hata kama kulikuwa hakujafanyika operesheni serious kama ya sasa katika Mkoa wa Morogoro, bado uongozi wa mkoa unawajibika kuhakikisha mambo katika ngazi za chini yanakwenda na chama kinakuwa hai, hakufanya hivyo katika nafasi yake.

Hatoi taarifa kwa ngazi za chini zinazotoka makao makuu, mara kadhaa amewa-misinform au kuwa wa-mislead for the interests best known to him. Wanachama wengi wanalalamika na kudai kuwa amekuwa aki-block ukuaji na ueneaji wa chama mkoani hapa katika nafasi yake kama mtendaji mkuu mkoani.

Mtu ambaye anaweza kukaguliwa na asiwe na nyaraka au taarifa zozote za chama zilizokuwa filed ni vigumu sana kuamini kuwa mko naye katika safari moja na anajua kweli anachotakiwa kukifanya. Kwa joto lililoko katika operesheni hii amepima mwenyewe...lakini pia kwa kasi ambayo CHADEMA inahitaji viongozi wake waende nayo katika kutimiza principle ya 'supply and demand', katika kuwatumikia watu na kukidhi matumaini makubwa waliyonayo katika mapambano haya, amepima mwenyewe na kuona maji ni marefu mno kwake.

Bila shaka atakuwa amesaidia vyombo vya maamuzi katika kuchukua hatua. Hakuna mwanachama makini angeweza kuvumilia uzembe wa kiuongozi kama wa Ruanda.

Nakumbuka wakati wa ziara ya kutembelea mikoa mitano mwezi Aprili, Katibu Mkuu, Dkt. Slaa alikuwa akisema mara kadhaa, uzembe wa aina yoyote hautavumiliwa, wala mtu yeyote ambaye anaona hawezi kuendana na kasi inayotakiwa kuwatumikia watu ajipime haraka...huyo ni miongoni mwa walioamua kujipima haraka na kuona hawawezi.

Kuna mahali Pasco umeandika ukweli ambao tayari hapa Morogoro unajulikana vyema na kila mtu makini anayetakia heri mapambano haya. Asisingizie M4C, malengo yanajulikana wazi. Hakuna siri katika hilo.
 
Wale wanaorudi nyuma hawakuaga warudi wakaage tutakutana kwenye majumuisho. Huyo ni wa Nape hatufai tena
 
Wanabodi,

Hii nimeipata ikiwa bado ya moto, na mimi nimeileta hivyo hivyo ikiwa bado inachemka, ili JF iwe the first to break this news!.

Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, ameachia ngazi!.

Katibu huyo, (jina litafuatia), ameachia ngazi rasmi kwa kuitisha press conference iliyomalizika soon mjini Morogoro!.

Katibu huyo ametoa sababu kuu za kuachia ngazi, ni sintofahamu kati yake na Mwenyekiti wake, Mhe. Susan Kiwanga kuhusiana na lengo la M4C!.

Kwa mujibu wa mtoa habari wangu, Katibu huyo ameanza rasmi ubomoaji wa Chadema kwa aliyoyazungumza
na nimeona sii bora kusema alichosema, bali nitawawekea hapa soon!.

MY Take.
Huyu jamaa anaweza kuwa anatumiwa, na naombeni mvute kidogo tuu subira, very soon ata defect kuelekea rasmi kule kwa walio mtuma!.

Pasco.

Hapo ndo huwa nashindwa kukuelewa Pasco, Unajichanganya mno sometimes
 
CDM tunahitaji wachapa kazi,wapiganaji n.k,nina shaka na uwezo wake wa kuongoza CDM Moro,nafasi yake itazibwa haraka na makamanda wengine wenye umahiri wa kuwatumikia wananchi,M4C inasonga mbele,
 
Lilikuwa linafikiri litapata hela za kukodi mafuso ili libebe watu kwenda kwenye Mikutano kumbe CDM watu huwa wanaenda peke yao kakosa pakuiba arudi kwa mafisadi wenzake apate hela za kuhonga watu wa kwenda kwenye mikutano Nyambaf
 
Pasco na wakuu wengine

Ni kweli jamaa...Abeli E. Ruanda, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro kajiuzulu. Ofcourse press conference kafanya leo, lakini ameandika barua tangu Agosti 21, 2012, kwa Katibu Mkuu.

Kuna mahali Pasco umeandika ukweli ambao tayari hapa Morogoro unajulikana vyema na kila mtu makini anayetakia heri mapambano haya. Asisingizie M4C, malengo yanajulikana wazi. Hakuna siri katika hilo.

Asante kwa kujibu na kufafanua hili mapema kabla upotoshaji haujaendelea. Lakini nina shaka na hapo kwenye RED kama ni sahihi ama kuna typing error
 
Abeli E. Ruanda, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro kajiuzulu. aliandika barua tangu Agosti 21, 2012, kwa Katibu Mkuu.

Amepima joto la M4C, ameliotea kwa mbali, lakini kasikia 'makali' yake,
Mfano hana mafaili ya chama wala offisi Morogoro
Amehodhi madaraka kwa kupenda ruzuku, Katibu wa Mkoa wa Morogoro, pia Mwenyekiti wa Wilaya ya Morogoro Vijijini, yenye majimbo mawili
Katika nafasi hiyo amekwamisha majimbo hayo yasifungue akaunti benki, hivyo hawapokeoi fedha za ruzuku kutoka makao makuu kama inavyotakiwa.

Chama kilikuwa kimedumaa
Hakujafanyika operesheni serious kama ya sasa katika Mkoa wa Morogoro,
Hakufanya mikutano kikatiba
Hakuunda miundo mbinu ya chama
Hakuwa na office
Bado uongozi wa mkoa unawajibika kuhakikisha mambo katika ngazi za chini yanakwenda na chama kinakuwa hai, hana hata tawi moja alilofungua acha kata.

Ruzuku
Kama alikuwa anapoke ruzuku sasa atoe ripoti ya matumizi.

Wanachama wengi wanalalamika na kudai kuwa amekuwa aki-block ukuaji na ueneaji wa chama mkoani hapa katika nafasi yake kama mtendaji mkuu mkoani.

Asisingizie M4C, malengo yanajulikana wazi. Hakuna siri katika hilo.

Kwa ujumla hafai uongozi wowote, hata wa mtaa.​
 
Nipo morogoro hoja yake kubwa anasema amejiona anatumikia chama ambacho kinaendeshwa kikabila zaidi,pia wale ambao wa kabila hilo na waliopo na kabila hilo wanasikilizwa zaidi,amebanwa na mwandishi ataje hilo kabila amesema wandishi wajue tu chadema ipo kikabila zaidi na amewalaumu wandishi wa habari kufumbia macho ukabila wa chadema,anaonekana ana wasi wasi sana!


Yani mtu amekuwa katibu wa mkoa kwa muda wote huo sasa leo ndio anauona ukabila ndani ya Chadema?
Amekosa kabisa cha kuongea kwani kutaja ukabila ni yeye mwenyewe kujidhalilisha. Mimi namshukuru kwa yeye mwenyewe kuamua kuachia ngazi kwani ametambua kwamba huko tuendako asingehimili vishindo, na kung'olewa katika nafasi hiyo ya katibu wa mkoa lilikuwa ni jambo la kusubiri wakati tu.
 
Back
Top Bottom