Mungu awe na wanainchi wote hapo tanzania swala la katiba likileta mgogoro.Kwa vile kuna kundi la watu ambao wanaamini kabisa kuwa hakuna mtu mwingine yoyote (ndani ya CCM au nje yake) ambaye anaweza kuliongoza Taifa letu na kuwa Tanzania bila ngwe ya pili ya Kikwete haiwezekani basi CCM na mashabiki wa utawala bora wa Kikwete waamue kubadilisha Katiba ili waondoe vikomo vya utawala na ikiwezekana wapitishe uamuzi wa kumtangaza Rais Kikwete kama Rais wa Maisha wa Tanzania.
Kwa kufanya hivi angalau tutajua tugombee mambo ya ubunge tu kwani Urais tayari una mwenyewe!