Katiba ibadilishwe? Kikwete awe Rais wa Maisha!

Kwa vile kuna kundi la watu ambao wanaamini kabisa kuwa hakuna mtu mwingine yoyote (ndani ya CCM au nje yake) ambaye anaweza kuliongoza Taifa letu na kuwa Tanzania bila ngwe ya pili ya Kikwete haiwezekani basi CCM na mashabiki wa utawala bora wa Kikwete waamue kubadilisha Katiba ili waondoe vikomo vya utawala na ikiwezekana wapitishe uamuzi wa kumtangaza Rais Kikwete kama Rais wa Maisha wa Tanzania.

Kwa kufanya hivi angalau tutajua tugombee mambo ya ubunge tu kwani Urais tayari una mwenyewe!
Mungu awe na wanainchi wote hapo tanzania swala la katiba likileta mgogoro.
 
kwa hali jinsi ilivyo sioni ni fahari kujiita mtanzania kama kuna watu ndio wenye tanzania
 
Katiba haitabadilishwa lakini JK atagombewa mara ya pili kama katiba inavyotaka period!

Katiba inakuruhusu wewe na kundi lako kuchukua form nakugombea ikiwa mnaamini kwamba JK ameshindwa na kuna chochote cha kuwafanyia wa Tanzania cha ziada Ok

Kikundi kinachoamini kwamba kikwete anafaa hakijasema kinataka kuvunja katiba iliyopo..wewe unataka kuwafundisha wavunje katiba kwa sababu za hisia zako shame on you..chukua form tukuone jukwaani...otherwise acha blah blah za kupotosha watu!

hafundishiwi mtu hapa kuvunja katiba, kichaoongelewa ni kwamba kama tunaona JK ni kiongozi bora na hakuna mrithi wake kwa sasa na ukizingatia makundi ya kijamii yanamkubali basi tu-edit katiba yetu tumfanye awe wa maisha, hakuna haja ya kuwa na michakato ya uchaguzi isiyoleta mabadiliko yoyote ili tuwe na taifa lenye mshikamano na umoja wa dhati. sisi wengine tukangombanie ubunge maana uraisi tayari utakuwa na mwenyewe.

Sasa we kitu gani kinakusumbua unakuwa mkali? au unauelewa udhaifu wa rais wako?
 
Ndio maana nimependekeza wamtangaze tu kuwa ni Rais wa maisha na hivyo itazima mjadala mzima wa nani agombee nani asigombee kwa miaka mingi ijayo. Wamarekani wanasema "if it ain't broke, don't fix it". Kwa vile wapo watu wanaoamini kuwa JK anafanya kazi nzuri kweli (it ain't broke) basi hakuna haja ya kumbadilisha (don't fix it).

Mimi nina maswali machache kwa Rais Kikwete mwenyewe juu ya wanaosema amefanya kazi nzuri,,je wewe mwenyewe mbona sikusikii ukiongelea kazi yako..??? je unadhani kwa dhati kabisa umefanya kazi nzuri kwa miaka hii mi4?? Na je unasemaje juu ya marais waliokutangulia je kuna ambaye hakufanya kazi nzuri??? Je wewe watanzania wakukumbuke kwa lipi jema ambalo hawawezi kubishana juu ya hilo? mfano Nyerere(Umoja wetu), Mwinyi( Ruksa), Mkapa( Uwanja wa Taifa)... je wewe?kuna lipi tukutaje kwa hilo au tukupe miaka mingine mitano ujifikirie...na je CCM wakukumbuke kwa lipi wewe? na makundi mbalimbali ya kisiasa na kidini wakukumbukeje?(Naomba jibu lako lisiwe Taifa Stars... utakasirisha waliotabasamu....maana sote tunajua jinsi walivyo wepesi wa kutangaza viingilio na sababu za kushindwa.....)..au bado miaka mitano? Naomba majibu mheshimiwa maana nataka kufanya maamuzi sahihi kama mpiga kura.
 
Wewe Mwanakijiji ushaambiwa atakayegombea Urais kumpinga Kikwete atakufa! hiyo ina maanisha nini kwako? Huo tayari ni mwanzo wa kumfanya Kikwete kuwa Rais wa maisha. Na Ikulu yenyewe imeunga mkono. Kwa hiyo usifikirie kugombea Urais, bado tunakuhitaji, usije ukatolewa kafara bure, si umesikia Gama katolewa kafara? Wakubwa tubanane tu kwenye ubunge, maana habari ya kwenda kufa huko na kuacha familia zetu, mmh hapo hapalipi
Kinachonishngaza hata watu wanaoishi nje ya nchi ambao hawajui tunapiga maendeleo kiasi gani wanaona kikwete hafai.haya ni kichekesho au mna agenda ya kutuletea kibaraka.
 
Kinachonishngaza hata watu wanaoishi nje ya nchi ambao hawajui tunapiga maendeleo kiasi gani wanaona kikwete hafai.haya ni kichekesho au mna agenda ya kutuletea kibaraka.

....maendeleo? hebu tutajie baadhi tu uliyoyapata.... na pili kila mwananchi wa nchi hii ana haki ya kutoa maoni yake, hayo ya kuleta vibaraka ni ya kwako.
 
Jamani MMM una nini na Kikwte? hawezi kuwa Raisi wa kudumu kwasababu Nchi yetu ni ya demokrasia ila tunampa vipindi 2 then tutampitisha mwingine, ikiwezekana wewe.
 
Jamani MMM una nini na Kikwte? hawezi kuwa Raisi wa kudumu kwasababu Nchi yetu ni ya demokrasia ila tunampa vipindi 2 then tutampitisha mwingine, ikiwezekana wewe.

Ni Lazima? Ni Kwanini?
 
Kweli kuna kazi sana maana kila mtu anajitahidi kulinda maslahi yake mwenyewe na pia kama kweli yeye bado ni chaguo la Mungu basi inapaswa washindanishwe na machaguo ya shetani maana ndio ulikuwa mwimbo wa taifa kipindi kile mzee wangu
 
Mwanakijiji unazeeka vibaya.
HAkuna kuwabembeleza wala nini hapa ni kupiga elimu jamii mpaka watu wafunguke akili na kufanya uamuzi sahihi.
Msiogope vitisho maana kama mbegu haifi haiwezi kuota
 
Jamani MMM una nini na Kikwte? hawezi kuwa Raisi wa kudumu kwasababu Nchi yetu ni ya demokrasia ila tunampa vipindi 2 then tutampitisha mwingine, ikiwezekana wewe.

kama anafanya vizuri na hakuna mtu mwingine wa kumrithi kwanini tumbadilishe. Demokrasia ni pamoja na kumpa mtu mwenye uwezo kuongoza haya mambo ya vikomo vya uongozi yamepitwa na wakati, mbona wabunge hawajawekewa vikomo?
 
Mzozo mwingi umezuka kwa wenzetu wa Tanzania Zanzibar wakidai kuvunja katiba ili Rais alioko madarakani aendelee kuwaoongoza.Haiwezekani kuvunja katiba kwa sababu ya interest za wachache na kwa gafla kias hicho tafikiria kwamba watanzania hawafikiri.Swala nikwamba wanapaswa kujipanga nakujiwekea mikakati na malengo ya kuishi kwa amani.Mamlaka ya kuishi kwa amani zanzibar yamo mikononi mwa wazanzibar wenyewe na siyo mwingine.
 
Makuzi ya akili za watu yameambatana na mazoea, hali inayokwamisha maendeleo na ukosefu wa amani ndani ya nchi kwa maana muda wote watu hawa, hawawezi kujiamini bila kuona kile walichokizoea.
 
Katiba haitabadilishwa lakini JK atagombewa mara ya pili kama katiba inavyotaka period!

Katiba inakuruhusu wewe na kundi lako kuchukua form nakugombea ikiwa mnaamini kwamba JK ameshindwa na kuna chochote cha kuwafanyia wa Tanzania cha ziada Ok

Kikundi kinachoamini kwamba kikwete anafaa hakijasema kinataka kuvunja katiba iliyopo..wewe unataka kuwafundisha wavunje katiba kwa sababu za hisia zako shame on you..chukua form tukuone jukwaani...otherwise acha blah blah za kupotosha watu!

Wewe Tumaini umeonyesha kabisa jinsi upeo wako wa kufikiri na kuchambua mabo ulivyo mdogo ndio maana hujaelewa kabisa nini Mwanakijiji anachojaribu kukiwakilisha. Kwa mchango wako finyu kiasi hichi hustahili hata kuwa member wa Jamii Forum, nenda kwenye udaku ukawajadili bongo flavour na wakina Kanumba.
 
ila tusijekushangaa baadaye wapinzani na wapigadebe wa ccm wakapitisha hili na likakubalika kwa nguvu zote
 
Ninahisi Mwanakijiji anamaanisha kuwa, kila kukicha wana zidi kutokea watu ambao wanataka kutuaminisha kuwa hakuna Rais bora kama Kikwete, na haswa kipindi hiki tunapoelekea kwa uchaguzi. Hata Makamba alisema Kikwete ndio mtaji wa CCM (REDET study). Na wengine wamehongwa ili watutishe kuwa atakayejitokeza kupingana na Kikwete 2010 basi atakufa ghafla.

Kama ni hivyo, na kama wote tunajiaminisha Kwelikweli kuwa this guy ni chaguo la Mungu, maana huwezi kuwa na sifa hizi zote afu ukaishia kwa vipindi viwili tu, Basi ndio maana Mwanakijiji anasema, tumpe Ruhusa (tubadili katiba) atuongoze maisha.

Vinginevyo kama kuna watu mbadala na tunajua wapo (what if this man dies - Mungu apishe mbali), tunawahitaji wajitokeze! Ili hizi blah blah za vibaraka hawa uchwara ziishe. Nchi inaongozwa kidemokrasia bwana, na hata kama sisi hatutaki, the wind of change itatuswaga na kutulazimishe tuelekee huko.

That is indirect kick to awake some slumbers, you know what? people will never realise that Jk is bad neither that they will confess this!

I guess this was awakening call for slumbers, awakening call for dormant opposition parties who they have unclear focus and dead strategies!
 
,
Na wewe tumechoka na ujinga wako sasa.
kama unaona vipi seti mambo mengine kwenye mtandao, rudi bongo na ingia kwenye siasa.

umekuwa mzushi sana bro na wivu kibao.

punguza domo.

This is one of so called great thinker in this society!

umechoka kwa ujinga? muelimishe basi
kwani wote walioko bongo wanasiasa?
kazusha nini -kanusha basi
wivu? amuonee nani wivu JK? yaani status ya MKJJ anaheshima zaidi kuliko JK.

Personally, hata unipe fedha za bajeti ya Tanzania na uniambie nibadili jina niitwe Jakaya Kikwete sitaki ng'o I would rather die! Kikwete kwangu ni mjerumani na mimi ni mkwawa!

Mkuu una matatizo because your post was unproductive ans useless, here we talk and discuss ideas not people!! tatizo la kuwa inferior hilo.

kwa mfano leo nikisema wewe mpumbavu, usikasirike ila inabidi unijibu kwa hoja kwa nini wewe sio mpumbavu! mfano tu, ila unaweza ukaanzia hapa kujibu hoja!!
 
Back
Top Bottom