Katiba ibadilishwe? Kikwete awe Rais wa Maisha!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Kwa vile kuna kundi la watu ambao wanaamini kabisa kuwa hakuna mtu mwingine yoyote (ndani ya CCM au nje yake) ambaye anaweza kuliongoza Taifa letu na kuwa Tanzania bila ngwe ya pili ya Kikwete haiwezekani basi CCM na mashabiki wa utawala bora wa Kikwete waamue kubadilisha Katiba ili waondoe vikomo vya utawala na ikiwezekana wapitishe uamuzi wa kumtangaza Rais Kikwete kama Rais wa Maisha wa Tanzania.

Kwa kufanya hivi angalau tutajua tugombee mambo ya ubunge tu kwani Urais tayari una mwenyewe!
 
Wewe Mwanakijiji ushaambiwa atakayegombea Urais kumpinga Kikwete atakufa! hiyo ina maanisha nini kwako? Huo tayari ni mwanzo wa kumfanya Kikwete kuwa Rais wa maisha. Na Ikulu yenyewe imeunga mkono. Kwa hiyo usifikirie kugombea Urais, bado tunakuhitaji, usije ukatolewa kafara bure, si umesikia Gama katolewa kafara? Wakubwa tubanane tu kwenye ubunge, maana habari ya kwenda kufa huko na kuacha familia zetu, mmh hapo hapalipi
 
Ndio maana nimependekeza wamtangaze tu kuwa ni Rais wa maisha na hivyo itazima mjadala mzima wa nani agombee nani asigombee kwa miaka mingi ijayo. Wamarekani wanasema "if it ain't broke, don't fix it". Kwa vile wapo watu wanaoamini kuwa JK anafanya kazi nzuri kweli (it ain't broke) basi hakuna haja ya kumbadilisha (don't fix it).
 
Wakubwa tubanane tu kwenye ubunge, maana habari ya kwenda kufa huko na kuacha familia zetu, mmh hapo hapalipi
Unaona sasa kumbe ubunge wenyewe kwa ajili ya familia yako na si wajimbo lako. Acheni uoga baadhi lazima wafe kwenye hii course ya mabadiliko itawasaidi wanao baadae.
 
Ikitokea hivyo, tutarudi kule kule kwenye kutafuta kupinduana. Maana nina amini, utaratibu huu wa kikatiba unasaidia kuendeleza amani kwa kiasi fulani. Nani asietaka kuwa kiongozi wa nchi siku moja?

Dunia ya sasa hakuna mtu anaeweza kusema yeye ni bora kuliko wengine wote. Infact, siwezi kusema natamani serikali hii iendelee kwa muda mrefu zaidi.

Msinifanye nihame nchi na kutafuta uraia wa nchi nyingine, jamani.
 
Kwa vile kuna kundi la watu ambao wanaamini kabisa kuwa hakuna mtu mwingine yoyote (ndani ya CCM au nje yake) ambaye anaweza kuliongoza Taifa letu na kuwa Tanzania bila ngwe ya pili ya Kikwete haiwezekani basi CCM na mashabiki wa utawala bora wa Kikwete waamue kubadilisha Katiba ili waondoe vikomo vya utawala na ikiwezekana wapitishe uamuzi wa kumtangaza Rais Kikwete kama Rais wa Maisha wa Tanzania.

Kwa kufanya hivi angalau tutajua tugombee mambo ya ubunge tu kwani Urais tayari una mwenyewe!
MMK umeniacha hapa aisee,sijakuelewa ati..Kwani JK si katiba inamruhusu kugombea kwa awamu nyingine???,kama ilivyokuwa kwa Mkapa na Mwinyi?..Naomba uniweke sawa hapa mkuu wangu
 
MMK umeniacha hapa aisee,sijakuelewa ati..Kwani JK si katiba inamruhusu kugombea kwa awamu nyingine???,kama ilivyokuwa kwa Mkapa na Mwinyi?..Naomba uniweke sawa hapa mkuu wangu

bila ya shaka; kwa mfumo wa sasa Kikwete atagombea awamu moja tu halafu basi; ina maana miaka mitano ijayo tutatakiwa kumchagua mtu mwingine. Lakini hadi hivi sasa kuna watu ndani ya CCM na nje ya CCM (kama REDET) ambao wanaamini kuwa Rais Kikwete ni zawadi ya Mungu kwa Tanzania na kuwa uongozi wake bora hauna mfano.

Hawa wanataka tuamini kabisa kuwa bila ya Kikwete nchi haiwezi kuongozwa na kuwa ni Kikwete ndiye kiongozi wetu bora na anayetufaa. Kama hoja yao hii ni kweli na wao ndio wanachama tawala na kama nikweli asilimia 70 hufuata mkumbo tu basi kwanini tugombanie kitu ambacho tayari yupo mtu?

Sasa, wakibadili Katiba na kuondoa kikomo cha awamu (term limits) Rais Kikwete ataweza kugombea tena 2015 na 2020. Lakini kwa vile tayari tunajua kwa maoni yao ndiye kiongozi bora basi hakuna hata haja ya kumpambanisha na watu wengine. Ni bora kumtangaza tu kuwa atakuwa ni Rais wa Maisha (wa kudumu) hadi pale atakapoamua kuchoka mwenyewe au tendo la Mungu liingilie kati.

Ukifikiria sana utaona kuwa pendekezo hili lina faida kubwa sana kwa utawala wa demokrasia, kwani litaendelea umoja, udugu, mshikamano na mustakabali bora kabisa wa taifa letu.
 
Ikitokea hivyo, tutarudi kule kule kwenye kutafuta kupinduana. Maana nina amini, utaratibu huu wa kikatiba unasaidia kuendeleza amani kwa kiasi fulani. Nani asietaka kuwa kiongozi wa nchi siku moja?

Dunia ya sasa hakuna mtu anaeweza kusema yeye ni bora kuliko wengine wote. Infact, siwezi kusema natamani serikali hii iendelee kwa muda mrefu zaidi.

Msinifanye nihame nchi na kutafuta uraia wa nchi nyingine, jamani.
The moment upuuzi huo wa mtu kujifanya hii nchi ni mali yake utakapowadia, basi ajiandae kwa laana zitakazo muandama. Watu watakataa huo upuuzi na tutamtengeneza shetani ambaye tutaona haya maisha yetu yote kumtazama usoni kwa jinsi ubaya wa uso wake ulivyo.Yes, tunaweza kabisa kuwandaa watu mfano wa kina Kapteni Moussa Dadis Camara
 
Kwa vile kuna kundi la watu ambao wanaamini kabisa kuwa hakuna mtu mwingine yoyote (ndani ya CCM au nje yake) ambaye anaweza kuliongoza Taifa letu na kuwa Tanzania bila ngwe ya pili ya Kikwete haiwezekani basi CCM na mashabiki wa utawala bora wa Kikwete waamue kubadilisha Katiba ili waondoe vikomo vya utawala na ikiwezekana wapitishe uamuzi wa kumtangaza Rais Kikwete kama Rais wa Maisha wa Tanzania.

Kwa kufanya hivi angalau tutajua tugombee mambo ya ubunge tu kwani Urais tayari una mwenyewe!
Katiba haitabadilishwa lakini JK atagombewa mara ya pili kama katiba inavyotaka period!

Katiba inakuruhusu wewe na kundi lako kuchukua form nakugombea ikiwa mnaamini kwamba JK ameshindwa na kuna chochote cha kuwafanyia wa Tanzania cha ziada Ok

Kikundi kinachoamini kwamba kikwete anafaa hakijasema kinataka kuvunja katiba iliyopo..wewe unataka kuwafundisha wavunje katiba kwa sababu za hisia zako shame on you..chukua form tukuone jukwaani...otherwise acha blah blah za kupotosha watu!
 
Hao wanaomtaka Kikwete inabidi watengeneze katiba yao na kijiji chao, halafu wampambe Kikwete kuwa Raisi (Mwenyekiti) wao wa maisha.
 
Sasa, wakibadili Katiba na kuondoa kikomo cha awamu (term limits) Rais Kikwete ataweza kugombea tena 2015 na 2020. Lakini kwa vile tayari tunajua kwa maoni yao ndiye kiongozi bora basi hakuna hata haja ya kumpambanisha na watu wengine. Ni bora kumtangaza tu kuwa atakuwa ni Rais wa Maisha (wa kudumu) hadi pale atakapoamua kuchoka mwenyewe au tendo la Mungu liingilie kati.
Cynically, naunga mkono hilo juu. Kwasababu zifuatazo:

  • Kuwepo kwa Rais wa Maisha kutapunguza gharama Kitaifa za mara kwa mara zitokanazo na heka heka za uchaguzi kila baada ya miaka mitano.
    -
  • Kutapunguza harakati mbalimbali za kifisadi kuibia Taasisi za umma ili kugharamia ushindi wa wabunge (kama vile tulivyoshuhudia wizi wa EPA BoT). Maana uwezekano wa wabunge wa kuteuliwa na viongozi wengi kubakia katika madaraka yao bila kubadilishwa utakuwa mkubwa. Pia uwezekano wa nafasi mbalimbali za uteuzi wa viongozi zinazofanywa na Mh. Rais kuongoza taasisi bila shaka zitakuwa za muda mrefu kulingana na njinsi anavyopatana nao. Na hii kwa namna moja au nyingine, itapunguza gharama za michakato itokanalo na hilo.
    -
  • Malipo ya ruzuku kwa viongozi wastaafu kama Mawaziri wakuu na hata Rais mwenyewe zitapungua, na hivyo kulipunguzia taifa gharama kwani kila mabadiliko ya viongozi yanapotokea wanaostaaf wanakuwa guaranteed malipo yao. And the likelihood ya viongozi wa kitaifa kubadilishwa badilishwa wakati Rais ni yuleyule huwa ni kidogo.
    -
  • Kuna uwezekano mkubwa kwamba kuwepo kwa Rais wa maisha kunaweza kabisa kupunguza haraka haraka za viongozi wetu hawa kutaka kujitajirisha wakiwa madarakani (kama tunavyoshuhudia pengi hapa Afrika yetu) katika kipindi kifupi wanachopewa. Kwani wanapoteza dira na umakini wa kuwa viongozi safi kutokana na wasiwasi wa kushindwa chaguzi zifuatazo na hivyo kupoteza madaraka. Wana lose focus ya maendeleo na hata mipango ya maendeleo ya muda mrefu inakuwa finyu, maana kilakitu wanakuwa wanafikiria kwa minajiri ya ngwee za madaraka yao.
    -
  • Kuwepo kwa Rais wa maisha kutaweza kabisa kupunguza manung'uniko ya mara kwa mara ya wapinzani na wananchi kwa ujumla. Jambo ambalo linakula resources nyingi sana kufatilia, kuliongelea n.k. katika majukwaa ya siasa na maofisini. In return, hii itaweza kuwafanya Watanzania wapunguze malumbano na kuweka concentration katika kutekeleza mambo mbalimbali. Kwani minong'ono ya alternative ya Rais inakuwa imefyekelewa mbali, na hivyo ku-save time kwakuwa na less evil to talk about.

Kwa kweli ni mengi ambayo yanaweza kuwa ni mambo chanya katika jamii ya Kitanzania kwa kuwa na Rais wa maisha. Hata hivyo nitaishia hapa, ngoja niongelee hapa chini moja ya negative attributes za kuwa na Rais wa maisha:

Ukifikiria sana utaona kuwa pendekezo hili lina faida kubwa sana kwa utawala wa demokrasia, kwani litaendelea umoja, udugu, mshikamano na mustakabali bora kabisa wa taifa letu.
--- Linaweza kuendeleza undugu badala ya udugu.

--- Litaweza kuleta ruling class (kama vile haipo), kwani viongozi watabakia madarakani muda mrefu na kwa vile jamii yetu ni ya kujali waliokaribu, tutajikuta matabaka katika jamii ya walionacho na wasio yanakua zaidi ya ilivyo sasa.

---KUPINDUANA kutakuja kama hakupo au hakujawahi kuwepo. Kwani hivyo ndivyo viongozi wa maisha wanavyobadilishwa!! Je, Tuko tayari na hili?!

SteveD.
 
Katiba haitabadilishwa lakini JK atagombewa mara ya pili kama katiba inavyotaka period!

Katiba inakuruhusu wewe na kundi lako kuchukua form nakugombea ikiwa mnaamini kwamba JK ameshindwa na kuna chochote cha kuwafanyia wa Tanzania cha ziada Ok

Kikundi kinachoamini kwamba kikwete anafaa hakijasema kinataka kuvunja katiba iliyopo..wewe unataka kuwafundisha wavunje katiba kwa sababu za hisia zako shame on you..chukua form tukuone jukwaani...otherwise acha blah blah za kupotosha watu!

Mkjj anataka agombee kupitia CCM, kikwazo ni lile tamko/ramli ya Sheikh Yahya ambayo Ikulu wameiridhia... sasa afanyeje asife au kuuliwa hali mapenzi yake ni CCM??!
 
REDET hao ndo walevi namba moja...tafiti zao zote zina makengeza..Yaani wanaona u hopeless wa serikali ya JK lakini bado wanasema JK safi kweli kwelii...
 
Wameshaanza Zanzibar wanataka Karume aongezewe miaka mitatu kwa kisingizio cha mwafaka. Baada ya Zanzibar itakuja bara watasema kwa vile Kikwete alichaguliwa kwa kishindo 2010 basi tusiwe na uchaguzi 2015 aongezewe miaka mingine mitatu ili aongoze serikali ya mpito itakayoundwa hadi 2018.
 
REDET hao ndo walevi namba moja...tafiti zao zote zina magengeza..Yaani wanaona u hopeless wa serikali ya JK lakini bado wanasema JK safi kweli kwelii...

...samahani mkuu; je ulimaanisha kuwa jamaa wale wana "makengeza"?!!
 
mkifikiria sana utaona kuwa pendekezo langu kwa kweli ndilo pendekezo bora zaidi la kutusaidia kuachana na uongozi uchwara. Maana hata yeye anashindwa kufanya kazi nyingi hasa kwa mfano mwaka huu akifikiria mambo ya uchaguzi! Anaogopa hata kwenda kufanyiwa upasuaji bwana.
 
Kumbe hilo ndo tatizo!This was the best opportunity to sort out the really health issue once and for all.What other 5 years term would add is more stress in the already stressed body.
 
Nyinyi wenye mawazo hayo mmelewa . utaratibu upo nani kasema mtu akiongoza vizuri anatakiwa kuongoza maisha . Huo uzuri kwanza mnauona nyinyi mafisadi , sisi tunaoteseka hatutaki hata kusikia .ama kweli Tanzania ina wenyewe. IT is all bull*** . ***and go to sleep.
 
Mkjj anataka agombee kupitia CCM, kikwazo ni lile tamko/ramli ya Sheikh Yahya ambayo Ikulu wameiridhia... sasa afanyeje asife au kuuliwa hali mapenzi yake ni CCM??!
Aagh! Kumbe mwanakijiji anaamini ushirikina wa yahaya..anayemuamini na kumuogopa yahaya ni mjinga wala hafai kuwa mwenyekiti wa tawi..

Hata hivyo anazo options...anaweza kugombea chadema au CUF katiba inamruhusu..

kwahiyo anaweza kufanya chochote under given constitution...kwahiyo aache blah blah za kupotosha wananchi ...
 
Back
Top Bottom